Bible Explorer

Gundua › Mada › Njaa na ukame

Mambo ya kushangaza

Njaa na ukame katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (33), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

Katika Mwanzo

  • Abram alishuka Misri kwa sababu njaa ilikuwa kaliMwa 12:10
    Aya
    Mwa 12:10Kulikuwa na njaa katika nchi, kwa hiyo Abram akaenda kukaa Misri, kwa kuwa njaa ilikua kali katika nchi.
  • Katika njaa nyingine Isaka alikwenda Gerari, si MisriMwa 26:1–2
    Aya
    Mwa 26:1–2Basi njaa ikatokea katika nchi, mbali na njaa ya kwanza iliyotokea siku za Ibrahimu. Isaka akaenda kwa Abimeleki, mfalme wa Wafilisiti huko Gerari. Basi Yahwe akamtokea na kumwambia, “Usishuke kwenda Misri; kaa katika nchi niliyokuambia.
  • Huko Misri miaka saba ya wingi, kisha miaka saba ya njaaMwa 41:29–30, Mwa 41:54
    Aya
    Mwa 41:29–30Tazama, miaka saba yenye utele mwingi inakuja katika nchi yote ya Misri. Na miaka saba ya njaa itakuja baada yake, na utele wote katika nchi ya Misri utasahaulika, na njaa itaiaribu nchi.
    Mwa 41:54Miaka saba ya njaa ikaanza, kama alivyokuwa amesema Yusufu. Kulikuwa na njaa katika nchi zote, lakini katika nchi yote ya Misri kulikuwa na chakula.
  • Yusufu aliweka akiba ya nafaka kama mchanga wa bahariMwa 41:48–49
    Aya
    Mwa 41:48–49Akakusanya chakula chote cha miaka saba iliyokuwako katika nchi ya Misri na kukiweka chakula katika miji. Akaweka katika kila mji chakula cha mashamba yaliyokizunguka. Yusufu akahifadhi nafaka kama mchanga wa bahari, kingi kiasi kwamba akaacha kuhesabu, kwa sababu kilikuwa hakihesabiki.
  • Kila taifa lilikuja kwa Yusufu huko Misri kununua nafakaMwa 41:56–57
    Aya
    Mwa 41:56–57Njaa ilikuwa juu ya uso wote wa nchi. Yusufu akafungua ghala zote na kuuza chakula kwa Wamisri. Njaa ilikuwa kali sana katika nchi ya Misri. Dunia yote ikaja Misri kununua nafaka kutoka kwa Yusufu, kwani njaa ilikuwa kali katika dunia yote.
  • Ndugu kumi wa Yusufu walishuka kununua nafakaMwa 42:1–3
    Aya
    Mwa 42:1–3Basi Yakobo akafahamu kwamba kuna nafaka huko Misri. Akawambia wanawe, “Kwa nini mnatazamana? Akasema, “Tazama, nimesikia kwamba kuna nafaka huko Misri. Shukeni huko mkatununulie chakula ili tuishi wala tusife.” Ndugu kumi wa Yusufu wakashuka Misri kununua chakula.
  • Miaka miwili ya njaa, na mitano zaidi bila kulima wala kuvunaMwa 45:6
    Aya
    Mwa 45:6Maana ni miaka miwili njaa imekuwa katika nchi, na bado kuna miaka mitano ambayo hakutakuwa na kulima wala kuvuna.
  • Wamisri walilipia chakula kwa fedha, kisha kwa mifugo yaoMwa 47:13–17
    Aya
    Mwa 47:13–17Basi hakukuwa na chakula katika nchi yote; kwani njaa ilikuwa kali sana. Nchi ya Misri na nchi ya Kanaani ikaharibika kwa sababu ya njaa. Yusufu akakusanya pesa yote iliyokuwa katika nchi ya Misri na nchi ya Kanaani, kwa kuwauzia wakaaji wake chakula. Kisha Yusufu akaleta ile pesa katika kasri la Farao. Pesa yote ya nchi za Misri na Kanaani ilipokwisha, Wamisri wote wakaja kwa Yusufu wakisema, “Tupe chakula! Kwa nini tufe mbele zako kwa maana pesa yetu imekwisha?” Yusufu akasema, “Ikiwa pesa yenu imekwisha, leteni wanyama wenu nami nitawapa chakula badala ya wanyama wenu.” Hivyo wakaleta wanyama wao kwa Yusufu. Yusufu akawapa chakula kwa kubadilishana na farasi, kondoo, mbuzi na kwa punda. Akawalisha kwa mkate kwa kubadilisha na wanyama wao mwaka ule.
  • Kisha waliuza mashamba yao, na nchi ikawa ya FaraoMwa 47:19–20
    Aya
    Mwa 47:19–20Kwa nini tufe mbele za macho yake, sisi na nchi yetu? Utununue sisi na nchi yetu badala ya chakula, na sisi na nchi yetu tutakuwa watumishi wa Farao. Tupe mbegu ili kwamba tuishi na tusife, na kwamba nchi isiwe tupu bila watu. Hivyo Yusufu akamnunulia Farao nchi yote ya Misri. Kwani kila Mmisri akauza shamba lake, kwa sababu njaa ilikuwa kali sana. Kwa njia hii, nchi ikawa mali ya Farao.
  • Tangu hapo sehemu ya tano ya mavuno ilienda kwa FaraoMwa 47:23–24
    Aya
    Mwa 47:23–24Kisha Yusufu akawambia watu, “Tazama, nimewanunua ninyi na nchi yenu leo kwa ajili ya Farao. Basi mbegu hii hapa kwa ajili yenu, nanyi mtapanda katika nchi. Wakati wa mavuno, mtampa Farao sehemu ya tano, na sehemu nne zitakuwa zenu, kwa mbegu za shamba na kwa chakula cha nyumba zenu na watoto wenu.”

Katika Israeli

  • Siku za waamuzi familia ya Bethlehemu ilihamia MoabuRut 1:1
    Aya
    Rut 1:1Ilitokea katika siku za utawala wa majaji kuwa kulikuwa na njaa katika nchi, na mtu mmoja wa Bethelehemu ya Yuda alikwenda katika nchi ya Moabu pamoja na mke wake na watoto wake walili wa kiume.
  • Naomi alirudi nyumbani aliposikia kuna chakula tenaRut 1:6
    Aya
    Rut 1:6Ndipo Naomi aliamua kuondoka Moabu pamoja na wake wa watoto wake na kurudi Yuda kwa sababu alikuwa amesikia katika mkoa wa Moabu kuwa Yahweh amewasaidia watu wake katika uhitaji na amewapa chakula.
  • Wakati wa Daudi njaa ilidumu miaka mitatu mfululizo2 Sam 21:1
    Aya
    2 Sam 21:1Kulikuwa na njaa kwa miaka mitatu katika siku za utawala wa Daudi, na Daudi akautafuta uso wa Yahwe. “Hivyo Yahwe akasema, “njaa hii ni kwa sababu ya mauaji ya Sauli na familia yake, kwa kuwa aliwauwa Wagibeoni.”
  • Eliya kwa Ahabu: hakuna umande wala mvua isipokuwa kwa neno langu1 Fal 17:1
    Aya
    1 Fal 17:1Eliyas Mtishibi, kutoka Tishibi ya Gileadi, akamwambia Ahabu, “Kama BWANA, Mungu wa Israeli aishivyo, ambaye ninasimama, hakutakuwa na umande wala mvua isiipokuwa kwa neno langu.”
  • Kunguru walimletea Eliya mkate na nyama asubuhi na jioni1 Fal 17:6
    Aya
    1 Fal 17:6Nao kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, naye akanywa maji ya kijito kile.
  • Unga katika mtungi wa mjane na mafuta katika chupa havikwisha1 Fal 17:14–16
    Aya
    1 Fal 17:14–16Kwa kuwa BWANA, Mungu wa Israeli anasema 'Lile pipa la unga halitaisha, wala ile chupa ya mafuta kukoma kutoa mafuta, mpaka siku ile BWANA atakapotuma mvua duniani.” Kwa hiyo yule mjane akafanya kama Eliya alivyomwelekeza, yeye, na Eliya, na mwanae wakala kwa siku nyingi. Lile pipa la Unga halikuisha, wala ile chupa ya mafuta haikukoma kutoa mafuta, kama vile neno la BWANA lilivyosema, kupitia kinywa cha Eliya.
  • Katika mwaka wa tatu njaa ilikuwa kali huko Samaria1 Fal 18:1–2
    Aya
    1 Fal 18:1–2Kwa hiyo baada ya siku nyingi neno la BWANA likamjia Eliya, katika mwaka wa tatu wa ukame, likisema, “Nenda ukajionyeshe mwenyewe kwa Ahabu nami nitainyeshea ardhi mvua.” Eliya akaenda kujionyesha mwenyewe kwa Ahabu; sasa njaa ilikuwa kali sana kule Samaria.
  • Ahabu alimtuma Obadia kutafuta majani kwa ajili ya farasi na nyumbu1 Fal 18:5
    Aya
    1 Fal 18:5Ahabu akamwambia Obadia, “Pita katika nchi yote na katika chemichemi zote za maji na vijito. Yamkini tunaweza kupata maji na nyasi ili tuwaokoa hawa farasi na nyumbu, ili tusiwakose wanyama wote.”
  • Ilikumbukwa baadaye: hakuna mvua kwa miaka mitatu na nusuLk 4:25, Yak 5:17
    Aya
    Lk 4:25Lakini nawaambia ninyi kweli kwamba kulikuwa na wajane wengi Israel katika kipindi cha Eliya, wakati mbingu ilipofungwa kusiwe na nvua kwa miaka mitatu na nusu, wakati kulipokuwa na njaa kubwa katika nchi yote.
    Yak 5:17Eliya alikuwa mtu mwenye hisia kama zetu, aliomba kwa juhudi kwamba mvua isinyeshe, na haikunyesha katika nchi kwa muda wa miaka mitatu na miezi sita.
  • Njaa huko Gilgali: matango mwitu katika mchuzi, “kifo kimo chunguni”2 Fal 4:38–40
    Aya
    2 Fal 4:38–40Kisha Elisha akarudi tena Gilgali. Kulikuwa na njaa katika nchi, na wana wa manabii walikuwa wamekaa mbele yake. Akamwambia mtumishi wake, “Weka sufuria kubwa kwenye moto na pika kwa ajili ya watoto wa manabii.” Mmoja wao akaenda kwenye shamba kukusanya mboga mboga. Alikuta matango ya porini na kukusanya ya kutosha hadi alipojaza kwenye nguo yake. Walizikata na kuziweka kwenye sufuria, lakini hakujua zilikuwa za aina gani. Basi, wakawapakulia na kusambaziwa kwa watu kwa ajili ya kula. Baadae, kadiri walivyokuwa wakiendelea kula, walipiga kelele na kusema, “Mtu wa Mungu, kuna kifo kwenye sufuria!” Hivyo wasingeweza kula tena.
  • Mwanamke Mshunami aliishi miaka saba kati ya Wafilisti wakati wa njaa2 Fal 8:1–3
    Aya
    2 Fal 8:1–3Basi, Elisha alikuwa amemwambia yule mwanamke ambaye alimfufulia mtoto wake. Akamwambia, “Inuka na uenede pamoja na nyumba yako, na uishi popote uwezapo katika nchi nyingine, kwa sababu Yahwe ameiita njaa ambayo itakuja katika hii nchi kwa miaka saba.” Basi yule mwanamke akainuka na akatii lile neno la mtumishi wa Mungu. Akaenda na nyumba yake na kuishi kwenye nchi ya Wafilisti miaka saba. Ikafika kama mwishoni mwa miaka saba yule mwanamke akarudi kutoka kwenye ile nchi ya Wafilisti, na kwenda kwa mfalme kumuomba nyumba yake na kwa ajili ya nchi yake.
  • Wakoma wanne waliikuta tupu kambi ya Washami nje ya Samaria2 Fal 7:3–5
    Aya
    2 Fal 7:3–5Basi, kulikuwa na watu wanne wenye ukoma upande wa nje wa lango la mji. Wakaambizana kila mmoja, “Kwa nini tukae hapa hadi hapo tutakapokufa? Kama tukisema kwamba tutaenda kwenye ule mji, maana mjini kuna njaa, na tutakufa hapo. Lakini kama tukiendelea kukaa hapa, bado tutakufa. Sawa, njoni, twendeni kwenye lile jeshi la Washami. Kama wakitupa uhai, tutakuwa hai, na kama wakituua, tutakufa tu.” Hivyo wakaamka asubuhi kabla giza halijaisha kwenda kwenye kambi ya Washami; Wakati walipofika sehemu ya mwanzo wa kambi, hapakuwa na mtu hapo.
  • Kisha kipimo cha unga laini kiliuzwa kwa shekeli moja2 Fal 7:16
    Aya
    2 Fal 7:16Wale watu wakatoka nje na wakaziteka nyara zile kambi za Washami. Hivyo kipimo cha unga mzuri uliuzwa kwa shekeli moja, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli moja, kama vile ambavyo neno la Yahwe lilivyosema.
  • Wakati wa kuzingirwa kwa Yerusalemu watu wa nchi hawakuwa na chakula2 Fal 25:3, Yer 52:6
    Aya
    2 Fal 25:3Katika siku ya tisa ya mwezi wa nne wa huo mwaka, njaa ilikuwa kali sana kwenye huo mji kwamba hapakuwa na chakula kwa ajili ya watu wa nchi.
    Yer 52:6Katika mwezi wa nne, siku ya tisa ya mwaka huo, njaa ikawa kali sana mjini hata hakukuwa na chakula kwa watu wa nchi.
  • Yeremia: ardhi imepasuka; kulungu jike humwacha mtoto wake kwa kukosa majaniYer 14:4–5
    Aya
    Yer 14:4–5Kwa sababu hii ardhi imepasuka, kwa maana hakuna mvua katika nchi. Wakulima huwa na aibu na kufunika vichwa vyao. Kwa maana hata kunguru huwaacha wanawe katika mashamba, kwa maana hakuna nyasi.
  • Maombolezo: watoto wadogo wanaomba mkateOmb 4:4
    Aya
    Omb 4:4Ulimi wa mtoto mchanga anaye nyonya unagota juu mdomo wake kwa kiu; watoto wanaomba chakula, lakini hakuna kwa ajili yao.
  • Siku za Nehemia watu waliweka rehani mashamba na nyumba ili kununua nafakaNeh 5:3
    Aya
    Neh 5:3Pia kulikuwa na baadhi ya watu ambao walisema, “Tunaweka rehani mashamba yetu, mizabibu yetu, na nyumba zetu ili tupate nafaka wakati wa njaa.”

Katika Agano Jipya

  • Katika hadithi ya Yesu njaa kali inamwacha mwana mdogo katika uhitajiLk 15:14
    Aya
    Lk 15:14Nae alipokua amekwisha tumia vyote njaa kuu iliingia nchi ile naye akaanza kuwa katika uhitaji.
  • Agabo alitabiri njaa kubwa; ilikuja wakati wa KlaudioMdo 11:28
    Aya
    Mdo 11:28Mmoja wao ni Agabo ndilo jina lake, akasimama akiashiriwa na Roho kuwa njaa kali itatokea ulimwenguni mwote. Hii ilitokea wakati wa siku za Klaudio.
  • Wanafunzi walipeleka msaada Uyahudi kupitia Barnaba na SauliMdo 11:29–30
    Aya
    Mdo 11:29–30Kwa hiyo, wanafunzi, kila mmoja alivyo fanikiwa, waliamua kupeleka misaada kwa ndugu walioko Uyahudi. Walifanya hivi; Walituma pesa kwa mkono wa Barnaba na Sauli.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0