Mambo ya kushangaza
Majitu katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (29), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
- Majitu makubwa yalikuwa duniani siku hizoMwa 6:4
Aya
Mwa 6:4Majitu makubwa yalikuwa juu ya uso wa nchi nyakati hizo, na hata baada ya hapo. Hii ilitokea wakati wana wa Mungu walipowaoa binti za wanadamu, na kupata watoto pamoja nao. Hawa walikuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.
- Wapelelezi: tulionekana kama panzi mbele ya uzao wa AnakiHesabu 13:32–33
Aya
Hesabu 13:32–33Kwa hiyo wakasambaza taarifa za kukatisha tamaa kwa Wana wa Israeli juu ya nchi ile waliyoipeleleza. Walisema, “Ile nchi tuliyoiona ni nchi inayowala watu wake. Watu wote tuliowaona ni watu warefu. Kule tuliiona majitu, wana wa uzao wa Anaki, ambao nii uzao wa majitu. Sisi tulionekana kama panzi machoni mwao tulipojilingsnisha nao, hivyo ndivyo tulivyoonekana machoni mwao pia.”
- Waanaki: watu wenye nguvu na warefuKum 1:28, Kum 9:2
Aya
Kum 1:28Tuende wapi sasa? Ndugu zetu wamefanya mioyo yetu kuyeyuka, kusema, Hao watu ni wakubwa na warefu zaidi yetu, miji yao ni mikubwa na imeimarishwa kwenda mbinguni; zaidi ya yote, tumewaona wana wa Anakim huko”
Kum 9:2watu wakuu na warefu, wana wa Anakimu, ambaye mnamjua, na yule mliomsikia watu wakisema, 'Nani atasimama mbele ya wana wa Anak?
- Waemi, warefu kama Waanaki, waliishi MoabuKum 2:10–11
Aya
Kum 2:10–11(Hapo awali waliishi Waemi, watu kama wakuu, wengi, na warefu kama Waanaki; hawa pia wanafikiriwa kuwa Rephaimu, kama Waanaki, lakini Wamoabi huwaita Waemi.
- Waamoni waliwaita Warefai wa nchi yao ZamzummimKum 2:20–21
Aya
Kum 2:20–21(Hiyo tena ilifikiriwa kuwa nchi ya Rephaimu. Warephaimu waliishi hapo awali-lakini Wammonites wanawaita Zamzummim, watu kama wakuu, wengi, na warefu kama Anakim. Lakini Yahwe aliwaharibu mbele ya Wammonites na waliwafuata na kuishi katika maeneo yao.
- Kedorlaoma aliwashinda Warefai, Wazuzi na WaemiMwa 14:5
Aya
Mwa 14:5Kisha katika mwaka wa kumi na nne, Kedorlaoma na wafalme waliokuwa pamoja nae walikuja na kuwashambulia Warefai katika Ashteroth Karnaimu, na Wazuzi katika Hamu, Waemi katika Shawe Kiriathaimu,
Ogu wa Bashani
- Ogu, mfalme wa Bashani, alikuwa wa mwisho wa WarefaiKum 3:11, Yos 12:4
Aya
Kum 3:11(Kwa mabaki ya Refaimu, mfalme Ogi pekee wa Bashani alikuwa amebaki. Tazama! Kitanda chake kilikuwa cha chuma. Hakuna huko Rabbah, ambako wazao wa Ammoni waliishi? Ilikuwa dhiraa tisa urefu na dhiraa nne upana, hiyo njia walitumia watu kupima.)
Yos 12:4Ogu, mfalme wa Bashani, mmoja kati ya mabaki ya Rephaimu, aliyeishi huko Shatarothi na Edrei.
- Kitanda chake cha chuma kilikuwa dhiraa tisa urefu na dhiraa nne upanaKum 3:11
Aya
Kum 3:11(Kwa mabaki ya Refaimu, mfalme Ogi pekee wa Bashani alikuwa amebaki. Tazama! Kitanda chake kilikuwa cha chuma. Hakuna huko Rabbah, ambako wazao wa Ammoni waliishi? Ilikuwa dhiraa tisa urefu na dhiraa nne upana, hiyo njia walitumia watu kupima.)
- Israeli walimshinda Ogu huko Edrei na kuchukua miji yake sitiniHesabu 21:33–35, Kum 3:1–4
Aya
Hesabu 21:33–35Kisha wakageuka na kuelekea njia inayoelekea Bashani. Ogu mfalme wa Bashani akatofautiana nao, yeye na Jeshi lake lote, ili apigane nao kule Ederei. Kisha BWANA akasema na Musa, “Msimwogope, kwa sababu nimewapeni ushindi dhidi yake, Jeshi lake lote na nchi yake. Mfanyeni kama mlivyomfanya Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akiishi Heshiboni.” Kwa hiyo wakamuua, na wanawe, na jeshi lake lote, mpaka wote wakaishi na hakubaki hata mmoja aliyebaki hai. Kisha wakaichukua nchi yake.
Kum 3:1–4Kisha tuligeuka na kwenda njia ya juu Bashani. Ogi, mfalme wa Bashani, alikuja na kutuvamia, yeye na watu wake wote, kupigana huko Edrei. Yahwe aliniambia mimi, “Usimuogope; kwa kuwa nimekupa ushindi dhidi yake na nimewaweka watu wake wote na nchi yake chini ya utawala wako. Utamfanya kama ulivyomfanya Sihoni, mfalme wa Amorites, aliyeishi Heshbon. Kwa hiyo Yahwe Mungu wetu pia alitupa ushindi dhidi ya Ogi mfalme wa Bashani, na watu wake wote waliwekwa chini ya utawala wetu. Na tulimpiga mpaka kufa na hakuna yoyote wa watu wake walibaki. Tulichukua miji yake yote kwa wakati huo; hapakuwa na mji hata mmoja ambao hatukuchukua kutoka kwao: miji sitini - mikoa ya Argobi yote, ufalme wa Ogi Bashani.
- Nchi yake ilipewa Rubeni, Gadi na nusu ya ManaseHesabu 32:33, Kum 29:7–8
Aya
Hesabu 32:33Kwa hiyo uzao wa Gadi na Reubeni, na pia nusu ya kabila la Manase mwana wa Yusufu, Musa akawapa ufalme wa Sihoni, mfalme wa Waamori, na wa Ogi, mafalme wa Bashani, Aliwapa hiyo nchi, na kuwagawia miji yake yote pamoja na mipaka yake, miji yote ya nchi inayowazunguka.
Kum 29:7–8Mlipokuja mahali hapa, Sihoni, mfalme wa Heshboni, na Ogu, mfalme wa Bashani, walikuja dhidi yetu kutupiga, na tukawapiga. Tulichukua ardhi yao na kuwapa kama urithi Wareubeni, kwa Wagadi, na kwa nusu ya kabila ya Manase.
Hebroni na Waanaki
- Hebroni zamani uliitwa Kiriathi Arba, kwa jina la Arba, Mwanaki mkuu kuliko woteYos 14:15, Yos 15:13
Aya
Yos 14:15Basi, jina la Hebroni hapo mwanzo lilikuwa ni Kiriathi Arba (Arba ambaye alikuwa ni mtu mkuu miongoni mwa Wanakim). Kisha nchi ikawa na raha bila vita.
Yos 15:13Katika kulitunza agizo la Yahweh kwa Yoshua, Yoshua alimpa Kalebu mwana wa Yefune mgao wa nchi ya. miongoni mwa kabila la Yuda, alimgawia nchi Kiriathi Arba, ambayo ndio Hebroni (Arba alikuwa ni baba wa Anaki).
- Kalebu aliwafukuza wana watatu wa Anaki: Sheshai, Ahimani, TalmaiYos 15:14, Amu 1:20
- Yoshua aliwaondoa Waanaki; wachache walibaki Gaza, Gathi na AshdodiYos 11:21–22
Aya
Yos 11:21–22Kisha Yoshua akaja kwa wakati ule na aliiangamiza Anakimu. Aliyafanya haya katika nchi ya milima, huko Hebroni, Debiri, Anabu, na katika nchi yote ya Yuda, na katika nchi yote ya milima ya Israeli. Yoshua aliwaangamiza kabisa pamoja na miji yao. Hakuna hata mmoja wa watu wa Anakimu aliyeachwa katika nchi ya Israeli, isipokuwa huko Gaza, Gathi na Ashidodi.
Goliathi na jamaa zake
- Goliathi wa Gathi alikuwa na urefu wa dhiraa sita na shibiri moja1 Sam 17:4
Aya
1 Sam 17:4Mtu mmoja mwenye nguvu akatoka katika kambi ya Wafilisti, mtu huyo aliitwa Goliathi wa Gathi, kimo chake mikono sita na shubiri moja.
- Deraya yake ilikuwa na uzito wa shekeli elfu tano1 Sam 17:5
Aya
1 Sam 17:5Alikuwa na chepeo ya shaba kichwani mwake, na alivaa dirii ya chuma. Hiyo dirii ilikuwa na uzito wa shekeli elfu hamsini za shaba.
- Ncha ya mkuki wake ilikuwa na uzito wa shekeli mia sita1 Sam 17:7
Aya
1 Sam 17:7Ule mpini wa mkuki wake ulikuwa mkubwa, wenye kamba iliyo na kitanzi kwa ajili ya kuutupia kama kamba ya sindano ya mfumaji. Kichwa cha mkuki wake kilikuwa na uzito wa shekeli mia sita za chuma. Aliyembebea ngao alitembea mbele yake.
- Kwa siku arobaini alijitokeza kila asubuhi na jioni1 Sam 17:16
Aya
1 Sam 17:16Kwa muda wa siku arobaini yule Mfilisti mwenye nguvu alikuwa akijitokeza asubuhi na jioni kwa ajili ya vita.
- Daudi alimuua kwa kombeo na jiwe1 Sam 17:49–50
Aya
1 Sam 17:49–50Daudi aliweka mkono wake mfukoni, akachukua jiwe kutoka humo, akalitupa kwa kombeo, na likampiga Mfilisti kwenye paji la uso, akaanguka chini kifudifudi. Daudi alimshinda Mfilisti kwa kombeo na kwa jiwe moja. Alimpiga huyo Mfilisti na kumuua. Mkononi mwa Daudi hakukuwa na upanga.
- Baadaye upanga wa Goliathi ulihifadhiwa umefungwa nyuma ya efodi1 Sam 21:9
Aya
1 Sam 21:9Kuhani akasema, “Ule upanga wa Mfilisti Goliathi, uliyemuua katika bonde la Ela, uko hapa umefunikwa katika nguo nyuma ya naivera. kama unataka kuuchukua huo, uchukue, maana hakuna silaha nyingine hapa.” Daudi akasema, “Hakuna silaha nyingine kama hiyo, nipatie hiyo.”
- Mkuki wa shaba wa Ishbibenobu ulikuwa na uzito wa shekeli mia tatu; Abishai alimuua2 Sam 21:16–17
Aya
2 Sam 21:16–17Ishbibenobu, wa uzao wa majitu, ambaye mkuki wake wa shaba ulikuwa na uzito wa shekeli mia tatu na alikuwa na upanga mpya, alitaka kumwua Daudi. Lakini Abishai mwana wa Seruya akamwokoa Daudi, akampiga Mfilisti na kumwua. Ndipo watu wa Daudi wakamwapia, kusema, “Hautakwenda vitani pamoja nasi tena usije ukaizima taa ya Israeli.”
- Elhanani alimuua Lami, ndugu wa Goliathi1 Nya 20:5
Aya
1 Nya 20:5Ikawa tena katika pambano na Wafilisti huko Gobu, kwamba Elhanani mwana wa Yari Mbethilehemu akamua Lami kaka wa Goliathi Mgiti, ambaye mkuki wake ulikuwa kama gongo la mshonaji.
- Mtu wa Gathi alikuwa na vidole sita kila mkono na sita kila mguu2 Sam 21:20–21, 1 Nya 20:6–7
Aya
2 Sam 21:20–21Ikawa katika vita nyingine huko Gathi kulikuwa na mtu mrefu sana mwenye vidole sita katika kila mkono na vidole sita katika kila mguu, jumla yake ishirini na vinne. Yeye naye alikuwa wa uzao wa Warefai. Alipowatukana Israeli, Yonathani mwana mwana wa Shama, nduguye Daudi, akamwua.
1 Nya 20:6–7Ikaja kuwa tena katika pambano lingine huko Gathi kwamba mwanaume mmoja aliye mrefu sana mwenye vidole sita kila mkono na vidole sita mguuni. Naye alikuwa pia wa uzao wa Refaimu. Alipo dhihaki jeshi la Israeli, Yehonadabu mwana wa Shimea, kaka wa Daudi, akamuua.
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0