Bible Explorer

Gundua › Mada › Funguo, mihuri na pete za muhuri

Mambo ya kushangaza

Funguo, mihuri na pete za muhuri katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (27), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

Funguo na makomeo

  • Ehudi alifunga milango ya chumba cha juu cha mfalme Egloni nyuma yakeAmu 3:23
    Aya
    Amu 3:23Kisha Ehudi akatoka kwenye ukumbi na akafunga milango ya chumba cha juu nyuma yake na akawafungia.
  • Watumishi walingoja, kisha wakachukua ufunguo na kufungua milangoAmu 3:24–25
    Aya
    Amu 3:24–25Baada ya Ehudi kuondoka, watumishi wa mfalme wakaja; wakaona milango ya chumba cha juu imefungwa, kwa hiyo wakafikiri, 'Hakika atakuwa anajitoa mwenyewe katika hali ya baridi ya chumba cha juu.' Walizidi kuwa na wasiwasi hata walipoanza kuhisi kuwa walikuwa wakipuuza wajibu wao wakati mfalme bado hakufungua milango ya chumba cha juu. Kwa hiyo walichukua ufunguo wakawafungua, tazama bwana wao, ameanguka chini, amekufa.
  • Walawi walilinda nyumba ya Mungu usiku na kuifungua kila asubuhi1 Nya 9:27
    Aya
    1 Nya 9:27Walitumia usiku wao sehemu walizowekwa kuzunguka nyumba ya Mungu, kwao ilikuwa ni wajibu wao kulinda. Na walifungua geti kila asubuhi.
  • Malango ya Yerusalemu yalijengwa upya pamoja na milango, makomeo na mapingoNeh 3:3
    Aya
    Neh 3:3Wana wa Senaa wakajenga lango la samaki. Wanaweka mihimili yake na kuweka milango yake na vyuma vyake na makomeo yake.

Mihuri na pete za muhuri

  • Yuda alimwachia Tamari muhuri wake, kamba na fimbo kama rehaniMwa 38:18
    Aya
    Mwa 38:18Akasema, “Nikupe rehani gani?” Naye akasema, “Mhuri wako na mshipi, na fimbo iliyo mkononi mwako.” Akampa na kulala naye. Akawa mjamzito.
  • Tamari: “Muhuri huu na kamba na fimbo hii ni vya nani?”Mwa 38:25
    Aya
    Mwa 38:25Alipoletwa nje, alipeleka ujumbe kwa mkwewe, “Mimi ni mjamzito kwa mtu mwenye vitu hivi.” Akasema, “Tambua tafadhari, mhuri huu na mshipi na fimbo ni vya nani.”
  • Farao aliweka pete yake ya muhuri kidoleni mwa YusufuMwa 41:42
    Aya
    Mwa 41:42Farao akavua pete yake ya mhuri kutoka katika mkono wake na kuiweka katika mkono wa Yusufu. Akamvika kwa mavazi ya kitani safi, na kuweka mkufu wa dhahabu shingoni mwake.
  • Yezebeli aliandika barua kwa jina la Ahabu na kuzitia muhuri wake1 Fal 21:8
    Aya
    1 Fal 21:8Kwa hiyo Yezebeli akaandika barua kwa jina la Ahabu, akaitia muhuri wake, akazituma kwa wazee na kwa watu tajiri alioketi nao kwenye vikao, na ambao pia waliishi karibu na Nabothi.
  • Ahasuero alimpa Hamani pete yake ya muhuriEst 3:10
    Aya
    Est 3:10Ndipo mfamle akavua pete yake ya muhuri na kumpa Hamani, adui wa Wayahudi.
  • Agizo la Hamani liliandikwa kwa jina la mfalme na kutiwa muhuri kwa peteEst 3:12
    Aya
    Est 3:12Kisha waandishi wa mfalme walikusanyika katika siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza, na mbiu iliyokuwa na matakwa ya Hamani yalikuwa yameandikwa na kupelekwa kwa wasimamizi wa majimbo, na wale wote waliokuwa juu ya wasimamizi wa majimbo yote, na wasimamizi wa watu, na kwa kila jimbo kwa andiko lao, na kila watu na lugha yao. Mbiu hii ilikuwa imeandikwa kwa jina la mfalme Ahusiero na kupigwa muhuri wa pete yake.
  • Pete, iliyochukuliwa kutoka kwa Hamani, ilipewa MordekaiEst 8:2
    Aya
    Est 8:2Kisha Mfalme akampa pete yake aliyokuwa amempa Hamani. Malkia Esta akampandisha Modekai ili awe mkuu katika shamba la Hamani.
  • Amri iliyotiwa muhuri kwa pete ya mfalme haiwezi kutanguliwaEst 8:8
    Aya
    Est 8:8Hivyo andika mbiu nyingine kwa ajili ya Wayahudi kwa jina la mfalme na uipige muhuri kwa pete ya mfalme. Kwa sababu mbiu imekwisha andikwa kwa jina la mfalme na kugongwa muhuri kwa pete ya mfamle na haiwezi kubatilishwa.”
  • Mordekai alizitia barua muhuri na kuzipeleka kwa matarishi wapanda farasiEst 8:10
    Aya
    Est 8:10Modekai akaandika kwa jina la Mfalme Ahusiero na akazipiga muhuri kwa pete ya mfalme. Akapeleka nyaraka kwa matarishi, akawapandisha kwenye farasi waendao kwa haraka waliotumika kwa huduma ya mfalme, waliozaliwa kwa mfalme.
  • Tundu la simba lilitiwa muhuri kwa pete ya mfalme na pete za wakuu wakeDan 6:17
    Aya
    Dan 6:17Jiwe lililetwa katika mlango wa tundu, na mfalme alilitia muhuri wa pete yake mwenyewe na pamoja na muhuri wa wakuu wake ili kwamba chochote kisiweze kubadilishwa kuhusiana na Danieli.
  • Agano lililoandikwa na kutiwa muhuri kwa majina ya viongozi, Walawi na makuhaniNeh 9:38, Neh 10:1
    Aya
    Neh 9:38Kwa sababu ya yote haya, tunafanya agano thabiti kwa kuandika. Kwenye hati iliyofungwa ni majina ya wakuu wetu, Walawi, na makuhani.”
    Neh 10:1Wale ambao waliweka majina yao kwenye nyaraka zilizofunikwa walikuwa Nehemia mwana wa Hakalia gavana, na makuhani waliowekwa walikuwa Sedekia,
  • Yeremia alitia sahihi na muhuri hati: nakala moja iliyotiwa muhuri, moja waziYer 32:10–11
    Aya
    Yer 32:10–11Kisha niliandika katika barua na kuitia muhuri, na kulikuwa na mashadi wakaishuhudia. Kisha nikampa fedha katika mizani. Kisha nikaichukua hati ya manunuzi ambayo ilikuwa imepigwa muhuri, kwa kuifuata amri na taratibu, na kama ilivyo ada.
  • Hati ziliwekwa katika chungu cha udongo ili zidumu muda mrefuYer 32:14
    Aya
    Yer 32:14Yahwe, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Chukua nyaraka hizi, vyote hati hii ya manunuzi iliyopigwa muhuri na nakala zisizopigwa muhuri za manunuzi, na uziweke katika chungu cha udongo ili vidumu kwa muda mrefu.
  • Kaburi la Yesu lililindwa kwa kulitia jiwe muhuri na kuweka walinziMt 27:66
    Aya
    Mt 27:66Hivyo walikwenda na kufanya kaburi kuwa salama, jiwe liligongwa mhuri na kuweka walinzi.

Kuchorwa kama muhuri

  • Mawe mawili ya shohamu yaliyochorwa kama muhuri kwa majina ya wana wa IsraeliKut 28:9, Kut 28:11, Kut 39:6
    Aya
    Kut 28:9Nawe utatwaa vito viwili vya shohamu, ya rangi ya chani-kiwiti, nawe utachora juu yake majina ya wana wa Israeli;
    Kut 28:11Kwa kazi mtu mwenye kuchora mawe kama vile muhuri ichorwavyo, utavichora hivi vito viwili, sawasawa na majina ya wana wa Israeli, nawe utavitia katika vijalizo vya dhahabu.
    Kut 39:6Kisha wakafanya mawe ya shohamu yaliyopangwa kwenye mapambo ya dhahabu, yaliyochongwa kwa michoro ya muhuri kulingana na majina ya wana wa Israeli.
  • Mawe kumi na mawili ya kifuko, kila moja limechorwa kama muhuri kwa jina la kabilaKut 28:21, Kut 39:14
    Aya
    Kut 28:21Na vile vito vitakuwa sawasawa na majina ya wana wa Israeli, kumi na viwili, sawasawa na majina yao. Mfano wa kuchora kwa muhuri kila kimoja sawasawa na jina lake, vitakuwa vya hizo kabila kumi na mbili.
    Kut 39:14Na mawe hayo yalikuwa kulingana na majina ya wana wa Israeli. Yalikuwa kumi na mawili kulingana na majina yao, kwa michongo ya muhuri, kila moja kulingana na jina lake kwa ajili ya yale makabila kumi na mawili.
  • Bamba la dhahabu lililochorwa kama muhuri: MTAKATIFU KWA BWANAKut 28:36, Kut 39:30
    Aya
    Kut 28:36Nawe fanya bamba la dhahabu safi na kuchora juu yake, mfano wa machoro ya muhuri, “Mtakatifu kwa Yahweh.”
    Kut 39:30Mwishowe wakafanya lile bamba linalong’aa, ishara takatifu ya wakfu, kutokana na dhahabu safi na kuandika juu yake maandishi kwa mchongo wa muhuri: “Utakatifu kwa Yahweh. ”
  • Msemo katika Wimbo Ulio Bora: “Niweke kama muhuri juu ya moyo wako”Wim 8:6
    Aya
    Wim 8:6Nieka kama muhuri kwenye moyo wako, kama muhuri kwenye mkono wako, kwa kuwa mapenzi yana nguvu kama mauti. Mapenzi mazito hayana kurudi kama kwenda kuzimu; miale yake yalipuka; ni miale ya moto inayo waka, miale yenye joto kuliko moto wowote.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0