Bible Explorer

Gundua › Mada › Matofali na utengenezaji wa matofali

Mambo ya kushangaza

Matofali na utengenezaji wa matofali katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (15), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Huko Babeli: “Na tufanye matofali na kuyachoma kabisa”Mwa 11:3
    Aya
    Mwa 11:3Wakasemezana, “Haya njoni, tufanye matofari na tuyachome kikamilifu.” Walikuwa na matofari badala ya mawe na lami kama chokaa.
  • Walitumia matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaaMwa 11:3
    Aya
    Mwa 11:3Wakasemezana, “Haya njoni, tufanye matofari na tuyachome kikamilifu.” Walikuwa na matofari badala ya mawe na lami kama chokaa.
  • Ezekieli alichora mji wa Yerusalemu juu ya tofaliEze 4:1
    Aya
    Eze 4:1“Lakini wewe, mwana wa adamu, chukua tofali wewe mwenyewe na uliweke mbele yako. Kisha chonga mji wa Yerusalemu juu yake.
  • Daudi aliwatumikisha Waamoni katika tanuri za matofali2 Sam 12:31
    Aya
    2 Sam 12:31Akawatoa watu waliokuwa mjini naye akawalazimisha kufanya kazi kwa misumeno, sululu na shoka; lakini pia akawalazimisha kutengeneza matofali. Daudi akailazimisha miji yote ya watu wa Amoni kufanya kazi hiyo. Kisha Daudi na jeshi lote wakarudi Yerusalemu
  • Yeremia alizika mawe katika sakafu ya matofali ya jumba la Farao huko TahpanhesiYer 43:9
    Aya
    Yer 43:9“Chukua mawe makubwa mkononi mwako, na, kwenye macho ya watu wa Yuda, yafiche kwenye chokaa kwenye njia ya kuingia katika nyumba ya Farao huko Tahpanhesi.
  • Majivuno katika Isaya: “Matofali yameanguka, lakini tutajenga kwa mawe”Isa 9:10
    Aya
    Isa 9:10Matofali yameanguka, lakini tutajenga tena kwa jiwe la patasi; mkuyu umekatwa chini, lakini tutaotesha mierezi katika eneo lao.
  • Isaya anataja uvumba uliofukizwa juu ya madhabahu za matofaliIsa 65:3
    Aya
    Isa 65:3Kuna watu wanoendelea kunipinga mimi, wanatoa sadaka zao katika bustani, na kuchoma ubani juu ya matofali.
  • Nahumu kwa Ninawi: “Kanyaga udongo; tengeneza tanuri ya matofali!”Nah 3:14
    Aya
    Nah 3:14Nenda ukachote maji kwenye boma iliyozingirwa; ziimarishe ngome zako; nenda kwenye udongo na kandamiza matope; finyanga kwa ajili ya matofali.

Huko Misri

  • Maisha ya Waisraeli yalifanywa machungu kwa kazi ya matofali na chokaaKut 1:14
    Aya
    Kut 1:14Waliyafanya maisha yao kuwa machungu kwa kuwafanyisha kazi ngumu kwa vinu na matofali na kwa kila aina ya kazi za shambani. Kazi zao zote zilikuwa ngumu.
  • Walijenga miji ya ghala ya Pithomu na RamesesiKut 1:11
    Aya
    Kut 1:11Hivyo wakawekea walinzi ambao waliwatesa kwa kuwatumikisha kazi ngumu. Waisraeli walijenga maghala ya miji kwa ajili ya Farao: Pishoni na Ramsei.
  • Farao: hakuna majani tena, lakini hesabu ileile ya matofaliKut 5:7–8
    Aya
    Kut 5:7–8“Tofauti na ilivyokuwa mwanzo, “Tofauti ni ilivyokuwa awali, msiwapatie tena watu majani ya kutengenezea tofali. Waacheni wao waende kujitafutia majani wenyewe. Ingawa wanapaswa kuleta hesabu sawa ya matofali watakayotengeneza kama ilivyokuwa awali. Msipokee pungufu, kwasababu wao ni wavivu. Ndiyo maana wanapiga kelele na kusema, 'turuhusu tuende tukamtolee sadaka Mungu wetu.'
  • Watu walitawanyika katika Misri kukusanya mabua badala ya majaniKut 5:12
    Aya
    Kut 5:12Basi watu hao wakatawanyika katika nchi yote ya Misri ili wapate kukusanya matakataka badala ya majani.
  • Wasimamizi Waisraeli walipigwa kwa kutotimiza hesabuKut 5:14
    Aya
    Kut 5:14Wanyapara wa Farao wakawapiga wasimamizi wa Waisraeli, watu walewale ambao waliwaweka kuwa wasimamizi wa watumishi. Wale Wanyapara wakakazana kuwauliza, “Kwanini hamjatimiza idadi ya matofali inayotakiwa kwenu, siku ya jana na hata leo kama ambavyo mlifanya siku za nyuma?”
  • “Hatupewi majani, lakini tunaambiwa: Fanyeni matofali!”Kut 5:16
    Aya
    Kut 5:16Sisi watumishi wako hatupewi majani tena, lakini bado wanatuambia sisi, “Tengenezeni tofali!' Sisi watumwa wako tunapigwa sasa, lakini kosa hilo ni la watu wako.”
  • “Msipunguze hesabu yenu ya matofali ya kila siku”Kut 5:18–19
    Aya
    Kut 5:18–19Sasa rudini kazini. Hamtapewa majani tena, lakini mnapaswa kutengeneza idadi ile ile ya matofali.” Wanyapara wa wana wa Israeli wakagundua ya kuwa walikuwa kwenye shida kubwa mara walipoambiwa, “Hamtapunguza kamwe idadi ya matofali mnayotengeneza kila siku.”

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0