Bible Explorer

Gundua › Mada › Nyota

Mambo ya kushangaza

Nyota katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (21), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Mungu aliumba mianga miwili mikubwa, na nyota piaMwa 1:16
    Aya
    Mwa 1:16Mungu akafanya mianga mikuu miwili, mwanga mkuu zaidi kutawala mchana, na mwanga mdogo kutawala usiku. Akafanya nyota pia.
  • Abraham anaambiwa ahesabu nyota, kama anawezaMwa 15:5
    Aya
    Mwa 15:5Kisha akamtoa nje, na akasema, Tazama mbinguni, na uzihesabu nyota, ikiwa unaweza kuzihesabu.” Kisha akamwambia, hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa.
  • Uzao kama nyota na kama mchangaMwa 22:17, Kum 1:10
    Aya
    Mwa 22:17hakika nitakubariki na nitakuzidishia uzao wako kama nyota za angani, na kama mchanga ulioko kwenye ufukwe wa bahari; na uzao wakowatamiliki lango la adui zao.
    Kum 1:10Yahwe Mungu wako amekuzidisha, na tazama, leo umekuwa umati wa nyota angani.
  • Huhesabu idadi ya nyota na kuziita kila moja kwa jinaZab 147:4
    Aya
    Zab 147:4Huzihesabu nyota, naye huzipa majina zote.
  • Nyota hutofautiana na nyota kwa fahari1 Kor 15:41
    Aya
    1 Kor 15:41Kuna utukufu mmoja wa jua, na utukufu mwingine wa mwezi, na utukufu mwingine wa nyota. Kwa kuwa nyota moja inatofautiana na nyota nyingine katika utukufu.
  • Yusufu aliota nyota kumi na moja zikimwinamiaMwa 37:9
    Aya
    Mwa 37:9Akaota ndoto nyingine na kuwasimulia ndugu zake. Alisema, “Tazama, nimeota ndoto nyingine: Jua na mwezi na nyota kumi na moja ziliniinamia.”
  • Nyota zilipigana kutoka njia zao dhidi ya SiseraAmu 5:20
    Aya
    Amu 5:20Nyota zilipigana kutoka mbinguni, kutoka katika njia zao za mbinguni zilipigana na Sisera
  • Nyota za asubuhi ziliimba pamojaAyu 38:7
    Aya
    Ayu 38:7wakati nyota za asubuhi zilipoimba pamoja na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?
  • Wasomi wa mashariki waliiona nyota yake masharikiMt 2:2
    Aya
    Mt 2:2“Yuko wapi yeye ambaye aliyezaliwa Mfalme wa Wayahudi? Tuliiona nyota yake mashariki nasi tumekuja kumwabudu.”
  • Nyota iliwatangulia na kusimama juu ya mahali paleMt 2:9–10
    Aya
    Mt 2:9–10Baada ya kuwa wamemsikia mfalme, waliendelea na safari yao, na nyota ile waliyokuwa wameiona mashariki iliwatangulia hadi iliposimama juu ya mahali mtoto aliyezaliwa alipokuwa. Wakati walipoiona nyota, walifurahi kwa furaha kuu mno.
  • Daudi hakuwahesabu walio chini ya miaka ishirini: Israeli wangekuwa kama nyota1 Nya 27:23
    Aya
    1 Nya 27:23Daudi hakuwa hesabu wenye umri wa miaka ishirini au chini zaidi, kwasababu Yahweh alihaidi kuongeza Israeli kama nyota za mbinguni.

Makundi ya nyota yaliyotajwa

  • Dubu, Orioni, Kilimia na makundi ya nyota ya kusiniAyu 9:9
    Aya
    Ayu 9:9ambaye huumba Dubu, Orioni, kilima, na makundi ya nyota ya kusini.
  • Je, waweza kuifunga Kilimia au kuufungua mshipi wa Orioni?Ayu 38:31–32
    Aya
    Ayu 38:31–32Je unaweza kuzifunga minyororo ya Kilimia, au kuvifungua vifundo vya Orioni? Je unaweza kuziongoza nyota kutokea katika nyakati zake? Je waweza kuongoza dubu pamoja na watoto wake?
  • Amosi: aliziumba Kilimia na OrioniAmo 5:8
    Aya
    Amo 5:8Mungu aliiumba Pleidezi na Orioni; amebadilisha giza kuwa asubuhu; hufanya siku kuwa giza na usiku na kuita maji ya bahari; yeye huyamwaga juu ya uso wa dunia. Yahwe ndilo jina lake!

Kuabudu nyota

  • Israeli waliambiwa wasiinamie jua, mwezi na nyotaKum 4:19
    Aya
    Kum 4:19Hautainua macho yako juu mbinguni na kutazama jua, mwezi, au nyota - jeshi lote la mbinguni- ukusogezwa na kuviabudu na kuvisujudia- vile vyote ambavyo Yahwe Mungu wenu amewapa hisa watu wote walio chini ya anga lote.
  • Israeli na Mfalme Manase walilisujudia jeshi lote la mbinguni2 Fal 17:16, 2 Fal 21:3
    Aya
    2 Fal 17:16Wakazipuuza amri zote za Yahwe Mungu wao. Wakatengeneza sanamu za kusubu za ndama wawili kuziabudu. Wakatengeza nguzo ya Ashera, na wakaziabudu nyota zote za mbinguni na Baali.
    2 Fal 21:3Kwa kupajenga tena mahala pa juu ambapo Hezekia baba yake alipaharibu, na akajenga madhabahu kwa ajili ya Baali, akafanya Ashera, kama Ahabu mfalme wa Israeli alivyofanya, akasujudu kwa nyota zote za mbinguni na kuwaabudu wao.
  • Yosia aliwaondoa makuhani waliofukiza uvumba kwa makundi ya nyota2 Fal 23:5
    Aya
    2 Fal 23:5Akawaondoa makuhani waliokuwa wanaabudu miungu ambao wafalme wa Yuda waliwachagua ili kwa ajili ya kufukiza ubani katika mahali pa juu kwenye miji ya Yuda na sehemu zinazoizunguka Yerusalemu-wale waliokuwa wanchoma ubani kwa Baali, kwa juana kwa mwezi, kwa sayari, na kwa nyota zote za mbinguni.
  • Watu walilisujudia jeshi la mbinguni juu ya mapaaYer 19:13, Sef 1:5
    Aya
    Yer 19:13kwa hiyo nyumba za Yerusalemu na wafalme wa Yuda watakuwa kama Tofethi, nyumba zote zilizo juu ya watu waovu wanaoabudu nyota zote za mbinguni na kumwaga sadaka za kinywaji kwa miungu mingine.'”
    Sef 1:5watu ambao juu ya nyumba huabudu miili ya mbinguni, na watu ambao huabudu na kuapa kwa Yahwe bali ambao pia huapa kwa mfalme wao.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0