Bible Explorer

Gundua › Mada › Mawe ya kusaga, tanuri na kuoka

Mambo ya kushangaza

Mawe ya kusaga, tanuri na kuoka katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (32), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

Mawe ya kusaga na kusaga

  • Mawe ya kusagia hayawezi kuchukuliwa kama rehani ya deniKum 24:6
    Aya
    Kum 24:6Mwanamume yeyote hatachukua kinu wala jiwe la kinu kama dhamana, kwa maana hivyo itakuwa kuchukua Maisha ya mtu kama dhamana.
  • Huko Misri mjakazi wa chini kabisa alifanya kazi nyuma ya jiwe la kusagiaKut 11:5
    Aya
    Kut 11:5Wazaliwa wa kwanza wote wa nchi ya Misri watakufa, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa Farao, anaye keti kiti chake cha enzi, mpaka mzaliwa wa kwanza wa misichana mtumwa anaye saga mbegu, na kwa wazaliwa wa kwanza wa mifugo.
  • Mana ilisagwa kwa jiwe la mkono au kutwangwa kinuniHesabu 11:8
    Aya
    Hesabu 11:8watu wakazunguka kisha wakakusanyika. Wakaisaga, wakaitwanga kwa vinu, wakaitokosa nyunguni, na kuitengeneza mikate. radha yake ilikuwa kama mafuta mapya ya mizeituni.
  • Huko Thebesi mwanamke alimdondoshea Abimeleki jiwe la juu la kusagiaAmu 9:53, 2 Sam 11:21
    Aya
    Amu 9:53Lakini mwanamke akatupa jiwe la juu, juu ya kichwa cha Abimeleki likavunja fuvu lake.
    2 Sam 11:21Ni nani aliyemwua Abimeleki mwana wa Yerubeshethi? Siye mwanamke aliyerusha jiwe la kusagia juu yake kutoka ukutani, hata akafa huko Thebesi? Kwanini basi mliukaribia ukuta jinsi hiyo? Nawe umjibu, 'Uria mtumishi wako amekufa pia.”
  • Samsoni, amepofushwa na kufungwa pingu, alisaga nafaka gerezani huko GazaAmu 16:21
    Aya
    Amu 16:21Wafilisti walimkamata na kumng'oa macho. Wakampeleka Gaza na kumfunga kwa shaba. Alikuwa akisaga ngano katika gerezani.
  • Yesu anazungumza juu ya wanawake wawili wakisaga pamojaMt 24:41, Lk 17:35
    Aya
    Mt 24:41Wanawake wawili watakuwa wanasaga pamoja - mmoja atachukuliwa, na mmoja atabaki.
    Lk 17:35Kutakua na wanawake wawili wanasaga nafaka pamoja, mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.”
  • Yesu: afadhali kuzamishwa na jiwe kubwa la kusagia shingoniMt 18:6
    Aya
    Mt 18:6Lakini yeyote asababishaye mmoja kati ya wadogo hawa wanaoniamini kuasi, itakuwa vizuri kwa mtu huyo jiwe kuu la kusagia likafungwa shingoni mwake, na kuzamishwa kilindini mwa bahari.
  • Yeremia anataja sauti ya mawe ya kusagia pamoja na sauti za bibi na bwana arusiYer 25:10
    Aya
    Yer 25:10Sauti ya furaha na sherehe-sauti ya bwana arusi na bibi arusi, sauti ya mawe ya kusagia na mwanga wa taa-nitafanya mambo yote haya kutoweka kutoka kwa mataifa haya.
  • Maombolezo: vijana wanataabika kwenye mawe ya kusagiaOmb 5:13
    Aya
    Omb 5:13Wanaume vijana wanalizimishwa kusaga mbegu kwa jiwe la kusagia, na wavulana wanajikwa chini ya vifurushi vya kuni.

Tanuri na kuoka

  • Vyura wangeingia katika tanuri na vyombo vya kukandia vya MisriKut 8:3
    Aya
    Kut 8:3Mito itajawa na vyura. Watatoka na kuingia nyumbani kwako, chumbani kwako, na kitandani kwako. Wataenda nyumbani mwa watumishi wako. Wataenda kwa watu wako, kwenye majiko yako, na vyombo vya kukandia mkate.
  • Sadaka za unga zingeweza kuokwa tanurini au kupikwa kwenye kikaangoLaw 2:4, Law 7:9
    Aya
    Law 2:4Kisha utakapotoa sadaka ya unga bila chachu iliyookwa kweye kiokeo, itakuwa mkate lainiya unga safi uliochanganywa na mafuta, au mkate mgumu usiokuwa na chachu, ambao umesambazwa na mafuta.
    Law 7:9Kila sadaka ya nafaka inayookwa mekoni, na kila sadaka kama hiyo ipikwayo kaangoni au kwenye sufuria itakuwa ya kuhani aitoaye.
  • Tanuri iliyoguswa na mzoga najisi ilipaswa kuvunjwaLaw 11:35
    Aya
    Law 11:35Na kitu chochote kinachoweza kunywewa kutoka kwenye chungu kama hicho kitakuwa najisi. Kila kitu kitakachoangukiwa juu yake na kipande cha mzoga wa mnyama najisi nacho kitakuwa najisi, ama liwe ni jiko au vyungu vya kupikia. Ni najisi na ni lazima kiwe najisi kwenu.
  • Laana katika Sheria: wanawake kumi wakioka mkate katika tanuri mojaLaw 26:26
    Aya
    Law 26:26Nitakapokomesha mgao wa chakula, wanawake kumi wataweza kuoka mkate wako katika chombo kimoja cha kuokea na watakugawia mkate wako kwa uzani. Nanyi mtakula lakini hamtatoshelezwa.
  • Sara anapaswa kukanda vipimo vitatu vya unga laini na kuoka mkateMwa 18:6
    Aya
    Mwa 18:6Kisha Abraham akaenda upesi hemani kwa Sara, na akasema, “Harakisha, chukua vipimo vitatu vya unga safi, uukande, na fanya mkate.”
  • Lutu aliwaokea wageni wake mikate isiyotiwa chachuMwa 19:3
    Aya
    Mwa 19:3Lakini akawasihi sana, mwishowe wakaondoka pamoja nae, na wakaingia katika nyumba yake. Akaandaa chakula na kuoka mkate usiotiwa chachu, wakala.
  • Mwokaji mkuu wa Farao aliota vikapu vitatu vya mkate kichwani pakeMwa 40:16–17
    Aya
    Mwa 40:16–17Mkuu wa waokaji alipoona kwamba tafsiri ilikuwa ya kuvutia, akamwambia Yusufu, “Mimi pia niliota ndoto, na tazama, vikapu vitatu vya mikate vilikuwa juu ya kichwa changu. Katika kikapu cha juu kulikuwa na kila aina za bidhaa ya kuokwa kwa Farao, lakini ndege wakavila ndani ya kikapu juu ya kichwa changu.”
  • Wakiondoka Misri, Israeli walioka mikate isiyotiwa chachu kwa unga uliokandwa walioubebaKut 12:34, Kut 12:39
    Aya
    Kut 12:34Watu wakachukuwa ngano yao pasipo kuongeza hamira yeyote. Bakuli zao zakukandia ngano zilifungiwa kwenye nguo zao na kwenye mabega yao.
    Kut 12:39Walioka mikate na unga wa ngano wenye hamira walio utoa Misri. Ulikuwa hauna hamira kwasababu waliondolewa Misri na hawakuweza chelewa kuandaa chakula.
  • Kabla ya Sabato: “Okeni mnachotaka kuoka”Kut 16:23
    Aya
    Kut 16:23Aliwaambia, “Hili ndilo Yahweh alililo lisema: 'Kesho ni mapumziko ya kujiliwaza, sabato takatifu kwa utukufu wa Yahweh. Oka kile unataka kuoka, na chemsha kile unataka kuchemsha. Vyote vitakavyo baki, jihifadhie hadi asubui.”'
  • Mikate kumi na miwili iliokwa kwa ajili ya meza ya dhahabu mbele za BwanaLaw 24:5–6
    Aya
    Law 24:5–6Yawapasa kuchukua unga laini na kuoka kwa huo mikate kumi na miwili. Ni lazima kuwe na mbili za kumi za efa za unga katika kila mkate. Kisha mtaipanga juu ya meza ya dhahabu safi mbele za Yahweh katika safu mbili, mikate sita katika kila safu,
  • Samweli: mfalme atawachukua binti zenu wawe wapishi na waokaji1 Sam 8:13
    Aya
    1 Sam 8:13Naye atawachukua binti zenu kuwa watengeneza manukato, wapishi, na waoka mikate.
  • Mpiga ramli wa Endori alikanda unga akamwokea Sauli mikate isiyotiwa chachu1 Sam 28:24
    Aya
    1 Sam 28:24Yule mwanamke alikuwa na ndama mnono hapo nyumbani; akafanya haraka na kumchinja; akachua unga, akaukanda, na akatengeneza mikate isiyotiwa chachu kwa unga huo.
  • Tamari alikanda unga akamwokea Amnoni maandazi2 Sam 13:8
    Aya
    2 Sam 13:8Tamari akaenda katika nyumba ya Amnoni nduguye alipokuwa amelala. Akachukua donge na kulifinyanga na kuandaa mkate mbele zake, kisha akauoka.
  • Eliya aliamka akakuta mkate uliookwa juu ya makaa ya moto1 Fal 19:6
    Aya
    1 Fal 19:6Eliya akatazama, karibu na kichwa chake kulikuwa na mkate uliokuwa umeokwa kwa mkaa na gudulia la maji. Kwa hiyo akala na kunywa na kulala tena.
  • Isaya: sehemu ya kuni huoka mkate, na iliyobaki inakuwa sanamuIsa 44:15, Isa 44:19
    Aya
    Isa 44:15Basi mtu hutumia kwa moto na kujipatia joto. Ndio, huwasha moto kuwooka mkate. Halafu hutengeneza miungu ili ausujudie;
    Isa 44:19Hakuna anayefikiria, wala kuelewa na kusema, ''Nimechoma sehemu ya mbao kwenye moto; na pia nimewooka mkate kwa kutumia makaa yake. Nimechoma nyama kwa makaa yake nikala. Sasa Je ninaweza kutengeneza kitu kinachochukiza kwa ajili ya kuabudia kwa sehemu ya mbao iliyobakia? Je ninaweza kusujudia sanamu ya mbao?''
  • Yeremia alipata mkate mmoja kila siku kutoka mtaa wa waokajiYer 37:21
    Aya
    Yer 37:21Kwa hiyo mfalme Sedekia alitoa amri. Wajakazi wake walimwekea mipaka Yeremia katika uwanja wa walinzi. Alipewa mkate kila siku kutoka mtaa wa waokaji mkate, mpaka mkate wote mjini uliisha. Basi Yeremia alibaki kwenye uwanja walinzi.
  • Ukuta wa Yerusalemu ulikuwa na Mnara wa TanuriNeh 3:11, Neh 12:38
    Aya
    Neh 3:11Malkiya mwana wa Harimu na Hashubu mwana wa Pahat Moabu, wajenga sehemu nyingine pamoja na mnara wa tanuu.
    Neh 12:38Na waimbaji wengine ambao walishukuru wakaenda upande mwingine. Niliwafuata juu ya ukuta pamoja na nusu ya watu, juu ya mnara wa vinyago, hadi kuta kubwa,

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0