Bible Explorer

Gundua › Mada › Kuhifadhi maiti na manukato ya kuzikia

Mambo ya kushangaza

Kuhifadhi maiti na manukato ya kuzikia katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (18), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Yusufu aliwaagiza waganga wake kuuhifadhi mwili wa baba yake YakoboMwa 50:2
    Aya
    Mwa 50:2Yusufu akawaagiza watumishi wake matabibu kumtia dawa babaye. Hivyo matabibu wakampaka dawa Israeli.
  • Kuhifadhi kulichukua siku arobaini; Wamisri waliomboleza sabiniMwa 50:3
    Aya
    Mwa 50:3Wakatimiza siku arobain, kwani huo ndio uliokuwa muda kamili wa kutia dawa. Wamisri wakamlilia kwa siku sabini
  • Yusufu alikufa akiwa na miaka 110, akahifadhiwa na kutiwa katika jeneza huko MisriMwa 50:26
    Aya
    Mwa 50:26Hivyo Yusufu akafa, mwenye miaka 110. Wakampaka dawa na akawekwa katika jeneza huko Misri.
  • Musa aliichukua mifupa ya Yusufu kutoka Misri, kama Yusufu alivyoombaKut 13:19
    Aya
    Kut 13:19Musa akachukuwa mifupa ya Yusufu pamoja naye, kwa kuwa Yusufu aliwaapisha Waisraeli na kusema, “Mungu atawaokoa, na muibebe mifupa yangu na nyie.”
  • Mifupa yake ilizikwa Shekemu, katika kipande cha shamba alichonunua YakoboYos 24:32
    Aya
    Yos 24:32Mifupa ya Yusufu ambayo watu wa Israeli waliileta kutoka Misri, waliizika huko shekemu, katika sehemu ya nchi ambayo Yakobo alikuwa ameinunua kutoka kwa wana wa Hamori, baba wa Shekemu. Aliinunua kwa vipande mia moja vya fedha, na ulikuwa urithi kwa wazawa wa Yusufu.

Manukato na sanda

  • Mfalme Asa alilazwa juu ya kitanda kilichojaa manukato na marashi yaliyochanganywa2 Nya 16:14
    Aya
    2 Nya 16:14Walimlaza juu ya kitanda kilichokuwa kimewekewa manukato na aina mbali mbali ya dawa zilizotayarishwa na wale mafundi wa manukato. KIsha wakatengeneza moto kwa heshima yake.
  • Moto mkubwa uliwashwa kwa heshima ya Asa; kwa Yehoramu haukuwashwa2 Nya 16:14, 2 Nya 21:19
    Aya
    2 Nya 16:14Walimlaza juu ya kitanda kilichokuwa kimewekewa manukato na aina mbali mbali ya dawa zilizotayarishwa na wale mafundi wa manukato. KIsha wakatengeneza moto kwa heshima yake.
    2 Nya 21:19Ikawa wakati ulipofika, katika mwisho wa miaka miwili, kwamba utumbo wake ukaaanguka nje kwa sababu ya ugonjwa wake, na kwamba akafa kwa ugonjwa mkali. Watu wake hawakutengeneza moto kwa ajili ya heshima yake kama walivyokuwa wamefanyia babu zake.
  • Martha: “Sasa ananuka. Tayari ni siku nne”Yn 11:39
    Aya
    Yn 11:39Yesu akasema, “Liondoweni jiwe.” Martha, dada yake na Lazaro, yeye aliyekufa, akamwambia Yesu, “Bwana, kwa muda huu, mwili utakuwa umeoza, kwa sababu amekwishakuwa maiti kwa siku nne.”
  • Lazaro alitoka amefungwa vitambaa vya kitani, uso wake umefungwa lesoYn 11:44
    Aya
    Yn 11:44Mfu alitoka nje amefungwa mikono na miguu kwa sanda za kuzikia, na uso wake ulifungwa na kitambaa.” Yesu akawaambia, “Mfungueni mkamwache aende.”
  • Yesu: amenipaka mwili wangu mapema kwa ajili ya mazikoMk 14:8, Yn 12:7
    Aya
    Mk 14:8Amefanya kile anachoweza: ameupaka mwili wangu mafuta kwa ajili ya maziko.
    Yn 12:7Yesu alisema, “Mwache aweke alicho nacho kwa ajili ya siku ya maziko yangu.
  • Nikodemo alileta manemane na udi nyingiYn 19:39
    Aya
    Yn 19:39Naye Nicodemo ambaye hapo awali alimfuata Yesu usiku naye akaja. Yeye alileta mchanganyiko wa manemane na udi, yapata uzito wa ratili mia moja.
  • Mwili wa Yesu ulifungwa kwa kitani pamoja na manukato, kama desturi ya Wayahudi ya kuzikaYn 19:40
    Aya
    Yn 19:40Kwa hiyo wakauchukua mwili wa Yesu wakaufanga kwenye sanda ya kitani na pamoja na yale manukato, kama ilivyokuwa desturi ya wayahudi wakati wa kuzika.
  • Wanawake waliandaa manukato na marashi, kisha wakapumzika siku ya SabatoLk 23:55–56
    Aya
    Lk 23:55–56Wanawake, waliokuja nao kutoka Galilaya, walimfuata, na wakaona kaburi na jinsi mwili wake ulivyolazwa. Walirudi na kuanza kuandaa manukato na marashi. Kisha siku ya sabato walipumzika kwa mujibu wa sheria.
  • Baada ya Sabato walinunua manukato ili kuupaka mwiliMk 16:1
    Aya
    Mk 16:1Wakati sabato ilipokwisha, Mariamu Magdalena na Mariamu mama yake na Yakobo, na Salome, walinunua manukato mazuri, ili waweze kuja na kuupaka mafuta mwili wa Yesu kwa ajili ya maziko.
  • Mapema sana siku ya kwanza walileta manukato kaburiniLk 24:1
    Aya
    Lk 24:1Mapema sana siku ya kwanza ya juma, walikuja kaburini, wakileta manukato ambayo walikuwa wameyaandaa.
  • Petro aliona vitambaa vya kitani, na kitambaa cha kichwa kimezongwa mbaliYn 20:6–7
    Aya
    Yn 20:6–7Kisha Simon Petro naye akafika akaingia ndani ya Kaburi. Akaiona ile sanda ya kitani imelala pale na ile leso iliyokuwa kichwani pake haikuwa imelala pamoja na zile sanda za kitani bali ilikuwa imelala pembeni peke yake.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0