Bible Explorer

Gundua › Mada › Udanganyifu na kujigeuza

Mambo ya kushangaza

Udanganyifu na kujigeuza katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (45), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

Katika Mwanzo

  • Nyoka anamwambia mwanamke: “Hakika hamtakufa”Mwa 3:4
    Aya
    Mwa 3:4Nyoka akamwambia mwanamke, “hakika hamtakufa.
  • Abram anamwomba Sarai aseme kuwa yeye ni dada yakeMwa 12:13
    Aya
    Mwa 12:13Hivyo wewe sema kuwa ni dada yangu, ili kwamba niwe salama kwa sababu yako, na kumba maisha yangu yatasalimika kwa sababu yako.”
  • Huko Gerari Abraham anasema tena kuhusu Sara: “Yeye ni dada yangu”Mwa 20:2
    Aya
    Mwa 20:2Abraham akasema kususu mkewe Sara, “ni dada yangu.” Kwa hiyo Abimeleki mfalme wa Gerari akatuma watu wake kumchukua Sara.
  • Isaka anasema Rebeka ni dada yake, akiogopa watu watamuuaMwa 26:7
    Aya
    Mwa 26:7Watu wa eneo hilo walipomwuliza juu ya mke wake, alisema, “Yeye ni dada yangu.” Aliogopa kusema, “Yeye ni mke wangu,” kwa kuwa alidhani, “Watu wa nchi hii wataniua ili wamchukue Rebeka, kwa kuwa ni mzuri wa uso.”
  • Rebeka anamvika Yakobo mavazi ya Esau na ngozi za mbuziMwa 27:15–16
    Aya
    Mwa 27:15–16Rebeka akachukua nguo nzuri za Esau, mwanawe mkubwa, alizokuwa nazo nyumbani mwake, na akamvika Yakobo, mwanawe mdogo. Akamvalisha ngozi ya mwanambuzi katika mikono yake na katika sehemu laini za shingo yake.
  • Yakobo anamwambia baba yake, asiyeweza kuona: “Mimi ni Esau, mzaliwa wako wa kwanza”Mwa 27:1, Mwa 27:19
    Aya
    Mwa 27:1Isaka alipozeeka na macho yake kuwa mazito kiasi cha kutokuona, alimwita Esau, mwanawe mkubwa, na akamwambia, “Mwanangu. Yeye akasema, “Mimi hapa.”
    Mwa 27:19Yakobo akamwambia baba yake, “Mimi ni Esau mzaliwa wako wa kwanza; nimefanya kama ulivyoniagiza. Basi kaa na ule sehemu ya mawindo yangu, ili unibariki.”
  • Labani anampa Lea badala ya Raheli; Yakobo: “Kwa nini umenidanganya?”Mwa 29:23, Mwa 29:25
    Aya
    Mwa 29:23Wakati wa jioni, Labani akamchukua Lea binti yake mkubwa na kumleta kwa Yakobo, aliyelala naye.
    Mwa 29:25Ilipofika asubuhi, tazama, kumbe ni Lea! Yakobo akamwambia Labani, “Ni nini hiki ulichonifanyia? Je sikukutumikia kwa ajili ya Raheli? Kwa nini basi umenihadaa?
  • Yakobo anaondoka kwa siri kwa Labani bila kumwambiaMwa 31:20
    Aya
    Mwa 31:20Yakobo pia akamdanganya Labani Mwarami, kwa kutomtaarifu kwamba anaondoka.
  • Raheli anaficha sanamu za nyumbani za Labani katika tandiko na kuziketiaMwa 31:34–35
    Aya
    Mwa 31:34–35Basi Raheli alikuwa ameichukua miungu ya nyumbani, na kuiweka katika ngozi ya ngamia, na kukaa juu yake. Labani akatafuta katika hema yote, lakini hakuiona. Akamwambia baba yake, “Usikasirike, bwana wangu, kwamba siwezi kusimama mbele yako, kwani nipo katika kipindi changu.” Hivyo akatafuta lakini hakuiona miungu ya nyumbani mwake.
  • Wana wa Yakobo wanawaomba watu wa Shekemu watahiriwe, kisha wanaushambulia mjiMwa 34:13, Mwa 34:15, Mwa 34:25
    Aya
    Mwa 34:13Wana wa Yakobo wakamjibu Shekemu na Hamori baba yake kwa hila, kwa sababu Shekemu alikuwa amemnajisi Dina dada yao.
    Mwa 34:15Kwa sharti hili peke yake tutakubaliana nanyi: iwapo mtatailiwa kama sisi, ikiwa kila mtu mme miongoni mwenu atatailiwa.
    Mwa 34:25Katika siku ya tatu, walipokuwa katika maumivu bado, wawili wa wana wa Yakobo (Simoni na Lawi, kaka zake Dina), wakachukua kila mmoja upanga wake na kuushambulia mji ambao ulikuwa na uhakika wa ulinzi wake, nao wakauwa wanamme wote.
  • Ndugu wanalichovya joho la Yusufu katika damu ya mbuzi na kumwonyesha YakoboMwa 37:31–33
    Aya
    Mwa 37:31–33Wakachinja mbuzi na kisha wakalichukua vazi la Yusufu na kulichovya katika damu. Kisha wakalipeleka kwa baba yao na kusema, “Tumeiona hii. Tafadhari angalia kwamba ni vazi la mwanao au hapana.” “Yakobo akaitambua na kusema, “Ni nguo ya mwanangu. Mnyama wa mwitu amemrarua. Bila shaka Yusufu ameraruliwa katika vipande.
  • Tamari anajifunika shela, na Yuda anamdhania kuwa kahabaMwa 38:14–15
    Aya
    Mwa 38:14–15Akavua mavazi yake ya ujane na akajifunika kwa ushungi. Akakaa katika lango la Enaimu, lililoko kando ya njia iendayo Timna. Kwa maana aliona kwamba Shela amekua lakini akupewe kuwa mke wake. Yuda alipomwona alidhani ni kahaba kwa maana alikuwa amefunika uso wake.
  • Yusufu anaagiza kikombe chake cha fedha kifichwe katika gunia la BenjaminiMwa 44:1–2
    Aya
    Mwa 44:1–2Yusufu akamwamru msimamizi wa nyumba yake, akisema, “Jaza magunia ya watu hawa kwa chakula, kiasi wawezacho kubeba, na uweke pesa ya kila mtu katika mdomo wa gunia lake. Uweke kikombe changu, cha fedha, katika mdomo wa gunia la mdogo, na pesa yake ya chakula pia.” Msimamizi akafanya kama Yusufu alivyosema.

Waamuzi na wafalme

  • Wagibeoni wanaleta magunia yaliyochakaa na mkate wenye ukungu, wakidai nchi ya mbaliYos 9:4–6
    Aya
    Yos 9:4–6walipanga mpango wa udanganyifu. Walienda kama wajumbe. Walichukua magunia yaliyochakaa na kuyaweka juu ya punda. Walichukua pia viriba vilivyochakaa na kuchanika chanika na vilivyozibwa zibwa. Walivaa miguuni mwao viatu vilivyozeeka na kutoboka toboka, na walivaa nguo kuukuu, zilichanika chanika. Na mikate yote katika chombo ilikuwa mikavu na yenye uvundo. Kisha wakamwendea Yoshua katika kambi huko Giligali na wakamwambia yeye pamoja wa watu wa Israeli wakisema, “
  • Siku tatu baada ya agano Israeli walijua kuwa ni majiraniYos 9:16
    Aya
    Yos 9:16Siku tatu baada ya Waisraeli kufanya agano pamoja nao, waligundua kuwa walikuwa ni majirani zao na ya kwamba waliishi karibu nao.
  • Yaeli anamkaribisha Sisera ndani, anampa maziwa, kisha anamuua akiwa amelalaAmu 4:18–21
    Aya
    Amu 4:18–21Jaeli akatoka kumlaki Sisera, akamwambia, karibu, bwana wangu; karibu kwangu, wala usiogope. Basi akakaribia kwake, akaingia hemani kwake, naye akamvika bushuti. Akamwambia, Tafadhali nipe maji kidogo ninywe, kwa maana nina kiu. Alifungua mfuko wa ngozi ya maziwa akampa anywe, kisha akamfunika tena. Akamwambia, “Simama mlangoni pa hema. Ikiwa mtu atakuja na kukuuliza, 'Je, kuna mtu hapa?', Sema 'Hapana'.” Kisha Jaeli (mke wa Heberi) akachukua kigingi cha hema na nyundo mkononi mwake akamwendea kwa siri, kwa sababu alikuwa amelala usingizi mzito, naye akakitia kigingi cha hema upande wa kichwa chake akamchoma na kikapenya kushuka chini. Hivyo akafa.
  • Mikali analaza sanamu yenye singa za mbuzi kitandani mwa Daudi: “Ni mgonjwa”1 Sam 19:13–16
    Aya
    1 Sam 19:13–16Mikali alichukua kinyago na kukilaza juu ya kitanda. Kisha akaweka mto wa singa za mbuzi kichwani pake, na akakifunika na nguo. Sauli alipowatuma wajumbe kumchukua Daudi, mkewe akasema, “ Daudi ni mgonjwa.” Kisha Sauli akawatuma wajumbe kumtazama; akisema, “Mleteni kwangu akiwa kitandani, ili nimuue.” Wale wajumbe walipoingia ndani, tazama, kile kinyago kilikuwa kitandani pamoja na mto wa singa za mbuzi kichwani.
  • Daudi anamwambia kuhani wa Nobu kuwa yuko katika kazi ya siri ya mfalme1 Sam 21:1–2
    Aya
    1 Sam 21:1–2Kisha Daudi akafika Nobu kumuona Ahimeleki kuhani. Ahimeleki akaja akutane na Daudi huku akitetemeka na kumwambia, “Kwa nini uko peke yako huna mtu wa kuambatana na wewe?” Daudi akamjibu Ahimeleki kuhani, “Mfalme amenituma kwa jambo maalum na ameniambia hivi, 'Asiwepo hata mtu mmoja anayejua chochote kuhusu shughuli niliyokutuma, na kile nilichokuagiza.' Nimewaelekeza vijana kwenda sehemu fulani.
  • Daudi anawavamia Wageshuri lakini anamwambia Akishi alivamia Negevi ya Yuda1 Sam 27:8, 1 Sam 27:10
    Aya
    1 Sam 27:8Daudi na watu wake walizipiga sehemu mbalimbali, wakiteka nyara Wageshuri, Wagirizi, na Waamaleki; kwa maana mataifa hayo ndio walikuwa wakaaji wa nchi, kwa uelekeo wa kwenda Shuri hadi kufika nchi ya Misri. Walikuwa wamekaa katika nchi hiyo toka nyakati za zamani.
    1 Sam 27:10Ndipo Akishi humuuliza, “Je, leo umefanya mashambulizi dhidi ya nani?” Daudi humjibu, “Nimefanya dhidi ya kusini mwa Yuda,” au dhidi ya kusini mwa Wayerameeli,” au “dhidi ya kusini mwa Wakeni.”
  • Amnoni anajifanya mgonjwa ili Tamari aje kwake2 Sam 13:6
    Aya
    2 Sam 13:6Hivyo Amnoni akalala na kujifanya kuwa mgonjwa. Mfalme alipokuja kumwona, Amnoni akamwambia mfalme, “Tafadhari mtume Tamari dada yangu aandaye chakula kwa ajili ya ugonjwa wangu mbele yangu ili kwamba nikile kutoka mkononi mwake.
  • Yoabu anamtuma mwanamke mwenye hekima wa Tekoa ajifanye mwombolezaji2 Sam 14:2–3
    Aya
    2 Sam 14:2–3Hivyo Yoabu akatuma neno huko Tekoa kumleta kwake mwanamke mwelevu. Akamwambia, “Tafadhari, vaa mavazi ya uombolezaji ujifanye kuwa mwombolezaji. Usijipake mafuta, lakini uwe kama mwanamke ambaye ameomboleza kwa muda mrefu kwa ajili yake aliyekufa. Kisha ingia kwa mfalme na umwambiye maneno nitakayokueleza.” Hivyo Yoabu akamwambia maneno ambayo angeyasema kwa mfalme.
  • Absalomu anaomba kwenda Hebroni kwa nadhiri, na kuanzisha uasi huko2 Sam 15:7, 2 Sam 15:10
    Aya
    2 Sam 15:7Ikawa mwishoni mwa miaka minne Absalomu akamwambia mfalme, “Tafadhari niruhusu niende ili nitimize nadhiri niliyoiweka kwa Yahwe huko Hebroni.
    2 Sam 15:10Kisha Absalomu akatuma wapelelezi katika jamaa zote za Israeli, kusema, “Mara msikiapo sauti ya tarumbeta semeni, 'Absalomu anatawala katika Hebroni.”
  • Hushai, rafiki wa Daudi, anamsalimu Absalomu: “Mfalme na aishi!”2 Sam 16:16
    Aya
    2 Sam 16:16Ikawa Hushai Mwarki, rafiki yake Daudi, akaja kwa Absalomu, naye akamwambia Absalomu, “Mfalme aishi daima! mfalme aishi daima.
  • Absalomu anapendelea shauri la Hushai kuliko la Ahithofeli2 Sam 17:14
    Aya
    2 Sam 17:14Kisha Absalomu na watu wa Israeli wakasema, “Shauri la Hushai Mwarki ni jema kuliko lile la Ahithofeli. Yahwe aliwafanya wakatae shauri jema la Ahithofeli ili kumwangamiza Absalomu.
  • Nabii mzee anadanganya ili kumrudisha mtu wa Mungu nyumbani kwake1 Fal 13:18
    Aya
    1 Fal 13:18Kwa hiyo yule nabii mzee akamwambia, “Mimi pia ni nabii kama ulivyo, na malaika amesema na mimi neno la BWANA, akisema, 'Mrudishe aje na wewe katika nyumba yako, ili aweze kula chakula na kunywa maji.'” Lakini alikuwa anamdanganya mtu wa Mungu.
  • Mke wa Yeroboamu anajigeuza; Ahiya, asiyeweza kuona, anamwita kwa jina1 Fal 14:2, 1 Fal 14:4, 1 Fal 14:6
    Aya
    1 Fal 14:2Yeroboamu akamwambia mke wake, “amka ujibadilishe, ili wasikutambue kuwa wewe ndiye mke wangu, na uende Shilo, kwa sababu nabii Ahiya yuko huko, yeye ndiye aliyeninea mimi kuwa nitakuwa mfalme juu ya watu hawa.
    1 Fal 14:4Mke wa Yeroboamu akafanya hivyo; akaenda Shilo mpaka kwenye nyumba ya Ahiya. Wakati huo Ahiya alikuwa hawezi kuona, kwa kuwa macho yake yalikuwa yameishiwa nguvu kwa sababu ya umri wake.
    1 Fal 14:6Naye Ahiya aliposikia sauti za miguu yake alipokuwa akiukaribia mlango, akasema, “karibu, mke wa Yeroboamu. Kwa nini unajifanya kuwa mtu mwingine? Nimetumwa kwako nikiwa na habaari mbaya.
  • Gehazi anabuni ujumbe wa Elisha ili kupata fedha kwa Naamani2 Fal 5:22, 2 Fal 5:25
    Aya
    2 Fal 5:22Gehazi akasema, “kila kitu kiko sawa. Bwana wangu amenituma, akisema, 'Tazama, sasa wamekuja kwangu kutoka nchi ya mlima ya Efraimu vijana wawili wa watoto wa manabii. Tafadhali, wapatie talanta ya fedha na nguo mbili za kubadilisha.”
    2 Fal 5:25Wakati Gehazi alipoingia na kusimama mbele ya bwana wake, Elisha akamwambia, “Umetokea wapi, Gehazi?” Akajibu, “Mtumishi wako hakwenda mahali.”
  • Yehu anatangaza dhabihu kubwa kwa Baali ili kuwakusanya watumishi wake2 Fal 10:19
    Aya
    2 Fal 10:19Basi niitieni manabii wote wa Baali, wote wamwabuduo, na makuhani wake wote. Asikosekane mtu hata mmoja, kwa kuwa nina dhabihu kubwa nataka kutoa kwa Baali. Yeyote atakayeshindwa kuja hataishi.” Lakini Yehu alifanya haya kwa udanganyifu, kwa dhamira ya kuwaua wanaomwabudu Baali.
  • Sanbalati anamwalika Nehemia uwandani wa Ono, akipanga kumdhuruNeh 6:2
    Aya
    Neh 6:2Sanbalati na Geshemu akatuma wajumbe akasema, “Njoni, tukutane pamoja mahali fulani katika tambarare ya Ono.” Lakini walitaka kunidhuru.
  • Mtu aliyeajiriwa anamhimiza Nehemia ajifiche hekaluniNeh 6:10, Neh 6:12
    Aya
    Neh 6:10Nikaenda nyumbani kwa Shemaya mwana wa Delaya, mwana wa Mehetabeli, aliyefungwa nyumbani mwake. Akasema, “Hebu tukutane pamoja katika nyumba ya Mungu, ndani ya hekalu, na tufunge milango ya hekalu, kwa maana wanakuja kukuua. Usiku wanakuja kukuua.”
    Neh 6:12Niligundua kwamba sio Mungu aliyemtuma, lakini alikuwa amefanya unabii dhidi yangu. Tobia na Sanbalati walimwajiri.

Katika Agano Jipya

  • Herode anawaambia Mamajusi kuwa naye anataka kuja kumwabudu MtotoMt 2:8
    Aya
    Mt 2:8Akawatuma Bethelehem, akisema, “Nendeni kwa uangalifu mkamtafute mtoto aliyezaliwa. Wakati mtakapomwona, nileteeni habari ili kwamba mimi pia niweze kuja na kumwabudu.”
  • Wakuu wa makuhani wanatafuta njia ya siri ya kumkamata YesuMk 14:1
    Aya
    Mk 14:1Ilikuwa siku mbili tu baada ya sikukuu ya Pasaka na ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Makuhani wakuu na waandishi walikuwa wakitafuta namna ya kumkamata Yesu kwa hila na kumuua.
  • Askari wanalipwa waseme kuwa wanafunzi waliiba mwiliMt 28:12–13
    Aya
    Mt 28:12–13Nao makuhani walipokuwa wamekutana na wazee na kulijadili jambo hilo pamoja nao, walitoa kiasi kikubwa cha pesa kwa wale askari na kuwaambia, “Waambieni wengine kuwa, 'wanafunzi wa Yesu walikuja usiku wakauiba mwili wa Yesu wakati sisi tulipokuwa tumelala.'
  • Anania na Safira wanazuia sehemu ya bei ya shamba laoMdo 5:1–2, Mdo 5:8
    Aya
    Mdo 5:1–2Hivyo, mtu mmoja aliyeitwa Anania, na Safira mkewe, waliuza sehemu ya mali, na akaficha sehemu ya fedha waliyouza (mke wake pia alilijua hili), na akaleta sehemu iliyobakia na kuiweka kwenye miguu ya mitume.
    Mdo 5:8Petro akamwambia, “Niambie, kama mliuza shamba kwa thamani hiyo.” Akasema, “Ndiyo, kwa thamani hiyo.”

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0