Bible Explorer

Gundua › Mada › Mauaji ya kisiri

Mambo ya kushangaza

Mauaji ya kisiri katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (23), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • “Amelaaniwa ampigaye jirani yake kwa siri”Kum 27:24
    Aya
    Kum 27:24Alaaniwe mwanamume atakayemuua jirani yake kwa siri’. Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina’.
  • Daudi aliwaua wauaji wa Ishboshethi2 Sam 4:9–12
    Aya
    2 Sam 4:9–12Daudi akawajibu Rekabu na Baana nduguye, wana wa Rimoni mbeerothi, akawambia, “Kama Yahwe aishivyo, aliyeuokoa uhai wangu na kila shida, mtu mmoja aliponiambia, 'Tazama, Sauli amekufa,' akifikiri alileta habari njema, nilimkamata na kumwua huko Siklagi. Huo ndio ujira niliompa kwa habari yake. Namna gani, mtu mwovu anapomwua mwenye haki kitandi mwake ndani ya nyumba, Je nisiitake damu yake kutoka katika mikono yenu, na kuwaondoa duniani?” Kisha Daudi akawaagiza vijana, nao wakawaua wakakata mikono na miguu yao na kuwatundika kando ya bwawa huko Hebroni. Lakini wakakichukua kichwa cha Ishboshethi na kukizika katika kaburi la Abneri katika Hebroni.

Mifano

  • Ehudi alimuua Mfalme Egloni wa Moabu kwa upanga uliofichwaAmu 3:15–22
    Aya
    Amu 3:15–22Wana wa Israeli walipomwomba Bwana, Bwana akamwinua mtu aliyewasaidia, Ehudi mwana wa Gera, Mbenjamini, mtu shoto. Wana wa Israeli wakamtuma kwa Egloni, mfalme wa Moabu, kwa malipo yao ya kodi. Ehudi akajifanyia upanga uliokuwa na makali kuwili, urefu wa dhiraa moja; aliufunga chini ya nguo zake juu ya mguu wake wa kulia. Akampa Egloni Mfalme wa Moabu malipo ya kodi. (Egloni alikuwa mtu mnene sana.) Baada ya Ehudi kulipa malipo ya kodi, aliondoka na wale waliokuwa wameibeba. Hata hivyo Ehudi mwenyewe, alipofikia mahali ambapo sanamu za kuchonga zilitengenezwa karibu na Gilgali, akageuka na kurudi, akasema, 'Nina ujumbe wa siri kwako, mfalme wangu.' Eglon akasema, 'Nyamazeni kimya!' Kwa hiyo wote waliomtumikia wakatoka kwenye chumba. Ehudi akaja kwake. Mfalme alikuwa amekaa peke yake, peke yake katika chumba cha juu cha baridi. Ehudi akasema, 'Nina ujumbe kutoka kwa Mungu kwa ajili yeko.' Mfalme akasimama kutoka katika kiti chake. Ehudi akanyoosha mkono wake wa kushoto na akachukua upanga kutoka mguu wake wa kulia, na akautia ndani ya mwili wa mfalme. Na kipini cha upanga kikaingia ndani yake baada ya upanga, nao ukatokea nyuma yake, na mafuta yakashikamana juu ya upanga, kwa kuwa Ehudi hakuutoa upanga nje ya mwili wake.
  • Abimeleki aliwaua ndugu zake juu ya jiwe moja; Yothamu alijifichaAmu 9:5
    Aya
    Amu 9:5Abimeleki akaenda nyumbani kwa baba yake huko Ofra; na juu ya jiwe moja akawaua ndugu zake sabini, wana wa Yerubaali. Yotamu ndiye aliyebaki, mwana mdogo kabisa wa Yerubaali, kwa kuwa alijificha.
  • Yoabu alimchoma Abneri katika lango la Hebroni2 Sam 3:27
    Aya
    2 Sam 3:27Abneri aliporudi Hebroni, Yoabu alimchukua kando kati ya lango ili aongee naye faraghani. Hapohapo Yoabu alimchoka tumboni na kumuua. Hivyo, akalipa kisasi cha damu ya Asaheli nduguye.
  • Rekabu na Baana walimuua Ishboshethi kitandani mwake adhuhuri2 Sam 4:5–7
    Aya
    2 Sam 4:5–7Hivyo wana wa Rimoni mbeerothi, Rekabu na Baana, wakasafiri mchana wakati wa jua kali mpaka nyumbani mwa Ishbothethi, yeye alikuwa amepumzika mchana. Mwanamke aliyekuwa akililinda lango alisinzia wakati akipepeta ngano, Rekabu na Baana waliingia ndani polepole na wakampita. Hivyo walipoingia ndani ya nyumba, walimpiga na kumuua wakati amelala chumbani mwake. Kisha wakakata kichwa chake na wakaondoka nacho, wakasafiri njiani usiku kucha mpaka Araba.
  • Watu wa Absalomu walimuua Amnoni alipofurahi kwa divai2 Sam 13:28–29
    Aya
    2 Sam 13:28–29Absalomu akawaamuru watumishi wake kusema, “Sikilizeni kwa makini. Amnoni atakapokuwa amelewa mvinyo, na nitakapowambia, 'Mpigeni Amnoni,' msiogope mwueni. Je siyo mimi niliyewamru? Mwe jasiri na hodari.” Hivyo watumishi wa Absalome wakamtendea Amnoni kama walivyoamriwa. Kisha wana wote wa mfalme wakainuka na kila mmoja akapanda nyumbu wake akakimbia.
  • Yoabu alimshika Amasa ndevu na kumchoma2 Sam 20:9–10
    Aya
    2 Sam 20:9–10Hivyo Yoabu akamwambia Amasa, “Haujambo binamu yangu?” Kwa utaratibu Yoabu akakishika kidevu cha Amasa kwa mkono wake wa kulia ili ambusu. Amasa hakutambua kwamba kulikuwa na jambia katika mkono wa kushoto wa Yoabu. Yoabu akamchoma Amasa tumboni na matumbo yake yakadondoka chini. Wala Yoabu hakumpiga tena, na Amasa akafa. Hivyo Yoabu na Abishai nduguye wakamfuatia Sheba mwana wa Bikri.
  • Baasha alimuua Mfalme Nadabu huko Gibethoni1 Fal 15:27–28
    Aya
    1 Fal 15:27–28Baasha mwana wa Ahiya, wa familia ya Isakari, akafanya hila dhidi ya Nadabu; Baasha akamwua huko Gibethoni, ambao ulikuwa mji wa Wafilisti, kwa kuwa Nadabu na Israeli walikuwa wakiuhusuru Gibethoni. Katika mwaka wa tatu wa Asa mfalme wa Yuda, Baasha alimwua Nadabu naye akawa mfalme mahali pake.
  • Zimri alimuua Mfalme Ela alipokuwa amelewa1 Fal 16:9–10
    Aya
    1 Fal 16:9–10Mtumishi wake Zimri, mkuu wa nusu ya magari yake akatengeneza hila dhidi yake. Wakati huo Ela alikuwa Tirza, akinywa na kulewa kwenye nyumba ya Arza, ambaye alikuwa mkuu wa watumishi wa nyumbani huko Tirza. Zimri akaiingia ndani, akamshambulia na kumwua, katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, naye akawa mfalme mahali pake.
  • Yehu alimpiga Mfalme Yoramu mshale kati ya mabega2 Fal 9:24
    Aya
    2 Fal 9:24Ndipo Yehu akauvuta upinde wake kwa nguvu zake zote na kumpiga Yoramu kati ya mabega yake; mshale ukaenda kwenye moyo wake, akaanguka chini kwenye gari lake la farasi.
  • Watu wa Yehu walimpiga mshale Mfalme Ahazia wa Yuda garini mwake2 Fal 9:27
    Aya
    2 Fal 9:27Wakati Ahazi yule mfalme wa Yuda alipoliona hili, akakimbia kwa njia ya Bethi Hagani. Lakini Yehu akamfuata, na kusema, “Muulie humo kwenye gari la farasi,” na wakampiga mahali pa kupandia Guri, karibu na Ebleamu. Ahazi akakimbilia Megido na kufia pale.
  • Yoashi aliuawa na watumishi wake huko Beth Milo2 Fal 12:20–21
    Aya
    2 Fal 12:20–21Watumishi wake wakainuka na kupanga pamoja; wakamteka Yoashi katika Bethi Milo, kwenye njia ya kushukia kwa Sila. Yozakari mwana wa Shimeathi, na Yehozabadi mwana wa Shomeri, watumishi wake, wakamshambulia na akafa. Wakamzika Yoashi pamoja na mababu zake katika mji wa Daudi, na Amazia, mtoto wake, akawa mfalme kwenye sehemu yake.
  • Wala njama walimfuata Amazia hadi Lakishi na kumuua2 Fal 14:19
    Aya
    2 Fal 14:19Wakafanya njama dhidi ya Amazia katika Yerusalimu, akakimbilia Lakishi. Akakimbia hadi Lakishi, lakini wakawatuma watu kumfuata hadi Lakishi na kumuua huko.
  • Katika Israeli Shalumu, Menahemu, Peka na Hoshea kila mmoja alimuua mfalme2 Fal 15:10, 2 Fal 15:14, 2 Fal 15:25, 2 Fal 15:30
    Aya
    2 Fal 15:10Shalumu mwana wa Yabeshi akafanya njama dhidi ya Zekaria, akamshambulia katika Ibleamu, na kumuua. Kisha akawa mfalme katika mahala pake.
    2 Fal 15:14Menahemu mwana wa Gadi akapanda kutoka Tirza kwenda Samaria. Akamshambulia Shalumu mwana wa Yabeshi hapo, katika Samria. Akamuua na kuwa mfalme katika mahali pake.
    2 Fal 15:25Pekahia alikuwa na afisa aliyekuwa anaitwa Peka mwana wa Remalia, ambaye alifanya njama dhidi yake. Pamoja na watu hamsini wa Gileadi, Peka akamuua Pekahia pamoja na Argobu na Arie katika Samaria, katika ngome ya nyumba ya mfalme. Peka akamuua alipomua Pekahia akawa mfalme katika mahala pake.
    2 Fal 15:30Hivyo Hoshea mwana wa Ela akafanya njama dhidi ya Peka mwana wa Remalia. Akaishambulia na kisha kumuua. Kisha akawa mfalme katika mahali pake, katika mwaka wa ishirini wa Yothamu mwana wa Uzia.
  • Mfalme Amoni aliuawa ikulu mwake na watumishi wake2 Fal 21:23
    Aya
    2 Fal 21:23Watumishi wa Amoni wakafanya njama dhidi yake na kumuua mfalme kwenye nyumba yake mwenyewe.
  • Senakeribu aliuawa na wanawe alipokuwa akiabudu2 Fal 19:37, Isa 37:38
    Aya
    2 Fal 19:37Baadaye, alipokuwa akiabudu kwenye nyumba ya Nisroki mungu wake, watoto wake Adramaleki na Shareza wakamuua kwa upanga. Kisha wakakimbilia kwenye nchi ya Ararati. Kisha Esarhodani mwanaye akawa mfalme katika mahali pake.
    Isa 37:38Baadaye, na alipokuwa anabudu katika nyumba ya Nisrochi mungu wake, mtoto wake Adramaleki na Shareza alimuua kwa upanga. Halafu wakakimbilia kwenye nchi ya Ararati. Halafu Esarhadoni mtoto wake akatawala katika sehemu ya baba yake.
  • Ishmaeli mwana wa Nethania alimuua Gedalia2 Fal 25:25
    Aya
    2 Fal 25:25Lakini ilitokea kwamba katika mwezi wa saba Ishmaeli mwana wa Nethania mwana wa Elishama, kutoka familia ya kifalme, wakaja na watu kumi na kumshambulia Gedalia. Gedalia akafa, pamoja na watu wa Yuda na Wababeli ambao walikuwa pamoja nae huko Mizpa.
  • Mordekai aligundua njama ya matowashi wawili ya kumuua AhasueroEst 2:21–23
    Aya
    Est 2:21–23katika siku hizo ambazo Modekai alikuwa ameketi getini kwa mfalme, Bighani na Tereshi, wasimamizi wa mfalme walio linda lando, walikasirika na wakatafuta kumuua mfalme Ahusiero. Jambo lilipowekwa wazi kwa Modekai, alimtaarifu Malkia Esta na Esta akamweleza kile achoelezwa na Modekai. Habari hii ilipepelelezwa na kuonekana kuwa kweli na wanaume wawili walinyongwa juu ya mti. Na habari hii ikaandikwa katika kitabu cha taarifa mbele ya mfalme.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0