Mambo ya kushangaza
Hesabu saba katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (49), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
Siku saba
- Mungu alipumzika siku ya saba; siku sita za kazi, kisha SabatoMwa 2:3, Kut 20:11, Kum 5:13–14
Aya
Mwa 2:3Mungu akaibarikia siku ya saba na akaitakasa, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika kutoka kwenye kazi yake yote ambayo aliifanya katika uumbaji.
Kut 20:11Kwa siku sita Yahweh aliumba mbingu na nchi, bahari, na vitu vyote vilivyomo, na siku ya saba alipumzika. Kwa hiyo Yahweh aliibariki siku ya Sabato na kuitenga.
Kum 5:13–14Kwa siku sita utafanya kazi na fanya kazi zako zote, lakini siku ya saba ni Sabato kwa Yahwe Mungu wako. Kwa siku hiyo hautafanya kazi yoyote- si wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mjakazi wako wa kiume, wala maksai wako, wala punda wako, wala mifugo wako, wala mgeni yeyote aliye katika malango yako. Hii ni kwamba mjakazi wako wa kiume na mjakazi wako wa kike wapate kumpuzika pamoja na wewe.
- Gharika ilikuja siku saba baada ya Nuhu kuingia safinaniMwa 7:4, Mwa 7:10
- Nuhu alisubiri siku saba kati ya kumtuma njiwaMwa 8:10, Mwa 8:12
- Yusufu alimwombolezea baba yake siku sabaMwa 50:10
Aya
Mwa 50:10Hata walipokuja katika sakafu ya kupuria ya Atadi upande mwingine wa Yordani, wakaomboleza kwa majonzi ya huzuni kubwa. Yusufu akafanya maombolezo ya siku saba kwa ajili ya babaye pale.
- Marafiki wa Ayubu walikaa naye siku saba kimyaAyu 2:13
Aya
Ayu 2:13Kisha wakaketi chini pamoja naye kwa muda wa siku saba-mchana na usiku. Hakuna hata mmoja aliyesema naye neno, kwa kuwa waliona kuwa huzuni yake ilikuwa kuu mno.
- Siku saba za mikate isiyotiwa chachu wakati wa PasakaKut 12:15
Aya
Kut 12:15Utakula mkate bila hamira wakati wa siku saba. Siku ya kwanza utaondoa hamira kwenye nyumba zenu. Yeyote atakaye kula mkate uliyotiwa chachu kwanzia siku ya kwanza mpaka siku ya saba, huyo mtu lazima akatwe kutoka Israeli.
- Siku saba vibandani katika Sikukuu ya VibandaLaw 23:34, Law 23:42
Aya
Law 23:34“Zungumza na watu ISraeli, uwaambie 'Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba kutakuwa na Sikukuu ya vibanda kwa Yahweh. nayo itadumu siku saba.
Law 23:42Mtaishi kwenye vibanda vidogovidogo kwa siku saba. Waisraeli wenyeji wa kuzaliwa wote itawapasa kuishi katika vibanda vidogovidogo kwa siku saba,
- Kuwekwa wakfu kwa makuhani kulichukua siku sabaKut 29:35
Aya
Kut 29:35Ni hivyo utakavyowatendea Aruni na wanawe kama nilivyo kuagiza. Utawaweka kwa kazi takatifu siku saba.
- Sauli alimsubiri Samweli siku saba huko Gilgali1 Sam 13:8
Aya
1 Sam 13:8Alisubiri kwa siku saba, muda uliopangwa na Samweli. Lakini Samweli hakufika huko Gilgali, na watu wakatawanyika mbali na Sauli.
- Watu wa Yabeshi waliomba siku saba kabla ya kujisalimisha1 Sam 11:3
Aya
1 Sam 11:3Basi wazee wa Yabeshi wakamjibu, “Tuache kwa siku saba, ili tuwatume wajumbe katika nchi yote ya Israeli. Ndiposa, kama hakuna mtu wa kutuokoa, tutasalimu amri kwako.”
- Watu wa Yabeshi walifunga siku saba baada ya kumzika Sauli1 Sam 31:13
Aya
1 Sam 31:13Kisha wakachukua mifupa yao na kuizika chini ya mti wa mkwaju huko Yabeshi, na wakafunga siku saba.
- Karamu ya harusi ya Samsoni na kitendawili chake vilichukua siku sabaAmu 14:12, Amu 14:17
Aya
Amu 14:12Samsoni akawaambia, Hebu nawaambieni kitendawili. Ikiwa mmoja wenu anaweza kuipata na kuniambia jibu wakati wa siku saba za sikukuu, nitatoa nguo za kitani thelathini na seti ya nguo thelathini.
Amu 14:17Alilia kwa siku saba ambazosikukuu yao iliendelea. Siku ya saba alimwambia jibu kwa sababu alimlazimisha sana. Akawaambia jibu jamaa zake.
- Ahasuero alifanya karamu ya siku saba katika bustani ya ikuluEst 1:5
Aya
Est 1:5Siku hizi zilipotimia, Mfalme aliaandaa karamu iliyodumu kwa siku saba. Karamu hii ilikuwa kwa watu wote walioishi katika ikulu ya Shushani, tangu mkubwa hadi mdogo. Behewa la bustani ya ikulu ya mfalme ndiyo karamu ilipofanyikia.
- Paulo alikaa siku saba huko TiroMdo 21:4
Aya
Mdo 21:4Baada ya kuwaona wanafunzi, tukakaa huko siku saba. Wanafunzi hawa wakamwambia Paulo kupitia kwa Roho kwamba yeye asikanyage Yerusalemu.
Miaka saba
- Yakobo alitumika miaka saba kwa ajili ya Raheli, kisha saba zaidiMwa 29:20, Mwa 29:27
- Miaka saba ya shibe, kisha saba ya njaa huko MisriMwa 41:53–54
Aya
Mwa 41:53–54Miaka saba ya shibe iliyokuwa katika nchi ya Misri ikafika mwisho. Miaka saba ya njaa ikaanza, kama alivyokuwa amesema Yusufu. Kulikuwa na njaa katika nchi zote, lakini katika nchi yote ya Misri kulikuwa na chakula.
- Njaa ya miaka saba katika siku za Elisha2 Fal 8:1–2
Aya
2 Fal 8:1–2Basi, Elisha alikuwa amemwambia yule mwanamke ambaye alimfufulia mtoto wake. Akamwambia, “Inuka na uenede pamoja na nyumba yako, na uishi popote uwezapo katika nchi nyingine, kwa sababu Yahwe ameiita njaa ambayo itakuja katika hii nchi kwa miaka saba.” Basi yule mwanamke akainuka na akatii lile neno la mtumishi wa Mungu. Akaenda na nyumba yake na kuishi kwenye nchi ya Wafilisti miaka saba.
- Sulemani alijenga hekalu kwa miaka saba1 Fal 6:38
Aya
1 Fal 6:38Mwaka wa kumi na moja mwezi wa Buli, ambao ndio mwezi wa nane, sehemu zote za hekalu zilimalizika na sharti zake zote. Sulemani alilijenga hekalu kwa miaka saba.
- Mara saba miaka saba hadi YubileLaw 25:8
Aya
Law 25:8Ni lazima kwenu kuhesabu Sabato saba za miaka, yaani, saba mara miaka saba, ikifanya jumla ya miaka arobaini na tisa.
Mara saba na saba saba
- Lameki: Kaini alipizwa kisasi mara saba, Lameki mara sabini na sabaMwa 4:24
Aya
Mwa 4:24Ikiwa Kaini atalipiwa kisasi mara saba, ndipo Lameki atalipiwa kisasi mara sabini na saba.”
- Jozi saba za kila mnyama safi ndani ya safinaMwa 7:2
Aya
Mwa 7:2Kwa kila mnyama aliye safi utakuja nao saba wa kiume na saba wa kike. Na kwa wanyama wasio safi, lete wawili wawili, wakiume na wakike.
- Abraham alimpa Abimeleki wana-kondoo saba wa kikeMwa 21:28–30
Aya
Mwa 21:28–30Kisha Abraham akatenga wanakondoo wa kike saba pekeyao. Abimeleki akamwambia Abraham, “Nini maana ya hawa wanakondoo wa kike saba ambao umewatenga pekeyao?” Akajibu, “Hawa wanakondoo wa kike saba utawapokea kutoka mkonono mwangu, ili kwamba uwe ushahidi kwangu, kuwa nichimba kisima hiki.”
- Yakobo aliinama hadi chini mara saba mbele ya EsauMwa 33:3
Aya
Mwa 33:3Yeye mwenyewe akatangulia mbele yao. Akasujudu mara saba kuelekea ardhi, hata alipomkaribia ndugu yake.
- Ndoto ya Farao: ng’ombe saba na masuke sabaMwa 41:2–7
Aya
Mwa 41:2–7Tazama, alikuwa amesimama kando ya Nile. Tazama, ng'ombe saba wakatoka katika mto Nile, wakupendeza na wanene, na wakajilisha katika nyasi. Tazama, ng'ombe wengine saba wakatoka katika Nile baada yao, wasiopendeza na wamekondeana. Wakasimama ukingoni mwa mto kando ya wale ng'ombe wengine. Kisha wale ng'ombe wasiopendeza na waliokonda wakawala wale waliokuwa wanapendeza na walionenepa. Kisha Farao akaamka. Kisha akalala na kuota mara ya pili. Tazama, masuke saba ya nafaka yalichipua katika mche mmoja, mema na mazuri. Tazama, masuke saba, membamba na yaliyokaushwa na upepo wa mashariki, yakachipua baada yake. Masuke membamba yakayameza yale masuke saba mema yote. Farao akaamka, na, tazama, ilikuwa ni ndoto tu.
- Kuhani alinyunyiza damu na mafuta mara sabaLaw 4:6, Law 14:16
- Balaamu aliomba madhabahu saba, mafahali saba, kondoo dume sabaHesabu 23:1
Aya
Hesabu 23:1Balaamu akamwabia Balaki, “Jenga madhabahu saba kwa ajili yangu na uandae mafahari saba na kondoo dume saba.”
- Makuhani saba, pembe saba, mara saba kuzunguka YerikoYos 6:4, Yos 6:15–16
Aya
Yos 6:4Makuhani saba lazima wabebe tarumbeta za pembe za kondoo waume mbele za sanduku. Na katika siku ya saba, ni lazima mtembee kwa kuuzunguka mji mara saba, na makuhani lazima wapulize tarumbeta.
Yos 6:15–16Ilikuwa ni katika siku ya saba ambayo waliamka mapema katika mapambazuko, na walitembea kuuzunguka mji kwa namna ile kama ilivyokuwa kawaida yao, katika siku hii walifanya mara saba. Ilikuwa ni katika siku ya saba ambapo makuhani walipiga tarumbeta, na ya kwamba Yoshua aliwaagiza watu, “Pigeni kelele! Kwa kuwa Yahweh amewapa ninyi mji.
- Mashungi saba ya SamsoniAmu 16:13, Amu 16:19
Aya
Amu 16:13Delila akamwambia Samsoni, “Mpaka sasa umenidanganya na kuniambia uongo. Niambie kwa namna gani unaweza kufungwa.” Samsoni akamwambia, 'Ikiwa utavifuma vifungo saba vya nywele zangu na kuvifunga kwenye kitambaa, kisha kufunga kwenye msumari, nitakuwa kama mtu mwingine yeyote.”
Amu 16:19Alimfanya alale katika magoti yake. Alimwita mtu avinyoe vifungo saba vya kichwa chake, naye akaanza kumshinda, kwa maana nguvu zake zilikuwa zimemwacha.
- Mtumishi wa Eliya alitazama upande wa bahari mara saba1 Fal 18:43–44
Aya
1 Fal 18:43–44Akamwambia mtumishi wake, “Nenda sasa, utazame upande wa bahari.” mtumishi wake akaenda na akasema, “Hakuna kitu,” Eliya akamwambia, “Nenda tena, mpaka mara saba.” Ile mara ya saba mtumishi wake akasema, “Tazama, kuna wingu linapanda kutoka baharini, ni dogo kama mkono wa mtu.” Eliya akamjibu, Nenda ukamwambie Ahabu, 'Andaa gari lako na ushuke kabla mvua haijakuzuia.'”
- Mwana wa Mshunami alipiga chafya mara saba2 Fal 4:35
Aya
2 Fal 4:35Baada ya hapo Elisha aliinuka na kuanza kutembea kuzunguka kile chumba na kurudi tena juu na kujinyoosha mwenyewe kwa yule kijana. Yule kijana alipiga chafya mara saba na kisha akafungua macho yake!
- Naamani alijichovya Yordani mara saba2 Fal 5:10, 2 Fal 5:14
Aya
2 Fal 5:10Elisha akamtumia mjumbe, akisema, “Nenda na ukazame mwenyewe katika Yordani mara saba, na ngozi ya mwili wako itajirudi; utakuwa msafi.”
2 Fal 5:14Ndipo akashuka chini na kuzama mwenyewe mara saba kwenye Yordani, akitii maelekezo ya mtu wa Mungu. Nyama ya mwili wake ikarudi tena kama nyama ya mwili ya mtoto mdogo, na alikuwa amepona.
- Nebukadneza aliitia tanuru moto mara saba zaidiDan 3:19
Aya
Dan 3:19Ndipo Nebukadneza alijawa na ghadhabu; mwonekano wa uso wake ulibadilika kinyume na Shadraka, Meshaki na Abedinego. Aliagiza kuwa tanuru lichochewe ukali mara saba zaidi kuliko lilivyokuwa kawaida.
- Matowashi saba na wakuu saba katika ikulu ya AhasueroEst 1:10, Est 1:14
Aya
Est 1:10katika siku ya saba moyo wa mfalme ulipokuwa na furaha kwa sababu ya mvinyo, aliwaagiza Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari na Karkas (hawa saba ndio waliohudumu mbele ya mfalme)
Est 1:14Carshena, Shethar, Admatha, Tarshish, Meres, Marsena, na Memucan, majimbo saba ya Uajemi na Umedi walikuwa karibu na mfalme na walikuwa na vyeo vikubwa katika ufalme.
- Samehe si mara saba tu, bali zaidi sanaMt 18:21–22
Aya
Mt 18:21–22Tena Petro akaja na kumwambia Yesu, “Bwana, ni mara ngapi ndugu yangu akinikosea nami nimsamehe? Hata mara saba?” Yesu akamwambia, “Sikuambii mara saba, lakini hata sabini mara saba.
- Mikate saba, na vikapu saba vilivyojaa vilibakiMt 15:34–37
Aya
Mt 15:34–37Yesu akawaambia, “Mna mikate mingapi?” Wakasema, “Saba, na samaki wadogo wachache.” Yesu akawaamuru umati uketi chini. Aliitwaa ile mikate saba na samaki, na baada ya kushukuru, akaimega na kuwapa wanafunzi. Wanafunzi wakawapa umati. Watu wote wakala na kutosheka. Na wakakusanya mabaki ya vipande vya chakula vilivyosalia vipande vipande, vilijaa vikapu saba.
- Wanaume saba walichaguliwa kuwahudumia waamini wa YerusalemuMdo 6:3
Aya
Mdo 6:3Kwa hiyo, ndugu, chagueni, wanaume saba, kutoka miongoni mwenu, watu wema, waliojaa Roho na hekima, ambao tunaweza kuwakabidhi huduma hii.
- Wana saba wa SkewaMdo 19:14
Aya
Mdo 19:14Waliofanya haya walikuwa wana saba wa kuhani Mkuu wa Kiyahudi, Skewa.
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0