Bible Explorer

Gundua › Mada › Minara na minara ya ulinzi

Mambo ya kushangaza

Minara na minara ya ulinzi katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (30), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Huko Babeli: mji wenye mnara unaofika mbinguniMwa 11:4
    Aya
    Mwa 11:4Wakasema, “njoni, na tujenge mji sisi wenyewe na mnara ambao kilele chake kitafika angani, na tujifanyie jina. Kama hatutafanya, basi tutatawanyika katika uso wa nchi yote.”
  • Bwana alishuka kuuona mji na mnaraMwa 11:5
    Aya
    Mwa 11:5Kwa hiyo Yahwe akashuka kuona mji na mnara ambao wazao wa Ibrahimu walikuwa wamejenga.
  • Waliacha kuujenga mji, nao ukaitwa BabeliMwa 11:8–9
    Aya
    Mwa 11:8–9Kwa hiyo Yahwe akawatawanya kutoka pale kwenda pande zote za uso wa nchi na wakaacha kujenga mji. Kwa hiyo, jina lake ukaitwa Babeli, kwa sababu hapo Yahwe alivuruga lugha ya nchi yote na tangu pale Yahwe akawatawanya ng'ambo juu ya uso wa nchi yote.
  • Yakobo alipiga hema lake ng’ambo ya mnara wa EderiMwa 35:21
    Aya
    Mwa 35:21Israeli akaendelea na safari na akaweka hema yake kuvuka mnara wa walinzi wa kondoo.

Minara vitani

  • Gideoni aliutishia mnara wa Penueli, kisha akaubomoaAmu 8:9, Amu 8:17
    Aya
    Amu 8:9Akawaambia pia watu wa Penieli, akasema, “Nitakapokuja kwa amani, nitauangusha mnara huu.”
    Amu 8:17Akaangusha mnara wa Penieli na kuwaua watu wa mji huo.
  • Watu wapatao elfu moja walikufa Abimeleki alipouchoma mnara wa ShekemuAmu 9:46, Amu 9:49
    Aya
    Amu 9:46Wakati wakuu wote wa mnara wa Shekemu waliposikia hayo, waliingia katika ngome ya nyumba ya El Berithi.
    Amu 9:49Basi kila mmoja akakata matawi, wakamfuata Abimeleki. Wakayafungia juu ya ukuta wa mnara, nao wakawasha moto, hata watu wote wa mnara wa Shekemu wakafa, wanaume na wanawake elfu.
  • Huko Thebesi watu walijifungia ndani ya mnara imaraAmu 9:50–52
    Aya
    Amu 9:50–52Abimeleki akaenda Tebezi, naye akapiga kambi dhidi ya Thebezi, akautwaa. Lakini kulikuwa na mnara wenye nguvu katika mji, wanaume na wanawake wote na viongozi wote wa mji walikimbilia na kujifungia wenyewe. Kisha wakaenda juu ya paa la mnara. Abimeleki alikwenda kwenye mnara na kupigana nao, naye akaenda karibu na mlango wa mnara ili kuuchoma.
  • Kutoka juu ya paa lake mwanamke alimdondoshea Abimeleki jiwe la kusagiaAmu 9:53
    Aya
    Amu 9:53Lakini mwanamke akatupa jiwe la juu, juu ya kichwa cha Abimeleki likavunja fuvu lake.
  • Mlinzi juu ya mnara huko Yezreeli aliona askari wa Yehu wakija2 Fal 9:17
    Aya
    2 Fal 9:17Mlinzi alikuwa amesimama juu ya mnara katika Yezreeli, akaliona lile kundi la Yehu alipokuwa akija kwa mbali kidogo; akasema, “Naona kundi la watu wanakuja.” Yoramu akasema, “Chukua mwendesha farasi, na umtume akakutane nao; mwambie aseme, “Je mnakuja kwa amani?””
  • “Tangu mnara wa walinzi hadi mji wenye ngome”2 Fal 17:9, 2 Fal 18:8
    Aya
    2 Fal 17:9Wana wa Israeli wakafanya kwa siri mambo mabaya dhidi ya Yahwe Mungu wao. Wakajijengea mahala pa juu katika miji yao yote, kutoka mnara wa walinzi hadi mji wenye boma.
    2 Fal 18:8Akawashambulia Wafilisti hadi Gaza na mipaka inayoizunguka, kutoka mnara wa walinzi hadi hadi mji wenye ngome.

Wafalme waliojenga minara

  • Asa: miji yenye kuta na minara, milango na makomeo2 Nya 14:7
    Aya
    2 Nya 14:7Kwa maana Asa aliwaambia Yuda, “Tuijenge miji hii na kuizungushia kuta, na minara, mageti, na makomeo; nchi bado yetu kwa sababu tumemtafuta Yahwe Mungu wetu. Tumemtafuta yeye, na ametupa amani katika kila upande.” Kwa hiyo walijenga na wakafanikiwa.
  • Uzia alijenga minara kwenye malango ya Yerusalemu na jangwani2 Nya 26:9–10
    Aya
    2 Nya 26:9–10Zaidi ya hayo, Uzia akajenga minara katika Yerusalemu katika kona ya Lango, kwenye Lango la Bonde, na pa kwenye kona ya ukuta, na akavizungushia ngome. Akajenga minara ya ulinzi katika nyika na akachimba mabwawa, kwa maana alikuwa na ng'ombe wengi, katika visiwa vya chini na katika nchi tambarare. Alikuwa na wakulima na wapandaji wa zabibu katika mwinuko wa nchi na katika mashamba yenye rutuba, kwa maana alipenda kulima.
  • Mitambo ya Uzia ilirusha mishale na mawe kutoka minarani2 Nya 26:15
    Aya
    2 Nya 26:15Katka Yerusalemu alijenga mitambo, iliyobuniwa na watu wenye ujuzi, ili iwe juu ya minara na juu ya buruji, kwa ajili ya kurushia mishale na mawe makaubwa. Umaarufu wake ukaenea hadi nchi za mbali, kwa maana alisaidiwa sana hadi alipokuwa na ngavu sana.
  • Yothamu alijenga ngome na minara misituni2 Nya 27:4
    Aya
    2 Nya 27:4Vilevile alijenga miji katika kilima cha Yuda, na katika mistu alijenga ngome na minara.
  • Hezekia alijenga upya ukuta uliobomoka na kuinua minara juu yake2 Nya 32:5
    Aya
    2 Nya 32:5Hezekia akijipa ujasiri na kuujeenga ukuta wote uliokuwa umeangushwa chini. Akaijenga minara mirefu, na pia ukuta mwingine nje. Pia akaiimarisha Milo katika mji wa Dudi, na akafanya kiasi kikubwa cha silaha na ngao.

Minara ya Yerusalemu

  • Mnara wa Mia na Mnara wa HananeliNeh 3:1, Neh 12:39
    Aya
    Neh 3:1Kisha Eliashibu, kuhani mkuu, akasimama pamoja na ndugu zake makuhani, wakajenga lango la kondoo. Walitakasa na kuweka milango yake. Waliweka wakfu hadi mnara wa Hamea na hadi mnara wa Hananeli.
    Neh 12:39na juu ya lango la Efraimu, na mlango wa kale, na kwa lango la samaki na mnara wa Hananeli na mnara wa Hamea, kwa lango la Kondoo, na wakasimama kwenye mlango wa walinzi.
  • Mnara wa TanuriNeh 3:11, Neh 12:38
    Aya
    Neh 3:11Malkiya mwana wa Harimu na Hashubu mwana wa Pahat Moabu, wajenga sehemu nyingine pamoja na mnara wa tanuu.
    Neh 12:38Na waimbaji wengine ambao walishukuru wakaenda upande mwingine. Niliwafuata juu ya ukuta pamoja na nusu ya watu, juu ya mnara wa vinyago, hadi kuta kubwa,
  • Mnara mkubwa uliojitokeza, karibu na ukuta wa OfeliNeh 3:25–27
    Aya
    Neh 3:25–27Palali, mwana wa Uzai, akajenga juu ya kona ya ukuta na mnara unaoenea juu kutoka nyumba ya juu ya mfalme katika uwanda wa walinzi. Baada yake Pedaya mwana wa Paroshi akajenga. Sasa watumishi wa hekalu waliokaa Ofeli walijenga mpaka upande wa Hifadhi ya Maji upande wa mashariki wa mnara unaojitokeza. Baada yake, Watekoi walijenga sehemu nyingine, kuelekea mnara mkubwa ulio nje, mpaka ukuta wa Ofeli.
  • Watu kumi na wanane waliuawa mnara wa Siloamu ulipoangukaLk 13:4
    Aya
    Lk 13:4Au wale watu kumi na nane katika Siloamu ambao mnara ulianguka na kuwaua, mnafikiri wao walikuwa wenye dhambi zaidi kuliko watu wengine katika Yerusalemu?

Mashamba ya mizabibu na misemo

  • Mwenye shamba la mizabibu anajenga mnara wa ulinzi na kuchimba shinikizoIsa 5:2, Mt 21:33
    Aya
    Isa 5:2Analilima, anaondoa mawe, na anaotesha aina ya mizabibu iliyo bora. Na hujenga mnara katikati ya shamba akichimba shinkizo ndani yake. Anasubiria mzabibu uzae matunda lakini unazaa zabibu mwitu.
    Mt 21:33Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu, mtu mwenye eneo kubwa la ardh. Alipanda mizabibu, akaiwekea uzio, akatengeneza na chombo cha kukamlia divai, akajenga na mnara wa walinzi, na akalikodisha kwa watunza zabibu. Kisha akaenda katika nchi nyingine.
  • Yesu: hesabu gharama kabla ya kujenga mnaraLk 14:28–30
    Aya
    Lk 14:28–30Maana ni nani kati yenu, ambaye anatamani kujenga mnara hataketi kwanza akadirie gharama kwa mahesabu kama ana kile anachohitaji ili kukamilisha hilo? Vinginevyo, baada ya kuweka msingi na kushindwa kumaliza, wote walioona wataanza kumdhihaki, wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.'
  • Mlinzi: siku baada ya siku nasimama juu ya mnara wa ulinziIsa 21:8
    Aya
    Isa 21:8Mlinzi analia nje, ''Bwana, ninasimama juu ya mnara siku zote, kila siku, na kwa nguzo yangu nitasimama usiku wote.''
  • Wimbo Ulio Bora: shingo yako ni kama mnara wa DaudiWim 4:4, Wim 7:4
    Aya
    Wim 4:4Shingo yako ni kama mnara wa Daudi ukiwa umejengwa kwa mistari ya mawe, na ngao elfu moja ikining'nia juu yake, ngao zote za wanajeshi.
    Wim 7:4Shingo yako ni kama mnara wa pembe; macho yako ni kama maziwa ya Heshiboni kwenye lango la Bathi Rabimu. Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni ambao watazama Damasko.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0