Bible Explorer

Gundua › Mada › Theluji

Mambo ya kushangaza

Theluji katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (17), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Siku ya theluji Benaya alimuua simba shimoni2 Sam 23:20
    Aya
    2 Sam 23:20Benaya kutoka Kabseeli mwana wa Yehoyada; alikuwa mtu hodari aliyefanya matendo makuu. Aliwauwa wana wawili wa Arieli wa Moabu. Pia alishuka shimoni na kuuwa simba wakati wa theruji.
  • Je, theluji ya Lebanoni huwahi kuondoka miteremkoni mwake?Yer 18:14
    Aya
    Yer 18:14Je, theluji ya Lebanoni imetoka milima yenye miamba juu ya pande zake? Je, mito ya mlima inayotoka mbali iliharibiwa, mito hiyo ya baridi?
  • Vijito vilivyotiwa giza na barafu na theluji inayoyeyukaAyu 6:16
    Aya
    Ayu 6:16ambayo imekuwa mieusi kwa sababu ya barafu juu yake, na kwa sababu ya theluji ambayo hujificha yenyewe ndani yake.
  • Mungu anaiambia theluji, “Anguka juu ya nchi”Ayu 37:6
    Aya
    Ayu 37:6Kwa kuwa huiambia theluji, 'Angukeni juu ya dunia'; hali kadhalika kwa manyunyu ya mvua, 'Iweni manyunyu makubwa ya mvua.'
  • Je, umeingia katika ghala za theluji?Ayu 38:22
    Aya
    Ayu 38:22Je ulishaingia katika ghala ya barafu, au umeshaiona ghala ya mawe ya mvua,
  • Hutandaza theluji kama sufuZab 147:16
    Aya
    Zab 147:16Huifanya theluji kama sufu, huitawanya barafu kama majivu.
  • Mvua na theluji huinywesha nchi na kuifanya ichipueIsa 55:10
    Aya
    Isa 55:10Maana kama mvua na theluji zishukavyo chini kutoka mbinguni na hazirudi tena pale isipokuwa kueneza nchi na kufanya uzalishaji na chipukizi na kutoa mbegu kwa wakulima waliopanda na mkate kwa walaji,
  • Kama theluji ikianguka juu ya SalmoniZab 68:14
    Aya
    Zab 68:14Mwenyezi Mungu aliwatawanya Wafalme huko, ilikuwa kama vile wakati wa theluji juu ya Mlima Salmoni.

Katika Mithali

  • Mjumbe mwaminifu ni kama ubaridi wa theluji wakati wa mavunoMit 25:13
    Aya
    Mit 25:13Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwa wenye kumtuma; huyahifadhi maisha ya mabwana wake.
  • Kama theluji wakati wa kiangazi, heshima haimfai mpumbavuMit 26:1
    Aya
    Mit 26:1Kama theluji wakati wa joto au mvua kwenye mavuno, ndivyo mpumbavu asivyostahili heshima.
  • Theluji ikianguka, haogopi; nyumba yake yote imevaa nguo nyekunduMit 31:21
    Aya
    Mit 31:21Haogopi theluji kwa ajili ya kaya yake, kwa maana nyumba yake yote imevika kwa nguo nyekundu.

Mweupe kama theluji

  • Mkono wa Musa, Miriamu na Gehazi: wenye ukoma, weupe kama thelujiKut 4:6, Hesabu 12:10, 2 Fal 5:27
    Aya
    Kut 4:6Yahwe pia alimwambia, “Sasaingiza mkono wako ndani ya vazi lako.” Hivyo Musa akaingiza mkono wake ndani ya vazi lake. Na alipoutoa nje, tazama, mkono wake ulikuwa na ukoma, mweupe kama theluji.
    Hesabu 12:10Lile wingu likainuka juu ya hema, Miriamu akapata ukoma ghafla - akawa mweupe kama theluji. Naye Haruni alipogeuka kumwona Miriamu, akamwona amepata ukoma.
    2 Fal 5:27Basi ukoma wa Naamani utakuwa kwenye uzao wako daima.” Basi Gehazi akatoka kwenye uwepo wake, mwenye ukoma kama theluji.
  • Ayubu: hata kama ningejiosha kwa thelujiAyu 9:30
    Aya
    Ayu 9:30Kama najiosha mwenyewe kwa maji ya theluji na kuitakasa mikono yangu na kuwa safi zaidi,
  • Ombi la Daudi: unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko thelujiZab 51:7
    Aya
    Zab 51:7Unisafishe kwa hisopo, nami nitakuwa safi; unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.
  • Malaika kaburini: mavazi meupe kama thelujiMt 28:3
    Aya
    Mt 28:3Sura yake ilikuwa kama ya umeme, na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0