Bible Explorer

Gundua › Mada › Vitendawili

Mambo ya kushangaza

Vitendawili katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (15), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

Kitendawili cha Samsoni

  • Samsoni aliwakuta nyuki na asali ndani ya simba aliyemuuaAmu 14:5–9
    Aya
    Amu 14:5–9Basi Samsoni akaenda Timna pamoja na baba yake na mama yake; nao wakafika kwenye mashamba ya mizabibu ya Timna. Na, tazama, kuna simba mdogo wa alikuja na alikuwa akiunguruma. Roho wa Bwana ghafla akaja juu yake, naye akamrarua simba kwa urahisi kama ambavyo angeweza kumrarua mbuzi mdogo, naye hakuwa na kitu mkononi mwake. Lakini hakuwaambia baba au mama yake kile alichofanya. Alikwenda na kuzungumza na mwanamke, na alipopomtazama, alimpendeza Samsoni. Siku chache baadaye aliporudi kumwoa, akageuka na kutafuta mzoga wa simba. Na, tazama, kulikuwa na kundi la nyuki na asali katika kile kilichobaki katika mwili wa simba. Akaweka asali mikononi mwake na akaenda, akala huku akienda. Alipokuja kwa baba yake na mama yake, akawapa, nao wakala. Lakini hakuwaambia kuwa amechukua asali nje ya kile kilichobaki kwenye mwili wa simba.
  • Dau: mavazi thelathini ya kitani na seti thelathini za nguoAmu 14:12–13
    Aya
    Amu 14:12–13Samsoni akawaambia, Hebu nawaambieni kitendawili. Ikiwa mmoja wenu anaweza kuipata na kuniambia jibu wakati wa siku saba za sikukuu, nitatoa nguo za kitani thelathini na seti ya nguo thelathini. Lakini ikiwa hamuwezi kuniambia jibu, basi utanipa nguo za kitani thelathini na seti za nguo thelathini. ' Wakamwambia, Utuambie kitendawili chako, ili tukisikie.
  • “Katika mlaji kilitoka chakula”Amu 14:14
    Aya
    Amu 14:14Akawaambia, 'Kati ya mtu aliyekula alikuwa kitu cha kula; nje ya nguvu ilikuwa kitu tamu. Lakini wageni wake hawakuweza kupata jibu katika siku tatu.
  • Mke wake alimsumbua siku saba, kisha akawaambia watu wakeAmu 14:15–17
    Aya
    Amu 14:15–17Siku ya nne wakamwambia mkewe Samsoni, 'Mdanganye mume wako ili atuambie jibu la kitendawili, au tutakuchoma moto wewe na nyumba ya baba yako. Je, umetualika hapa ili kutufanya maskini? ' Mke wa Samsoni alianza kulia mbele yake; Akasema, 'Yote unayoyafanya ni kunichukia! Hunipendi. Umesema kitendawili kwa baadhi ya watu wangu, lakini hujawaambia jibu. ' Samsoni akamwambia, 'Angalia hapa, kama sijawaambia baba yangu au mama yangu, nikuambie wewe?' Alilia kwa siku saba ambazosikukuu yao iliendelea. Siku ya saba alimwambia jibu kwa sababu alimlazimisha sana. Akawaambia jibu jamaa zake.
  • “Ni nini kitamu kuliko asali? Ni nini chenye nguvu kuliko simba?”Amu 14:18
    Aya
    Amu 14:18Na watu wa mji wakamwambia, siku ya saba kabla ya jua kuzama, 'Ni nini kilicho bora zaidi kuliko asali? Ni kitu gani chenye nguvu kuliko simba? ' Samsoni akawaambia, 'Ikiwa hamkulima na ng'ombe wangu, hamtapata jibu la kitendawili changu.'

Vitendawili vingine

  • Malkia wa Sheba alimjaribu Sulemani kwa maswali magumu1 Fal 10:1–3, 2 Nya 9:1–2
    Aya
    1 Fal 10:1–3Malkia wa Sheba aliposikia uvumi wa Sulemani kuhusu jina la BWANA, alikuja kumjaribu kwa maswali magumu. Alikuja Yerusalemu na msafara mrefu, pamoja na ngamia waliokuwa wamebeba mizigo ya manukato, dhahabu nyingi, na mawe mengi ya thamani, akamwambia Sulemani yote yaliyokuwa moyoni mwake. Sulemani akajibu maswali yake yote. Hapakuwepo na swali ambalo aliuliza na mfalme akashindwa kujibu.
    2 Nya 9:1–2Malikia wa Sheba aliposikia kuhusu umaarufu wa Selemani, akaja Yerusalemu kumjaribu kwa maswali magumu. Akaja pamoja na msafara mkubwa sana, pamoja na ngamia waliosheheni manukato, dhahabu nyingi, na vito vingi vya thamani. Alipofika kwa Selemani, akamwambia yaliyokuwa moyoni mwake. Selemani akamjibu maswaali yake yote; hakuna kitu kilichokuwa kigumu sana kwa Selemani; hakuna swali ambalo hakulijibu.
  • Mungu anaongea na Musa waziwazi, si kwa mafumboHesabu 12:8
    Aya
    Hesabu 12:8Mimi huongea na Musa moja kwa moja, si kwa maono wala mafumbo. Yeye huniona umbo langu. Kwa hiyo, kwa nini hamuogoopi kumnenea kinyume, mtumishi wangu Musa?”
  • Mtunga zaburi anaeleza fumbo lake kwa kinubiZab 49:4
    Aya
    Zab 49:4Nitaelekeza sikio langu kwenye mfano; nitaanza mfano wangu kwa kinubi.
  • Mithali ni za kuelewa vitendawili vya wenye hekimaMit 1:6
    Aya
    Mit 1:6kwa kuelewa mithali, misemo, vitendawili na maneno ya wenye busara.
  • Danieli aliweza kueleza vitendawili na kutatua matatizo magumuDan 5:12
    Aya
    Dan 5:12Roho bora, ufahamu, weledi, kutafsiri ndoto, kufafanua mafumbo na kutatua matatizo - hizi ni sifa zilizopatikana kwa mtu huyu Danieli, ambaye mfalme alimwita Belteshaza. Sasa mwiteni Danieli naye atawaambia maana ya kile kilichoandikwa.”
  • Ezekieli anaambiwa ategee kitendawili kuhusu tai mkubwaEze 17:2–3
    Aya
    Eze 17:2–3“Mwanadamu, tega kitendawili na sema fumbo kwa nyumba ya Israeli. Sema, 'Bwana Yahwe asema hivi: Tai mkubwa pamoja na mabawa makubwa na vipapatio virefu, mwenye kujaa manyoya, na aliyekuwa na rangi nyingi alienda Lebanoni na kuchukua kilele cha mti wa mkangazi.
  • Maneno ya Aguri: mambo matatu, mambo manneMit 30:15–16, Mit 30:18–19, Mit 30:24–28
    Aya
    Mit 30:15–16Ruba anamabinti wawili, “ Toa na Toa” wanalia. Kuna vitu vitatu ambavyo havitosheki, vinne ambavyo havisememi, “Inatosha”: Kuzimu, tumbo tasa, nchi yenye kiu kwa maji, na moto usiosema, “Inatosha.”
    Mit 30:18–19Kuna vitu vitatu ambavyo vinanishangaza, vinne ambavyo sivifahamu: njia ya tai angani; njia ya nyoka juu ya mwamba; njia ya meli kwenye moyo wa bahari; na njia ya mtu pamoja mwanake kijana.
    Mit 30:24–28Vitu vinne duniani ni vidogo na bado vinabusara: mchwa ni viumbe ambao sio imara, lakini huandaa chakula chao wakati wa hari, Wibari siyo viumbe wenye nguvu, lakini hutengeneza makazi yake kwenye miamba. Nzige hawana mfalme, lakini wote wanamwendo wa mpangilio. Kama mjusi, unaweza kumkunja kwa mikono yako miwili, lakini wanapatikana katika majumba ya wafalme.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0