Gundua › Mada › Uchawi na ishara
Mambo ya kushangaza
Uchawi na ishara katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (32), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
Katika Sheria
- Uaguzi, ishara, uganga, waaguzi na kuwauliza wafu vimekatazwaLaw 19:26, Law 19:31, Kum 18:10–11
Aya
Law 19:26Usile nyama yoyote amabayo damu ingalimo ndani yake. Usiulize kwa roho juu ya wakati ujao,
Law 19:31Msiwageukie wale wanaoongea na wafu au roho wachafu. msiwatafute, la sivyo watawanajisi ninyi, Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
Kum 18:10–11Pasipatikana miongoni mwenu mmoja anayemweka kijana wake au binti yake kwenye moto, yeyote anatumia uganga, yeyote anatabiri, au mchawi, mchawi yeyote, yeyote aongeae na wafu, au yeyote aongeae na roho.
- Mchawi wa kike asiachwe haiKut 22:18
Aya
Kut 22:18Hautamwacha mchawi kuishi.
- Mwaguzi au mwenye pepo alipaswa kupigwa kwa maweLaw 20:27
Aya
Law 20:27Mwanaume au mwanamke anayeongea na wafu au anayeongea na roho hakika atauawa. Watu watawaponda kwa mawe. Wanayo hatia na wanastahili kufa.
Vilivyofanywa
- Labani: “Nimejifunza kwa uaguzi”Mwa 30:27
Aya
Mwa 30:27Labani akamwambia, “Ikiwa nimepata kibali machoni pako, subiri, kwa sababu nimejifunza kwa kutumia uaguzi kwamba Yahwe amenibariki kwa ajili yako.”
- Kikombe cha fedha cha Yusufu, kilichosemekana kutumika kwa uaguziMwa 44:5
Aya
Mwa 44:5Je hiki siyo kikombe ambacho bwana wangu hukinywea, na kikombe akitumiacho kwa uaguzi? Mmefanya vibaya, kwa jambo hili mlilolifanya.”
- Waganga wa Farao waliiga ishara kwa uganga wao, lakini si chawaKut 7:11, Kut 7:22, Kut 8:7, Kut 8:18
Aya
Kut 7:11Kisha naye Farao akawaita wazee wenye hekima na wachawi. Wakafanya jambo hilo hilo kwa uchawi wao.
Kut 7:22Lakini wachawi walifanya vivyo hivyo na uchawi wao. Kwaiyo moyo wa Farao ukawa mgumu, na akakataa kuwasikiliza Musa na Aruni, kama Yahweh alivyo sema itatokea.
Kut 8:7Lakini wachawi walifanya vivyo hivyo na uchawi wao: waliwatoa vyura juu ya nchi ya Misri.
Kut 8:18Wachawi walijaribu kufanya chawa kwa uganga wao lakini hawakuweza. Palikuwa na chawa kwa watu na kwa wanyama.
- Wazee wa Moabu walimletea Balaamu ada ya uaguziHesabu 22:7
Aya
Hesabu 22:7Kwa hiyo wazee wa Moabu na wale wa Midiani wakaondoka, pamoja nao wakachukua malipo ya uganga. Wakafika kwa Balaamu wakamwambia maneno ya Balaki.
- Sauli aliwaondoa waaguzi, kisha akamwendea mmoja Endori akiwa amejibadilisha1 Sam 28:3, 1 Sam 28:7–8
Aya
1 Sam 28:3Samweli alikuwa amefariki; Waisraeli wote walimwomboleza na kumzika huko Rama, katika mji wake mwenyewe. Wakati huo Sauli alikuwa amewafukuza kutoka nchini wote walioongea na wafu au pepo.
1 Sam 28:7–8Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, “Mnitafutie mwanamke ambaye anaweza kuongea na wafu, ili ni mwendee na kutafuta msaada wake.” Watumishi wake wakamwambia, “Tazama, yupo mwanamke huko Endori awezaye kuongea na wafu.” Basi Sauli akajigeuza, akavaa nguo nyingine tofauti, akaondoka yeye pamoja na watu wawili; wakamwendea yule mwanamke wakati wa usiku. Akasema, “Nitabirie, nakuomba, kwa kuongea na wafu, na uniinulie yule nitakayekutajia.”
- Mwaguzi anamwona Samweli na kumtambua Sauli1 Sam 28:11–14
Aya
1 Sam 28:11–14Kisha yule mwanamke akasema, “Je, nikuinulie nani?” Sauli akasema, “Niinulie Samweli.” Yule mwanamke alipomwona Samweli, akalia kwa sauti kuu na kusema na Sauli, akisema, “Kwa nini umenidanganya? Maana wewe ni Sauli.” Mfalme akamwambia, “Usiogope. Unaona kitu gani?” Yule mwanamke akamwambia Sauli, “Naona mungu akitoka katika nchi.” Akamuuliza mwanamke, “Je, anafanana na nani?” Mwanamke akajibu, “Mtu mzee anazuka; naye amevaa kanzu.” Sauli akafahamu kuwa huyo ni Samweli, naye Sauli akainamisha uso wake hadi chini akionesha heshima.
- Mambo ya Nyakati: Sauli alikufa, miongoni mwa mengine, kwa kumwuliza mwaguzi1 Nya 10:13
Aya
1 Nya 10:13Kwaiyo Sauli akafa kwa kuwa hakuwa mwaminifu kwa Yahweh. Hakutii maelekezo ya Yahweh, lakini akauliza ushauri kwa mtu anaye ongea na wafu.
- Yehu anataja uchawi mwingi wa Yezebeli2 Fal 9:22
Aya
2 Fal 9:22Wakati Yoramu alipomuona Yehu, alisema, “Je unakuja katika hali ya amani, Yehu?” Akajibu, “Amani gani hapo, wakati uzinzi wa ukahaba hufanywa na uchawi wa mama yako Yezebeli umejaa tele?”
- Mfalme Manase alifanya uchawi na kuwauliza waaguzi2 Fal 21:6, 2 Nya 33:6
Aya
2 Fal 21:6Akamuweka mtoto wake wa kiume kwenye moto; akatazama bao ushirikina na kujishuhulisha pamoja wale ambao wenye pepo wa utambuzi na wale wachawi. Akafanya maovu mengi usoni kwa Yahwe na kuchochea hasira kwa Mungu.
2 Nya 33:6Katika bonde la Beni Hinomu akawaweka wanaye katika moto. Akafanya misemo ya ubashiri, na uchawi, akassoma utabiri; akashauriana na wale waliozungumza na wafu na wale waliozungumza na na roho. Akafanaya maaovu mengi katika mcho ya Yahwe na alimfanya Mungu akasirike.
- Mfalme Yosia aliwaondoa waaguzi na wenye pepo2 Fal 23:24
Aya
2 Fal 23:24Yosia pia akawafukuza wale ambao waliokuwa wameongea na wafu au na roho. Pia aliifukuza miungu ya sananmu, sanamu, na vitu vyote ambavyo ni chukizo vilivyokuwa vinaonekana katika nchi ya Yuda na katika Yerusalemu, hivyo kwa kuthibitisha yale maneno ya sheria ambayo iliyokuwa imeandikwa kwenye kitabu cha Hilkia yule kuhani aliyekuwa amepatikana kwenye nyumba ya Yahwe.
- Mfalme wa Babeli anatafuta ishara: mishale, sanamu, iniEze 21:21
Aya
Eze 21:21Kwa kuwa mfalme wa Babeli atasimama kwenye makutano ya barabara, kwenye njia panda, ili kufanya uganga. Alitingisha mishale na kuuliza mwelekeo kutoka kwa sanamu na atalichunguza ini.
- Wanajimu wa Babeli wanatazama nyota na kutabiri kila mweziIsa 47:13
Aya
Isa 47:13Umejaribu sana kwa kushauriwa sana; waache hao watu wasimame na kukuokoa wewe- wale wanaoangalia mbingu na wanoangalia nyota, wale wanotangaza mwenzi mpya- waache wawaokoe nyie kutoka kwenye yaliyowapata.
- Waganga, wachawi na wanajimu wa Nebukadneza wanashindwa kueleza ndoto yakeDan 2:2, Dan 2:10, Dan 4:7
Aya
Dan 2:2Ndipo mfalme alipowaita waganga na wale wenye kuongea na wafu. Lakini pia aliwaita wachawi na watu wenye hekima. Aliwataka wamwambie juu ya ndoto zake. Basi walikuja na kusimama mbele za mfalme.
Dan 2:10Watu wenye hekima wakamjibu mfalme, “ Hakuna mtu katika dunia anayeweza kutimiza matakwa ya mfalme. Hakuna mfalme yoyote mkuu na mwenye nguvu ambaye alishataka jambo kama hilo kutoka kwa wachawi, wala wenye kuongea na wafu, wala mwenye hekima.
Dan 4:7Kisha walikuja wachawi, wale ambao hudai kuzungumza na wafu, watu wenye hekima, na wasoma nyota. Niliwaambia juu ya ndoto, lakini hawakuweza kunitafsiria.
- Wenye hekima wa Belshaza hawawezi kusoma maandishi ukutaniDan 5:7–8, Dan 5:15
Aya
Dan 5:7–8Mfalme alitoa agizo kwa kupiga kelele, waletwe ndani wale ambao hudai wanaweza kuzungumza na wafu, watu wenye hekima, na wataalamu wa nyota. Mfalme akawaambia wale waliojulikana kwa hekima katika Babeli, “Yeyote atakayeyaeleza maandishi haya na maana yake atavikwa nguo za zambarau na atavikwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwake. Naye atakuwa mtawala wa tatu wa juu kwa mamlaka katika ufalme.” Ndipo watu wote wa mfalme walikuwa wakijulikana kwa hekima yao waliingia ndani, lakini hawakuweza kuyasoma maandishi wala kueleza maana yake kwa mfalme.
Dan 5:15Na sasa watu wanaojulikana kwa hekima na wale wanaozungumza na wafu, wamekwisha kuletwa mbele yangu, ili kusoma maandishi haya na kunijulisha maana ya tafsiri yake, lakini hawakuweza kunijulisha tafsiri yake.
- Simoni wa Samaria aliwashangaza watu kwa uchawi wakeMdo 8:9–11
Aya
Mdo 8:9–11Lakini palikuwa na mtu mmoja katika mji ule jina lake Simon, ambaye alikuwa akifanya uchawi; ambao aliutumia kuwashangaza watu wa taifa la Samaria, wakati akisema kuwa yeye ni mtu wa muhimu. Wasamaria wote tangu mdogo hata mkubwa, wakamsikiliza; wakasema;”mtu huyu ni ile nguvu ya Mungu ambayo ni kuu.” Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mrefu kwa uchawi wake.
- Elima, au Bar Yesu, mchawi huko PafoMdo 13:6–8
Aya
Mdo 13:6–8Walipokwenda katika kisiwa chote mpaka Pafo, walikuta mtu fulani mchawi, Myahudi nabii wa uongo, ambaye jina lake lilikuwa Bar Yesu. Mchawi huyu alishirikiana na Liwali Sergio Paulus, aliyekuwa mtu mwenye akili. Mtu huyu aliwaalika Barnaba na Sauli, kwa sababu alihitaji kusikia neno la Mungu. Lakini Elima “yule mchawi” (hivyo ndivyo jina lake lilivyo tafsiriwa) aliwapinga; alijaribu kumgeuza yule liwali atoke kwenye imani.
- Mtumwa msichana huko Filipi aliwapatia wenye kumiliki fedha kwa kubashiriMdo 16:16–19
Aya
Mdo 16:16–19Ikawa kwamba, tulipokuwa tunaenda mahali pa kuomba, msichana mmoja aliyekuwa na pepo la utambuzi akakutana nasi. Alimletea bwana wake faida nyingi kwa kubashiri. Mwanamke huyu alimfuata Paulo pamoja na sisi, akipiga kelele na kusema “Hawa wanaume ni watumishi wa Mungu aliye Mkuu, wanaowatangazia ninyi habari ya wokovu”. Alifanya hivyo kwa siku nyingi, lakini Paulo akiwa amekasirishwa na tendo hilo, aligeuka nyuma na kumwambia pepo, “ Nakuamuru kwa Jina la Yesu umtoke ndani yake.” Naye akatoka na kumwacha mara moja. Mabwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limeondoka, waliwakamata Paulo na Sila na kuwaburuza sokoni mbele ya wenye mamlaka.
- Wana saba wa Skewa wanajaribu kutoa pepoMdo 19:13–16
Aya
Mdo 19:13–16Lakini palikuwapo Wayahudi wapunga pepo wakisafiri kupitia eneo hilo, wakilitumia jina la Yesu kwa ajili ya matumizi yao wenyewe. Wakiwaambia wale walikuwa na pepo wachafu; Wakisema, “Ninawaamuru mtoke kwa jina la Yesu ambaye Paulo anamhubiri.” Waliofanya haya walikuwa wana saba wa kuhani Mkuu wa Kiyahudi, Skewa. Roho wachafu wakawajibu, “Yesu namjua, na Paulo namjua; lakini ninyi ni nani? “ Yule roho mchafu ndani ya mtu akawarukia wapunga pepo na akawashinda nguvu na kuwapiga. Ndipo wakakimbia kutoka ile nyumba wakiwa uchi na kujeruhiwa.
- Huko Efeso vitabu vya uchawi vya drakma elfu hamsini vilichomwaMdo 19:19
Aya
Mdo 19:19Wengi waliokuwa wakifanya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma mbele ya kila mtu. Wakati wao walipohesabu thamani ya vitu hivyo, ilikuwa vipande hamsini elfu vya fedha.
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0