Bible Explorer

Gundua › Mada › Magereza na minyororo

Mambo ya kushangaza

Magereza na minyororo katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (45), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

Katika Agano la Kale

  • Yusufu alitiwa gerezani walimowekwa wafungwa wa mfalmeMwa 39:20
    Aya
    Mwa 39:20Bwana wa Yusufu akamchukua na kumweka gerezani, mahali walipowekwa wafungwa wa mfalme. Akawa pale kifungoni.
  • Mkuu wa gereza aliwaweka wafungwa wote chini ya uangalizi wa YusufuMwa 39:22
    Aya
    Mwa 39:22Mlinzi wa gereza akawaweka mikononi mwa Yusufu wafungwa wote waliokuwa gerezani. Chochote walichokifanya, kilikuwa chini ya uangalizi wa Yusufu.
  • Mnyweshaji na mwokaji wa Farao waliwekwa katika gereza hilohiloMwa 40:3
    Aya
    Mwa 40:3Akawaweka katika lindo katika nyumba ya kapteni wa walinzi, katika gereza lile Yusufu alimofungwa.
  • Yusufu alitolewa shimoni, akanyoa na kubadilisha mavazi yakeMwa 41:14
    Aya
    Mwa 41:14Ndipo Farao alipotuma na kumwita Yusufu. Kwa haraka wakamtoa gerezani. Akajinyoa mwenyewe, akabadili mavazi yake, na akaingia kwa Farao.
  • Yusufu aliwaweka ndugu zake siku tatu, kisha akamfunga SimeoniMwa 42:17, Mwa 42:24
    Aya
    Mwa 42:17Akawaweka kifungoni kwa siku tatu.
    Mwa 42:24Akatoka kwao na kulia. Akarudi kwao na kuongea nao. Akamchukua Simoni miongoni mwao na kumfunga mbele ya macho yao.
  • Ahabu: mtieni Mikaya gerezani kwa mkate na maji1 Fal 22:27
    Aya
    1 Fal 22:27Mwambie, 'mfalme anasema mweke huyo gerezani na awe anampa mkate kidogo na maji kidogo, mpaka nitakaporudi salama.'”
  • Asa, akiwa na hasira, alimtia gerezani mwonaji Hanani2 Nya 16:7, 2 Nya 16:10
    Aya
    2 Nya 16:7Wakati huo Hanani mwonaji akaenda kwa Asa, mfalme wa Yuda, na akamwambia, “Kwa sababu umemtegemea mfalme wa Aramu, na hukumtegemea Yahwe Mungu wako, jeshi la mfalme wa Aramu limetoroka nje ya mikono yako.
    2 Nya 16:10hili. Wakati huo huo, aliwagandamiza baadhi ya watu
  • Mfalme wa Ashuru alimtia gerezani mfalme Hoshea2 Fal 17:4
    Aya
    2 Fal 17:4Kisha mfalme wa Ashuru akaona kwamba Hoshea alikuwa na njama dhidi ya yake, kwa kuwa Hoshea aliwatuma wajumbe kwa So mfalme wa Misri; pia, hakumpatia kodi mfalme wa Ashuru, kama alivyofanya mwaka hadi mwaka.
  • Manase alichukuliwa Babeli kwa ndoana na pingu za shaba2 Nya 33:10–11
    Aya
    2 Nya 33:10–11Yahwe akasema kwa Manase, na kwa watu wake wote, lakini hawakumsikiliza. Kwa hiyo Yahwe akaleta juu yao maamri jeshsi wa jeshi la Ashuru, ambao walimchukua Manase katika minyonyoro, wakamfunga kwa pingu, na wakampeleka Babeli.
  • Sedekia, amepofushwa, alichukuliwa Babeli katika pingu za shaba2 Fal 25:7, Yer 52:11
    Aya
    2 Fal 25:7Kama kwa watoto wa Sedekia, wakawachinja mbele ya macho yake. Kisha akamtoa macho Sedekia, wakamfunga pingu, na kumpeleka hadi Babeli.
    Yer 52:11Kisha akayaondoa macho ya Sedekia, akamfunga katika vifungo vya shaba, na kumleta Babeli. Mfalme wa Babeli akamweka kifungoni hata siku ya kufa kwake.
  • Yekonia aliachiliwa baada ya miaka thelathini na saba akala mezani pa mfalme2 Fal 25:27–29
    Aya
    2 Fal 25:27–29Ilitokea baadaye katika mwaka wa thelathini na saba wa utumwa wa Yekonia mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na saba ya mwezi, Evil-merodaki mfalme wa Babeli akamtoa Yekonia mfalme wa Yuda kutoka gerezani. Hii ilitokea katika mwaka ambao Evil-Merodaki alipoanza kutawala. Akaongea naye kwa ukarimu na kumpatia kiti kizuri zaidi kuliko kile cha wafalme wengine ambao walikuwa pamoja naye Babeli. Evil-Merodaki akamvua Yekonia nguo za gerezani,

Yeremia

  • Alipigwa na kutiwa mkatale kwenye Lango la Juu la BenjaminiYer 20:2
    Aya
    Yer 20:2Basi Pashuri akampiga nabii Yeremia, akamtia katika masanduku yaliyokuwa kwenye lango la juu la Benyamini ndani ya nyumba ya Bwana.
  • Alifungwa katika chumba cha shimoni nyumbani kwa mwandishi YonathaniYer 37:15–16
    Aya
    Yer 37:15–16Maafisa walikuwa wamemkasirikia Yeremia. Walimpiga na kumweka gerezani, ambayo ilikuwa nyumba ya Yonathani mwandishi, kwa kuwa waligeuza kuwa gereza. Kwa hiyo Yeremia alikuwa amewekwa kwenye kifungo cha chini, ambako alikuwa huko kwa siku nyingi.
  • Aliwekwa katika ua wa walinzi, akipewa mkate mmoja kila sikuYer 32:2, Yer 37:21
    Aya
    Yer 32:2Katika wakati huo, jeshsi la mfalme wa Babeli lilikuwa limeuzunguka Yerusalemu, na Nehemia nabii alikuwwa amefungwa katika uwanja wa walinzi katika nyumba ya mfalme wa Yuda.
    Yer 37:21Kwa hiyo mfalme Sedekia alitoa amri. Wajakazi wake walimwekea mipaka Yeremia katika uwanja wa walinzi. Alipewa mkate kila siku kutoka mtaa wa waokaji mkate, mpaka mkate wote mjini uliisha. Basi Yeremia alibaki kwenye uwanja walinzi.
  • Alishushwa kwa kamba ndani ya kisima kisicho na maji, bali matope tuYer 38:6
    Aya
    Yer 38:6Kisha walimchukua Yeremia na kumtupa kwenye kisima cha Malkiya, mwana wa mfalme. Kisima kilikuwa kwenye uwanja wa mlinzi. Walimshusha Yeremia chini kwa kamba. Hapakuwa na maji kwenye kisima, lakini kulikuwa na matope, na alizama chini ya matope.
  • Aliachiliwa huko Rama kutoka minyororo mikononi mwakeYer 40:1, Yer 40:4
    Aya
    Yer 40:1Hili lilikuwa neno ambalo lilikuja kwa Yeremia toka kwa Yahwe baada ya Nebuzaradni, amri wa walinzi wa mfalme, amemtuma mbali kutoka Ramah. Huko ndiko Yeremia alikuwa amechukuliwa, na huko alikuwa amefungwa kwa minyororo. Alikuwa miongoni mwa mateka wote ya Yerusalem na Yuda ambayo walipaswa kuwa matekani Babeli.
    Yer 40:4Nimekuacha huru leo toka kwenye minyororo iliyokuwa kwenye mikono yako. Kama ni vizuri katika macho yako kuja nami Babeli, njoo, na nitakujali. Lakini kama si vizuri katika macho yako kuja pamoja nami, basi usifanye hivyo. Tazama nchi yote mbele yako. Nenda ambapo ni pazuri na sawa katika macho yako kwenda.”

Katika Agano Jipya

  • Herode alimfunga Yohana na kumtia gerezaniMt 14:3
    Aya
    Mt 14:3Kwa kuwa Herode alikuwa amemkamata Yohana akamfunga na kumtupa gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo kaka yake.
  • Kutoka gerezani Yohana aliwatuma wanafunzi wake kwa YesuMt 11:2
    Aya
    Mt 11:2na Yohana akiwa gereszani aliposikia akiwa juu ya matendo ya Kristo, alituma ujumbe kupitia wanafunzi wake,
  • Yohana alikatwa kichwa gerezaniMt 14:10
    Aya
    Mt 14:10Alituma Yohana aletwe kutoka gerezani
  • Baraba alikuwa gerezani kwa sababu ya uasi na uuajiLk 23:19
    Aya
    Lk 23:19Baraba alikuwa ni mtu ambaye amewekwa gerezani kwa sababu ya uasi fulani katika jiji na kwa kuua.
  • Yesu: “Nalikuwa gerezani mkaja kunitazama”Mt 25:36
    Aya
    Mt 25:36Nilikuwa uchi, na mlinivika nguo; Nilikuwa mgonjwa na mkanitunza; Nilikuwa kifungoni na mkaniijia.'
  • Petro na Yohana waliwekwa usiku kucha kwa sababu ilikuwa jioniMdo 4:3
    Aya
    Mdo 4:3Waliwakamata na kuwaweka gerezani hadi asubuhi iliyofuata, kwani tayari ilikuwa jioni.
  • Mitume hawakuwemo gerezani, ingawa lilikuwa limefungwa na kulindwaMdo 5:18–19, Mdo 5:23
    Aya
    Mdo 5:18–19wakanyosha mikono yao kuwakamata mitume na kuwaweka ndani ya gereza la jumla. Na wakati wa usiku malaika wa Bwana akaifungua milango ya gereza na kuwaongoza nje na kusema,
    Mdo 5:23“Tumekuta gereza limefungwa vizuri salama, na walinzi wamesimama langoni, lakini tulipokuwa tukifungua, hatukuona mtu ndani.”
  • Akilindwa sana, Petro alilala amefungwa minyororo kati ya askari wawiliMdo 12:4, Mdo 12:6
    Aya
    Mdo 12:4Alipomkamata, akamweka gerezani na akaweka vikosi vinne vya askari ili kumlinda, alikuwa akitarajia kumpeleka kwa watu baada ya Pasaka.
    Mdo 12:6Siku kabla Herode hajaenda kumtoa, Usiku huo Petro alikuwa amelala katikati ya maaskari wawili, akiwa amefungwa na minyororo miwili, na walinzi mbele ya mlango walikuwa wakilinda gereza.
  • Minyororo ilianguka, na lango la chuma likajifungua lenyeweMdo 12:7, Mdo 12:10
    Aya
    Mdo 12:7Tazama, malaika wa Bwana ghafla akamtokea na nuru ikang'aa ndani. Akampiga Petro ubavuni na kumwamsha akisema, “Amka haraka.”ndipo minyororo aliyokuwa amefungwa ikafunguka kutoka mikononi mwake.
    Mdo 12:10Baada ya kupita lindo la kwanza na la pili, wakafika kwenye geti la chuma la kuingilia kwenda mjini, likafunguka lenyewe kwa ajili yao. Wakatoka nje wakashuka kwenye mtaa, mara Malaika akamwacha.
  • Huko Filipi: chumba cha ndani, miguu imefungwa katika mkataleMdo 16:23–24
    Aya
    Mdo 16:23–24Baada ya kuwachapa viboko vingi, waliwatupa gerezani na kumuamuru askari wa gereza kuwalinda vyema. Baada ya kupokea amri hiyo, askari wa gereza aliwatupa katika chumba cha ndani ya gereza na kuwafunga miguu yao kwenye sehemu alipowahifadhi.
  • Usiku wa manane tetemeko lilifungua milango, na minyororo yote ikafungukaMdo 16:25–26
    Aya
    Mdo 16:25–26Wakati wa usiku wa manane, Paulo na Sila wakawa wakiomba na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, huku wafungwa wengine wakiwasikiliza, Ghafla kukatokea tetemeko kuu na misingi ya gereza ikatikiswa, milango ya gereza ikafunguka, na minyororo ya wafungwa wote ikalegezwa.
  • Huko Yerusalemu Paulo alifungwa kwa minyororo miwiliMdo 21:33
    Aya
    Mdo 21:33Kisha mkuu wa jeshi alimkaribia na akamshika Paulo, na akaamuru afungwe minyororo miwili. Akamuuliza yeye ni nani na amefanya nini.
  • Feliki alimwacha Paulo gerezani miaka miwiliMdo 24:27
    Aya
    Mdo 24:27Ila miaka miwili ilipopita, Porkio Festo akawa Liwali baada ya Feliki, ila Feliki alitaka kujipendekeza kwa Wayahudi, hivyo akamwacha Paulo chini ya uangalizi.
  • Huko Roma Paulo aliishi na askari akimlinda, amefungwa kwa mnyororoMdo 28:16, Mdo 28:20
    Aya
    Mdo 28:16Tulipoingia Roma, Paulo aliruhusiwa kuishi peke yake pamoja na yule askari aliyekuwa akimlinda.
    Mdo 28:20Kwa sababu ya kukata kwangu rufaa, hivyo, niliomba kuwaona na kuongea nanyi. Ni kwa sababu ya kile ambacho Israel anaujasiri kwacho, nimefungwa na kifungo hiki.
  • Alikaa miaka miwili mizima katika nyumba yake ya kupangaMdo 28:30
    Aya
    Mdo 28:30Paulo alikaa katika nyumba yake ya kupanga kwa miaka yote miwili, na aliwakaribisha wote waliokuja kwake.
  • Onesiforo hakuionea aibu minyororo ya Paulo2 Tim 1:16
    Aya
    2 Tim 1:16Bwana airehemu nyumba ya Onesiforo kwa kuwa mara nyingi aliniburudisha na hakuionea aibu minyororo yangu.

Mikufu ya dhahabu

  • Farao alimvika Yusufu mkufu wa dhahabu shingoniMwa 41:42
    Aya
    Mwa 41:42Farao akavua pete yake ya mhuri kutoka katika mkono wake na kuiweka katika mkono wa Yusufu. Akamvika kwa mavazi ya kitani safi, na kuweka mkufu wa dhahabu shingoni mwake.
  • Belshaza aliagiza Danieli avikwe mkufu wa dhahabu shingoniDan 5:29
    Aya
    Dan 5:29Ndipo Belshaza alitoa agizo, na walimvalisha Danieli mavazi ya zambarau. Mkufu wa dhahabu walimvisha shingoni, na mfalme alitoa tamko juu ya Danieli kuwa atakuwa mtawala mwenye mamlaka ya nafasi ya tatu katika ufalme.
  • Gideoni alichukua mikufu kutoka shingoni mwa ngamia wa MidianiAmu 8:26
    Aya
    Amu 8:26Uzito wa pete za dhahabu alizoomba zilikuwa shekeli 1,700 za dhahabu. Nyara hizi zilikuwa ni pamoja na mapambo ya makoja, vidani, nguo ya rangi ya zambarau waliyovaa na wafalme wa Midiani, na zaidi ya minyororo iliyokuwa karibu na shingo za ngamia zao.
  • Sulemani alitundika minyororo ya dhahabu mbele ya patakatifu pa ndani1 Fal 6:21
    Aya
    1 Fal 6:21Sulemani alifunika ndani ya hekalu kwa dhahabu safi na akaweka mikufu ya dhahabu iliyopita mbele ya chumba cha ndani, na kulifunika eneo la mbele kwa dhabahu.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0