Gundua › Mada › Siku za kuzaliwa
Mambo ya kushangaza
Siku za kuzaliwa katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (8), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
- Siku ya kuzaliwa kwa Farao alifanya karamu kwa maafisa wakeMwa 40:20
Aya
Mwa 40:20Ikawa siku ya tatu ambayo ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa Farao. Akafanya sherehe kwa watumishi wake wote. “Akakiinua juu” kichwa cha mkuu wa wanyweshaji na kichwa cha mkuu wa waokaji, kati ya watumishi wake.
- Siku hiyo alimrudisha mnyweshaji kazini na kumtundika mwokajiMwa 40:21–22
Aya
Mwa 40:21–22Akamrudisha mkuu wa wanyweshaji katika majukumu yake, na akakiweka tena kikombe katika mkono wa Farao. Lakini akamtundika mkuu wa waokaji, kama Yusufu alivyokuwa amewatafsiria.
- Siku ya kuzaliwa kwa Herode alifanya karamu kwa viongozi wa GalilayaMk 6:21
Aya
Mk 6:21Hata ilipofika wakati mwafaka ikiwa imekaribia siku ya kuzaliwa Herode akawaandalia moafisa wake karamu, na makamanda, na viongozi wa Galilaya.
- Binti wa Herodia alicheza na kuomba kichwa cha YohanaMt 14:6–8
Aya
Mt 14:6–8Lakini wakati siku ya kuzaliwa Herode ilipofika binti wa Herodia alicheza katikati ya watu na kumpendeza Herode. Katika kujibu kili aliahidi kwa kiapo kwamba atampa chochote atakachoomba. Baada ya kushauriwa na mama yake, alisema, “Nipe mimi hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji.”
- Ayubu aliilaani siku ya kuzaliwa kwakeAyu 3:1–3
Aya
Ayu 3:1–3Baada ya hayo, Ayubu akafunua kinywa chake na kuilani siku aliyozaliwa. Akasema, “Na ipotelee mbali siku niliyozaliwa mimi, usiku uliosema, 'Mimba ya mtoto wa kiume imetungwa.'
- Yeremia: ilaaniwe siku niliyozaliwaYer 20:14, Yer 20:18
- Jina jema ni bora kuliko manukato, siku ya kufa kuliko ya kuzaliwaMhu 7:1
Aya
Mhu 7:1Jina zuri ni bora kuliko manukato ya gharama, na siku ya kufa ni bora kuliko siku ya kuzaliwa.
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0