Bible Explorer

Gundua › Mada › Ngamia

Mambo ya kushangaza

Ngamia katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (26), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Ngamia hakupaswa kuliwaLaw 11:4
    Aya
    Law 11:4Hata hivyo, kuna baadhi ya wanyama ambao ama hawacheui au hana kwato zilizogawanyika, nanyi msiwale hao, wanyama kama ngamia, kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato zilizogawanyika. Kwa hiyo ngamia ni najisi kwenu.
  • Abram, Yakobo na Ayubu walihesabu ngamia katika utajiri waoMwa 12:16, Mwa 30:43, Ayu 1:3
    Aya
    Mwa 12:16Farao akamtendea kwa wema Abram kwa ajili yake, na akampatia kondoo, maksai, punda waume watumishi wa kiume, watumishi wa kike, punda wake, na ngamia.
    Mwa 30:43Mtu huyo akastawi sana. Akawa na kundi kubwa la kondoo, wajakazi na wajoli, ngamia na punda.
    Ayu 1:3Alimiliki kondoo elfu saba, ngamia elfu tatu, jozi mia moja za maksai, na punda mia tano na idadi kubwa ya watumishi. Mtu huyu alikuwa mtu mkuu wa watu wote wa mashariki.
  • Ayubu alikuwa na ngamia 3,000, baadaye 6,000Ayu 1:3, Ayu 42:12
    Aya
    Ayu 1:3Alimiliki kondoo elfu saba, ngamia elfu tatu, jozi mia moja za maksai, na punda mia tano na idadi kubwa ya watumishi. Mtu huyu alikuwa mtu mkuu wa watu wote wa mashariki.
    Ayu 42:12Yahweh aliubarikiwa mwisho wa maisha ya Ayubu kuliko mwanzo wake; alikuwa na kondoo kumi na nne elfu, ngamia elfu sita, jozi elfu moja, na punda jike elfu moja.
  • Obili Mwishmaeli alisimamia ngamia wa Daudi1 Nya 27:30
    Aya
    1 Nya 27:30Msimamizi wa ngamia alikuwa Obili Mishimaeli, na juu ya punda wakike alikuwa Yehideia kutoka Meronothi. Juu ya mifugo alikuwa Yazizi Mhagri.

Katika masimulizi

  • Mtumishi wa Abraham alichukua ngamia kumi kumtafutia Isaka mkeMwa 24:10
    Aya
    Mwa 24:10Mtumwa akachukua ngamia kumi wa bwana wake na akaondoka. Akachukua pia aina zote za zawadi kutoka kwa bwana wake. Akaondoka na kwenda katika mkoa wa Aramu Naharaimu, mji wa Nahori.
  • Aliwapigisha ngamia magoti kando ya kisima jioniMwa 24:11
    Aya
    Mwa 24:11Akawapigisha magoti ngamia nje ya mji karibu na kisima cha maji. Ilikuwa jioni wakati ambao wanawake huenda kuchota maji.
  • Rebeka aliwatekea maji ngamia wake woteMwa 24:14, Mwa 24:19–20
    Aya
    Mwa 24:14Na itokee hivi kwamba. Nikimwambia msichana, tafadhari tua mtungi wako ili niweze kunywa maji,' na akiniambia, 'Kunywa, na kwamba nitawanywesha ngamia wako pia,' huyo ndiye awe ambaye umemchagulia mtumwa wako Isaka. Kwa njia hii nitajua kuwa umeonesha agano la uaminifu kwa bwana wangu.”
    Mwa 24:19–20Alipokuwa amemaliza kumpatia maji, akasema, “Nitachota maji kwa ajili ya ngamia wako pia, mpaka watakapomaliza kunywa.” Hivyo akaharakisha akamwaga maji yaliyokuwa mtungini kwenye chombo cha kunywshea mifugo, kisha akakimbia tena kisimani kuchota maji, na kuwanywesha ngamia wake wote.
  • Rebeka alipanda ngamia kwenda kukutana na IsakaMwa 24:61, Mwa 24:64
    Aya
    Mwa 24:61Kisha Rebeka akasimama, yeye na watumishi wake kwa hesabu ya ngamia, na wakamfuata yule mtu. Hivyo watumishi wakamchukua Rebeka, na wakaenda zao.
    Mwa 24:64Rebeka akatazama na alipomwona Isaka, akaruka kutoka kwenye ngamia.
  • Raheli alificha sanamu za Labani katika tandiko la ngamia na kuzikaliaMwa 31:34
    Aya
    Mwa 31:34Basi Raheli alikuwa ameichukua miungu ya nyumbani, na kuiweka katika ngozi ya ngamia, na kukaa juu yake. Labani akatafuta katika hema yote, lakini hakuiona.
  • Zawadi ya Yakobo kwa Esau ilijumuisha ngamia 30 wanaonyonyesha pamoja na wana waoMwa 32:15
    Aya
    Mwa 32:15ngamia wakamwao thelathini na wana wao, ng'ombe madume arobaini na madume kumi ya ng'ombe, punda wa kike ishirini na madume yake ishirini.
  • Ngamia wa Waishmaeli walibeba viungo kwenda MisriMwa 37:25
    Aya
    Mwa 37:25Wakakaa chini kula mkate. Walipoinua macho yao na kuangalia, na, tazama, msafara wa Waishmaeli ulikuwa ukija kutoka Gileadi, pamoja na ngamia wao waliochukua viungo, malhamu na manemane. Walikuwa wakisafiri kuvichukua kuelekea Misri.
  • Ngamia wa Wamidiani hawakuhesabika kama mchangaAmu 7:12
    Aya
    Amu 7:12Wamidiani, Waamaleki, na watu wote wa mashariki walikaa karibu na bonde, wengi kama wingu la nzige. Ngamia zao walikuwa zaidi ya mawingu; walikuwa zaidi kuliko idadi ya mchanga katika bahari.
  • Gideoni alichukua mapambo ya mwezi mwandamo kutoka kwa ngamia wa wafalmeAmu 8:21
    Aya
    Amu 8:21Ndipo Zeba na Salmuna wakasema, simama mwenyewe, utuue! Kwa maana kama mtu alivyo, ndivyo zilivyo nguvu zake. Gideoni akasimama na kumwua Zeba na Salmuna. Pia aliondoa mapambo yaliyokuwa juu ya shingo za ngamia zao.
  • Waamaleki mia nne walimkimbia Daudi juu ya ngamia1 Sam 30:17
    Aya
    1 Sam 30:17Daudi akawashambulia tangu jua lilipozama hadi jioni ya siku ya pili. Hakuna mtu aliyeponyoka isipokuwa vijana mia nne, waliopanda ngamia na kukimbia.
  • Malkia wa Sheba alikuja na ngamia waliobeba viungo na dhahabu1 Fal 10:2
    Aya
    1 Fal 10:2Alikuja Yerusalemu na msafara mrefu, pamoja na ngamia waliokuwa wamebeba mizigo ya manukato, dhahabu nyingi, na mawe mengi ya thamani, akamwambia Sulemani yote yaliyokuwa moyoni mwake.
  • Hazaeli alimletea Elisha zawadi mizigo ya ngamia arobaini2 Fal 8:9
    Aya
    2 Fal 8:9Basi Hazaeli akaenda kuonana naye na kuchukua zawadi zake za kila kitu kizuri cha Damskasi, akabeba ngamia arobaini. Hivyo Hazaeli akaja na kusimama mbele ya Elisha na kusema, “Mtoto wako Ben Hadadi mfalme wa Shamu amenituma kwako, kusema, “Je nitapona huu ugonjwa?”
  • Wavamizi Wakaldayo waliwachukua ngamia wa AyubuAyu 1:17
    Aya
    Ayu 1:17Wakati alipokuwa akiendelea kusema, akatokea mwingine pia na kusema, “Wakaldayo walifanya vikundi vitatu, wakawashambulia ngamia, na kuondoka nao. Kwa wale watumishi, wamewaua kwa makali ya upanga. Mimi pekee nimeokoka kukuletea habari.”
  • Yohana alivaa vazi la manyoya ya ngamiaMt 3:4, Mk 1:6
    Aya
    Mt 3:4Sasa Yohana alivaa manyoya ya ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.
    Mk 1:6Yohana alikuwa anavaa vazi la manyoya ya ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake, na alikuwa anakula nzige na asali ya porini.

Maneno ya Yesu

  • Ni rahisi ngamia kupita katika tundu la sindanoMt 19:24
    Aya
    Mt 19:24Tena nawaambieni, ni rahisi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko kwa mtu tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.”
  • Mnamchuja mbu lakini mnameza ngamiaMt 23:24
    Aya
    Mt 23:24Enyi viongozi vipofu, ninyi ambao mnachuja mdudu mdogo lakini mnameza ngamia!

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0