Gundua › Mada › Meli na safari za baharini
Mambo ya kushangaza
Meli na safari za baharini katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (31), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
- Safina ya Nuhu: mti wa mvinje, vyumba, imepakwa lamiMwa 6:14–15
Aya
Mwa 6:14–15Tengeneza safina ya mti wa mvinje kwa ajili yako. Tengeneza vyumba katika safina, na vifunike kwa lami ndani na nje. Hivi ndivyo utakavyofanya: urefu wa safina dhiraa miatatu, upana wake dhiraa hamsini, kwenda juu kwake dhiraa thelathini.
- Sulemani alitengeneza merikebu Ezioni Geberi kando ya Bahari ya Shamu1 Fal 9:26
Aya
1 Fal 9:26Tena Sulemani alitengeneza merikebu kule Ezioni Geberi, ambayo iko karibu na Elathi katika ufukwe wa bahari ya shamu, katika nchi ya Edomu.
- Mabaharia wa Hiramu walileta talanta 450 za dhahabu kutoka Ofiri2 Nya 8:18
Aya
2 Nya 8:18Hiramu akatuma meli zake kupitia watumishi wake ambao walikuwa wana maji wenye uzoefu. Wakasafiri na Selemani na watumishi wa Semani hadi Ofiri. Wakachukua kutoka huko talanta 450 za dhahabu ambazo walimletea Selemani.
- Kila miaka mitatu: dhahabu, fedha, pembe, nyani na tausi1 Fal 10:22
Aya
1 Fal 10:22Mfalme alikuwa na merikebu za kusafiri pamoja na merikebu za Hiramu. Mara moja kila mwaka merikebu zilileta dhahabu, fedha, na pembe za ndovu, pamoja na nyani na tumbili.
- Meli za Yehoshafati zilivunjika kabla hazijasafiri1 Fal 22:48, 2 Nya 20:36–37
Aya
1 Fal 22:48Yehoshafati alijenga merikebu: ziende Tarshishi na Ofri kuleta dhahabu, lakini hazikusafiri kwa sababu zile merikebu zilivunjika kule Esioni Geberi. Kisha
2 Nya 20:36–37Akapatana naye kujenga meli za kwenda Tarshishi; Wakazijenga meli hizo huko Esion-geberi. Kisha Eliezeli, mwana wa Dadavahu wa Maresha, akatoa unabii juu ya Yehoshafati; akasema, “kwa sababu umepatana na Ahazia, Yahwe ameiharibu miradi yako.” Meli zilivunjika ili kwamba zisiweze kusafiri.
- Ezekieli anaeleza Tiro kama meli ya msonobari, mwerezi, mwaloni na kitaniEze 27:5–7
Aya
Eze 27:5–7Wametengeneza mbao nene na pana kwa mvinje kutoka Mlima Hermoni; wamechukua mkangazi kutoka Lebanoni kuufanya mlingoti. Wametengeneza makasia yako kutoka kwenye mialo ya Bashani; wametengeza sitaha zako kwa mbao za mvinje kutoka Kitimu, na wametengeneza kwa pembe. Tanga zako zilikuwa za rangi za kitani kutoka Misri ambazo zilikuwa kama beramu!
- Mashua za mafunjo ziliwabeba wajumbe majiniIsa 18:2
Aya
Isa 18:2wanowatuma mabalozi wao kwa kupitia bahari, na vyombo vya majani juu ya maji. Nendeni enyi wajumbe wepesi, kwa watu warefu na laini waishio kwenye nchi, kwa watu wanogopa mbali na karibu, taifa lenye nguvu, wakanyagao watu, ambao mito imegawanya nchi yao.
- Meli kubwa huongozwa na usukani mdogo sanaYak 3:4
Aya
Yak 3:4Tambua pia kwamba meli, ingawa ni kubwa na husukumwa na upepo mkali, zinaongozwa kwa usukani mdogo sana kwenda popote anakotaka nahodha.
- Njia ya meli baharini: ajabu mno kwa AguriMit 30:18–19
Aya
Mit 30:18–19Kuna vitu vitatu ambavyo vinanishangaza, vinne ambavyo sivifahamu: njia ya tai angani; njia ya nyoka juu ya mwamba; njia ya meli kwenye moyo wa bahari; na njia ya mtu pamoja mwanake kijana.
Safari
- Yona alilipa nauli ya meli iendayo TarshishiYon 1:3
Aya
Yon 1:3Lakini Yona akaondoka kukimbia kutoka mbele ya Bwana na kwenda Tarshishi. Akatelemka mpaka Yafa na akaona melikebu inayokwenda Tarshishi. Kwa hiyo alilipa nauli na akapanda melikebu kwenda nayo Tarishishi, mbali na uwepo wa Yahweh.
- Katika dhoruba mabaharia walitupa mizigo bahariniYon 1:4–5
Aya
Yon 1:4–5Lakini Bwana akatuma upepo mkubwa juu ya bahari, ikawa tufani juu ya bahari. Hivi karibuni ikaonekana kwamba meli ilikuwa inataka kuvunjika. Wale baharia waliogopa sana na kila mtu alilia kwa mungu wake mwenyewe. Wakatupa mizigo bahari iliyokuwa merikebuni ili kuifungua. Yona alikuwa ameshuka hapa pande za ndani ya melikebu, naye alikuwa amelala huko usingizi.
- Walipiga makasia kwa nguvu lakini hawakuweza kufika nchi kavuYon 1:13
Aya
Yon 1:13Hata hivyo, watu hao wavuta makasia kwa bidii ili kurudi nchi kavu, lakini hawakuweza kufanya hivyo kwa sababu bahari ilikuwa imechafuka zaidi dhidi yao.
- Yesu aliufundisha umati kutoka mashua ya SimoniLk 5:2–3
Aya
Lk 5:2–3Aliona mashua mbili zimetia nanga pembeni mwa ziwa. Wavuvi walikuwa wametoka na walikuwa wakiosha nyavu zao. Yesu akaingia katika mojawapo ya zile mashua, ambayo ilikuwa ya Simoni na kumwomba aipeleke majini mbali kidogo na nchi kavu. Kisha akakaa na kufundisha kutokea kwenye mashua.
- Yesu alilala juu ya mto upande wa nyuma wa mashua wakati wa dhorubaMk 4:37–38
Aya
Mk 4:37–38Na upepo mkali wa dhoruba na mawimbi yalikuwa yakiingia ndani ya mtumbwi na mtumbwi tayali ulikuwa umejaa. Lakini Yesu mwenyewe alikuwa kwenye shetri, amelala kwenye mto. Wakamwamsha, wakisema, “Mwalimu, haujali sisi tunakufa?”
- Wanafunzi walitaabika kupiga makasia dhidi ya upepoMk 6:48
Aya
Mk 6:48Na aliwaona wakitaabika kupiga makasia kwa sababu upepo uliwazuia. Ilipokaribia asubuhi akawaendea, akitembea juu ya maji, na alitaka kuwapita.
- Paulo alivunjikiwa meli mara tatu na akakaa siku moja katika bahari kuu2 Kor 11:25
Aya
2 Kor 11:25Mara tatu nilipigwa kwa fimbo. Mara moja nilipigwa mawe. Mara tatu nilinusurika melini. Nimetumia usiku na mchana katika bahari wazi.
Safari ya Paulo kwenda Roma
- Meli kutoka Adramitamu, kando ya pwani ya AsiaMdo 27:2
Aya
Mdo 27:2Tukapanda meli kutoka Adramitamu, ambayo ilikuwa isafiri kandokando ya pwani ya Asia. Hivyo tukaingia baharini. Aristaka kutoka Thesolanike ya Makedonia akaenda pamoja nasi.
- Kusafiri baharini kulikuwa hatari baada ya KufungaMdo 27:9
Aya
Mdo 27:9Tulikuwa tumechukua muda mwingi sana, na muda wa mfungo wa Kiyahudi ulikuwa umepita pia, na sasa ilikuwa ni hatari kuendelea kusafiri. Hivyo Paulo akatuonya,
- Upepo wa kaskazini mashariki ulivuma; walizungusha kamba chini ya meliMdo 27:14, Mdo 27:17
Aya
Mdo 27:14Lakini baada ya muda mfupi upepo mkali, ulioitwa Wa kaskazini mashariki, ukaanza kutupiga kutoka ng'ambo ya kisiwa.
Mdo 27:17Baada ya kuwa wameivuta, walitumia kamba kuifunga meli. Waliogopa kwamba tungeweza kwenda kwenye eneo la mchanga mwingi la Syiti, hivyo wakashusha nanga na waliendeshwa kandokando.
- Mizigo, kisha vifaa vya meli, vilitupwa bahariniMdo 27:18–19
Aya
Mdo 27:18–19Tulipigwa kwa nguvu sana na dhoruba, hivyo siku iliyofuata mabaharia wakaanza kutupa mizigo kutoka melini. Siku ya tatu, mabaharia wakaanza kuyatoa maji kwa mikono yao wenyewe.
- Vipimo vya kina: maji yanazidi kupungua kinaMdo 27:28
Aya
Mdo 27:28Walitumia milio kupima kina cha maji na wakapata mita thelathini na sita, baada ya muda mfupi wakapima tena wakapata mita ishirini na saba.
- Nanga nne zilishushwa kutoka shetriMdo 27:29
Aya
Mdo 27:29Waliogopa kwanza tunaweza kugonga miamba, hivyo wakashusha nanga nne kutoka katika sehemu ya kuwekea nanga na wakaomba kwamba asubuhi ingekuja mapema.
- Mabaharia walijaribu kutoroka kwa mashua ndogo; askari wakaikata kambaMdo 27:30, Mdo 27:32
- Melini walikuwa watu 276Mdo 27:37
Aya
Mdo 27:37Tulikuwa watu 276 ndani ya meli.
- Walitupa ngano baharini ili kuipunguzia meli uzitoMdo 27:38
Aya
Mdo 27:38Walipokwisha kula vya kutosha, waliifanya meli nyepesi kwa kutupa ngano ndani ya bahari.
- Meli ilikwama na shetri likavunjikaMdo 27:41
Aya
Mdo 27:41Lakini wakaja mahali ambapo mikondo miwili ya maji inakutana, na meli ikaelekea mchangani. Na ile sehemu ya mbele ya meli ikakwama pale na haikuweza kutoka, lakini sehemu ya mbele ya meli ikaanza kuvunjika kwa sababu ya ukali wa mawimbi.
- Wote walifika nchi kavu, wengine juu ya mbaoMdo 27:44
Aya
Mdo 27:44Kisha wanaume wengine watafuata, wengine juu ya vipande vya mbao na wengine juu ya vitu vingine kutoka kwenye meli. Kwa njia hii ikatokea kwamba wote tutafika salama nchi kavu.
- Kuendelea Roma kwa meli ya Iskanderia, Ndugu MapachaMdo 28:11
Aya
Mdo 28:11Baada ya miezi mitatu, tulisafiri ndani ya meli ya Iskanda ambayo ilikuwa imepigwa baridi hapo kisiwani, ambayo viongozi wake walikuwa ndugu wawili mapacha.
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0