Bible Explorer

Gundua › Mada › Wanadhiri na nadhiri yao

Mambo ya kushangaza

Wanadhiri na nadhiri yao katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (27), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

Katika Sheria

  • Mwanamume au mwanamke angeweza kuweka nadhiri maalum ya MnadhiriHesabu 6:2
    Aya
    Hesabu 6:2'Nena na wana wa Israeli, uwaambie, 'Kama mume au mke ataweka nadhiri kwa BWANA kwa kiapo maalumu cha mnadhiri, ndipo atajiepusha na divai na vileo. hatakunywa siki itokanayo na divai.
  • Hakuna divai, kileo, siki, maji ya zabibu, zabibu wala zabibu kavuHesabu 6:3
    Aya
    Hesabu 6:3Asinywe kileo kitokanacho na siki au kilevi. Asinywe maji ya divai yeyote au kula zabibu mbichi wala zilizokauka.
  • Hakuna kitu cha mzabibu, hata mbegu wala magandaHesabu 6:4
    Aya
    Hesabu 6:4Katika siku zote ambazo amejitenga kwa ajili yangu, asile chochote kinachotokana na zabibu, wala kitu chochote kitokanacho na makokwa hadi maganda.
  • Wembe usipite kichwani: nywele lazima zirefukeHesabu 6:5
    Aya
    Hesabu 6:5Wakati wote wa nadhiri yake, wembe usiipite kichwani mwake mpaka siku zake za nadhiri kwa BWANA zitimilike. Lazima ajitenge kwa BWANA. Ataziacha nywele zake zikue kichwani mwake.
  • Asikaribie maiti, hata ya baba au mama yakeHesabu 6:6–7
    Aya
    Hesabu 6:6–7Wakati wote wa kujidhiri kwake kwa BWANA, asiikaribie maiti. Asijinajisi kwa namna yeyote hata kama atakufa baba yake, mama, dada, au ndugu yake. Hii ni kwa sababu amejitenga kwa ajili ya Mungu, kama ambavyo kila mmoja anavyoweza kumuona kwa uerfu wa nywele zake.
  • Mtu akifa ghafla karibu naye: anyoe kichwa siku ya sabaHesabu 6:9
    Aya
    Hesabu 6:9Ikitokea mtu amekufa ghafla pembeni yake na kukitia unajisi kichwa chake kitakatifu, ndipo atakaponyoa kichwa chake katika siku ya kujitakasa —Siku ya saba atanyoa kichwa chake.
  • Siku ya nane: hua wawili au makinda mawili ya njiwaHesabu 6:10
    Aya
    Hesabu 6:10Siku ya nane atamletea kuhani njiwa wawili au makinda mawili ya njiwa kwenye lango la hema ya kukutania.
  • Siku za mwanzo hazikuhesabiwa; nadhiri ilianza upyaHesabu 6:12
    Aya
    Hesabu 6:12Atajitenga kwa BWANA tena katika siku hizo za utakaso. Ataleta kondoo mume mwenye umri wa mwaka mmoja kama sadaka ya hatia. Zile siku zake kabla ya kunajisika hazitahesabiwa, kwa sababu kujiweka wakfu kwake kulinajisika.
  • Mwishoni: mwana kondoo dume, mwana kondoo jike, kondoo dume na mkate usiotiwa chachuHesabu 6:13–15
    Aya
    Hesabu 6:13–15Hii ndiyo sheria ya mnadhiri wakati wa muda wa kujidhiri unapokuwa umetimia. Ataletwa kwenye mlango wa hema ya kukutania. Ataleta sadaka yake kwa BWANA. Atatoa mwanakondoo mume wa mwaka mmoja asiye na hila kama sadaka ya kuteketezwa. Ataleta kondoo mke wa mwaka mmoja asiye na hila kama sadaka ya dhambi. Ataleta kondoo mume asiye na hila kama sadaka ya amani. Ataleta kikapu cha mikate iliyotengenezwa bila amira, mikate ya unga mwembamba iliyokandwa kwa mafuta, mikate ya kaki isiyo na amira iliyopakwa mafuta, pamoja na sadaka za unga na sadaka za vinywaji.
  • Mnadhiri alinyoa kichwa chake na kuweka nywele motoniHesabu 6:18
    Aya
    Hesabu 6:18Mnadhiri atanyoa nywele zake kama ishara ya kujitenga kwa ajili ya Mungu kwenye mlango wa hema ya kukutania. Atazitoa nywele zake kichwani kwake na kuzichoma kwa moto ulio chini ya sadaka ya amani.
  • Baada ya hapo, Mnadhiri anaweza kunywa divaiHesabu 6:20
    Aya
    Hesabu 6:20Kisha kuhani atavitikisa kuwa sadaka kwa BWANA, sehemu takatifu kwa kuhani, pamoja na kidari cha kutikiswa na paja lililotolewa kwa kwa kuhani. Baadaye, Mnadhiri anaweza kunywa divai.

Wanadhiri waliotajwa

  • Mama wa Samsoni asinywe divai wala kula kitu chochote najisiAmu 13:4, Amu 13:7, Amu 13:14
    Aya
    Amu 13:4Sasa kuwa makini usinywe divai au kileo, wala usile kitu chochote kilicho najisi.
    Amu 13:7Akaniambia, 'Tazama! Utakuwa mjamzito, na utazaa mtoto. Basi usinywe divai au kileo, wala usile chakula chochote ambacho sheria inasema kuwa si safi, kwa kuwa mtoto huyo atakuwa Mnaziri kwa Mungu tangu akipokuwa tumboni mwako mpaka siku ya kufa kwake.”
    Amu 13:14Asile kitu chochote kinachotokana na mizabibu, wala usimruhusu kunywa divai au kileo; usimruhusu ale chakula chochote ambacho sheria inasema kuwa si safi. Anapaswa kutii kila kitu nilichoamuru afanye.
  • Samsoni angekuwa Mnadhiri tangu tumboni; wembe usipite kichwani pakeAmu 13:5
    Aya
    Amu 13:5Angalia, utakuwa na mjamzito na kuzaliwa mtoto mwanaume. Hakuna wembe itakayotumiwa juu ya kichwa chake, kwa kuwa mtoto atakuwa Mnaziri kwa Mungu kutoka tumboni, naye ataanza kuwaokoa Israeli kutoka mkono wa Wafilisti.
  • Samsoni: “Nywele zangu hazijawahi kunyolewa”Amu 16:17
    Aya
    Amu 16:17Basi Samsoni alimwambia kila kitu, akamwambia, “Wembe haujawahi kukata nywele juu ya kichwa changu, kwa maana nimekuwa Mnaziri kwa Mungu kutoka tumboni mwa mama yangu. Ikiwa kichwa changu kitanyolewa, basi nguvu zangu zitaniacha, nami nitakuwa dhaifu na kuwa kama kila mtu mwingine. '
  • Delila aliagiza nywele za kichwa chake zinyoleweAmu 16:19
    Aya
    Amu 16:19Alimfanya alale katika magoti yake. Alimwita mtu avinyoe vifungo saba vya kichwa chake, naye akaanza kumshinda, kwa maana nguvu zake zilikuwa zimemwacha.
  • Hana aliweka nadhiri kwamba wembe hautapita kamwe kichwani pa mwanawe1 Sam 1:11
    Aya
    1 Sam 1:11Aliweka nadhili na kusema, “BWANA wa majeshi, kama utalitazama teso la mjakazi wako na kunikumbuka, na usipomsahau mjakazi wako, na kumpatia mjakazi wako mtoto wa kiume, ndipo nitamtoa huyo mtoto kwa BWANA siku zote za maisha yake, na wembe hautapita juu ya kichwa chake kamwe”.
  • Yohana Mbatizaji hakupaswa kamwe kunywa divai wala kileoLk 1:15, Lk 7:33
    Aya
    Lk 1:15Kwa kuwa atakuwa mkuu mbele ya macho ya Bwana. Hatakunywa divai au kinywaji kikali, na atakuwa amejazwa na Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mama yake.
    Lk 7:33Yohana mbatizaji alikuja hakula mkate wala hakunywa divai, na mkasema “Ana pepo.
  • Amosi: Wanadhiri waliinuliwa kutoka kwa vijana wenu, lakini mliwanywesha divaiAmo 2:11–12
    Aya
    Amo 2:11–12Nimewainua manabii kutoka miongoni mwa watoto wanu wawe Wanadhiri kutoka vijana wenu. Je sio hivyo, watu wa Israeli? -hivi ndivyo Yahwe asemavyo. Lakini mmewashawishi Wanadhiri kunywa mvinyo na kuwaamuru manabii wasifanye unabii.

Nadhiri katika Matendo

  • Paulo alinyoa kichwa chake huko Kenkrea kwa sababu ya nadhiriMdo 18:18
    Aya
    Mdo 18:18Paulo, baada ya kukaa pale kwa muda mrefu, aliwaacha ndugu na kwenda kwa meli Siria pamoja na Prisila na Akwila. Kabla ya kuondoka bandarini, alinyoa nywele zake kwani alikuwa ameapa kuwa Mnadhiri.
  • Paulo aliwalipia gharama watu wanne wenye nadhiri ili wanyoe vichwaMdo 21:23–24, Mdo 21:26
    Aya
    Mdo 21:23–24Hivyo fanya kile sisi tunachokuambia sasa: tunao watu wanne ambao wameweka nadhiri. Wachukue watu hawa na ujitakase mwenyewe pamoja nao, na uwalipie gharama zao, ili waweze kunyoa vichwa vyao. Hivyo kila mmoja apate kujua kwamba mambo waliyoambiwa kuhusu wewe ni ya uongo. Watajifunza kwamba wewe pia unafuata sheria.
    Mdo 21:26Ndipo, Paulo aliwatwaa wanaume, na siku ya pili, akajitakasa mwenyewe pamoja nao, akaingia Hekaluni, kutangaza kipindi cha siku za kujitakasa, hadi sadaka itolewa kwa ajili ya kila mmoja wao.

Warekabi

  • Warekabi hawakunywa divai, kama babu yao Yonadabu alivyoagizaYer 35:6, Yer 35:14
    Aya
    Yer 35:6Lakini walisema, “hatutakunywa divai yoyote, kwa maana babu yetu, Yonadabu mwana wa Rekabu, alituamuru, Msinywe divai yoyote, ninyi wala uzao wenu, milele.
    Yer 35:14Maneno ya Yonadabu mwana wa Rekabu aliyowapa wanawe kama amri. wasinywe divai yoyote, yameheshimiwa hadi leo. Wameitii amri ya babu yao. Lakini mimi, nimekuwa nikifanya matangazo kwenu bila kukoma, lakini hamnisikilizi.
  • Hawakujenga nyumba, hawakupanda mbegu, na waliishi katika mahemaYer 35:7
    Aya
    Yer 35:7Pia, msijenge nyumba yoyote, kupanda mbegu zozote, wala kupanda shamba lolote la mizabibu; hivi siyo kwa ajili yenu. Kwa maana lazima muishi katika hema maisha yenu yote, ili kwamba muweze kuishsi siku nyingi katika nchi mnayoishi kama wageni.'

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0