Bible Explorer

Gundua › Mada › Ndoto

Mambo ya kushangaza

Ndoto katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (36), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Mwenye njaa huota anakula, kisha anaamka bado ana njaaIsa 29:8
    Aya
    Isa 29:8Itakuwa kama mtu mwenye njaa anayeota anakula, lakini pindi anapoamka tumbo halina kitu. Itakuwa kama mtu mwenye kiu anayeota anakunywa maji, lakini anapoamka, anazirai, kwa sababu ya kiu na sio kuizima. Ndio, itakavyokuwa idadi kubwa ya wapiganaji dhidi ya Mlima Sayuni.
  • Ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingiMhu 5:3
    Aya
    Mhu 5:3Kama una mambo mengi ya kufanya na kuhangaika, pengine utapata ndoto mbaya. Na pengine utaongea maneno mengi ya upumbavu.
  • Sheria kuhusu mwotaji wa ndoto anayeshawishi kuabudu miungu mingineKum 13:1–5
    Aya
    Kum 13:1–5Kama miongoni mwenu ainuka nabii au muota ndoto, na kama anawapa ishara au maajabu, na kama ishara au maajabu yanatokea, kama alivyozungumza kwenu na kusema, “ Ebu tuifuate miungu mingine, ambayo hatuijui, na tuiabudu. Usisikilize maneno ya nabii huyo, au kwa huyo muota ndoto, kwa kuwa Yahwe Mungu wako anakujaribu kujua kama unampenda Yahwe Mungu wako kwa moyo wako wote na roho yako yote. Mtatembea baada ya Yahwe Mungu wenu, mheshimu, mzishike amri zake, na mtii sauti yake, na mtamwabudu na kushikamana naye. Nabii huyo au muota ndoto atauwawa, kwa sababu amezungumza uasi dhidi ya Yahwe Mungu wenu, ambaye aliwaleta toka nchi ya Misri, na aliyewakomboa kutoka nyumba ya utumwa. Hivyo nabii anataka kuwaondoa katika njia ambayo Yahwe Mungu wenu aliwaamuru kutembea. Kwa hiyo weka mbali maouvu kutoka kwenu.
  • Yeremia kuhusu manabii wanaosema daima, “Nimeota ndoto!”Yer 23:25–28
    Aya
    Yer 23:25–28Nimesikia yale waliyosema manabii, wale waliokuwa wanatabiri uongo kwa jina langu. Wakisema, 'Nilikuwa na ndoto! Nilikuwa na ndoto!' Je, hii itaendelea mpaka lini, manabii wanaotabiri uongo kutoka kwa akili zao, na wanasema nini kutokana na udanganyifu mioyoni mwao? Wana mpango wa kuwafanya watu wangu kusahau jina langu kwa ndoto ambazo wanazoripoti, kila mmoja kwa jirani yake, kama vile babu zao walivyosahau jina langu kwa ajili ya jina la Baali. Nabii aliye na ndoto, aseme ndoto hiyo. Lakini yule ambaye nimemwambia kitu fulani, basi aseme neno langu kwa kweli. Je, majani yanahusiana na nafaka? - hili ni tamko la Bwana-

Ndoto zilizosimuliwa katika Biblia

  • Abimeleki anaonywa katika ndoto kuhusu SaraMwa 20:3
    Aya
    Mwa 20:3Lakini Mungu akamtokea Abimeleki usiku katika ndoto, akamwambia, “Tazama, wewe ni mfu kutokana na mwanamke uliye mchukua, kwa kuwa ni mke wa mtu.”
  • Yakobo anaota ngazi inayofika mbinguniMwa 28:12
    Aya
    Mwa 28:12Akaota na kuona ngazi imewekwa juu ya nchi. Ncha yake ilifika hata mbinguni na malaika wa Mungu walikuwa wakishuka na kupanda juu yake.
  • Yakobo anaota mifugo yenye milia, madoadoa na marakarakaMwa 31:10–13
    Aya
    Mwa 31:10–13Wakati fulani wa majira ya kupandana, niliona katika ndoto mabeberu yaliyowapanda kundi. Mabeberu yalikuwa ya milia, mabaka na madoa. Malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, 'Yakobo.' Nikasema, 'Mimi hapa.' Akasema, 'Inua macho yako uone mabeberu wanaolipanda kundi. Wana milia, madoa na na mabaka, kwani nimeona kila jambo Labani analokutendea. Mimi ni Mungu wa Betheli, mahali ulipoitia nguzo mafuta, mahali uliponitolea nadhiri. Basi sasa inuka na uondoke katika nchi hii na kurudi katika nchi uliyozaliwa.
  • Labani anaonywa katika ndoto asimdhuru YakoboMwa 31:24
    Aya
    Mwa 31:24Basi Mungu akaja kwa Labani Mwarami katika ndoto usiku na kumwambia, “Ujiadhari kumwambia Yakobo jambo lolote liwe jema au baya.”
  • Yusufu anaota miganda ikiinamia mganda wakeMwa 37:5–8
    Aya
    Mwa 37:5–8Yusufu akaota ndoto, na akawambia ndugu zake. Wakamchukia zaidi. Aliwambia, “Tafadhari sikilizeni ndoto hii niliyoiota. Tazama, tulikuwa tukifunga miganda ya nafaka shambani na tazama, mganda wangu ukainuka na kusimama wima, na tazama, miganda yenu ikasogea na kuuinamia mganda wangu” Ndugu zake wakamwambia, “Je ni kweli utatutawala? Je utatutawala juu yetu? Hata wakamchukia zaidi kwa ajili ya ndoto zake na maneno yake.
  • Yusufu anaota jua, mwezi na nyota kumi na moja zikimwinamiaMwa 37:9–10
    Aya
    Mwa 37:9–10Akaota ndoto nyingine na kuwasimulia ndugu zake. Alisema, “Tazama, nimeota ndoto nyingine: Jua na mwezi na nyota kumi na moja ziliniinamia.” Akamwambia baba yake vile vile alivyowambia ndugu zake, na baba yake akamkemea. Akamwambia, Je umeota ndoto ya namna gani hii? Je mama yako na mimi na ndugu zako kweli tutakuja kukuinamia mpaka chini?”
  • Mnyweshaji anaota mzabibu wenye matawi matatuMwa 40:9–13
    Aya
    Mwa 40:9–13Mkuu wa wanyweshaji akamwambia Yusufu ndoto yake. Akamwambia, “Katika ndoto yangu, tazama, kulikuwa na mzabibu mbele yangu. Na kulikuwa na matawi matatu katika mzabibu huo. Ulipochipua, ukachanua maua na kuzaa vichala vya zabibu. Kikombe cha Farao kilikuwa mkononi mwangu. Nikachukua zabibu na kuzikamua katika kikombe cha Farao, na kukiweka kikombe katika mkono wa Farao.” Yusufu akamwambia, “Tafsiri yake ni hii. Yale matawi matatu ni siku tatu. Ndani ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako na kukurudisha katika nafasi yako. Utakiweka kikombe cha Farao katika mkono wake, kama ulivyokuwa ulipokuwa mnyweshaji wake.
  • Mwokaji anaota vikapu vitatu vya mikate kichwani pakeMwa 40:16–19
    Aya
    Mwa 40:16–19Mkuu wa waokaji alipoona kwamba tafsiri ilikuwa ya kuvutia, akamwambia Yusufu, “Mimi pia niliota ndoto, na tazama, vikapu vitatu vya mikate vilikuwa juu ya kichwa changu. Katika kikapu cha juu kulikuwa na kila aina za bidhaa ya kuokwa kwa Farao, lakini ndege wakavila ndani ya kikapu juu ya kichwa changu.” Yusufu akajibu na kusema, “Tafsiri ni hii. Vikapu vitatu ni siku tatu. Ndani ya siku tatu Fareao atakiinua kichwa chako kutoka kwako na atakutundika juu ya mtu. Ndege watakula mwili wako.”
  • Farao anaota ng’ombe saba wanono na saba waliokondaMwa 41:1–4
    Aya
    Mwa 41:1–4Ikawa mwishoni mwa miaka miwili mizima Farao akaota ndoto. Tazama, alikuwa amesimama kando ya Nile. Tazama, ng'ombe saba wakatoka katika mto Nile, wakupendeza na wanene, na wakajilisha katika nyasi. Tazama, ng'ombe wengine saba wakatoka katika Nile baada yao, wasiopendeza na wamekondeana. Wakasimama ukingoni mwa mto kando ya wale ng'ombe wengine. Kisha wale ng'ombe wasiopendeza na waliokonda wakawala wale waliokuwa wanapendeza na walionenepa.
  • Kisha masuke saba manono na saba membambaMwa 41:5–7
    Aya
    Mwa 41:5–7Kisha Farao akaamka. Kisha akalala na kuota mara ya pili. Tazama, masuke saba ya nafaka yalichipua katika mche mmoja, mema na mazuri. Tazama, masuke saba, membamba na yaliyokaushwa na upepo wa mashariki, yakachipua baada yake. Masuke membamba yakayameza yale masuke saba mema yote. Farao akaamka, na, tazama, ilikuwa ni ndoto tu.
  • Mmidiani anaota mkate wa shayiri ukipindua hemaAmu 7:13–14
    Aya
    Amu 7:13–14Gideoni alipofika huko, mtu alikuwa akimwambia mwenzake ndoto. Mtu huyo akasema, “Angalia! Niliota ndoto, na nikaona mkate wa shayiri umeanguka ndani ya kambi ya Midiani. Ukaja hemani, na kuipiga kwa nguvu sana hata ikaanguka chini ikapinduka na kulala chini. ' Mtu mwingine akasema, 'Hii si kitu kingine isipokuwa upanga wa Gideoni (mwana wa Yoashi), Mwisraeli. Mungu amempa ushindi juu ya Midiani na jeshi lake lote. '
  • Huko Gibeoni Sulemani anaomba hekima katika ndoto1 Fal 3:5–15
    Aya
    1 Fal 3:5–15BWANA akaonekana kwa Sulemani huko Gibioni katika ndoto ya usiku; akasema, “Omba! uanataka nikupe nini?” Kwa hiyo Sulemani akasema, “umeonyesha uaminifu wa agano mkuu kwa mtumishi wako, Daudi baba yangu, kwa sababu alitembea mbele yako kwa ukweli na uaminifu, katika haki ya moyo na katika unyofu wa moyo. Umetunza kwa ajili yake hili agano kuu kwa uaminifu na umempa mwana wake kuketi kwenye kiti chake cha enzi leo. Na sasa, BWANA, Mungu wangu, umemfanya mtumishi wako kuwa mfalme katika nafasi ya Daudi baba yangu, japo mimi ni mtoto mdogo. Sijui namna ya kuiingia na kutoka. Mtumishi wako yuko katikati ya watu wako uliowachagua, kundi kubwa, watu wangi wasiohesabika. Kwa hiyo umpe mtumishi wako moyo wa uelewa wa kuwahukumu watu wako. Kwani ni nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi?” Ombi hili la Sulemani likampendeza Bwana. Kwa hiyo Mungu akamwambia. “Kwa sababu umeomba jambo hili na haujajiombea maisha marefu au utajiri au uhai wa maadui wako, lakini umeomba ufahamu wa kutambua hukumu ya haki, Tazama sasa nitafanya yote uliyoniomba wakati uliponipa ombi lako. Ninakupa moyo wa hekima na ufahamu, kwa kuwa hapajawahi kuwa na mtu wa kuwa kama wewe kabla yako, na hakuna wa kuwa kama wewe atakayeinuka baada yako. Pia ninakupa hata ambayo hujaomba, vyote heshima na utajiri, ili kwamba pasije pakawa na mfalme wa kuwa kama wewe katika siku zako zote. Kama utatembea katika njia zangu na kuyatunza maagizo yangu na maagizo yangu, kama alivyofanya baba yako Daudi, ndipo nitakapoziongeza siku zako.” Kisha Sulemani alipoamka, na tazama, ilikuwa ndoto. Akaja Yerusalemu na akasimama mbele ya sanduku na agano la Bwana. Akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, na akawafanyia sherehe watumishi wake wote.
  • Nebukadneza anawataka wenye hekima wamwambie ndoto yenyeweDan 2:1–9
    Aya
    Dan 2:1–9Katika mwaka wa pili wa utawala wa Nebukadneza, alikuwa na ndoto. Akili yake ilisumbuka, na hakuweza kulala. Ndipo mfalme alipowaita waganga na wale wenye kuongea na wafu. Lakini pia aliwaita wachawi na watu wenye hekima. Aliwataka wamwambie juu ya ndoto zake. Basi walikuja na kusimama mbele za mfalme. Mfalme akawambia, “Nilikuwa na ndoto, na akili yangu ina mashaka nataka kujua ndoto hiyo nini maana yake.” Kisha watu wenye hekima wakamwambia mfalme katika Kiaramaiki, “ Mfalme, aishi milele! Twambie sisi ndoto, watumishi wako, nasi tutaifunua maana yake.” Mfalme akawajibu watu wenye hekima, “ Jambo hili limeshamalizika. Kama hamtaweza kuiweka wazi ndoto kwangu na kuitafsiri, miili yenu itakatwa vipande vipande na nyumba zenu zitafanywa kuwa vichuguu vya uchafu. Lakini kama mtaniambia ndoto na maana yake, mtapokea zawadi kutoka kwangu, thawabu, na heshima kubwa. Basi niambie ndoto na maana yake.” Wakamjibu tena na kusema, “Mfalme na atuambie, watumishi wake, ndoto nasi tukwambia maana yake.” Mfalme akawajibu, “ Ninajua kwa hakika mnahitaji muda zaidi kwasababu mmeona maamuzi yangu ni magumu kuhusu jambo hili. Lakini kama hamtaweza kuniambia ndoto, kuna sentensi moja tu kwa ajili yenu. Mmeamua kuandaa uongo na maneno ya kudanganya ambayo mmekubaliana kwa pamoja kuniambia mpaka pale nitakapobadili akili zangu. Basi, niambieni ndoto, na kisha nitajua kuwa mnaweza kuitafsiri kwa ajili yangu.”
  • Ndoto yake ya sanamu kubwa ya dhahabu, fedha, shaba, chuma na udongoDan 2:31–35
    Aya
    Dan 2:31–35Mfalme, uliangalia juu na ukaona sanamu kubwa. Sanamu hii ambayo ilikuwa yenye nguvu na yenye kung'aa, ilisimama mbele yako. Mng'ao wake ulikuwa unatisha. Kichwa cha sanamu kilikuwa kimetengenezwa kwa dhahabu safi. Matiti yake na mikono ilikuwa ya fedha. Sehemu ya katikati na mapaja yake yalikuwa yametengenezwa kwa shaba, na miguu yake ilikuwa imetengenezwa kwa chuma. Miguu yake ilikuwa ilitengenezwa kwa sehemu chuma na sehemu kwa udongo. Ulitazama juu, na jiwe lilikuwa limechongwa, ingawa si kwa mikono ya wanadamu, na liliipiga sanamu katika miguu yake ya chuma na udongo, na ponda ponda. Kisha chuma, udongo, fedha, na dhahabu zilivunjwa katika vipande vipande kwa wakati mmoja na yakawa kama makapi yaliyo katika sakafu za kupuria kipindi cha kiangazi. Upepo huyapeperushia mbali na hakuna alama inayoachwa. Lakini jiwe lililoipiga sanammu likawa mlima mkubwa na kuijaza dunia yote.
  • Ndoto yake ya mti mkubwa uliokatwaDan 4:10–17
    Aya
    Dan 4:10–17Haya ndiyo niliyoyaona katika akili zangu nilipokuwa nimejilaza katika kitanda changu: Nilitazama, na kulikuwa na mti katikati ya dunia, na urefu wake ulikuwa ni mkubwa sana. Mti ulikua na ukawa wenye nguvu. Na sehemu ya juu yake ilifika mbinguni, uliweza kuonekana kutoka miisho ya dunia yote. Majani yake yalikuwa mazuri, matunda yake yalikuwa ni mengi, na juu yake kulikuwa na chakula kwa ajili ya wote. Wanyama wa mwituni walipata kivuli chini yake, na ndege wa angani waliisha katika matawi yake. Viumbe vyote hai vililishwa katika mti huo. Nilipokuwa nimelala kitandani kwangu, niliona katika akili zangu, mjumbe mtakatifu alishuka kutoka mbinguni. Alipiga kelele na kusema, 'Ukateni mti na yafyekeni matawi yake, yapukutisheni majani yake, na kuyasambaza matunda yake. Wanyama na wakimbie kutoka chini yake na ndege wapae mbali kutoka katika matawi yake. Mkiache kisiki cha mizizi yake katika nchi, mkifunge na fungu la chuma na shaba, katikati ya mche mororo wa shambani. Na kilowanishwe na umande wa kutoka mbinguni. Kiacheni kiishi na wanyama kati ya mimea ya ardhini. Akili yake na ibadilishwe kutoka akili ya kibinadamu, na apewe akili ya mnyama mpaka ipite miaka saba. Uamuzi huu ni kutokana na amri iliyotolewa na mjumbe. Ni uamuzi uliofanya na yeye aliye mtakatifu ili kwamba hao walio hai wajue kwamba Mungu aliye juu sana anatawala juu ya falme za watu na huwapa kwa kila mmoja apendaye kumweka juu yao, hata kwa watu wale wanyenyekevu sana.'
  • Danieli anaandika ndoto ya wanyama wanneDan 7:1–3
    Aya
    Dan 7:1–3Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza mfalme wa Babelli, Danieli alikuwa na ndoto na maono katika akili zake wakati alipokuwa amelala kitandani kwake. Kisha akayaandika yale aliyoyaona katika ndoto. Aliandika matukio ya muhimu sana: Danieli alieleza, “Usiku katika ndoto zangu niliona pepo nne za mbinguni zilikuwa zinaitikisa bahari kuu. Wanyama wakubwa wanne, kila mmoja alikuwa tofauti na mwenzake, walitoka katika bahari.
  • Yusufu anaambiwa katika ndoto amchukue Mariamu kuwa mke wakeMt 1:20–21
    Aya
    Mt 1:20–21Alipokuwa akifikiri juu ya mambo haya, Malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema,'' Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu kama mkeo, kwa sababu mimba aliyonayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Atajifungua mtoto wa kiume na utamwita jina lake Yesu, kwa maana atawaokoa watu wake na dhambi zao.''
  • Wasomi wa mashariki wanaonywa katika ndoto wasirudi kwa HerodeMt 2:12
    Aya
    Mt 2:12Mungu aliwaonya katika ndoto wasirudi kwa Herode, hivyo, waliondoka kurudi katika nchi yao kwa njia nyingine.
  • Yusufu anaambiwa katika ndoto akimbilie Misri, kisha arudiMt 2:13, Mt 2:19–22
    Aya
    Mt 2:13Baada ya kuwa wameondoka, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto na kusema, “Inuka, mchukue mtoto na mama yake na mkimbilie Misri. Bakini huko mpaka nitakapowaambia, kwa kuwa Herode atamtafuta mtoto ili amwangamize.
    Mt 2:19–22Herode alipo kufa, tazama malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri na kusema, “Inuka mchukue mtoto na mama yake, na mwende katika nchi ya Israeli kwa maana waliokuwa wakitafuta uhai wa mtoto wamekufa.” Yusufu aliinuka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, na wakaja katika nchi ya Israeli. Lakini aliposikia kuwa Arikelau alikuwa anatawala Yuda mahali pa baba yake Herode, aliogopa kwenda huko. Baada ya Mungu kumuonya katika ndoto, aliondoka kwenda mkoa wa Galilaya
  • Mke wa Pilato anateseka katika ndoto kwa sababu ya YesuMt 27:19
    Aya
    Mt 27:19Wakati alipokuwa akiketi kwenye kiti chake cha hukumu, mke wake alimtumia neno na kusema, “Usitende jambo lolote kwa mtu huyo asiye na hatia. Kwani nimeteswa mno hata leo katika ndoto kwa sababu yake.”

Maono ya usiku

  • Mungu anamwambia Yakobo usiku kuhusu kushuka kwenda MisriMwa 46:2–4
    Aya
    Mwa 46:2–4Mungu akamwambia Israeli katika ndoto usiku, akisema, “Yakobo, Yakobo.” Akasema, “Mimi hapa.” Akasema, “Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako. Usiogope kushuka Misri, kwa maana nitakufanya taifa kubwa huko. Nitakwenda pamoja nawe huko Misri, Nami nitakupandisha huku tena bila shaka. Na Yusufu akayafunika macho yako kwa mikono wake.”
  • Elifazi anasikia mnong’ono katika maono ya usikuAyu 4:12–16
    Aya
    Ayu 4:12–16Sasa nililetewa kwangu jambo fulani kisiri, na sikio langu likapokea uvumi kuhusu hilo. Kisha yakaja mawazo kupitia ndoto wakati wa usiku, wakati uwaangukiwapo usingizi mzito watu.. Ilikuwa usiku wakati nilipopatwa hofu na kutetemeka, na mifupa yangu yote ikatikisika. Kisha nafsi ikapita mbele ya uso wangu, na nywele zangu za mwili zilisimama. Nafsi ilisimama kimya, lakini sikuweza kupambanua sura yake. Umbo lilikuwa mbele ya macho yangu; kulikuwa kimya, nami nikasikia sauti ikisema,
  • Paulo anamwona mtu wa Makedonia akiita, “Vuka uje utusaidie”Mdo 16:9
    Aya
    Mdo 16:9Maono yalimtokea Paulo usiku, kulikuwa na mtu wa Makedonia amesimama, akimwita na kusema “Njoni mtusaidie huku Makedonia”.
  • Katika dhoruba malaika anamwambia Paulo kwamba wote melini wataishiMdo 27:23–24
    Aya
    Mdo 27:23–24Kwa sababu usiku uliopita malaika wa Mungu, ambaye huyo Mungu mimi ni wake, na ambaye ninamwabudu pia - malaika wake alisimama pembeni mwangu na kusema, “Usiogope Paulo. Lazima usimame mbele ya Kaisari, na tazama, Mungu katika wema wake amekupa hawa wote ambao wanasafiri pamoja nawe.

Wafasiri

  • Yusufu anafasiri ndoto za mnyweshaji na mwokajiMwa 40:8, Mwa 40:12–13, Mwa 40:18–19
    Aya
    Mwa 40:8Wakamwambia, Sisi wote tumeota ndoto na hakuna wakuitafsiri.” Yusufu akawambia, “Je tafsiri haitoki kwa Mungu? Niambieni, tafadhari.”
    Mwa 40:12–13Yusufu akamwambia, “Tafsiri yake ni hii. Yale matawi matatu ni siku tatu. Ndani ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako na kukurudisha katika nafasi yako. Utakiweka kikombe cha Farao katika mkono wake, kama ulivyokuwa ulipokuwa mnyweshaji wake.
    Mwa 40:18–19Yusufu akajibu na kusema, “Tafsiri ni hii. Vikapu vitatu ni siku tatu. Ndani ya siku tatu Fareao atakiinua kichwa chako kutoka kwako na atakutundika juu ya mtu. Ndege watakula mwili wako.”
  • Yusufu anafasiri ndoto za Farao: miaka saba ya shibe, saba ya njaaMwa 41:25–32
    Aya
    Mwa 41:25–32Yusufu akamwambia Farao, “Ndoto za Farao ni moja. Mungu amemwambia Farao kuhusu jambo analokwenda kulifanya. Wale ng'ombe saba wema ni miaka saba, na masuke saba mema ni miaka saba. Ndoto ni moja. Na wale ng'ombe saba wembamba na wabaya waliokuja baadaye ni miaka saba, na pia masuke saba membamba yaliyokaushwa na upepo wa mashariki itakuwa miaka saba ya njaa. Hilo ni jambo nililomwambia Farao. Mungu amemfunulia Farao jambo analokwenda kulifanya. Tazama, miaka saba yenye utele mwingi inakuja katika nchi yote ya Misri. Na miaka saba ya njaa itakuja baada yake, na utele wote katika nchi ya Misri utasahaulika, na njaa itaiaribu nchi. Utele hautakumbukwa katika nchi kwa sababu ya njaa itakayofuata, kwa kuwa itakuwa kali sana. Kwamb ndoto ilijirudia kwa Farao sababu ni kwamba jambo hili limeanzishwa na Mungu, na Mungu atalitimiza hivi karibuni.
  • Danieli anamwambia Nebukadneza ndoto yake, kisha anaifasiriDan 2:27–30, Dan 2:36, Dan 4:19–24
    Aya
    Dan 2:27–30Danieli alimjibu mfalme na kusema, “Siri ambayo mfalme ameiomba haiwezi kufunuliwa na watu wenye hekima, wala wale wenye kuongea na wafu, wala wachawi, na wala wataalamu wa nyota. Isipokuwa kuna Mungu ambaye anaishi mbinguni, ambaye hufunua siri, na amekwisha kukujulisha wewe, mfalme Nebukadneza, kile kitakachotokea katika siku zijazo. Hizi ndizo Ndoto na maono ya akili zako uliyoyaona wakati ulipokuwa umelala kitandani mwako. Na kwako Wewe, mfalme, mawazo yako kitandani mwako yalikuwa ni juu ya mambo yajayo, na yule afichuaye siri ameifanya ijulikane kwako kuhusu kile kilicho karibu kutokea. Na kuhusu mimi, siri hii haikufunuliwa kwangu kwa sababu ya hekima yoyote niliyo nayo zaidi ya mtu yoyote anayeishi. Siri hii imefunliwa kwangu ili kwamba wewe, mfalme, uweze kufahamu maana, na ili kwamba ujuwe mawazo yaliyo ndani mwako.
    Dan 2:36Hii ndiyo ilikuwa ndotoyako. Na sasa tutamwambia mfalme maana yake.
    Dan 4:19–24Ndipo Danieli aliyeitwa pia Belteshaza, alihuzunishwa kwa muda, na mawazo yake yalimshitua. Mfalme akasema, “ Belteshaza, usifadhaishwe na ndoto au tafsiri yake.” Belteshaza akajibu, “ Bwana wangu, ndoto hii na iwe kwa ajili ya watu wanaokuchukia, na tafsiri yake na iwe kwa ajili ya adui zako. Mti ule uliouona - uliokua na ukawa na wenye nguvu, na ambao sehemu yake ya juu ilifika hata mbinguni, na ambao waweza kuonekana kutoka miisho ya dunia yote - ambao majani yake ni mazuri, na matunda yake yalikuwa ni mengi, ili kwamba ndani yake kulikuwa na chakula cha wote, na chini yake wanyama wa mwituni walipata kivuli, na ndani yake ndege wa angani waliishi - huu mti ni wewe, mfalme, wewe uliyekua na kuwa na nguvu. Ukuu wako umeongezeka na kufika mbinguni, na mamlaka yako yamefika hata miisho ya dunia. Ewe mfalme, ulimwona mjumbe akishuka kutoka mbinguni na akisema, “Ukateni mti na uteketezeni, lakni kiacheni kisiki cha mizizi yake katika nchi, kifungeni kwa ukanda wa chuma na shaba, katikati ya mche mororo katika shamba. Na kilowanishwe na umande kutoka mbinguni. Kiache kiishi katika wanyama wa mwituni katika mashamba mpaka ipite miaka saba.' Mfalme, hii ni tafsiri yake. Ni agizo la Yeye Aliye Juu ambalo limekufikia, bwana wangu mfalme.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0