Bible Explorer

Gundua › Mada › Visima

Mambo ya kushangaza

Visima katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (20), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Hajiri aliona kisima akampa kijana maji anyweMwa 21:19
    Aya
    Mwa 21:19Kisha Mungu akayafunua macho ya Hajiri, natazama akaona kisima cha maji. Akaenda akajaza kiriba maji, na akampatia kijana akanywa.
  • Abraham alitoa wana-kondoo saba kuthibitisha kwamba alichimba kisima cha BeerishebaMwa 21:25–31
    Aya
    Mwa 21:25–31Abraham pia akamlalamikia Abimeleki kuhusu kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki wamekinyang'anya. Abimeleki akasema, “Sijui ni nani amefanya jambo hili. Hukuniambia mapema; na sijalisikia ila leo hii.” Kwa hiyo Abraham akachukua kondoo na ng'ombe maksai akampatia Abimeleki, na wawili hawa wakafanya agano. Kisha Abraham akatenga wanakondoo wa kike saba pekeyao. Abimeleki akamwambia Abraham, “Nini maana ya hawa wanakondoo wa kike saba ambao umewatenga pekeyao?” Akajibu, “Hawa wanakondoo wa kike saba utawapokea kutoka mkonono mwangu, ili kwamba uwe ushahidi kwangu, kuwa nichimba kisima hiki.” Kwa hiyo akaita mahali pale Beerisheba, kwa sababu mahali pale wote wawili wali apa kiapo.
  • Wafilisti walifukia visima vya Abraham; Isaka akavichimbua tenaMwa 26:15, Mwa 26:18
    Aya
    Mwa 26:15Basi visima vyote watumishi wa baba yake walikuwawamevichimba katika siku za Ibrahimu baba yake, Wafilisiti wakavikatalia kwa kwa kuvijaza kifusi.
    Mwa 26:18Kwa mara nyingine tena Isaka akachimba visima vya maji, vilivyokuwa vimechimbwa siku za Ibrahimu baba yake. Wafilisiti walikuwa wamevizuia baada ya kufa kwake Ibrahimu. Isaka akaviita visima kwa majina aliyokuwa ameviita baba yake.
  • Ugomvi juu ya visima: Eseki, Sitina, kisha RehobothiMwa 26:20–22
    Aya
    Mwa 26:20–22Wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaka, na kusema, “Haya ni maji yetu.”Hivyo Isaka akakiita kisima hicho “Eseki,” kwa sababu waligombana naye. Wakachimba kisima kingine, wakakigombania hicho nacho, hivyo akakiita “Sitina.” Akatoka hapo na akachimba kisima kingine, lakini hicho hawakukigombania. Hivyo akakiita Rehobothi, na akasema, “Sasa Yahwe ametufanyia nafasi, na tutafanikiwa katika nchi.”
  • Watumishi wa Isaka walipata maji: Shiba, BeerishebaMwa 26:32–33
    Aya
    Mwa 26:32–33Siku hiyohiyo watumishi wake wakaja na kumwambia juu ya kisima walichokuwa wamekichimba. Wakasema, “Tumeona maji.” Akakiita kile kisima Shiba, hivyo jina la mji ule ni Beersheba hata leo.
  • Kisima kilichoitwa BeerlahairoriMwa 16:14
    Aya
    Mwa 16:14Kwa hiyo kisima kiliitwa Beerlahairori; Tazama, kiko kati ya Kadeshi na Beredi.
  • Rebeka alikuja chemchemini na mtungi wakeMwa 24:16
    Aya
    Mwa 24:16Msichana huyu alikuwa mzuri na alikuwa bikira. Hapana mwanaume aliye kuwa amekwisha lala naye. Akashuka kisimani na kuujaza mtungi wake, na kupanda juu.
  • Jiwe kubwa lilifunika mdomo wa kisima huko HaraniMwa 29:2–3
    Aya
    Mwa 29:2–3Hata alipotazama, akaona kisima kondeni, na, tazama, makundi matatu ya kondoo yalikuwa yamelala kando yake. Kwani kutoka katika hicho wangeyanywesha makundi, na jiwe juu ya mdomo wa kisima lilikuwa kubwa. Wakati makundi yote yangekusanyika pale, wachungaji wangevingirisha jiwe kutoka katika mdomo wa kisima na kuwanywesha kondoo, na kisha kurudisha jiwe juu ya mdomo wa kisima, mahali pake.
  • Yakobo alivingirisha jiwe na kunywesha kundi la RaheliMwa 29:10
    Aya
    Mwa 29:10Yakobo alipomwona Raheli, binti wa Labani, kaka wa mamaye, na kondoo wa Labani, kaka wa mama yake, Yakobo akaja juu, akalivingirisha jiwe kutoka mlangoni mwa kisima, na akawanywesha kondoo wa Labani, kaka wa mama yake.
  • Musa aliketi kando ya kisima huko Midiani na kuwasaidia dada sabaKut 2:15–17
    Aya
    Kut 2:15–17Farao aliposikia habari hizi, alijaribu kumuua Musa. Lakini Musa alikimbia na kwenda kuishi katika nchi ya Wamidiani. Kule alikaa chini kando ya mto. Wakati huo kuhani wa Midiani alikuwa na mabinti saba. Walikuja mtoni kuchota maji na kujaza vyombo vyao ili wawanyweshe mifuko ya baba yao. Wachungaji walikuja na kutaka kuwafukuza, lakini Musa alienda kuwasaidia. Kisha akawanywesha mifugo wao.
  • Israeli waliimbia kisima: “Bubujika, ewe kisima!”Hesabu 21:16–18
    Aya
    Hesabu 21:16–18Kutoka pale wakasafiri mpaka Beeri, hapo ndipo palipo na kisima ambacho Bwana alimwambia Musa, “Wakusanye watu kwa ajili yangu ili uwape maji,” Ndipo Israeli waipoimba wimbo huu: “enyi visima, yajazeni maji. Imbeni juu ya kisima hiki. Kisima ambacho viongozi wetu walichimba, kisima ambacho wenye hekima walichimba kwa fimbo ya kifalme na kwa fimbo ya kutembelea.” Kisha kutoka jangwani walitembea mpaka Matanaha.
  • Nchi ya ahadi ilikuwa na visima ambavyo hawakuchimbaKum 6:11
    Aya
    Kum 6:11na nyumba zilizojaa kila aina ya vitu vizuri ambavyo hamkuzifanya, visima ambavyo hamkuvichimba, mashamba na miti ya mizeituni ambayo hamkuipanda, mtakula na kutosheka-
  • Wapelelezi wa Daudi walijificha ndani ya kisima huko Bahurimu2 Sam 17:18–19
    Aya
    2 Sam 17:18–19Lakini kijana mmoja akawaoni mara akamwambia Absalomu. Hivyo Yonathani na Ahimaasi wakaenda kwa haraka na wakaingia katika nyumba ya mtu mmoja huko Bahurimu, aliyekuwa na kisima katika ua wake wakaingia humo. Mke wa mtu huyo akachukua kifuniko na kukikufunika kwenye mlango wa kisima kisha akaanika nafaka juu yake, hivyo hakuna aliyejua kwamba Yonathani na Ahimaasi walikuwa kisimani.
  • Mashujaa watatu walimletea Daudi maji kutoka kisima cha Bethlehemu2 Sam 23:15–16
    Aya
    2 Sam 23:15–16Daudi alitamani maji na akasema, “Kama ingekuwa mtu mmoja angenipa maji ya kunywa kutoka kisima kilichopo Bethlehemu, kisima kilichopo langoni!” Hivyo mashujaa hawa watatu wakapita kati ya jeshi la Wafilisti na kuchota maji katika kisima cha Bethlehemu, kilichopo langoni. Wakachukua maji na kuyaleta kwa Daudi, lakini yeye akakataa kuyanywa. Badala yake akayamwaga mbele za Yahwe.
  • Uzia alichimba mabirika mengi kwa ajili ya mifugo yake2 Nya 26:10
    Aya
    2 Nya 26:10Akajenga minara ya ulinzi katika nyika na akachimba mabwawa, kwa maana alikuwa na ng'ombe wengi, katika visiwa vya chini na katika nchi tambarare. Alikuwa na wakulima na wapandaji wa zabibu katika mwinuko wa nchi na katika mashamba yenye rutuba, kwa maana alipenda kulima.
  • Yusufu alitupwa katika shimo tupu lisilo na majiMwa 37:24
    Aya
    Mwa 37:24Wakamchukua na kumtupa shimoni. Shimo lilikuwa tupu bila maji.
  • Yeremia alizama katika matope ya birika lisilo na majiYer 38:6
    Aya
    Yer 38:6Kisha walimchukua Yeremia na kumtupa kwenye kisima cha Malkiya, mwana wa mfalme. Kisima kilikuwa kwenye uwanja wa mlinzi. Walimshusha Yeremia chini kwa kamba. Hapakuwa na maji kwenye kisima, lakini kulikuwa na matope, na alizama chini ya matope.
  • Yesu aliketi kando ya kisima cha Yakobo yapata saa sitaYn 4:6
    Aya
    Yn 4:6Na kisima cha Yakobo kilikuwa hapo. Yesu alikuwa amechoka kwa ajili ya safari na akakaa karibu na kisima. Ilikuwa muda wa mchana.
  • Mwanamke: huna chombo cha kutekea, na kisima ni kirefuYn 4:11
    Aya
    Yn 4:11Mwanamke akajibu, “Bwana hauna ndoo ya kuchotea, na kisima ni kirefu. Utayapata wapi Maji ya Uzima.?

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0