Bible Explorer

Gundua › Mada › Hesabu arobaini

Mambo ya kushangaza

Hesabu arobaini katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (31), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

Siku arobaini

  • Mvua ilinyesha juu ya nchi siku arobaini mchana na usikuMwa 7:4, Mwa 7:12, Mwa 7:17
    Aya
    Mwa 7:4Kwa kuwa ndani ya siku saba nitasababisha mvua kunyesha juu ya nchi muda wa siku arobaini mchana na usiku. Nitaharibu kila kiumbe hai nilichokiumba juu ya uso wa ardhi.”
    Mwa 7:12Mvua ikaanza kunyesha juu ya nchi kwa siku arobaini mchana na usiku.
    Mwa 7:17Kisha gharika ikaja juu ya nchi kwa siku arobaini, na maji yakaongezeka na kuinua safina juu ya nchi.
  • Baada ya siku arobaini Nuhu alifungua dirisha la safinaMwa 8:6
    Aya
    Mwa 8:6Ikatokea kwamba baada ya siku arobaini Nuhu alifungua dirisha la safina ambayo aliitengeneza.
  • Kumpaka Yakobo dawa kulichukua siku arobainiMwa 50:3
    Aya
    Mwa 50:3Wakatimiza siku arobain, kwani huo ndio uliokuwa muda kamili wa kutia dawa. Wamisri wakamlilia kwa siku sabini
  • Musa alikaa mlimani siku arobaini mchana na usikuKut 24:18, Kut 34:28, Kum 9:9
    Aya
    Kut 24:18Musa akaingia kwenye wingu na kwenda juu ya mlima. Alikuwa mlimani siku arobaini na usiku arobaini.
    Kut 34:28Musa alikuwa huko na Yahweh kwa siku arobaini na usiku; hakula chakula chochote wala kunywa maji yeyote. Aliandika katika mbao maneno ya agano, Amri kumi.
    Kum 9:9Wakati nilipoenda juu ya mlima kupokea mbao za mawe, mbao za agano ambalo Yahwe alifanya nanyi, Nilibaki kwenye mlima kwa siku arobaini na usiku arobaini; Wala sikula mkate wala kunywa maji.
  • Wapelelezi walirudi baada ya siku arobainiHesabu 13:25
    Aya
    Hesabu 13:25Baada ya siku arobaini, wakarudi kutoka kuipeleleza nchi.
  • Goliathi alijitokeza kwa siku arobaini, asubuhi na jioni1 Sam 17:16
    Aya
    1 Sam 17:16Kwa muda wa siku arobaini yule Mfilisti mwenye nguvu alikuwa akijitokeza asubuhi na jioni kwa ajili ya vita.
  • Eliya alitembea siku arobaini mchana na usiku hadi Horebu1 Fal 19:8
    Aya
    1 Fal 19:8Kwa hiyo akainuka na kula na kunywa, naye akasafiri kwa nguvu ya chakula hicho kwa siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu.
  • Yona: siku arobaini zaidi na Ninawi utaangamizwaYon 3:4
    Aya
    Yon 3:4Yona akaanza kuingia ndani ya mji, na baada ya safari ya siku, akapaza sauti, akasema, “Katika siku arobaini Ninawi itaangamizwa.”
  • Yesu alifunga siku arobaini mchana na usikuMt 4:2
    Aya
    Mt 4:2Alipokuwa amefunga kwa siku arobaini mchana na usiku alipata njaa.
  • Baada ya kufufuka, Yesu alionekana kwa muda wa siku arobainiMdo 1:3
    Aya
    Mdo 1:3Baada ya mateso yake, Yeye alionekana kwao akiwa hai pia na vithibitisho vingi vikishuhudia. Kwa siku arobaini alijidhihirisha kwao, na alizungumza kuhusu ufalme wa Mungu.

Miaka arobaini

  • Israeli walikula manna miaka arobaini jangwaniKut 16:35
    Aya
    Kut 16:35Watu wa Israeli walikula manna miaka arobaini mpaka walipo kuja nchi yenye watu. Walikula mpaka walipo fika kwenye mipaka ya nchi ya Kanani.
  • Miaka arobaini ya kutangatanga, mwaka mmoja kwa kila siku ya upeleleziHesabu 14:34
    Aya
    Hesabu 14:34Kama vile ilivyo hesabu ya siku ambayo mliipeleleza nchi—siku arobaini, vivyo hivyo mtabeba madhara ya dhambi zenu kwa muda wa miaka arobaini—mwaka mmoja kwa kila siku moja, na mtajua kuwa ni sawa na kuwa adui yangu.
  • Isaka alimwoa Rebeka akiwa na miaka arobainiMwa 25:20
    Aya
    Mwa 25:20Isaka alikuwa na umri wa miaka arobaini alipomuoa Rebeka, binti wa ethueli Mshami wa Padani Aramu, ndugu wa Labani Mshami.
  • Musa alikuwa na miaka arobaini alipowatembelea watu wake; arobaini baadaye, kichakaMdo 7:23, Mdo 7:30
    Aya
    Mdo 7:23Lakini baada ya kutimiza miaka arobaini, ikamjia katika moyo wake kuwatembelea ndugu zake, wana wa Israeli.
    Mdo 7:30Baada ya miaka arobaini kupita, malaika akamtokea katika jangwa la mlima Sinai, katika mwali wa moto ndani ya kichaka.
  • Chini ya waamuzi kadhaa nchi ilipumzika miaka arobainiAmu 3:11, Amu 5:31, Amu 8:28
    Aya
    Amu 3:11Nchi ilikuwa na amani kwa miaka arobaini. Ndipo Otinieli mwana wa Kenazi akafa.
    Amu 5:31Naam, adui zako wote wataangamia, Ee Bwana! Lakini marafiki zako watakuwa kama jua wakati linapoongezeka kwa uwezo wake. Na nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini.
    Amu 8:28Kwa hiyo Midiani ilishindwa mbele ya watu wa Israeli na hawakuinua vichwa vyao tena. Na nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini siku za Gideoni.
  • Wafilisti walitawala Israeli miaka arobainiAmu 13:1
    Aya
    Amu 13:1Watu wa Israeli wakafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, naye akawatia mikononi mwa Wafilisti kwa miaka arobaini.
  • Eli aliwaamua Israeli miaka arobaini1 Sam 4:18
    Aya
    1 Sam 4:18Alipotamka sanduku la Mungu, Eli alianguka chali kutoka kwenye kiti chake karibu na mlango. akavunjika shingo lake, na kufariki, kwa sababu alikuwa mzee tena mzito. Naye alikuwa mwamuzi wa Israeli kwa miaka arobaini.
  • Miaka arobaini chini ya Sauli, asema PauloMdo 13:21
    Aya
    Mdo 13:21Baada ya haya, watu waliomba mfalme, hivyo Mungu aliwapa Sauli mwana wa Kishi, mtu wa kabila la Benjamini, kuwa mfalme kwa miaka arobaini.
  • Daudi alitawala miaka arobaini: saba Hebroni, thelathini na tatu Yerusalemu2 Sam 5:4, 1 Fal 2:11
    Aya
    2 Sam 5:4Daudi alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza kutawala, naye akatawala miaka arobaini.
    1 Fal 2:11Siku ambazo Daudi alitwala Israeli zilikuwani miaka arobaini. Alikuwa ametawala kwa miaka saba kule Hebroni na kwa miaka thelethini na tatu kule Yerusalemu.
  • Sulemani alitawala miaka arobaini1 Fal 11:42
    Aya
    1 Fal 11:42Sulemani? Sulemani alitawala Yerusalemu juu ya Israeli yote kwa miaka arobaini.
  • Yoashi alitawala Yerusalemu miaka arobaini2 Fal 12:1
    Aya
    2 Fal 12:1Katika mwaka wa saba wa Yehu, utawala wa Yoashi ulianza; alitawala kwa mda wa miaka arobaini huko Yerusalimu. Mama yake alikuwa anaitwa Sibia, wa Beersheba.

Viboko arobaini

  • Sheria haikuruhusu zaidi ya viboko arobainiKum 25:3
    Aya
    Kum 25:3Muamuzi anaweza kumpatia mapigo arobaini, lakini hapaswi kuvuka idadi hiyo; kwa maana akivuka idadi hiyo na kumpiga kwa mapigo mengi zaidi, basi Muisraeli mwenzako atakuwa kaaibishwa mbele ya macho yenu.
  • Paulo alipigwa mara tano viboko arobaini kasoro kimoja2 Kor 11:24
    Aya
    2 Kor 11:24Kutoka kwa Wayahudi nimepokea mara tano “mapigo arobaini kutoa moja.”

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0