Mambo ya kushangaza
Barabara katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (15), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
- Israeli waliomba kupita katika njia kuu ya mfalme kupitia EdomuHesabu 20:17–19
Aya
Hesabu 20:17–19Tunakuomba uturuhusu kupita katika nchi yako. Hatutapita mashambani wala kwenye mashamba ya mizabibu, wala hatutakunywa maji ya visima vyako. Tutapita kwenye njia kuu ya mfalme. Hatutageuka upande wa kulia wala upande wa kushoto mpaka tutakapopita mpaka wako.” Lakini mfalme wa Edomu akamjibu, “Msipite hapa. Kama mtafanya hivyo, Nitakuja na upanga kukuvamia.” Ndipo wana wa Israeli wakamwambia,”tutapitia njia kuu. Kama sisi au wanyama wetu watakunywa maji yako, basi tutalipa. Tunaomba uturuhusu tupite tukitembea kwa miguu yetu, bila kufanya jambo lolote lile.”
- Ombi lilo hilo kwa Sihoni wa WaamoriHesabu 21:22, Kum 2:27
Aya
Hesabu 21:22Tunaomba tupite katika nchi yako. hatutapita katika shamba au kwenye shamba la mizabibu. Hatutakunywa maji ya visima vyako. Tutapita katika njia kuu ya mfalme mpaka tutakapopita mpaka wako.”
Kum 2:27Hebu nipite katika nchi yako; nitapita kwenye barabara kuu, sitageuka mkono wa kulia wala kushoto.
- Barabara zilitengenezwa kwenda miji ya makimbilioKum 19:3
Aya
Kum 19:3Mnapaswa kujenga barabara na kugawa mipaka ya nchi yenu katika maeneo matatu, nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anafanya kuimiliki, ili kwamba kila mmoja anayeua mtu mwingine apate kukimbia hapo.
- Raheli alizikwa njiani kwenda EfrathiMwa 35:19
Aya
Mwa 35:19Raheli akafa na kuzikwa katika njia iendayo Efrathi (ndio Bethlehemu).
- Yoshua aliwafuatia adui kwenye mpando wa Bethi HoroniYos 10:10
Aya
Yos 10:10Na Yahweh alichanganya maadui mbele za Israeli - ambao waliwaua mauaji makubwa mno huko Gibeoni, na wale waliowafuata njiani iendayo Bethi Horoni, nao waliuwaua katika njia iendayo Azeka na Makeda.
- Siku za Shamgari barabara kuu zilikuwa hazina watuAmu 5:6
Aya
Amu 5:6Katika siku za Shamgari (mwana wa Anathi), katika siku za Jael, barabara kuu ziliachwa, na wale ambao walitembea tu walitumia njia za upepo.
- Shilo, mashariki mwa barabara kutoka Betheli kwenda ShekemuAmu 21:19
Aya
Amu 21:19Wakasema, “Mnajua kuwa kuna sikukuu kwa Bwana kila mwaka huko Shilo (ambayo ni kaskazini ya Betheli, mashariki ya barabara inayopanda kutoka Betheli hadi Shekemu, na kusini mwa Lebona).
- Ng’ombe walivuta sanduku moja kwa moja barabarani kwenda Bethi Shemeshi1 Sam 6:12
Aya
1 Sam 6:12Hao ng'ombe waliondoka moja kwa moja kuelekea Beth Shemeshi. Walikwenda kwa kuifuata nija moja kuu, wakiteremka walipokuwa wakienda, na hwakugeuka upande wa kushoto au kulia. Viongozi wa Wafilisti walifuata kwa nyuma hadi mpaka wa Beth Shemeshi.
- Njia ya kwenda uwanja wa Dobi karibu na mferejiIsa 7:3
Aya
Isa 7:3Ndipo Yahwe akamwambia Isaya, ''Nenda nje na kijana wako, Sheari Jashubu ukaonane na Ahazi mwisho wa mfereji wa birika la juu, katika njia kuu ya uwanja Dobi.
- Mtu aliyeshuka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko aliangukia kati ya wanyang’anyiLk 10:30–31
Aya
Lk 10:30–31Yesu akijibu akasema, “Mtu fulani alikuwa akitelemka kutoka Yerusalem kwenda Yeriko. Akaangukia kati ya wanyang'anyi, waliomnyang'anya mali yake, na kumpiga na kumuacha karibu akiwa nusu mfu.. Kwa bahati kuhani fulani alikuwa akishuka katika njia hiyo, alipo muona alipita upande mwingine.
- Batimayo aliketi kando ya barabara akitoka YerikoMk 10:46
Aya
Mk 10:46Wakaja Yeriko. Alipokuwa akiondoka Yeriko na wanafunzi wake na kundi kubwa, mwana wa Timayo, Batimayo, kipofu mwombaji, alikaa kando ya barabara.
- Emmau, karibu maili saba kutoka YerusalemuLk 24:13
Aya
Lk 24:13Na tazama, wawili miongoni mwao walikuwa wakienda siku hiyo hiyo katika kijiji kimoja kiitwacho Emmau, ambacho kilikuwa maili sitini kutoka Yerusalemu.
- Barabara ya jangwani kutoka Yerusalemu kwenda GazaMdo 8:26
Aya
Mdo 8:26Basi malaika wa Bwana akanena na Filipo na kusema, “Angaza na uende kusini katika njia iendayo chini ya Yerusalemu kuelekea Gaza.” (Njia hii iko katika jangwa).
- Yesu ilimbidi apite Samaria akienda GalilayaYn 4:3–5
Aya
Yn 4:3–5alitoka Judea na akaenda Galilaya. Hivyo ilikuwa muhimu kupitia Samaria. Na akafika kwenye mji wa Samaria, unaoitwa Sikari, karibu na eneo ambalo Yakobo alimpa mwanae Yusufu.
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0