Bible Explorer

Gundua › Mada › Matetemeko ya ardhi

Mambo ya kushangaza

Matetemeko ya ardhi katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (15), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Zaburi zinasema juu ya nchi ikitikisika na milima ikitetemekaZab 18:7, Zab 46:2–3, Zab 104:32
    Aya
    Zab 18:7Kisha nchi ikatikisika na kutetemeka; misingi ya milima pia ilitetemeka na kutikiswa kwa sababu Mungu alikuwa amekasirika.
    Zab 46:2–3Hivyo hatutaogopa, hata kama dunia italazimika kubadilika, hata kama milima italazimika kutetemeka na kuangukia kwenye mtima wa bahari, hata kama maji yatavuma kwa kishindo kikuu, hata kama milima itatetemeka kwa vurugu ya maji. Selah
    Zab 104:32Yeye hutazama nchi, nayo hutikisika; huigusa milima, nayo hutoa moshi.

Mifano

  • Mlima Sinai wote ulitetemeka sanaKut 19:18, Zab 68:8
    Aya
    Kut 19:18Mlima Sina ulijwa kabisa na moshi kwasababu Yahweh alishuka na moto na moshi. Moshi ulipanda juu kama moshi wa tanuru, na mlima wote ulitikisika kwa vurugu.
    Zab 68:8nchi ilitetemeka; mbingu pia zilidondosha mvua katika uwepo wa Mungu, uweponi mwa Mungu wakati alipokuja Sinai, uweponi mwa Mungu, Mungu wa Israeli.
  • Ardhi ilipasuka chini ya Kora, Dathani na AbiramuHesabu 16:31–32
    Aya
    Hesabu 16:31–32Mara ghafla Musa alipomaliza kusema maneno haya, aridhi ya pale walipokuwa ikafunguka. Dunia ikafungua makanwa yake na kuwameza, familia zao na watu wote wa Kora, pamoja na mali zao zote.
  • Nchi ilitetemeka katika kambi ya Wafilisti baada ya shambulio la Yonathani1 Sam 14:15
    Aya
    1 Sam 14:15Kukawa na hofu kubwa katika kambi, uwandani, na katika watu. Hata ngome ya jeshi na watekaji nyara nao wakawa na hofu kubwa
  • Eliya huko Horebu: upepo, tetemeko, moto, kisha sauti ndogo ya utulivu1 Fal 19:11–12
    Aya
    1 Fal 19:11–12BWANA akamwambia, “Nenda nje ukasimame kwenye mlima mbele yangu.” Kisha BWANA akapita, na upepo mkali ukaupiga mlima ukavunja miamba katika vipande vipande mbele ya BWANA, lakini BWANA hakuwemo kwenye huo mlima. Kisha baada ya upepo, tetemeko lakaja, lakini BWANA hakuwemo kwenye hilo tetemeko. Kisha baada ya tetemeko, moto ukaja, lakini BWANA hakuwemo kwenye moto. Ndipo baada ya moto, sauti ya upole ikaja.
  • Amosi alinena miaka miwili kabla ya tetemeko, siku za UziaAmo 1:1
    Aya
    Amo 1:1Haya ni mambo yanayoihusu Israeli ambayo Amosi, mmoja wa wachungaji katika Tekoa, aliyapokea katika ufunuo. Alipokea haya mambo katika siku za Uzia mfalme wa Yuda, na pia katika siku za Yeroboamu mwana wa Yoashi mfalme wa Israeli, miaka miwili kabla ya tetemeko la aridhi.
  • Zekaria anakumbuka watu wakikimbia tetemeko katika siku za UziaZek 14:5
    Aya
    Zek 14:5Ndipo mtakapokimbia katika bonde kati ya milima ya Yahwe, kwa kuwa bonde kati ya hiyo milima litafika hata Azali. Mtakimbia kama siku mliyokimbia tetemeko la nchi siku za Uzia, mfalme wa Yuda. Ndipo Yahwe Mungu wangu atakapokuja na watakatifu wake wote.
  • Yesu alipokufa nchi ilitetemeka na miamba ikapasukaMt 27:51
    Aya
    Mt 27:51Tazama, Pazia la hekalu lilipasuka sehemu mbili kutokea juu hadi chini. Na ardhi ikatetemeka na miamba ikapasuka vipande.
  • Akida aliona tetemeko na akaogopa sanaMt 27:54
    Aya
    Mt 27:54Basi yule akida na wale ambao walikuwa wakimtazama Yesu waliona tetemeko na mambo yaliyokuwa yakitokea, walijawa na woga sana na kusema, “Kweli huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”
  • Tetemeko kubwa wakati jiwe lilipovingirishwa kutoka kaburiniMt 28:2
    Aya
    Mt 28:2Tazama kulikuwa na tetemeko kubwa, kwa sababu malaika wa Bwana alishuka na kulivingirisha lile jiwe, kisha akalikalia.
  • Mahali walipokuwa wakiomba waamini palitikiswaMdo 4:31
    Aya
    Mdo 4:31Walipomaliza kuomba, eneo ambalo walikusanyika kwa pamoja likatikiswa, na wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, na walinena neno la Mungu kwa ujasili.
  • Huko Filipi tetemeko lilifungua milango ya gerezaMdo 16:26
    Aya
    Mdo 16:26Ghafla kukatokea tetemeko kuu na misingi ya gereza ikatikiswa, milango ya gereza ikafunguka, na minyororo ya wafungwa wote ikalegezwa.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0