Mambo ya kushangaza
Mvua na ukame katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (21), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
- Kabla mmea wowote haujachipua, hakukuwa na mvua dunianiMwa 2:5
Aya
Mwa 2:5Hapakuwa na msitu wa shambani uliokuwa katika nchi, na hapakuwa na mmea wa shambani uliokuwa umechipuka, kwa kuwa Yahwe Mungu alikuwa hajasababisha mvua kunyesha juu ya nchi, na hapakuwa na mtu wa kulima ardhi.
- Mvua za vuli na za masikaKum 11:14
Aya
Kum 11:14kwamba nitawapa mvua nchi yenu kwa majira yake, mvua za awali na mvua za badaye, ili kwamba mweze kukusanya nafaka zenu, mvinyo wenu mpya, na mafuta yenu.
- Kusanyiko la Ezra liliketi likitetemeka katika mvua ya mwezi wa tisaEzr 10:9, Ezr 10:13
Aya
Ezr 10:9Hivyo watu wote wa Yuda na Benjamini wakakusanyika Yerusalem kwa siku tatu. Ilikuwa ni mwezi wa tisa na siku ya ishirini ya mwezi. watu wote wakasimama mbele ya nyumba ya Mungu na wakatetemeka kwa sababu ya neno na mvua.
Ezr 10:13haijalishi, kuna watu wengi na ni kipindi cha mvua. Hatuna nguvu ya kusimama nje na hii si siku moja au mbili za kufanya kazi, kwa kuwa tumekosea katika jambo hili.
- Upepo wa kaskazini huleta mvuaMit 25:23
Aya
Mit 25:23Ni hakika upepo wa kaskazini huleta mvua, ndivyo mtu anayesema siri hufanya sura zikasirike.
- Mawingu yakijaa, hunyesha mvuaMhu 11:3
Aya
Mhu 11:3Kama mawingu yamejaa mvua, yanajivua yenyewe chini ya nchi. Na kama mti ukianguka kuelekea kusini au kuelekea kaskazini, popote mti unapoangukia papo hapo utabakia.
- Huwanyeshea mvua wenye haki na wasio hakiMt 5:45
Aya
Mt 5:45Ili kwamba muwe watoto wa baba yenu aliye mbinguni. Kwa kuwa anafanya jua liwaangazie wabaya na wema, na anawanyeshea mvua waovu na wema.
- Mvua ilinyesha na mafuriko yakaipiga nyumbaMt 7:25
Aya
Mt 7:25Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, na upepo ukaja na ukaipiga nyumba hiyo, lakini haikuweza kuanguka chini, kwa kuwa ilikuwa imejengwa juu ya mwamba.
Gharika
- Madirisha ya mbinguni yalifunguka; mvua ilinyesha siku arobaini mchana na usikuMwa 7:11–12
Aya
Mwa 7:11–12Katika mwaka wa mia sita wa maisha yake Nuhu, katika mwezi wa pili, katika siku ya kumi na saba ya mwezi, katika siku iyo hiyo, chemchemi zote za vilindi vikuu zilipasuka na kufunguka, na madirisha ya mbinguni yakafunguka. Mvua ikaanza kunyesha juu ya nchi kwa siku arobaini mchana na usiku.
- Kisha madirisha yakafungwa na mvua ikazuiliwaMwa 8:2
Aya
Mwa 8:2Chemichemi za vilindi pamoja na madirisha ya mbingu vikafungwa, na mvua ikakoma kunyesha.
- Upinde wa mvua: kamwe tena gharika ya kuiharibu duniaMwa 9:11–15
Aya
Mwa 9:11–15Kwa sababu hii ninalithibitisha agano langu pamoja nanyi, kwamba hapatatokea kuangamizwa kwa mwenye mwili kwa njia ya maji ya gharika. Tena hapatatokea gharika ya kuangamiza nchi.” Mungu akasema, “ na hii ndiyo ishara ya agano ambalo ninafanya kati yangu na ninyi pamoja na kila kiumbe hai kilicho pamoja nanyi, kwa vizazi vyote vya baadaye: Nimeweka upinde wangu wa mvua katika wingu, na itakuwa ndiyo ishara ya agano kati yangu na nchi. Hata itakuwa nitakapoleta wingu juu ya nchi na upinde wa mvua ukaonekana katika wingu, ndipo nitakumbuka agano langu, ambalo ni kati yangu na ninyi na kila kiumbe hai cha wote mwenye mwili. Maji hayatafanyika tena gharika kuharibu wote wenye mwili.
Dhoruba
- Mvua ya mawe na radi viliipiga Misri, lakini si GosheniKut 9:23–26
Aya
Kut 9:23–26Musa akanyoosha mkono na gongo lake kuelekea mbiguni, na Yahweh akatuma mngurumo, mawe ya barafu, na radi kwenye nchi. Pia alinyesha mvua kwenye nchi ya Misri. Hivyo kulikuwa na radi iliyo changanyika na mawe ya barafu, ilikuwa hatari sana, kuliko yeyote iliyowai kutokea kwenye nchi ya Misri tangu liwe taifa. Katika nchi yote ya Misri, barafu ya mawe ilipiga kila kitu kwenye shamba, watu na wanyama. Ilipiga kila mmea shambani na kuvunja kila mti. Isipo kuwa tu nchi ya Gosheni, walipo ishi Waisraeli, hapakuwa na mawe ya barafu.
- Samweli aliomba radi na mvua wakati wa mavuno ya ngano1 Sam 12:17–18
Aya
1 Sam 12:17–18Je, leo si mavuno ya ngano? Nitamwomba BWANA, naye ataleta ngurumo na mvua. Ndipo mtajua na kuona kwamba uovu wenu ni mwingi, mlioufanya machoni pa BWANA, kujiombea mfalme wenu ninyi wenyewe.” Hivyo Samweli akamwomba BWANA; na siku iyo hiyo BWANA akatuma ngurumo na mvua. Ndipo watu wote wakamwogopa sana BWANA pamoja na Samweli.
Ukame
- Eliya: hakutakuwa na umande wala mvua ila kwa neno langu1 Fal 17:1
Aya
1 Fal 17:1Eliyas Mtishibi, kutoka Tishibi ya Gileadi, akamwambia Ahabu, “Kama BWANA, Mungu wa Israeli aishivyo, ambaye ninasimama, hakutakuwa na umande wala mvua isiipokuwa kwa neno langu.”
- Katika mwaka wa tatu wa ukame, mvua iliahidiwa1 Fal 18:1
Aya
1 Fal 18:1Kwa hiyo baada ya siku nyingi neno la BWANA likamjia Eliya, katika mwaka wa tatu wa ukame, likisema, “Nenda ukajionyeshe mwenyewe kwa Ahabu nami nitainyeshea ardhi mvua.”
- Wingu dogo kama mkono, kisha mvua kubwa1 Fal 18:44–45
Aya
1 Fal 18:44–45Ile mara ya saba mtumishi wake akasema, “Tazama, kuna wingu linapanda kutoka baharini, ni dogo kama mkono wa mtu.” Eliya akamjibu, Nenda ukamwambie Ahabu, 'Andaa gari lako na ushuke kabla mvua haijakuzuia.'” Ikatokea baada ya muda mfupi mbingu zikawa nyeusi kwa mawingu na upepo, na kulikuwa na mvua kubwa. Ahabu akapanda gari akaenda zake Yezreeli,
- Mbingu zilifungwa miaka mitatu na nusuLk 4:25, Yak 5:17–18
Aya
Lk 4:25Lakini nawaambia ninyi kweli kwamba kulikuwa na wajane wengi Israel katika kipindi cha Eliya, wakati mbingu ilipofungwa kusiwe na nvua kwa miaka mitatu na nusu, wakati kulipokuwa na njaa kubwa katika nchi yote.
Yak 5:17–18Eliya alikuwa mtu mwenye hisia kama zetu, aliomba kwa juhudi kwamba mvua isinyeshe, na haikunyesha katika nchi kwa muda wa miaka mitatu na miezi sita. Na Eliya aliomba tena, na mbingu zilimwaga mvua juu ya nchi na nchi ikatoa mavuno.
- Mvua juu ya mji mmoja, si juu ya mwingineAmo 4:7
Aya
Amo 4:7Pia nimeizuia mvua kutoka kwenu wakati bado kulikuwa na miezi mitatu kwa mavuno. Nikaifanya inyeshe juu ya mji, na kuifanya isinyeshe katika mji mwingine. Kipande kimoja cha nchi ilinyesha, lakini kipande kingine cha nchi ambapo haikunyesha palikuwa pakavu.
- Ardhi ilipasuka; wakulima walifunika vichwa vyaoYer 14:4
Aya
Yer 14:4Kwa sababu hii ardhi imepasuka, kwa maana hakuna mvua katika nchi. Wakulima huwa na aibu na kufunika vichwa vyao.
- Sulemani anaomba mvua mbingu zitakapofungwa1 Fal 8:35–36
Aya
1 Fal 8:35–36Kama mbingu zitafungwa na mvua hazinyeshi kwa sababu watu wamekutenda dhambi wewe - na kama wataomba mahali hapa, na kulikiri jina lako, na kugeuka toka dhambi zao na kama umewapiga - basi sikia tokea mbinguni na usamehe dhambi za watumishi wako na za watu wako Israeli, utakapowafundisha njia njema inayowapasa; basi uinyeshee mvua nchi yako, ambayo uliwapa watu wako kuwa urithi.
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0