Bible Explorer

Gundua › Mada › Wapelelezi na wachunguzi

Mambo ya kushangaza

Wapelelezi na wachunguzi katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (34), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Yusufu anawashtaki ndugu zake: “Ninyi ni wapelelezi!”Mwa 42:9, Mwa 42:14
    Aya
    Mwa 42:9Yusufu akazikumbuka ndoto aliyoziota kuhusu wao. Akawambia, “Ninyi ni wapelelezi. Mmekuja kuona sehemu za nchi zisizolindwa.”
    Mwa 42:14Yusufu akawambia, “Ndivyo nilivyowambia; ninyi ni wapelelezi.
  • Ndugu wanajibu: “Watumishi wako ni watu waaminifu, si wapelelezi”Mwa 42:11
    Aya
    Mwa 42:11Sisi sote ni wana wa baba mmoja. Ni watu wa kweli. Watumishi wako siyo wapelelezi.”

Wapelelezi kumi na wawili

  • Musa anamtuma kiongozi mmoja wa kila kabila kuipeleleza KanaaniHesabu 13:2, Kum 1:23
    Aya
    Hesabu 13:2Tuma mwanamume mmoja kutoka kila jamaa ya kabila. Kila mwanamume awe kiongozi katika kabila lake.”
    Kum 1:23Shauri hilo lilinibariki mimi, 'Nilichukua watu kumi na mbili kutoka kwenu, mtu moja kwa kila kabila.
  • Maagizo yao: waone kama watu ni hodari au dhaifu, wachache au wengiHesabu 13:17–18
    Aya
    Hesabu 13:17–18Musa akawatuma kwenda kuipeleleza ile nchi ya Kanani. Naye akawaambia, “ Mkaanzie Negebu hadi mahali pa milima. Kaipelelezeni nchi kujua ni nchi ya namna gani. Wachunguzeni watu wake, kama ni watu wenye nguvu au dhaifu, kama ni wachache au ni wengi.
  • Walikwenda kutoka Jangwa la Sini mpaka RehobuHesabu 13:21
    Aya
    Hesabu 13:21Kwa hiyo wale wanaume wakaenda kuipeleleza ile nchi kutoka jangwa la Sini mpaka Rehobi, karibu na Lebo Hamati.
  • Huko Eshkoli watu wawili walibeba kwenye mti kichala kimoja cha zabibuHesabu 13:23
    Aya
    Hesabu 13:23Nao walipofika katika bonde la Eshikoli, walikata matawi ya mizabibu lenye kishada cha zabibu. Na makundi mawili ya wapelelezi wakakibeba kwenye mti. Pia wakaleta makomamanga na mtini.
  • Walirudi baada ya siku arobainiHesabu 13:25
    Aya
    Hesabu 13:25Baada ya siku arobaini, wakarudi kutoka kuipeleleza nchi.
  • Taarifa yao: nchi inayotiririka maziwa na asali, lakini miji yenye ngomeHesabu 13:27–28
    Aya
    Hesabu 13:27–28Wakamwambia Musa, “Tulifika katika ile nchi uliyotutuma. Kwa hakika ni nchi ya kutiririka maziwa na asali. Na baadhi ya matunda yake ni haya hapa. Hata hivyo, watu wanaoishi huko ni wenye nguvu. Miji yao ni mikubwa tena ina maboma. Pia tuliwaona wana wa Anaki huko.
  • Kalebu: “Hakika tunaweza kuishinda!” Wengine hawakukubaliHesabu 13:30–31
    Aya
    Hesabu 13:30–31Kisha Kalebu akawatuliza watu waliokuwa mbele ya Musa, akasema, “Twendeni tukaiteke nyara hiyo nchi, kwa kuwa tuna uhakika wa kuikamata.” Lakini wale watu waliokuwa wameenda naye walisema, “Hatutaweza kuwashinda hao watu kwa kuwa wao ni hodari kuliko sisi.”
  • “Tulionekana kama panzi machoni petu wenyewe”Hesabu 13:33
    Aya
    Hesabu 13:33Kule tuliiona majitu, wana wa uzao wa Anaki, ambao nii uzao wa majitu. Sisi tulionekana kama panzi machoni mwao tulipojilingsnisha nao, hivyo ndivyo tulivyoonekana machoni mwao pia.”
  • Siku arobaini za upelelezi zikawa miaka arobaini jangwani, mwaka kwa sikuHesabu 14:34
    Aya
    Hesabu 14:34Kama vile ilivyo hesabu ya siku ambayo mliipeleleza nchi—siku arobaini, vivyo hivyo mtabeba madhara ya dhambi zenu kwa muda wa miaka arobaini—mwaka mmoja kwa kila siku moja, na mtajua kuwa ni sawa na kuwa adui yangu.
  • Kati ya wapelelezi, ni Yoshua na Kalebu tu waliobaki haiHesabu 14:36–38
    Aya
    Hesabu 14:36–38Kwa hiyo wale wanaume ambao Musa aliwatuma kwenda kuingalia ile nchi wote walikufa kwa tauni mbele ya BWANA. Hawa ni wale ambao waliorudi na kutoa taarifa mbaya juu ya nchi. Hii iliwafanya watu wote wamlalamikie Musa. Kati ya watu wale waliokuwa wameenda kuiangalia nchi ile, ni Joshua mwana wa Nuni na Kalebu mwana wa Yefune tu ndio waliobaki hai.

Yeriko na Rahabu

  • Yoshua anawatuma kwa siri wapelelezi wawili kutoka Shitimu; wanakaa kwa RahabuYos 2:1
    Aya
    Yos 2:1Kisha Yoshua mwana wa Nuni aliwatuma watu wawili kwa siri kama wapelelezi kutoka Shitimu. Akisema, “Nendeni mkaiangalie nchi, hasa Yeriko.” Walienda na wakafika katika nyumba ya kahaba ambaye jina lake ni Rahabu, na wakalala hapo.
  • Rahabu anawaficha chini ya mabua ya kitani juu ya paa lakeYos 2:4–6
    Aya
    Yos 2:4–6Lakini mwanamke alikuwa amekwisha kuwachukua wale watu wawili na kuwaficha. Na akasema, “Ndiyo, watu walikuja kwangu, lakini sikujua walikotoka. Ilipokuwa jioni wakati wa kufungwa kwa lango la mji, waliondoka. Sijui mahali walikoelekea. Mnaweza kuwakamata kama mtawafuata upesi. Lakini yeye aliwapandisha juu darini na kuwaficha kwa mabua ya kitani ambayo alikuwa ameyalaza darini.
  • Anawashusha kwa kamba kutoka nyumba yake iliyo ukutani mwa mjiYos 2:15
    Aya
    Yos 2:15hivyo aliwashusha chini kwa kupitia dirishani kwa kutumia kamba. Nyumba ambayo alikuwa anaishi ilijengwa katika ukuta wa mji.
  • Ishara waliyokubaliana: kamba nyekundu iliyofungwa dirishaniYos 2:18
    Aya
    Yos 2:18Tutakapokuja katika nchi, ni lazima uifunge kamba hii nyekundu katika dirisha ulilotushushia chini, na utawakusanya katika nyumba baba yako, mama yako, kaka zako na wote wa nyumba ya baba yako.
  • Wanajificha siku tatu milimani, kisha wanampa Yoshua taarifaYos 2:16, Yos 2:22–23
    Aya
    Yos 2:16Akawaambia, “Nendeni milimani la sivyo watu waliowafuata watawaona. Jificheni huko kwa siku tatu mpaka watu waliowafuata watakaporudi. Kisha nendeni zenu.”
    Yos 2:22–23Wakaondoka na kwenda juu milimani na walikaa huko kwa siku tatu hadi pale wale waliowafuatilia waliporudi. Wale waliowafuata walitafuta njiani pote bila kuwaona. Wale watu wawili walirudi na kuvuka mto na wakafika kwa Yoshua mwana wa Nuni, na walimwambia kila kitu kilichotokea kwao.
  • Wapelelezi wawili wanamtoa Rahabu na familia yake yoteYos 6:22–23
    Aya
    Yos 6:22–23Kisha Yoshua akawaambia wale watu wawili walioipeleleza nchi, “Nendeni katika nyumba ya kahaba, mtoeni mwanamke na wote walio pamoja naye, kama mlivyomwapia.” Basi, vijana wale walioipeleleza nchi waliingia ndani na kumtoa Rahabu nje. Walimtoa nje baba yake, mama, kaka, na ndugu wote waliokuwa pamoja naye. waliwaleta katika sehemu ya nje ya kambi ya Waisraeli.
  • Waebrania na Yakobo wanamkumbuka Rahabu kwa kuwakaribisha wapeleleziEbr 11:31, Yak 2:25
    Aya
    Ebr 11:31Ilikuwa ni kwa imani kwamba Rahabu yule kahaba hakuangamia pamoja na wale ambao hawakuwa watiifu, kwa sababu alikuwa amewapokea wapelelezi na kuwahifadhi salama.
    Yak 2:25Hali kadhalika, je, hakuwa Rahabu yule kahaba alihesabiwa haki kwa matendo, alipowakaribisha wajumbe na kuwapeleka kwa barabara nyingine?

Wapelelezi wengine

  • Baada ya wapelelezi kwenda Yazeri, Israeli waliteka vijiji vyakeHesabu 21:32
    Aya
    Hesabu 21:32Kisha Musa akatuma watu kwenda kuingalia Yaziri. Waliviteka vijiji vyake na kuwafukuza Waamori waliokuwa wakiishi humo.
  • Wapelelezi waliotumwa Ai wanaripoti: watu elfu mbili au tatu wanatoshaYos 7:2–3
    Aya
    Yos 7:2–3Yoshua alituma watu kutoka Yeriko kwenda Ai, mji uliokuwa karibu na Bethi Aveni, mashariki mwa Betheli. Aliwaambia, “Nendeni na mkaipeleleza nchi.” Wale watu walikwea na kuipeleleza Ai. Waliporudi kwa Yoshua, walimwambia, “Usitume watu wote kwenda Ai. Tuma tu watu elfu mbili au elfu tatu waende kuiteka Ai. Usiwafanye watu wateseke katika vita, kwani ni watu wachache.”
  • Wadani watano wanaipeleleza Laishi: watu watulivu wasio na washirikaAmu 18:2, Amu 18:7
    Aya
    Amu 18:2Watu wa Dani walituma watu watano kutoka kwa idadi yote ya kabila lao, wanaume wenye ujasiri kutoka Sora na kutoka Eshtaoi, ili kukagua ardhi kwa miguu, na kuiangalia. Wakawaambia, “Nendeni mkaangalie nchi.' Wakafika nchi ya mlima wa Efraimu, kwa nyumba ya Mika wakalala huko.
    Amu 18:7Kisha wale watu watano wakaondoka na wakafika Laishia, na waliona watu waliokuwa pale waliishi salama- vivyo hivyo Wasidoni waliishi bila kusumbuliwa na kwa usalama. Hapakuwa na mtu aliyewashinda katika nchi hiyo, au aliyewasumbua kwa namna yoyote. Waliishi mbali na Wasidoni, na hawakuwa na ushirikiano na mtu yeyote.
  • Daudi anatuma wapelelezi kuhakikisha kwamba Sauli amefika1 Sam 26:4
    Aya
    1 Sam 26:4Hivyo Daudi akawatuma wapelelezi na akafahamu kwamba hakika Sauli alikuwa amekuja.
  • Wakuu wa Waamoni wanashuku kuwa wafariji wa Daudi ni wapelelezi2 Sam 10:3
    Aya
    2 Sam 10:3Lakini viongozi wa watu wa Amoni wakamwambia Hanuni bwana wao, “Je unathani kwa hakika Daudi anamweshimu baba yako hata ametuma watu kukutia moyo? Daudi hajawatuma watumishi wake kwako ili kuuangalia mji, kuupeleleza, ili kuupindua?
  • Absalomu anatuma wapelelezi katika makabila: kwa sauti ya tarumbeta, semeni “Absalomu anatawala”2 Sam 15:10
    Aya
    2 Sam 15:10Kisha Absalomu akatuma wapelelezi katika jamaa zote za Israeli, kusema, “Mara msikiapo sauti ya tarumbeta semeni, 'Absalomu anatawala katika Hebroni.”
  • Wana wa makuhani Ahimaazi na Yonathani watampelekea Daudi habari2 Sam 15:35–36
    Aya
    2 Sam 15:35–36Je haunao pamoja nawe Sadoki na Abiathari makuhani? Hivyo chochote ukisikiacho katika kasri, uwaambie Sadoki na Abiathari makuhani. Tazama wanao pamoja nao wana wao wawili, Ahimaasi, mwana wa Sadoki, na Yonathani mwana wa Abiathari. Mniletee habari juu ya kila mnachokisikia.”
  • Mjakazi anawaletea habari huko Enrogeli; wanajificha kisimani2 Sam 17:17–19
    Aya
    2 Sam 17:17–19Yonathani na Ahimaasi walikuwako katika chemichemi za En Rogeli. Hivyo kijakazi mmoja alikuwa akienda na kuwapasha habari waliyopaswa kuifahamu, ili kwamba wasihatarishe maisha yao kwa kuonwa wakiingia mjini. Ujumbe ulipofika ndipo huenda na kumtaarifu mfalme Daudi. Lakini kijana mmoja akawaoni mara akamwambia Absalomu. Hivyo Yonathani na Ahimaasi wakaenda kwa haraka na wakaingia katika nyumba ya mtu mmoja huko Bahurimu, aliyekuwa na kisima katika ua wake wakaingia humo. Mke wa mtu huyo akachukua kifuniko na kukikufunika kwenye mlango wa kisima kisha akaanika nafaka juu yake, hivyo hakuna aliyejua kwamba Yonathani na Ahimaasi walikuwa kisimani.
  • Wapelelezi wanaojifanya wanyofu wanajaribu kumnasa Yesu kwa maneno yakeLk 20:20
    Aya
    Lk 20:20Walimuangalia kwa makini, wakatuma wapelelezi waliojifanya kuwa watu wa haki, ili wapate kupata kosa kwa hotuba yake, ili kumpelekakwa watawala na wenye mamlaka.
  • Paulo: ndugu wa uongo waliingia kupeleleza uhuru wetuGal 2:4
    Aya
    Gal 2:4Jambo hili lilitokea kwa sababu ya ndugu wa uongo waliokuja kwa siri kupeleleza uhuru tuliokuwa nao katika Kristo Yesu. Walitamani kutufanya sisi kuwa watumwa wa sheria.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0