Bible Explorer

Gundua › Mada › Ukoma

Mambo ya kushangaza

Ukoma katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (25), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

Katika Sheria

  • Kuhani alichunguza kila uvimbe, upele au doa jeupe ngoziniLaw 13:2–3
    Aya
    Law 13:2–3Mtu yeyote anayeonekana na uvimbe au pele au doa ling'aalo juu ya ngozi ya mwili wake, na likawa limeambukizwa ugonjwa wa ngozi mwilini mwake, ni lazima aletwe kwa Aroni kuhani mkuu au kwa mmoja wa wanawe makuhani. Naye kuhanai atachunguza ugonjwa huo kwenye ngozi ya mwili wake. Iwapo malaika zilizopo eneo lenye ugonjwa zimegeuka kuwa nyeupe, na iwapo ugonjwa umejitokeza juu ya ngozi, huo ni ugonjwa wa kuambukiza. Baada cha kuhani kumchunguza, atamtangaza kuwa ni najisi.
  • Mgonjwa alivaa nguo zilizoraruka na kupiga kelele, “Najisi, najisi!”Law 13:45
    Aya
    Law 13:45Mtu aliye na ugojwa wa kuambukiza atavaa nguo zilizochanika, ni lazima nywele zake ziachwe wazi, na yampasa kufunika uso wake mpaka puani na kupiga kelele, 'Najisi, najisi.'
  • Ilimbidi aishi peke yake nje ya kambiLaw 13:46, Hesabu 5:2
    Aya
    Law 13:46Naye atakuwa najisi siku zote za ugonjwa wake wa kuambukiza. Kwa sababu anao ugonjwa unaosambaa, yapasa kuishi peke yake nje ya kambi.
    Hesabu 5:2“Waamuru wana wa Israel wawatoe watu wote wenye magonjwa ya ngozi yanayoambukiza, na kila mwenye mwenye vidonda vinavyotoa harufu, na ambaye amenajisika kwa kugusa maiti.
  • Sheria hiyo hiyo ilihusu ukungu katika nguo na nyumbaLaw 13:47, Law 14:34
    Aya
    Law 13:47Kuna wakati fulani vazi la mtu hupata ukungu juu yake. Laweza kuwa vazi, ama la sufu au kitani,
    Law 14:34“Wakati mtakuja katika nchi ya Kanaani ambayo nimewapa kama miliki, na kama naweka ukungu unaenea ndani ya nyumba katika nchi ya miliki yenu,
  • Kutakaswa: ndege wawili, mti wa mwerezi, uzi mwekundu na hisopoLaw 14:4
    Aya
    Law 14:4Ndipo kuhani ataamuru kwamba mtu mwenye kutakaswa lazima achukue ndege safi wawili, waliohai, mti wa mwerezi, kitani nyekundu na hisopo.
  • Mtu aliyetakaswa alinyoa nywele zake zote na kuogaLaw 14:8–9
    Aya
    Law 14:8–9Mtu aliyetakaswa atafua nguo zake, atanyoa nywele zake zote, ataoga kwa maji, na ndipo atakuwa safi. Baada ya hayo lazima aje kwenye kambi, lakini ataishi nje ya hema lake kwa siku saba. Katika siku ya saba lazima anyoe nywele za kichwa chake, na lazima pia anyoe ndevu zake na nyusi. Lazima anyoe nywele zake zote, na lazima afue nguo zake na aoge kwenye maji; ndipo atakuwa safi.

Mifano

  • Mkono wa Musa ulipata ukoma, mweupe kama thelujiKut 4:6
    Aya
    Kut 4:6Yahwe pia alimwambia, “Sasaingiza mkono wako ndani ya vazi lako.” Hivyo Musa akaingiza mkono wake ndani ya vazi lake. Na alipoutoa nje, tazama, mkono wake ulikuwa na ukoma, mweupe kama theluji.
  • Miriamu alipata ukoma na akafungiwa nje ya kambi siku sabaHesabu 12:10, Hesabu 12:15
    Aya
    Hesabu 12:10Lile wingu likainuka juu ya hema, Miriamu akapata ukoma ghafla - akawa mweupe kama theluji. Naye Haruni alipogeuka kumwona Miriamu, akamwona amepata ukoma.
    Hesabu 12:15Kwa hiyo Miriamu akafungiwa nje ya kambi kwa siku saba. Watu hawakusafiri mpaka aliporudi kambini.
  • Naamani, jemadari wa Shamu, alikuwa na ukoma2 Fal 5:1
    Aya
    2 Fal 5:1Basi Naamani, amri jeshi wa mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa na mtu mwenye kuheshimiwa mbele ya bwana wake, kwa sababu kwa ajili yake Yahwe aliwapa ushindi Washami. Pia alikuwa hodari, mtu shujaa, lakini alikuwa anaukoma.
  • Alijichovya mara saba Yordani na ngozi yake ikapona2 Fal 5:14
    Aya
    2 Fal 5:14Ndipo akashuka chini na kuzama mwenyewe mara saba kwenye Yordani, akitii maelekezo ya mtu wa Mungu. Nyama ya mwili wake ikarudi tena kama nyama ya mwili ya mtoto mdogo, na alikuwa amepona.
  • Gehazi aliondoka kwa Elisha mwenye ukoma, mweupe kama theluji2 Fal 5:27
    Aya
    2 Fal 5:27Basi ukoma wa Naamani utakuwa kwenye uzao wako daima.” Basi Gehazi akatoka kwenye uwepo wake, mwenye ukoma kama theluji.
  • Wakoma wanne langoni pa Samaria waliikuta kambi ya Washami tupu2 Fal 7:3–8
    Aya
    2 Fal 7:3–8Basi, kulikuwa na watu wanne wenye ukoma upande wa nje wa lango la mji. Wakaambizana kila mmoja, “Kwa nini tukae hapa hadi hapo tutakapokufa? Kama tukisema kwamba tutaenda kwenye ule mji, maana mjini kuna njaa, na tutakufa hapo. Lakini kama tukiendelea kukaa hapa, bado tutakufa. Sawa, njoni, twendeni kwenye lile jeshi la Washami. Kama wakitupa uhai, tutakuwa hai, na kama wakituua, tutakufa tu.” Hivyo wakaamka asubuhi kabla giza halijaisha kwenda kwenye kambi ya Washami; Wakati walipofika sehemu ya mwanzo wa kambi, hapakuwa na mtu hapo. Kwa kuwa Bwana alikuwa ameunda jeshi la Washami kusikia sauti ya magari ya farasi, na sauti za farasi-sauti za jeshi jingine kubwa, ndipo wakaambizana kila mmoja wao, “Yule mfalme wa Israeli amekodisha wafalme wa Wahiti na Wamisri waje wapigane dhidi yetu.” Hivyo wale maaskari wakaondoka kungali giza; waliacha mahema yao, punda zao, na kambi kama ilivyokuwa, na kukimbia kwa ajili ya maisha yao. Wakati wale watu wenye ukoma walipokuja sehemu ya mwisho wa kambi, wakaenda kwenye hema moja na kula na kunywa, na kubeba fedha na dhahabu na nguo, na kwenda na kuzificha. Wakarudi na kuingia kwenye hema nyingine na kubeba kutoka pale pia, na kwenda kuvificha.
  • Ukoma ulimtokea Mfalme Uzia kwenye paji la uso hekaluni2 Nya 26:19–20
    Aya
    2 Nya 26:19–20Kisha Uzia akakasirika. Alikuwa ameshikilia chetezo mkononi kwa ajili ya kufukiza uvumba. Wakati alipowaghadhabikia makuhani, ukoma ukatokea juu ya uso wake mbele ya makuhani katika nyumba ya Yahwe, pembeni mwa madhabahu ya uvumba. Azaria kuhani mkuu na makuhani wote wakamwanagalia, na, tazama, alikuwa amepatwa ukoma juu ya uso wake. Walimwondoa pale haraka. Kwa hakika, aliharakisha kwenda nje, kwa maana Yahwe alikuwa amempiga.
  • Uzia aliishi katika nyumba ya peke yake mpaka kufa kwake2 Fal 15:5, 2 Nya 26:21
    Aya
    2 Fal 15:5Yhawe akampiga mfalme hivyo basi akawa na ukoma mpaka siku ya kifo chake na alikaa kwenye nyumba ya pekee. Yothamu, mtoto wa mfalme, alikuwa juu ya watu na kuwaongoza watu wa nchi.
    2 Nya 26:21Uzia, mfalme, alikuwa mwenye ukoma hadi siku ya kufa kwake na aliishi katika nyumba ya kutengwa tangu alipokuwa mwenye ukoma, kwa maan alitengwa na nyumba ya Yahwe. Yothamu, mwanaye, alikuwa mkuu wa anyumba ya mfalme na aliwatawala watu wa nchi.
  • Alizikwa shambani karibu na makaburi ya wafalme2 Nya 26:23
    Aya
    2 Nya 26:23Kwa hiyo Uzia akalala pamoja na babu zake; walimzka pamoja na babu zake katika uwanja wa maziko wa Mfalme, kwa maana walisema, “Ni mwenye ukoma”. Yothamu, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake.
  • Yesu alimgusa mwenye ukoma naye akatakasikaMk 1:40–42
    Aya
    Mk 1:40–42Mwenye ukoma mmoja alikuja kwake. Alikuwa akimsihi; alipiga magoti na alimwambia, “Kama unataka, waweza kunifanya niwe safi.” Akisukumwa na huruma, Yesu alinyosha mkono wake na kumgusa, akimwambia, “Ninataka. Uwe msafi.” Mara moja ukoma ukamtoka, na alifanywa kuwa safi.
  • Alimtuma akajionyeshe kwa kuhaniMt 8:4, Lk 5:14
    Aya
    Mt 8:4Yesu akamwambia, “Angalia kwamba usiseme kwa mtu yeyote. Shika njia yako, na jioneshe mwenyewe kwa kuhani na utoe zawadi ambayo Musa aliagiza, kwa ajili ya ushuhuda kwao”
    Lk 5:14“Alimwagiza asimwambie mtu yeyote, lakini alimwambia, “Nenda zako, na ukajionyeshe kwa makuhani na utoe sadaka ya utakaso wako, sawasawa na kile Musa alichokiamuru, kwa ushuhuda kwao.”
  • Kati ya wakoma kumi walioponywa, ni Msamaria tu aliyerudi kushukuruLk 17:12–16
    Aya
    Lk 17:12–16Alipokua akiingia kwenye kijiji kimoja, huko alikutana na watu kumi waliokuwa na ukoma. Wakasimama mbali wakapaza sauti wakasema “Yesu, Bwana tuhurumie.” Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani.” nao walipokua wakienda wakatakasika. Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa sauti kuu akimsifu Mungu. Akapiga magoti miguuni mwa Yesu akamshukuru. Yeye alikua msamaria.
  • Yesu alikula Bethania nyumbani kwa Simoni mwenye ukomaMt 26:6, Mk 14:3
    Aya
    Mt 26:6Wakati Yesu alipokuwa Bethania katika nyumba ya Simoni mkoma,
    Mk 14:3Wakati Yesu alipokuwa Bethania nyumbani kwa Simoni mkoma, na alipokuwa akielekea mezani, mwanamke mmoja alikuja kwake akiwa na chupa ya marashi ya nardo safi yenye gharama kubwa sana, aliivunja chupa na kuimimina juu ya kichwa chake.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0