Bible Explorer

Gundua › Mada › Nywele na ndevu

Mambo ya kushangaza

Nywele na ndevu katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (36), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zoteMt 10:30, Lk 12:7
    Aya
    Mt 10:30Lakini hata idadi ya nywele zenu zimehesabiwa.
    Lk 12:7Lakini mjue kuwa, nywele za vichwa vyenu vimehesabiwa. Msiogope. Ninyi ni wa thamani kubwa kuliko shomoro wengi.
  • Huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusiMt 5:36
    Aya
    Mt 5:36Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
  • Paulo: nywele ndefu ni aibu kwa mwanaume, utukufu kwa mwanamke1 Kor 11:14–15
    Aya
    1 Kor 11:14–15Je hata asili peke yake haiwafundishi ya kwamba mwanamume akiwa na nywele ndefu ni aibu kwake? Je asili haiwafundishi ya kwamba mwanamke akiwa na nywele ndefu ni utukufu kwake? Maana amepewa zile nywele ndefu kama vazi lake.
  • Uzuri usitokane na kusuka nywele1 Tim 2:9, 1 Pet 3:3
    Aya
    1 Tim 2:9Vivyo hivyo, nataka wanawake wajivike mavazi yanayokubalika, kwa heshima na kujizuia. Wasiwe na nywele zilizosukwa, au dhahabu, au Lulu, au mavazi ya gharama kubwa.
    1 Pet 3:3Hii ifanyike siyo kwa mapambo ya nje—kusuka nywele, vito vya dhahabu, au mavazi ya mtindo.

Katika Sheria

  • Msinyoe nywele za pembeni wala kukata pembe za ndevuLaw 19:27
    Aya
    Law 19:27Usitafute kuwadhibiti wengine kwa njia ya nguvu za kichawi. Msifuate tabia za kipagani kama vile kunyoa denge au kunyoa pembe za ndevu zeu.
  • Makuhani wasinyoe upara wala pembe za ndevu zaoLaw 21:5
    Aya
    Law 21:5Makuhanai hawatanyoa vichwa vyo wala kunyoa pembeni mwa ndevu zao, wala hawatachanja chale miili yao.
  • Msinyoe paji la uso kwa ajili ya mfuKum 14:1
    Aya
    Kum 14:1Ninyi ni watu wa Yahwe Mungu wenu. Msijikate wenyewe, wala kunyoa sehemu za nyuso zenu kwa ajili ya wafu.
  • Mtu anayepoteza nywele zake bado ni safiLaw 13:40–41
    Aya
    Law 13:40–41Iwapo nywele za mtu zimenyonyoka kichwani, yeye ni kipara lakini yu safi. Na iwapo nywele zake zimenyonyoka upande wa mbele wa kichwa chake, na iwapo paji lake la uso lina kipara, yeye yu safi.
  • Mnadhiri aliziacha nywele zake zikue na kuzichoma nadhiri ilipokwishaHesabu 6:5, Hesabu 6:18
    Aya
    Hesabu 6:5Wakati wote wa nadhiri yake, wembe usiipite kichwani mwake mpaka siku zake za nadhiri kwa BWANA zitimilike. Lazima ajitenge kwa BWANA. Ataziacha nywele zake zikue kichwani mwake.
    Hesabu 6:18Mnadhiri atanyoa nywele zake kama ishara ya kujitenga kwa ajili ya Mungu kwenye mlango wa hema ya kukutania. Atazitoa nywele zake kichwani kwake na kuzichoma kwa moto ulio chini ya sadaka ya amani.

Mifano

  • Yusufu alinyoa kabla ya kuingia kwa FaraoMwa 41:14
    Aya
    Mwa 41:14Ndipo Farao alipotuma na kumwita Yusufu. Kwa haraka wakamtoa gerezani. Akajinyoa mwenyewe, akabadili mavazi yake, na akaingia kwa Farao.
  • Wembe haukupaswa kupita kichwani pa SamsoniAmu 13:5, Amu 16:17
    Aya
    Amu 13:5Angalia, utakuwa na mjamzito na kuzaliwa mtoto mwanaume. Hakuna wembe itakayotumiwa juu ya kichwa chake, kwa kuwa mtoto atakuwa Mnaziri kwa Mungu kutoka tumboni, naye ataanza kuwaokoa Israeli kutoka mkono wa Wafilisti.
    Amu 16:17Basi Samsoni alimwambia kila kitu, akamwambia, “Wembe haujawahi kukata nywele juu ya kichwa changu, kwa maana nimekuwa Mnaziri kwa Mungu kutoka tumboni mwa mama yangu. Ikiwa kichwa changu kitanyolewa, basi nguvu zangu zitaniacha, nami nitakuwa dhaifu na kuwa kama kila mtu mwingine. '
  • Delila aliagiza kichwa chake kinyolewe; kisha nywele zake zikaota tenaAmu 16:19, Amu 16:22
    Aya
    Amu 16:19Alimfanya alale katika magoti yake. Alimwita mtu avinyoe vifungo saba vya kichwa chake, naye akaanza kumshinda, kwa maana nguvu zake zilikuwa zimemwacha.
    Amu 16:22Lakini nywele juu ya kichwa chake zilianza kukua tena baada ya kunyolewa.
  • Daudi aliacha mate yatiririke ndevuni mwake, akijifanya mwendawazimu1 Sam 21:13
    Aya
    1 Sam 21:13Daudi akabadili mwenendo wake mbele yao na akajifanya kuwa mwendawazimu machoni pao; akachora-chora alama kwenye vizingiti vya milango huku akitiririsha mate yake chini ya ndevu zake.
  • Hanuni alinyoa nusu ya ndevu za wajumbe wa Daudi2 Sam 10:4
    Aya
    2 Sam 10:4Hivyo Hanuni akawachukuwa watumishi wa Daudi, akawanyoa nusu ya ndevu zao, akachana mavazi yao hadi kwenye matako, naye akawaacha waende zao.
  • Daudi: kaeni Yeriko mpaka ndevu zenu zimee tena2 Sam 10:5
    Aya
    2 Sam 10:5Daudi alipoelezwa kuhusu hili, akatuma watu kwenda kuwalaki, kwa kuwa walikuwa wamefedheheshwa sana. Mfalme akawambia, “Kaeni Yeriko mpaka ndevu zenu zitakapoota, ndipo mrudi.”
  • Nywele za Absalomu alizonyoa kila mwaka zilikuwa na uzito wa shekeli mia mbili2 Sam 14:26
    Aya
    2 Sam 14:26Alipokata nywele za kichwa chake mwishoni mwa kila mwaka, kwa sababu zilikuwa nzito juu yake, alipima nywele zake zaidi ya shekeli mia mbili, kwa kiwango cha kipimo cha mfalme.
  • Mefiboshethi hakupunguza masharubu yake wakati Daudi hayupo2 Sam 19:24
    Aya
    2 Sam 19:24Kisha Mefiboshethi mwana wa Sauli akashuka ili kumlaki mfalme. Hakuwa ameivalisha miguu yake wala kunyoa ndevu zake wala kufua nguo zake tangu siku mfalme alipoondoka hata siku aliporudi kwa amani.
  • Yoabu alishika ndevu za Amasa kana kwamba ambusu2 Sam 20:9
    Aya
    2 Sam 20:9Hivyo Yoabu akamwambia Amasa, “Haujambo binamu yangu?” Kwa utaratibu Yoabu akakishika kidevu cha Amasa kwa mkono wake wa kulia ili ambusu.
  • Eliya alikuwa mtu mwenye nywele nyingi na mshipi wa ngozi2 Fal 1:8
    Aya
    2 Fal 1:8Wakamjibu, “Alikuwa amevaa kanzu yenye manyaya na alikuwa na mkanda wa ngozi kiunanoni kwake.'” Hivyo mfalme akajibu, '“Yule alikuwa Eliya Mtishbi.”
  • Vijana walimdhihaki Elisha: “Panda juu, wewe mwenye upara!”2 Fal 2:23
    Aya
    2 Fal 2:23Ndipo Elisha akapanda kutoka pale mpaka Betheli. Naye alipokuwa akienda hadi kwenye barabara, wakatokea vijana nje ya mji na kumtania, wakamwambia, “Panda juu, wewe mwenye kipara! Panda juu, wewe mwenye kipara!”
  • Ndevu za Haruni na mafuta mazuri yanayotiririka juu yakeZab 133:2
    Aya
    Zab 133:2Ni kama mafuta mazuri kichwani yashukayo ndevuni. Ndevu za Haruni, na yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake.
  • Ayubu alinyoa kichwa chake kwa huzuniAyu 1:20
    Aya
    Ayu 1:20Kisha Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, akanyoa kichwa chake, akaanguka chini kifudifudi na kumwabudu Mungu.
  • Ezra aling’oa nywele za kichwa na ndevu zake kwa mshtukoEzr 9:3
    Aya
    Ezr 9:3Niliposikia haya, nikachana nguo zangu na kanzu na kunyoa nywele kichwani na ndevu na nikakaa chini kutafakari.
  • Waombolezaji themanini walikuja nyumbani kwa Yahwe wakiwa wamenyoa ndevuYer 41:5
    Aya
    Yer 41:5Wanaume baadhi walikuja toka Shechem, toka Shiloh, na toka Samaria-wanaume semanini ambayo walikuwa wamenyoa ndevu zao, walirarua nguo zao, na kujikata wenyewe- pamoja na chakula cha sadaka na ubani katika mikono yao kwenda kwa nyumba ya Yahwe.
  • Nywele za Nebukadneza zilikua kama manyoya ya taiDan 4:33
    Aya
    Dan 4:33Agizo hili kinyume na Nebukadneza lilitekelezwa ghafla. Aliondolewa miongoni mwa watu. Alikula majani kama ng'ombe, na mwili wake ulilowa kwa umande wa kutoka mbinguni. Nywele zake zilirefuka kama manyoa ya tai, na makucha yake yalikuwa kama makucha ya ndege.
  • Mwanamke alipangusa miguu ya Yesu kwa nywele zakeLk 7:38, Yn 12:3
    Aya
    Lk 7:38Alisimama nyuma yake karibu na miguu yake huku akilia. Tena alianza kulowanisha miguu yake kwa machozi, na kuifuta kwa nywele za kichwa chake, akiibusu miguu yake na kuipaka manukato.
    Yn 12:3Kisha Mariamu akachukua ratli ya manukato yaliyotengenezwa kwa nardo safi, yenye thamani kubwa, akampaka Yesu miguuni, na kumfuta miguu kwa nywele zake; nyumba yote ilijaa harufu ya manukato.
  • Paulo alinyoa kichwa chake huko Kenkrea kwa sababu ya nadhiriMdo 18:18
    Aya
    Mdo 18:18Paulo, baada ya kukaa pale kwa muda mrefu, aliwaacha ndugu na kwenda kwa meli Siria pamoja na Prisila na Akwila. Kabla ya kuondoka bandarini, alinyoa nywele zake kwani alikuwa ameapa kuwa Mnadhiri.

Katika maombolezo

  • Vichwa vilivyonyolewa na ndevu zilizokatwa kama ishara za maombolezoIsa 15:2, Yer 48:37, Mik 1:16
    Aya
    Isa 15:2Wamenda juu hekaluni, watu wa Diboni wamenda juu kuomboleza; Moabu wanaomboleza juu ya Nebo na juu ya madeba. Vichwa vyao vimenyolewa viko wazi na na ndevu zao zimenyolewa.
    Yer 48:37Maana kila kichwa kina upaa na kila kidevu kimenyolewa. Chale zipo katika kila mkono, na nguo za magunia katika viuno vyao.
    Mik 1:16Kata kipara chako na kata nywele zako kwa ajili ya watoto ambao unaowafurahisha. Fanya kipara chako mwenyewe kama tai, kwa ajili ya watoto wako watakao kwenda utumwani kutoka kwako

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0