Bible Explorer

Gundua › Mada › Saa na zamu za usiku

Mambo ya kushangaza

Saa na zamu za usiku katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (49), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • “Ikawa jioni, ikawa asubuhi — siku ya kwanza”Mwa 1:5
    Aya
    Mwa 1:5Mungu akaiita nuru “ mchana” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni na asubuhi, siku ya kwanza.
  • Yesu: “Je, hakuna saa kumi na mbili za mchana?”Yn 11:9
    Aya
    Yn 11:9Yesu akawajibu, “Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu anapotembea mchana hawezi kujikwaa, kwa sababu anaona kwa nuru ya mchana.
  • Mwendo wa siku moja: Eliya alikwenda umbali huo nyikani1 Fal 19:4
    Aya
    1 Fal 19:4Lakini yeye mwenyewe akaenda mwendo wa siku moja huko jangwani, akaja akakaa chini ya mti wa mretemu. Akajiombea mwenyewe kufa, akasema, “Sasa yatosha, BWANA, ichukue roho yangu, kwa kuwa mimi si mzuri kuliko mababu zangu waliokufa.”
  • Mwendo wa siku ya Sabato: kutoka Mlima wa Mizeituni hadi YerusalemuMdo 1:12
    Aya
    Mdo 1:12Ndipo wakarudi Yerusalemu kutoka kwenye mlima wa mizeituni, ambao uko karibu na Yerusalemu, mwendo wa siku ya Sabato.
  • Siku ya Maandalizi: siku iliyotangulia SabatoMk 15:42, Yn 19:31
    Aya
    Mk 15:42Kulipokuwa jioni, na kwa kuwa ilikuwa siku ya maandalio, siku kabla ya Sabato,
    Yn 19:31Kwa vile ilikuwa ni wakati wa maandalio, na kwa sababu miili haikutakiwa kubaki juu ya msalaba wakati wa Sabato (kwa kuwa Sabato ilikuwa siku ya muhimu), wayahudi walimwomba Pilato kuwa miguu yao wale wliokuwa wamesulibishwa ivunjwe, na kwamba miili yao ishushwe.
  • Nehemia alifunga malango vivuli vya jioni vilipoingia kabla ya SabatoNeh 13:19
    Aya
    Neh 13:19Mara ilipokuwa giza kwenye milango ya Yerusalemu kabla ya Sabato, niliamuru milango ifungwe na kwamba haifai kufunguliwa hadi baada ya Sabato. Niliwaweka baadhi ya watumishi wangu kwenye malango ili mzigo wowote usiweze kuletwa siku ya Sabato.
  • Kivuli kilirudi nyuma hatua kumi kwenye ngazi za Ahazi2 Fal 20:9–11
    Aya
    2 Fal 20:9–11Isaya akajibu, “Hii ndiyo itakuwa ishara kwako kutoka kwa Yahwe, kwamba Yahwe atafanya kitu amacho alichokisema. Je kivuli kitaenda mbele hatua saba, au kurudi nyuma hatua saba?” Hezekia akajibu, “Ni kitu chepesi kwa kivuli kwenda mbele hatua kumi. Hapana, hicho kivuli kirudi nyuma hatua kumi.” Hivyo Isaya nabii akamlilia Yahwe, na akaleta kivuli hatua kumi nyuma, kutoka pale ambapo zilikuwa zimevuka kwenye ngazi za Ahazi.

Zamu za usiku

  • Maombolezo: “Lia usiku tangu zamu ya kwanza”Omb 2:19
    Aya
    Omb 2:19Nyanyuka, lia usiku, mwanzo usiku wa manane! Mwaga moyo wako kama maji mbele za uso wa Bwana. Nyoosha juu mikono yako kwa ajili ya uzima wa watoto wako wanao zimia kwa njaa kwenye njia ya kila mtaa.
  • Gideoni alifika mwanzoni mwa zamu ya kati, baada ya walinzi kubadilishanaAmu 7:19
    Aya
    Amu 7:19Basi Gideoni na watu mia moja waliokuwa pamoja naye walifika mwisho wa kambi, hapo mwanzoni mwa saa ya kati. Wakati Wamidiani walikuwa wakibadilisha walinzi, walipiga tarumbeta na kuvunja mitungi iliyokuwa mikononi mwao.
  • Katika zamu ya asubuhi kambi ya Wamisri ilivurugwaKut 14:24
    Aya
    Kut 14:24Lakini masaa ya mapema ya asubui, Yahweh alitazama chini jeshi la Wamisri kupitia nguzo ya moto na wingu. Alisababisha hofu miongoni mwa Wamisri.
  • Sauli alishambulia kambi ya Waamoni wakati wa zamu ya asubuhi1 Sam 11:11
    Aya
    1 Sam 11:11Siku iliyofuata Sauli akawapanga watu katika vikosi vitatu. Wakafika katikati ya Kambi wakati wa asubuhi, wakawashambulia na kuwashinda Waamoni ilipofika mchana. Waliosalimika nao walitawanyika, kiasi kwamba hata watu wawili hawakuachwa pamoja.
  • Yesu alitembea juu ya bahari katika zamu ya nne ya usikuMt 14:25, Mk 6:48
    Aya
    Mt 14:25Katika usiku wa zamu ya nne Yesu aliwakaribia, akitembea juu ya maji.
    Mk 6:48Na aliwaona wakitaabika kupiga makasia kwa sababu upepo uliwazuia. Ilipokaribia asubuhi akawaendea, akitembea juu ya maji, na alitaka kuwapita.
  • Bwana anaweza kuja zamu ya pili au ya tatuLk 12:38
    Aya
    Lk 12:38Kama Bwana atakuja kwa zamu ya pili ya ulinzi ya usiku, au hata zamu ya tatu ya ulinzi, na kuwakuta wakiwa tayari, itakuwa ni heri kwa hao watumishi.
  • Jioni, usiku wa manane, jogoo awikapo, au asubuhiMk 13:35
    Aya
    Mk 13:35Kwa hiyo iweni macho! Kwani hamjui ni lini bwana wa nyumba atakaporudi nyumbani, yawezekana ni jioni, usiku wa manane, wakati jogoo atakapowika, au asubuhi.
  • Mtunga zaburi anatafakari katika zamu za usikuZab 63:6, Zab 119:148
    Aya
    Zab 63:6nikufikiripo kitandani mwangu na kukutafakari wewe wakati wa saa za usiku.
    Zab 119:148Ninatumaini katika maneno yako. Macho yangu yako wazi usiku kucha ili niweze kutafakari juu ya neno lako.

Saa za mchana

  • Petro: “Ni saa tatu tu ya mchana!”Mdo 2:15
    Aya
    Mdo 2:15Watu hawa hawajalewa kama mnavyodhani, sababu saa hizi ni asubuhi saa tatu.
  • Wafanyakazi walioajiriwa saa tatu, sita, tisa na kumi na mojaMt 20:3, Mt 20:5–6
    Aya
    Mt 20:3Alienda tena baada ya masaa matatu hivi na aliona wafanyakazi wengine wakiwa wamesimama bila kazi katika eneo la soko.
    Mt 20:5–6Akaenda tena baada ya masaa sita na tena katika saa ya tisa, na alifanya hivyo hivyo. Mara nyingine tena mnamo saa kumi na moja, alienda na kuwakuta watu wengine wamesimama bila kazi. Aliwaambia, 'kwanini mmesimama hapa bila kazi yoyote kwa siku nzima?
  • Jioni ilipofika wote walilipwa, walioajiriwa mwisho kwanzaMt 20:8–9
    Aya
    Mt 20:8–9Wakati wa jioni ulipofika, mwenye shamba la mizabibu alimwambia msimamizi wake, 'Waite wafanyakazi na uwalipe mishahara, kwa kuanza na wa mwisho hadi wa kwanza.' Walipokuja wale walioajiriwa saa kumi na moja, kila mmoja wao alipokea dinari.
  • Ilikuwa saa tatu walipomsulubisha YesuMk 15:25
    Aya
    Mk 15:25Yapata saa tatu asubuhi walipomsulibisha.
  • Giza tangu saa sita hadi saa tisaMt 27:45, Mk 15:33, Lk 23:44
    Aya
    Mt 27:45Sasa kutoka saa sita kulikuwa na giza katika nchi yote hadi saa tisa.
    Mk 15:33Ilipofika saa sita, giza likaja juu ya nchi yote hadi saa tisa.
    Lk 23:44Hapo ilikuwa karibu saa ya sita, giza likaja juu ya nchi yote hadi saa ya tisa,
  • Pilato: “Tazama, Mfalme wenu!” Ilikuwa karibu saa sitaYn 19:14
    Aya
    Yn 19:14Siku ya maandalizi ya pasaka ilipofika, panapo muda wa saa ya sita. Pilato akawaambia Wayahudi, “Tazameni mfalme wenu huyu hapa!”
  • Homa ilimwacha mwana wa afisa saa sabaYn 4:52
    Aya
    Yn 4:52Hivyo akawauliza ni muda gani alipata nafuu. Wakajibu, “Jana muda wa saa saba homa ilipomwacha.”
  • Wanafunzi wawili walikwenda na Yesu karibu saa kumiYn 1:39
    Aya
    Yn 1:39Akawambia, “Njooni na mwone.”Kisha walikwenda na kuona mahali alipokuwa akiishi; walikaa pamoja naye siku hiyo, kwa kuwa ilikuwa yapata kama saa kumi hivi.
  • Petro na Yohana walikwenda hekaluni saa tisa, saa ya maombiMdo 3:1
    Aya
    Mdo 3:1Sasa Peter na Yohana walikuwa wanaelekea katika hekalu wakati wa maombi, saa tisa.
  • Kornelio alikuwa akiomba saa tisaMdo 10:3, Mdo 10:30
    Aya
    Mdo 10:3Muda wa saa tisa za mchana, akaona maono Malaika wa Mungu anakuja kwake. Malaika akamwambia “Kornelio!
    Mdo 10:30Kornelio akasema, “Siku nne zilizopita, wakati kama huu nilikuwa naomba muda wa saa tisa mchana ndani ya nyumba yangu; Nikaona mbele yangu mtu amesimama akiwa na mavazi meupe,
  • Petro alipanda juu ya paa kuomba karibu saa sitaMdo 10:9
    Aya
    Mdo 10:9Siku iliyofuata muda wa saa sita wakiwa njiani na wamekaribia mjini, Petro akapanda juu darini kuomba.
  • Askari waliondoka kwenda Kaisaria saa tatu ya usikuMdo 23:23
    Aya
    Mdo 23:23Akawaita maakida wawili akasema watayarisheni askari mia mbili kwenda Kaisaria na askari wapanda farasi sabini, na wenye mikuki mia mbili, mtaondoka zamu ya tatu ya usiku.

Asubuhi, adhuhuri na usiku wa manane

  • Danieli aliomba mara tatu kwa siku, madirisha yake wazi kuelekea YerusalemuDan 6:10
    Aya
    Dan 6:10Danieli alipojua kuwa nyaraka imekwisha kusainiwa kuwa sheria, alienda ndani ya nyumba yake (madirisha yake katika chumba cha juu yalikuwa wazi kuelekea Yerusalemu), na alipiga magoti yake, kama alivyokuwa akifanya mara tatu kwa siku, na aliomba na kushukuru mbele ya Mungu wake, kama alivyofanya hapo kabla.
  • Zaburi: “Jioni, asubuhi na adhuhuri nitalia”Zab 55:17
    Aya
    Zab 55:17Wakati wa jioni, asubuhi na mchana ninalalamika na kuomboleza; yeye atasikia sauti yangu.
  • Abraham aliketi mlangoni pa hema lake wakati wa joto la mchanaMwa 18:1
    Aya
    Mwa 18:1Yahwe alimtokea Abraham katika Mialoni ya Mamre, alipokua ameketi mlangoni pa hema wakati wa jua.
  • Isaka alitoka kwenda shambani mapema jioniMwa 24:63
    Aya
    Mwa 24:63Isaka akaenda kutafakari shambani jioni. Alipotazama akaona, natazama, kulikuwa na ngamia wakija!
  • Wana kondoo wa Pasaka walichinjwa jioniKut 12:6
    Aya
    Kut 12:6Lazima umtunze mpaka siku ya kumi na nne ya huo mwezi. Kisha kusanyiko lote la Israeli lazima liwaue hawa wanyama jioni.
  • Eliya aliomba wakati wa dhabihu ya jioni1 Fal 18:36
    Aya
    1 Fal 18:36Ikawa wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, nabii Eliya akasogea na akasema, “BWANA, Mungu wa Abrahamu, na wa Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo kwamba wewe ndiye Mungu wa Israeli, na kwamba mimi ni mtumishi wako, na kwamba nimeyafanya mambo haya yote kwa jina lako.
  • Watu wa Nehemia walishika mikuki tangu alfajiri hadi nyota zilipotokeaNeh 4:21
    Aya
    Neh 4:21Kwa hiyo tulifanya kazi hiyo. Nusu yao walikuwa wakichukua mikuki kutoka kupambazuka asubuhi hadi kutokea kwa nyota.
  • Usiku wa manane Samsoni aling’oa milango ya lango la mji wa GazaAmu 16:3
    Aya
    Amu 16:3Samsoni akalala kitandani mpaka usiku wa manane. Usiku wa manane akaamka na akashika mlango wa jiji na miimo yake miwili. Akavivuta kutoka nje, komeo na vyote, akaviweka kwenye mabega yake, akavichukua hadi juu ya kilima, mbele ya Hebroni.
  • Usiku wa manane Boazi aliamka akakuta mwanamke amelala miguuni pakeRut 3:8
    Aya
    Rut 3:8Panapo usiku wa manane Boazi alisituka. Akajigeuza, na hapo mwanamke alikuwa amelala katika miguu yake!
  • Karibu usiku wa manane Paulo na Sila waliomba na kuimba nyimbo gerezaniMdo 16:25
    Aya
    Mdo 16:25Wakati wa usiku wa manane, Paulo na Sila wakawa wakiomba na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, huku wafungwa wengine wakiwasikiliza,
  • Paulo aliongea hadi usiku wa manane, na Eutiko akaanguka kutoka dirishaniMdo 20:7, Mdo 20:9
    Aya
    Mdo 20:7Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekusanyika pamoja ili kuumega mkate, Paulo alizungumza na Waamini. Alikuwa akipanga kuondoka kesho yake, hivyo akaendelea kuongea hadi usiku wa manane.
    Mdo 20:9Katika dirisha alikuwa amekaa kijana mmoja jina lake Utiko, ambaye alielemewa na usingizi mzito. Hata Paulo alipokuwa akihutubu kwa muda mrefu, kijana huyu, akiwa amelala, akaanguka chini kutoka ghorofa ya tatu na aliokotwa akiwa amekufa.
  • Jogoo aliwika mara ya pili, na Petro akakumbukaMk 14:30, Mk 14:72
    Aya
    Mk 14:30Yesu alimwambia, “Kweli nakuambia, usiku huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, utakuwa umenikana mara tatu.”
    Mk 14:72Kisha jogoo aliwika mara ya pili. Kisha Petro alikumbuka maneno ambayo Yesu aliyokuwa amemwambia: “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Na alianguka chini na kulia.
  • Mapema sana siku ya kwanza, jua lilipochomoza tu, walikwenda kaburiniMk 16:2
    Aya
    Mk 16:2Asubuhi na mapema siku ya kwanza ya juma, walienda kwenye kaburi wakati jua lilipochomoza.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0