Bible Explorer

Gundua › Mada › Majina mapya

Mambo ya kushangaza

Majina mapya katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (16), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Jina jema ni bora kuliko utajiri mwingiMit 22:1
    Aya
    Mit 22:1Jina jema huchaguliwa dhidi ya utajiri mwingi na fadhila ni bora kuliko fedha na dhahabu.

Mifano

  • Abram akawa AbrahamMwa 17:5
    Aya
    Mwa 17:5Wala jina lako halitakuwa tena Abram, bali jina lako litakuwa Abraham - kwa kuwa ninakuchagua kuwa baba wa mataifa mengi.
  • Sarai akawa SaraMwa 17:15
    Aya
    Mwa 17:15Mungu akamwambia Abraham, “kwa habari ya Sarai mkeo, usimuite tena Sarai. Badala yake jina lake litakuwa Sara.
  • Yakobo akawa IsraeliMwa 32:28
    Aya
    Mwa 32:28“Jina lako halitakuwa Yakobo tena, ila Israeli. Kwa kuwa umeshindana na Mungu na wanadamu na umeshinda.”
  • Raheli alimwita mwanawe Benoni; baba yake akamwita BenjaminiMwa 35:18
    Aya
    Mwa 35:18Hata alipokaribia kufa, kwa pumzi yake ya mwisho akamwita jina lake Benoni, lakini baba yake akamwita jina lake Benjamini.
  • Farao alimwita Yusufu Zafenathi PaneaMwa 41:45
    Aya
    Mwa 41:45Farao akamwita Yusufu jina la Zafenathi Panea.” Akampa Asenathi, binti wa Potifera kuhani wa On, kuwa mke wake. Yusufu akaenda juu ya nchi yote ya Misri.
  • Musa alimpa Hoshea mwana wa Nuni jina YoshuaHesabu 13:16
    Aya
    Hesabu 13:16Haya ndiyo majina ya wanaume ambao Musa aliwatuma kwenda kuipelelza ile nchi. Musa akamwita Hoshea mwana wa Nuni kwa jina la Joshua.
  • Naomi: msiniite Naomi, niiteni Mara (Mchungu)Rut 1:20
    Aya
    Rut 1:20Lakini aliwaambia, “Msiniite Naomi. Niiteni Mchungu, kwa kuwa Mwenyezi Mungu amenitenda mambo machungu sana.
  • Sulemani aliitwa pia Yedidia2 Sam 12:24–25
    Aya
    2 Sam 12:24–25Daudi akamfariji Bethsheba mkewe, akaingia kwake, na akalala naye. Baadaye akazaa mtoto wa kiume, naye akaitwa Selemani. Yahwe akampenda naye akatuma neno kupitia nabii Nathani kumwita Yedidia, kwa sababu Yahwe alimpenda.
  • Farao Neko alimbadilisha Eliakimu jina kuwa Yehoyakimu2 Fal 23:34
    Aya
    2 Fal 23:34Farao Neko akamfanya Eliakimu mwana wa Yosia mfalme katika mahali pa Yosia baba yake, na kubadilisha jina lake kuwa Yehoyakimu. Lakini akamchukua mfalme Yehoahazi kwenda Misri, na Yehoahazi akafia huko.
  • Mfalme wa Babeli alimbadilisha Matania jina kuwa Sedekia2 Fal 24:17
    Aya
    2 Fal 24:17Mfalme wa Babeli akamfanya Matania, kaka yake na baba yake na Yehokimu, mfalme katika sehemu yake, na kubadilisha jina lake kuwa Sedekia.
  • Danieli, Hanania, Mishaeli, Azaria: Belteshaza, Shadraka, Meshaki, AbedinegoDan 1:7
    Aya
    Dan 1:7Afisa mkuu aliwapa majina: Danieli alimwita Belteshaza, Hanania alimwita Shadraka, Mishaeli alimwita Meshaki, na Azaria alimwita Abedinego.
  • Simoni aliitwa Kefa, yaani, PetroYn 1:42
    Aya
    Yn 1:42Akamleta kwa Yesu. Yesu akamtazama na akasema, “Wewe ni Simoni mwana wa Yohana” utaitwa Kefa,” (maana yake 'Petro').
  • Yakobo na Yohana waliitwa Bonagesi, wana wa ngurumoMk 3:17
    Aya
    Mk 3:17Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana ndugu yake Yakobo, aliyepewa jina la Bonagesi, hao ni, wana wa ngurumo,
  • Yusufu wa Kipro aliitwa Barnaba, mwana wa farajaMdo 4:36
    Aya
    Mdo 4:36Yusufu, mlawi, mtu kutoka Kipro, alipewa jina la Barnabasi na mitume (hiyo ikitafasiriwa, ni mwana wa faraja).
  • Sauli, aliyeitwa pia PauloMdo 13:9
    Aya
    Mdo 13:9Lakini Sauli aliyeitwa Paulo, alikuwa amejazwa na Roho Mtakatikfu, akamkazia macho

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0