Mambo ya kushangaza
Dubu katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (7), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
- Daudi aliwapiga simba na dubu waliochukua wana-kondoo1 Sam 17:34–37
Aya
1 Sam 17:34–37Lakini Daudi akamwambia Sauli, “Mtumishi wako alikuwa akichunga kondoo za baba yake. Mara simba au dubu alikuja akamchukua mwana kondoo kutoka kundini, Nilimfukuza na kumshambulia na kumpokonya kutoka kinywani mwake. Na aliponirukia, nilimshika ndevu zake, nilimpiga, na kumuua. Mtumishi wako amekwisha kmuua simba na dubu. N huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wa wanyama hao, kwa kuwa ameyadharau majeshi ya Mungu aliye hai.” Daudi akasema, “BWANA aliyeniokoa kutoka makucha ya simba na makucha ya dubu. Ataniokoa kutoka mkono wa Mfilisti huyu.” Kisha Sauli akamwambia Daudi, “Nenda, BWANA awe pamoja nawe.”
- Dubu wawili wa kike waliwararua vijana arobaini na wawili waliomdhihaki Elisha2 Fal 2:23–24
Aya
2 Fal 2:23–24Ndipo Elisha akapanda kutoka pale mpaka Betheli. Naye alipokuwa akienda hadi kwenye barabara, wakatokea vijana nje ya mji na kumtania, wakamwambia, “Panda juu, wewe mwenye kipara! Panda juu, wewe mwenye kipara!” Elisha alipotazama nyuma yake na kuwaona; alimwambia Yahwe awalaani. Ndipo dubu wa kike wawili wakatokea kichakani na kuwajeruhi vijana arobaini na mbili.
- Daudi na watu wake ni wakali kama dubu aliyenyang’anywa watoto wake2 Sam 17:8
Aya
2 Sam 17:8Hushai akaongeza, “Unamjua baba yako na kwamba watu wake ni mashujaa na kwa sasa wanauchungu, ni kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake mwituni. Baba yako ni mtu wa vita; hatalala na jeshi usiku huu.
- Afadhali kukutana na dubu aliyenyang’anywa watoto kuliko mpumbavu katika upumbavu wakeMit 17:12
Aya
Mit 17:12Ni bora kukutana na dubu aliyeporwa watoto wake kuliko kukutana na mpumbavu katika upumbavu wake.
- Mtawala mkali ni kama dubu anayeshambuliaMit 28:15
Aya
Mit 28:15Kama simba anayeunguruma au dubu anayeshabulia ni kama mtawala mwovu juu ya watu masikini.
- Kumkimbia simba, na kukutana na dubuAmo 5:19
Aya
Amo 5:19kama wakati mtu anamkimbia simba na kukutana na dubu, au aliingia katika nyumba na kuweka mkono wake kwenye ukuta na kung'atwa na nyoka.
- Sote tunanguruma kama dubuIsa 59:11
Aya
Isa 59:11Sisi tunaunguruma kama dubu na kuomboleza kama njiwa; tunasubiria haki, lakini hakuna kitu; kwa ukombozi, lakini uko mbali na sisi.
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0