Bible Explorer

Gundua › Mada › Maisha marefu

Mambo ya kushangaza

Maisha marefu katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (37), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Kabla ya gharika Yahwe anaweka kikomo cha siku za mwanadamuMwa 6:3
    Aya
    Mwa 6:3Yahwe akaema, “ roho yangu haitasalia kwa mwanadamu milele, kwa kuwa wao ni nyama. Wataishi miaka 120.”
  • Zaburi: siku zetu ni miaka sabini, au themanini tukiwa na nguvuZab 90:10
    Aya
    Zab 90:10Miaka yetu ni sabini, au themanini tukiwa na afya; lakini hata hivyo miaka yetu mizuri imetiwa alama ya taabu na huzuni. Ndiyo, inapita haraka, kisha tunatoweka.

Kabla ya gharika

  • Adamu aliishi miaka 930Mwa 5:5
    Aya
    Mwa 5:5Adamu akaishi miaka 930 kisha akafariki.
  • Sethi aliishi miaka 912Mwa 5:8
    Aya
    Mwa 5:8Sethi akaishi miaka 912 kisha akafariki.
  • Enoshi aliishi miaka 905Mwa 5:11
    Aya
    Mwa 5:11Enoshi aliishi miaka 905 na kisha akafariki.
  • Kenani aliishi miaka 910Mwa 5:14
    Aya
    Mwa 5:14Kenani aliishi miaka 910, na kisha akafariki.
  • Mahalaleli aliishi miaka 895Mwa 5:17
    Aya
    Mwa 5:17Mahalaleli aliishi miaka 895 na kisha akafariki.
  • Yaredi aliishi miaka 962Mwa 5:20
    Aya
    Mwa 5:20Yaredi aliishi miaka 962 na kisha akafariki.
  • Henoko: miaka 365, kisha hakuonekana tenaMwa 5:23–24
    Aya
    Mwa 5:23–24Henoko aliishi miaka 365. Henoko alienenda na Mungu, na kisha alitoweka, kwa kuwa Mungu alimtwaa.
  • Methusela aliishi miaka 969Mwa 5:27
    Aya
    Mwa 5:27Methusela aliishi miaka 969. Kisha akafariki.
  • Lameki aliishi miaka 777Mwa 5:31
    Aya
    Mwa 5:31Lameki aliishi miaka 777. Kisha akafariki.
  • Nuhu aliishi miaka 350 baada ya gharika, 950 kwa jumlaMwa 9:28–29
    Aya
    Mwa 9:28–29Baada ya gharika, Nuhu aliishi miaka miatatu na hamsini. Siku zote za Nuhu zilikuwa ni miaka mia tisa na hamsini, na kisha alikufa.

Baada ya gharika

  • Shemu: mwana akiwa na miaka 100, kisha miaka mingine 500Mwa 11:10–11
    Aya
    Mwa 11:10–11Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya Shemu. Shemu alikuwa na umri wa miaka mia moja, na akamzaa Alfaksadi miaka miwili baada ya gharika. Shemu akaishi miaka miatano baada ya kumzaa Alfaksadi. Pia akazaa wana wengine wa kiume na wa kike.
  • Alfaksadi: mwana akiwa na miaka 35, kisha miaka mingine 403Mwa 11:12–13
    Aya
    Mwa 11:12–13Wakati Alfaksadi alipokuwa ameishi miaka thelathini na mitano akamzaa Shela. Alfaksadi aliishi miaka 403 baada ya kumzaa Shela. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
  • Shela: mwana akiwa na miaka 30, kisha miaka mingine 403Mwa 11:14–15
    Aya
    Mwa 11:14–15Wakati Shela alipokuwa ameishi miaka thelathini, akamzaa Eberi. Shela aliishi miaka 403 baada ya kumzaa Eberi. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
  • Eberi: mwana akiwa na miaka 34, kisha miaka mingine 430Mwa 11:16–17
    Aya
    Mwa 11:16–17Wakati Eberi alipokuwa ameishi miaka thelathini na minne, akamzaa Pelegi. Eberi aliishi miaka 430 baada ya kumzaa Pelegi. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
  • Pelegi: mwana akiwa na miaka 30, kisha miaka mingine 209Mwa 11:18–19
    Aya
    Mwa 11:18–19Wakati Pelegi alipokuwa ameishi miaka thelathini, akamzaa Reu. Pelegi aliishi miaka 209 baada ya kumza a Reu. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
  • Nahori: mwana akiwa na miaka 29, kisha miaka mingine 119Mwa 11:24–25
    Aya
    Mwa 11:24–25Wakati Nahori alipokuwa ameishi miaka ishirini na tisa, akamzaa Tera. Nahori aliishi mika 119 baada ya kumzaa Tera. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
  • Tera aliishi miaka 205 na akafa HaraniMwa 11:32
    Aya
    Mwa 11:32Tera akaishi miaka 205 kisha akafa hapao Harani.

Maisha ya baadaye

  • Sara aliishi hadi miaka 127Mwa 23:1
    Aya
    Mwa 23:1Sara akaishi mika mia moja na ishirini na saba. Hii ndiyo ilikuwa ni miaka ya maisha ya Sara.
  • Abraham aliishi miaka 175Mwa 25:7
    Aya
    Mwa 25:7Hizi ndizo zilikuwa siku za miaka ya uhai wake Abraham alizoishi, miaka 175.
  • Ishmaeli naye aliishi maisha marefuMwa 25:17
    Aya
    Mwa 25:17Hii ndiyo ilikuwa miaka ya Ishimaeli, miaka 137: akapumua pumzi yake ya mwisho na akafa, na akakusanywa pamoja na watu wake.
  • Isaka aliishi miaka 180Mwa 35:28
    Aya
    Mwa 35:28Isaka akaishi miaka mia moja na themanini.
  • Yakobo aliishi miaka 147, kumi na saba ya mwisho huko MisriMwa 47:28
    Aya
    Mwa 47:28Yakobo akaishi katika nchi ya Misri miaka kumi na saba, kwa hiyo miaka ya maisha ya Yakobo ilikuwa miaka mia moja arobaini na saba.
  • Yusufu alikufa akiwa na miaka 110 na akapakwa dawa huko MisriMwa 50:26
    Aya
    Mwa 50:26Hivyo Yusufu akafa, mwenye miaka 110. Wakampaka dawa na akawekwa katika jeneza huko Misri.
  • Lawi aliishi miaka 137, Kohathi 133, Amramu 137Kut 6:16, Kut 6:18, Kut 6:20
    Aya
    Kut 6:16Hapa yameorodheshwa majina ya wana wa Lawi, pamoja na uzo wao. Walikuwa ni Gerishoni, Kohathi, na Merari. Lawi aliishi mpaka alipo kuwa na miaka 137.
    Kut 6:18Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Izhari, Hebroni, na uzieli. Kohathi aliishi hadi miaka 133.
    Kut 6:20Amramu alimuoa Yokebedi, dada yake baba yake. Alimzalia Aruni na Musa. Amramu aliishi miaka 137 na akafa.
  • Haruni alikufa juu ya Mlima Hori akiwa na miaka 123Hesabu 33:39
    Aya
    Hesabu 33:39Haruni alikuwa na umri wa mika 123 alipokufa pale juu ya Mlima Hori.
  • Musa alikufa akiwa na miaka 120, macho yake hayakufifiaKum 34:7
    Aya
    Kum 34:7Musa alikuwa na umri wa miaka mia moja na ishirini alipokufa; macho yake hayakufifia, wala nguvu asili zake hazikupungua.
  • Kalebu akiwa na miaka 85: bado na nguvu kama siku Musa alipomtumaYos 14:10–11
    Aya
    Yos 14:10–11Tazama! sasa, Yahweh amenihifadhi hai kwa miaka hii arobaini na tano, kama alivyosema - tangu kipindi kile Yahweh alivyomwambia Musa neno hili, wakati huo Waisraeli walikuwa wakitembea jangwani. Tazama! sasa katika siku hii ya leo nina miaka themanini na mitano. Bado hata siku hii ya leo nina nguvu kama nilivyokuwa katika siku ile ambayo Musa alinituma. Nguvu zangu za sasa ni sawa na nguvu zangu za kipindi kile, kwa ajili ya vita na kwa kwenda na kwa kuja.
  • Yoshua alikufa akiwa na miaka 110Yos 24:29
    Aya
    Yos 24:29Baada ya mambo haya, Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Yahweh, alikufa akiwa na miaka 110.
  • Eli alikuwa na miaka 98 na hakuweza kuona1 Sam 4:15
    Aya
    1 Sam 4:15Basi Eli alikuwa na umri wa miaka tisini na nane; macho yake yamepofuka, na hakuweza kuona.
  • Barzilai, mwenye miaka themanini, alikuwa amemhudumia Mfalme Daudi2 Sam 19:32
    Aya
    2 Sam 19:32Basi Berzilai alikuwa mzee sana mwenye umri wa miaka themanini. Alikuwa amemsaidia mfalme kwa mahitaji alipokuwako Mahanaimu kwani alikuwa na mali nyingi.
  • Kuhani Yehoyada alikufa akiwa na miaka 1302 Nya 24:15
    Aya
    2 Nya 24:15Yehoyada akazeeka na alaaikuwa amejaa siku, na kisha akafa; alikuwa na umri wa mika 130 alipokufa.
  • Ayubu aliishi miaka mingine 140 na akaona vizazi vinneAyu 42:16–17
    Aya
    Ayu 42:16–17Baada ya haya, Ayubu aliishi miaka 140; aliwaona wana wake na wana wa wanawe, hata kizazi cha nne. Basi Ayubu alifariki, akiwa mzee na akijawa na siku nyingi.
  • Ana, mjane mpaka miaka themanini na minne, hakuondoka hekaluniLk 2:36–37
    Aya
    Lk 2:36–37Nabii mwanamke aliyeitwa Ana pia alikuwako hekaluni. Yeye alikuwa binti wa Fanueli kutoka kabila la Asheri. Alikuwa na miaka mingi sana. Naye aliishi na mume wake kwa miaka saba baada ya kuoana, na ndipo akawa mjane kwa miaka themanini na minne. Naye hakuwahi kuondoka hekaluni na alikuwa akiendelea kumwabudu Mungu pamoja na kufunga na kuomba, usiku na mchana.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0