Maisha ya kila siku
Ugomvi katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (32), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
Mifano
- Wachungaji wa Abram na wa Lutu wanagombana, hivyo wawili wanatenganaMwa 13:7–9
Aya
Mwa 13:7–9Pia, kulikuwa na ugomvi kati ya wachunga wanyama wa Abram na wachunga wanyama wa Lutu. Wakanaani pamoja na Waperizi walikuwa wakiishi katika nchi ile wakati huo. Kwa hiyo Abram akamwambia Lutu, “Pasiwe na ugomvi kati yako na mimi, na kati ya wachunga wanyama wako na wachunga wanyama wangu; licha ya hayo sisi ni familia. Je nchi hii yote haiko mbele yako? Nenda na ujitenge na mi. Ikiwa utakwenda kushoto, mimi nitakwenda kulia. au ikiwa utakwenda kulia, mimi nitakwenda kushoto.”
- Abraham analalamika kuhusu kisima kilichonyang’anywa na watumishi wa AbimelekiMwa 21:25
Aya
Mwa 21:25Abraham pia akamlalamikia Abimeleki kuhusu kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki wamekinyang'anya.
- Musa anawakuta Waebrania wawili wakipiganaKut 2:13, Mdo 7:26
Aya
Kut 2:13Alienda tena siku iliyofuata, na tazama, Waebrania wawili walikuwa wanapigana. Alimwambia yule aliyekuwa na makosa, “Kwa nini unampigia mwenzako?”
Mdo 7:26Siku iliyofuata akaenda kwa baadhi ya Waisraeli waliokuwa wanagombana; akajaribu kuwapatanisha; akisema,' Mabwana, Ninyi ni ndugu; mbona mnakoseana ninyi kwa ninyi,?
- Musa hawezi kubeba peke yake migogoro yote ya watuKum 1:12
Aya
Kum 1:12Lakini inawezekanaje mimi peke yangu kubeba shehena zako, mizigo yako, na migogoro yako?
- Efraimu wanamtisha Yeftha; “Shibolethi” kwenye vivuko vya YordaniAmu 12:1–6
Aya
Amu 12:1–6Watu wa Efraimu walitoka pamoja; nao wakapitia Zafoni, wakamwambia Yeftha, Kwa nini umetangulia kupigana na wana wa Amoni, wala hukutuita twende pamoja nawe? Tutachoma nyumba yako. Yeftha akawaambia, Mimi na watu wangu tulikuwa katika vita kubwa na wana wa Amoni. Nilipokuita, hukuniokoa kutoka kwao. Nilipoona ya kuwa hamkuniokoa, nikaweka uhai wangu na nguvu yangu mwenyewe, na kupita kipita ili kupigana na wana wa Amoni, na Bwana alinipa ushindi. Kwa nini mmekuja kupigana nami leo?” Yeftha akawakusanya watu wote wa Gileadi na akapigana na Efraimu. Watu wa Gileadi waliwaangamiza wana wa Efraimu kwa sababu walisema, “Ninyi Wagileadi ni wakimbizi katika Efraimu-katika Efraimu na Manase.” Wagileadi waliteketeza ngome za Yordani zinaelekea Efraimu. Ikiwa yeyote kati ya waliopona wa Efraimu akisema, Nipe ruhusa niende juu ya mto; watu wa Gileadi wakamwambia, “Je, wewe ni Mwefraimu?” Ikiwa akasema, “Hapana,” basi watamwambia, Sema Shiboleth. Na kama akisema 'Sibboleth' (kwa maana hakuweza kutamka neno hilo kwa usahihi), Wagileadi watamkamata na kumwua kwenye mabwawa ya Yordani. Waefraimu elfu arobaini waliuawa wakati huo.
- Hadithi ya mwanamke wa Tekoa: wana wawili wanapigana shambani2 Sam 14:6
Aya
2 Sam 14:6Mimi, mtumishi wako, nilikuwa na wana wawili, wakagombana shambani, na hakukuwa na wa kuwaachanisha. Mmoja wao akampiga mwenziwe na kumwua.
- Wanafunzi wanabishana nani kati yao ni mkubwa zaidiMk 9:33–34, Lk 22:24
Aya
Mk 9:33–34Ndipo walifika Karperinaumu. Wakati akiwa ndani ya nyumba aliwauliza, ''Mlikuwa mnajadili nini njiani”? Lakini walikuwa kimya. Kwani walikuwa wanabishana njiani kwamba nani alikuwa mkubwa zaidi.
Lk 22:24Kisha yakatokea mabishano katikati yao kwamba ni nani anaye dhaniwa kuwa mkuu kuliko wote.
- Mjadala mkali huko Antiokia kuhusu toharaMdo 15:1–2
Aya
Mdo 15:1–2Watu fulani walishuka kutoka Uyahudi na kuwafundisha ndugu, wakisema, “msipotahiriwa kama desturi ya Musa, hamwezi kuokolewa.” Wakati Paulo na Barnaba walipokuwa na mapambano na mjadala pamoja nao, ndugu waliamua kwamba Paulo, Barnaba, na wengine kadhaa waende Yerusalem kwa mitume na wazee kwa ajili ya swali hili.
- Paulo na Barnaba wanatengana kwa sababu ya MarkoMdo 15:37–39
Aya
Mdo 15:37–39Barnaba alihitaji pia kumchukua pamoja nao Yohana aliyeitwa Marko. Lakini Paulo alifikiria haikuwa vizuri kumchukua Marko, aliyewaacha huko Pamfilia na hakuendelea nao katika kazi. Kisha hapo kukatokea mabishano makubwa kwa hiyo walitengana, na Barnaba alimchukua Marko na kusafiri kwa meli mpaka Kipro,
- Mafarisayo na Masadukayo wanagombana kuhusu ufufuoMdo 23:7–10
Aya
Mdo 23:7–10Alipoyasema haya, malumbano makubwa yakatokea baina ya Mafarisayo na Masadukayo, na mkutano ukagawanyika. Kwani Masadukayo husema hakuna ufufuo, malaika wala hakuna roho, ila Mafarisayo husema haya yote yapo. Ghasia kubwa ikatokea na baadhi ya waandishi waliokuwa upande wa Mafarisayo wakasimama na kujadili, wakisema, “hatujaona chochote kibaya dhidi ya mtu huyu. Vipi kama roho au malaika ameongea na yeye?” Wakati kulitokea hoja kubwa, mkuu wa majeshi aliogopa kwamba Paulo angeraruliwa vipande vipande na wao, hivyo akaamuru wanajeshi washuke chini na kumchukua kwa nguvu kutoka kwa wajumbe wa baraza, na kumleta katika ngome.
- Paulo anampinga Kefa uso kwa uso huko AntiokiaGal 2:11
Aya
Gal 2:11Wakati Kefa alipokuja Antiokia, nilimpinga waziwazi kwa sababu alikuwa amekosea.
- Wakorintho: “Mimi ni wa Paulo,” “Mimi ni wa Apolo”1 Kor 1:11–12
Aya
1 Kor 1:11–12Kwani watu wa nyumba ya Kloe wamenitaarifu kuwa kuna mgawanyiko unaoendelea miongoni mwenu. Nina maana hii: Kila mmoja wenu husema, “Mimi ni wa Paulo,” au “Mimi ni wa Apolo”, au “Mimi ni wa Kefa” au “Mimi ni wa Kristo”.
- Waumini wanashtakiana mahakamani1 Kor 6:6–7
Aya
1 Kor 6:6–7Lakini kama ilivyo sasa, mwamini mmoja huenda mahakamani dhidi ya muumini mwingine, na mashitaka hayo huwekwa mbele ya hakimu asiyeamini! Ukweli ni kwamba kuna matatizo katikati ya Wakristo yaliyoleta tayari usumbufu kwenu. Kwanini msiteseke kwa mabaya? Kwanini mnakubali kudanganywa?
- Paulo anawasihi Eudia na Sintike wapataneFlp 4:2
Aya
Flp 4:2Ninakusihi wewe Eudia, pia ninakusihi wewe Sintike, mrejeshe mahusiano ya amani kati yenu, kwa sababu ninyi, nyote wawili mliungana na Bwana.
Katika Sheria
- Aliyeumizwa katika ugomvi analipwa kwa kazi iliyopotea na matibabuKut 21:18–19
Aya
Kut 21:18–19Kama wanaume watapigana na mmoja akimpiga mwengine kwa jiwe au ngumi, na huyo mtu asife, lakini alazwe kitandani; kisha akapona na anaweza kutembea kwa gongo lake, yeye aliye mpiga lazima alipe muda aliye mpotezea; na lazima alipe matibabu yake yote. Lakini huyo mtu hana hatia ya mauaji.
- Ugomvi kati ya watu unapelekwa mahakamani kuamuliwaKum 25:1
Aya
Kum 25:1Iwapo kutakuwa na malumbano kati ya wanaume na wakaenda mahakamani, na waamuzi wakawahukumu, basi watamwachilia mtakatifu na kumhukumu muovu.
Katika Mithali
- Chuki huchochea ugomvi; upendo hufunika makosaMit 10:12
Aya
Mit 10:12Chuki huchochea mafarakano, bali upendo hufunika juu ya makwazo yote.
- Mtu mwenye hasira huchochea ugomviMit 15:18, Mit 29:22
- Afadhali kipande cha mkate mkavu kwa utulivu kuliko karamu yenye ugomviMit 17:1
Aya
Mit 17:1Ni bora kuwa na utulivu pamoja chembe za mkate kuliko nyumba yenye sherehe nyingi pamoja na ugomvi.
- Kuanzisha ugomvi ni kama kufungulia mafurikoMit 17:14
Aya
Mit 17:14Mwanzo wa mafarakano ni kama mtu anayefungulia maji kila mahali, hivyo ondoka kwenye mabishano kabla ya kutokea.
- Ni heshima kuacha ugomvi; kila mpumbavu hugombanaMit 20:3
Aya
Mit 20:3Ni heshima kwa mtu yeyote kujiepusha na mafarakano, bali kila mpumbavu hurukia kwenye mabishano.
- Mfukuze mwenye dharau, na ugomvi utakomaMit 22:10
Aya
Mit 22:10Mfukuze mbali mwenye dhihaka, na ugomvi utaondoka, mashindano na matukano yatakoma.
- Kujiingiza katika ugomvi wa mwingine ni kama kumshika mbwa masikioMit 26:17
Aya
Mit 26:17Kama mtu anayeshikilia masikio ya mbwa, ndivyo alivyo mpitajia anayepata hasira kwenye ugomvi ambao si wake.
- Mke mgomvi ni kama kudondoka kwa maji daima siku ya mvuaMit 27:15, Mit 25:24
Kwingineko
- Patana upesi na mshtaki wako mkiwa njiani kwenda mahakamaniMt 5:25
Aya
Mt 5:25Patana na mshitaki wako upesi, ukiwa pamoja naye njiani kuelekea mahakamani, vinginevyo mshtaki wako anaweza kukuacha mikononi mwa hakimu, na hakimu akuache mikononi mwa askari, nawe utatupwa gerezani.
- Ikiwezekana, ishini kwa amani na watu woteRum 12:18
Aya
Rum 12:18Kama inawezekana, kama ilivyowekwa kwenu, muwe na amani na watu wote.
- Maswali ya kipumbavu huzaa ugomvi2 Tim 2:23–24
Aya
2 Tim 2:23–24Lakini ukatae upumbavu na maswali ya kipuuzi. Kwani unajua ya kuwa huzaa ugomvi. Mtumishi wa Bwana hapaswi kugombana, badala yake inampasa kuwa mpole kwa watu wote, awezaye kufundisha, na mvumilivu.
- “Ni nini kinachosababisha vita na ugomvi kati yenu?”Yak 4:1
Aya
Yak 4:1Ugonvi na migogoro miongoni mwenu vyatoka wapi? Haviinuki kutoka katika tamaa zenu mbaya zinazoleta vita ndani ya washirika wenu?
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0