Gundua › Mada › Uwindaji na mitego
Maisha ya kila siku
Uwindaji na mitego katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (14), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
- Nimrodi, “mwindaji hodari mbele za Bwana”Mwa 10:9
Aya
Mwa 10:9Alikuwa mwindaji mkuu mbele ya Yahwe. Hii ndiyo sababu hunenwa, “Kama Nimrod mwindaji mkuu mbele za Yahwe.”
- Ishmaeli anakua nyikani na kuwa mpiga upinde hodariMwa 21:20
Aya
Mwa 21:20Mungu akawa pamoja na kijana, na akakua. Akaishi jangwani akawa mwindaji.
- Esau anakuwa mwindaji stadi, mtu wa nyikaniMwa 25:27
Aya
Mwa 25:27Vijana hawa wakakua, Hesau akawa mwindaji hodari, mtu wa nyikani; lakini Yakobo alikuwa mtu mkimya, aliye tumia muda wake akiwa katika mahema.
- Isaka anapenda nyama ya mawindo na anampenda EsauMwa 25:28
Aya
Mwa 25:28Kisha Isaka akampenda Esau kwa sababu alikula wanyama ambao alikuwa anawinda, lakini Rebeka akampenda Yakobo.
- Isaka anamtuma Esau na podo na upinde kuwindaMwa 27:3–5
Aya
Mwa 27:3–5Kwahiyo chukua silaha zako, podo lako na upinde wako, na uende uwandani ukaniwindie mnyama. Uniandalie chakula kitamu, aina ile niipendayo, uniletee ili nikile na kukubariki kabla sijafa. Basi Rebeka akasikia Isaka alipoongea na Esau mwanawe. Esau akaenda uwandani kuwinda mawindo na kuja nayo.
- Esau anarudi kutoka kuwinda akiwa amechelewa kwa barakaMwa 27:30–33
Aya
Mwa 27:30–33Mara Isaka alipomaliza kumbariki Yakobo, na Yakobo ndo ametoka mbele ya Isaka baba yake, Esau ndugu yake akaja kutoka kuwinda. Yeye pia akaandaa chakula kitamu na kukileta kwa baba yake. Akamwambia baba yake, “Baba, inuka na ule baadhi ya mawindo ya mwanao, ili uweze kunibariki.” Isaka baba yake akamwambia, “U nani wewe? Akasema, “Mimi ni mwanao, Esau, mzaliwa wako wa kwanza.” Isaka akatetemeka sana na kusema, “Alikuwa nani aliyewinda mawindo nakuniletea? Nilikula chote kabla haujaja, nami nimembariki. Atabarikiwa, kwa kweli.”
Katika Sheria
Mitego na nyavu
- Wavu, matundu, mtego, tanzi na kamba iliyofichwa ardhiniAyu 18:8–10
Aya
Ayu 18:8–10Kwa maana yeye atatupwa katika mtego kwa miguu yake mwenyewe; yeye atatembea katika mahangaiko. Tanzi litamchukua yeye kwa kisigino; mtego utabaki kushikilia juu yake. Tanzi limefichwa kwa ajili yake chini ya ardhi; na mtego kwa ajili yake katika njia.
- Paa aliyenaswa wavuniIsa 51:20
Aya
Isa 51:20Watoto wako walizimia; walilala kila kona ya mtaa, kama swala kwenye mtego; Wamejawa na hasira ya Yahwe, Laana ya Mungu wako.
- Wawindaji wa ndege huvizia na kutega mitegoYer 5:26
Aya
Yer 5:26Kwa watu waovu wamo kati ya watu wangu. Wanatazama kama mtu anayenyatia ili kukamata ndege; wanaweka mitego na kukamata watu;
- Kamba za wavu zimetandazwa njiani, na chambo kimewekwaZab 140:5
Aya
Zab 140:5Wenye majivuno wameweka mtego kwa ajili yangu; wameeneza nyavu; wameweka kitanzi kwa ajili yangu. Selah
Ulinganisho
- Daudi: kama mtu awindaye kwale milimani1 Sam 26:20
Aya
1 Sam 26:20Kwa hiyo, sasa, usiiachilie damu yangu ianguke ardhini mbali na uwepo wa BWANA; kwa kuwa mfalme wa Israeli ametoka nje kutafuta kiroboto, kama vile mtu awindavyo kware milimani.”
- “Adui zangu wameniwinda kama ndege”Omb 3:52
Aya
Omb 3:52Nimewindwa kama ndege hao walio kuwa maadui zangu; wameniwinda pasipo sababu.
- Ameokolewa “kutoka mtego wa mwindaji”Zab 91:3
Aya
Zab 91:3Kwa maana yeye atakuokoa dhidi ya mtego wa mwindaji na dhidi ya pigo liletalo mauti.
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0