Bible Explorer

Gundua › Mada › Mabusu

Maisha ya kila siku

Mabusu katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (32), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

Salamu na kuagana

  • Yakobo anambusu Raheli kisimani na kulia kwa sautiMwa 29:11
    Aya
    Mwa 29:11Yakobo akambusu Raheli na akalia kwa sauti.
  • Labani anawabusu wajukuu na binti zake kwa kuwaagaMwa 31:55
    Aya
    Mwa 31:55Labani akaamka asubuhi na mapema, akawabusu wajuu zake na binti zake na kuwabariki. Kisha Labani akaondoka na kurudi kwake.
  • Esau anakimbia kwa Yakobo, anamkumbatia na kumbusuMwa 33:4
    Aya
    Mwa 33:4Esau akakimbia kumlaki, akamkumbatia, akakumbatia shingo yake na kumbusu. Kisha wakalia.
  • Yusufu anawabusu ndugu zake wote, akiliaMwa 45:15
    Aya
    Mwa 45:15Akawabusu ndugu zake wote na kulia kwa ajili yao. Baada ya hayo ndugu zake wakaongea naye.
  • Haruni anakutana na Musa kwenye mlima wa Mungu na kumbusuKut 4:27
    Aya
    Kut 4:27Yahwe akamwambia Aroni, “Nenda nyikani ukutane na Musa.” Aroni akaenda na kukutana naye katika mlima wa Mungu, na kumbusu.
  • Musa anamsujudia mkwewe na kumbusuKut 18:7
    Aya
    Kut 18:7Musa alitoka kwenda kukutana na baba mkwe wake, akamwinamia, na kumbusu. Wakajuliana hali na wakaingia ndani ya hema.
  • Naomi anawabusu wakwe zake; Oripa anambusu kwa kumuagaRut 1:9, Rut 1:14
    Aya
    Rut 1:9Mungu awajalie ninyi kupata pumziko, kila mmoja wenu katika nyumba ya mme mwingine.” Kisha akawabusu, na wakapaza sauti zao na kulia.
    Rut 1:14Ndipo wake wa watoto wake wakapaza sauti zao na kulia tena. Oripa alimuaga kwa kumbusu, lakini Ruth aliendelea kubaki naye.
  • Daudi na Yonathani wanabusiana na kulia pamoja1 Sam 20:41
    Aya
    1 Sam 20:41Punde tu kijana alipoondoka, Daudi akasimama kutokea upande wa kusini, akiwa amelala kifudifudi, akainama mara tatu. Walibusiana wao kwa wao na wote wakalia kwa pamoja, Daudi akilia zaidi.
  • Daudi anambusu Barzilai kando ya Yordani2 Sam 19:39
    Aya
    2 Sam 19:39Kisha watu wote wakavuka Yordani, mfalme naye akavuka, kisha mfalme akambusu Berzilai na kumbariki. Kisha Berzilai akarudi nyumbani kwake.
  • Elisha anaomba kuwabusu baba yake na mama yake kwa kuwaaga1 Fal 19:20
    Aya
    1 Fal 19:20Elisha naye akawaacha wale makisai akamkimbilia Eliya; akamwambia, “Tafadhali naomba nikambusu baba yangu na mama yangu kisha nitakufuata.” Naye Eliya akamwambia, “Rudi, lakini fikiria juu ya kile nilichokufanyia.”
  • Baba anakimbia kwa mwanawe anayerudi na kumbusuLk 15:20
    Aya
    Lk 15:20Ndipo akaondoka akaenda kwa baba yake. Alipokua angali mbali baba yake alimuona akamwonea huruma akaenda mbio na kumkumbatia na kumbusu.
  • Wazee wa Efeso wanamkumbatia Paulo na kumbusuMdo 20:37
    Aya
    Mdo 20:37Wote wakalia sana na kumwangukia Paulo shingoni na kumbusu.

Familia na mapenzi

  • Isaka: “Sogea karibu unibusu, mwanangu”Mwa 27:26–27
    Aya
    Mwa 27:26–27Kisha Isaka baba yake akamwambia, “Sogea karibu nami na unibusu, mwanangu.” Yakobo akasogea na kumbusu, naye akanusa harufu ya nguo zake na kumbariki. Akasema, “Tazama, harufu ya mwanangu ni kama harufu ya shamba alilolibariki Yahwe.
  • Yakobo mzee, karibu kipofu, anawabusu wana wa YusufuMwa 48:10
    Aya
    Mwa 48:10Basi macho ya Israeli yalikuwa yanashindwa kwa ajili ya umri wake, hivyo hakuweza kuona. Hivyo Yusufu akawasogeza karibu yake, na akawabusu na kuwakumbatia.
  • Yusufu analia juu ya baba yake aliyekufa na kumbusuMwa 50:1
    Aya
    Mwa 50:1Yusufu akahuzunika sana hata akauangukia uso wa baba yake, akamlilia, na kumbusu.
  • Samweli anampaka Sauli mafuta na kumbusu1 Sam 10:1
    Aya
    1 Sam 10:1Ndipo Samweli akachukua chupa ya mafuta, akayamimina juu ya kichwa cha Sauli, na akambusu. Akasema, “Je, Mungu hajakutia mafuta uwe mtawala juu ya urithi wake?
  • Mfalme Daudi anambusu Absalomu baada ya kurudi kwake2 Sam 14:33
    Aya
    2 Sam 14:33Hivyo Yoabu akaenda kwa mfalme na kumwambia. Mfalme alipomwita, Absalomu alikuja kwa mfalme na akainama hadi juu ya uso nchi mbele ya mfalme na mfalme akambusu Absalomu.
  • “Na anibusu kwa mabusu ya kinywa chake!”Wim 1:2
    Aya
    Wim 1:2O, laiti ungenibusu na mabasu ya mdomo wako, kwa kuwa upendo wako ni bora kuliko mvinyo.
  • Jibu la kweli ni kama busu midomoniMit 24:26
    Aya
    Mit 24:26Anayetoa jibu la kweli hutoa busu kwenye midomo.

Mabusu ya udanganyifu

  • Mabusu ya adui ni ya udanganyifuMit 27:6
    Aya
    Mit 27:6Mwaminifu ni jeraha zilizosababishwa na rafiki, lakini adui anaweza kukubusu kwa kuomba radhi mno.
  • Absalomu anawavuta watu kwa kuwabusu2 Sam 15:5
    Aya
    2 Sam 15:5Hivyo ikawa kila mtu aliyekuja kumweshimu Absalomu yeye hunyosha mkono na kumshika na kumbusu.
  • Yoabu anashika ndevu za Amasa kana kwamba ambusu, na kumchoma2 Sam 20:9–10
    Aya
    2 Sam 20:9–10Hivyo Yoabu akamwambia Amasa, “Haujambo binamu yangu?” Kwa utaratibu Yoabu akakishika kidevu cha Amasa kwa mkono wake wa kulia ili ambusu. Amasa hakutambua kwamba kulikuwa na jambia katika mkono wa kushoto wa Yoabu. Yoabu akamchoma Amasa tumboni na matumbo yake yakadondoka chini. Wala Yoabu hakumpiga tena, na Amasa akafa. Hivyo Yoabu na Abishai nduguye wakamfuatia Sheba mwana wa Bikri.
  • Yuda: “Nitakayembusu ndiye huyo”Mt 26:48–49, Lk 22:48
    Aya
    Mt 26:48–49Tena mtu aliyekusudia kumsaliti Yesu alikuwa amewapa ishara, akisema, “Yule nitakayembusu, ndiye yeye. Mkamateni.” Mara hiyo alikuja kwa Yesu na kusema, “Salamu, Mwalimu!” Na akambusu.
    Lk 22:48lakini Yesu akamwambia, “Yuda, je unamsaliti Mwana wa Adamu kwa busu?”

Ibada na kanisa la kwanza

  • Kubusu sanamu: Baali na ndama1 Fal 19:18, Hos 13:2
    Aya
    1 Fal 19:18Lakini nitawaacha watu elfu saba katika Israeli kwa ajili yangu, ambao magoti yao hayajawahi kupigwa kwa Baali, na ambao midomo yao haijambusu.”
    Hos 13:2Sasa wanafanya dhambi zaidi na zaidi. Wanatengeneza sanamu za chuma kutoka kwenye fedha zao, sanamu kwa kadiri ya ufanisi wao, zote ni kazi ya mafundi. Watu wanasema juu yao, 'Watu hawa watoao dhabihu na kumbusu ndama.'
  • Mwanamke anabusu miguu ya Yesu; mwenyeji wake hakumpa busuLk 7:38, Lk 7:45
    Aya
    Lk 7:38Alisimama nyuma yake karibu na miguu yake huku akilia. Tena alianza kulowanisha miguu yake kwa machozi, na kuifuta kwa nywele za kichwa chake, akiibusu miguu yake na kuipaka manukato.
    Lk 7:45Hukunibusu, lakini yeye, tangu alipoingia humu hakuacha kunibusu miguu yangu.
  • Salimianeni kwa busu takatifuRum 16:16, 1 The 5:26, 1 Pet 5:14
    Aya
    Rum 16:16Nisalimie kila mmoja kwa busu takatifu. Makanisa yote katika Kristo yawasalimu.
    1 The 5:26Wasalimuni ndugu wote kwa busu takatifu.
    1 Pet 5:14Salimianeni kila mmoja kwa busu la upendo. Na amani iwe kwenu mliondani ya Kristo.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0