Bible Explorer

Gundua › Mada › Ulafi

Maisha ya kila siku

Ulafi katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (18), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Unakula na mtawala? Weka kisu kooni mwakoMit 23:1–3
    Aya
    Mit 23:1–3Unapoketi kula pamoja na mtawala, angalia kwa uangalifu kilichopo mbele yako, na kama ni mtu unayependa kula chakula sana weka kisu kooni. Usitamani vinono vyake maana ni chakula cha uongo.
  • Ukipata asali, kula kiasi kinachokutosha tuMit 25:16
    Aya
    Mit 25:16Kama utapata asali, kula ya kutosha- vingenevyo, ukila nyingi sana, utaitapika.
  • Rafiki wa walafi humwaibisha baba yakeMit 28:7
    Aya
    Mit 28:7Yeye anayetunza sheria ni mwana mwenye ufahamu, bali mwenye ushirika na walafi humwaibisha baba yake.
  • Usijiunge na wale wanaojishibisha kwa nyamaMit 23:20–21
    Aya
    Mit 23:20–21Usishirikiane pamoja na walevi, au pamoja na walaji wa nyama walafi, maana mlevi na mlafi wanakuwa masikini na usingizi utawavika kwa matambara.
  • Heri nchi ambayo wakuu wake hula kwa wakati ufaaoMhu 10:17
    Aya
    Mhu 10:17Lakini umebarikiwa ardhi kama mfalme wako ni mwana wa waungwana, na kama vingozi wako hula wakati muafaka, kwa nguvu, na sio kwa ulevi.
  • “Na tule na kunywa, kwa kuwa kesho tutakufa!”Isa 22:13, 1 Kor 15:32
    Aya
    Isa 22:13Lakini angalia, badala yake sherehe na furaha, kuuwa ng'ombe na kuchinga kondoo, njooni tule na kunjwa mvinjo maana kesho tutakufa.
    1 Kor 15:32Inanifaidia nini, katika mtazamo wa wanadamu, kama nilipigana na wanyama wakali huko Efeso, kama wafu hawafufuliwi? “Acha basi tule na kunywa, kwa kuwa kesho tunakufa.”
  • Wakijinyoosha juu ya vitanda vya pembe, wakila wana-kondoo na ndamaAmo 6:4
    Aya
    Amo 6:4Wamelala juu ya vitanda vya pembe na kupumzika juu ya viti vyao. Wakala wana kondoo kutoka kwenye kundi na ndama kutoka kwenye zizi.
  • Tajiri mpumbavu: “Kula, kunywa, ufurahi!”Lk 12:19–20
    Aya
    Lk 12:19–20Nitaiambia nafsi yangu, “Nafsi, umejiwekea akiba ya vitu vingi kwa miaka mingi. Pumzika, ule, unywe na kustarehe.” Lakini Mungu akamwambia, ewe mtu mpumbavu, usiku wa leo wanahitaji roho kutoka kwako, na vitu vyote ulivyoviandaa vitakuwa vya nini?
  • “Mungu wao ni tumbo lao”Flp 3:19
    Aya
    Flp 3:19Mwisho wao ni uharibifu. Kwa kuwa Mungu wao ni tumbo, na kiburi chao kiko katika aibu yao. Wanafikiria mambo ya kidunia.
  • Mmoja wao: “Wakrete ni… wavivu na walafi”Tit 1:12
    Aya
    Tit 1:12Mmoja wao, mtu mwenye busara, alisema, “Wakrete wana uongo usio na mwisho, wabaya na wanyama wa hatari, wavivu na walafi.”

Mifano

  • Esau mwenye njaa anauza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa mchuzi mwekunduMwa 25:29–34
    Aya
    Mwa 25:29–34Yakobo akapika mchuzi. Esau akaja kutoka nyikani, akiwa dhaifu kutokana na njaa. Esau akamwambia Yakobo, “Nilishe mchuzi mwekundu. Tafadhari, nimechoka!” Na hii ndiyo sababu jina lake aliitwa Edomu. Yakobo akasema, “Kwanza uniuzie haki yako ya mzaliwa wa kwanza.” Esau akasema, “Tazama, nakaribia kufa. Ni nini kwangu haki ya mzaliwa wa kwanza?” Yakobo akasema, “Kwanza uape kwangu mimi,” kwa hiyo Esau akaapa kiapo na kwa njia hii akawa ameuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa Yakobo. Yakobo akampatia Esau mkate pamoja na mchuzi wa dengu. Akala na kunywa, kisha akainuka na akaenda zake. Kwa njia hii Esau akawa ameidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.
  • Israeli wanalilia samaki, matango na matikiti ya MisriHesabu 11:4–6, Zab 78:18
    Aya
    Hesabu 11:4–6Baadhi ya wageni wakaanza kuweka kambi zao pamoja na wana wa wa Israeli. Walitaka kula chakula kizuri. Kisha wana wa Israeli walipoanza kulia wakisema, “Ni nani atakayetupatia nyama za kula? Tunakumbuka samaki tulizokula bure kule Misri, yale matango, na matikiti maji, na mboga na vitunguu na vitunguu saumu. Na sasa hatuna hamu ya kula, kwa sababu tunaona mana tu.
    Zab 78:18Walimjaribu Mungu mioyoni mwao kwa kuomba chakula cha kuwatosheleza hamu zao.
  • Watu wanakusanya kware siku mbili; tauni inafuataHesabu 11:31–33
    Aya
    Hesabu 11:31–33Kisha upepo ukavuma kutoka kwa BWANA ukaja na kware kutokea baharini. Wakaanguka karibu na kambi, kiasi cha umbali wa safari ya siku moja upande huu na umbali wa siku moja upande mwingine. Wale kware wakaizunguka kambi kiasi cha mita moja toka uso wa dunia. Watu wakawakusanya hao kware kwa bidii mchana huo wote na usiku huo wote, na mchana wote uliofuatia. Hakuna aliyekusanya pungufu ya mita mbili za uajazo. Wakawaanika kweye ardhi yote hapo kambini. Wakati ile nyama ikiwa bado iko kwenye meno yao, wakiwa bado wanatafuna, BWANA akawakasirikia. Akwapiga watu wale kwa gonjwa kubwa sana.
  • Mtumishi wa wana wa Eli ananyakua nyama kwa uma wa meno matatu1 Sam 2:12–17
    Aya
    1 Sam 2:12–17Basi, watoto wa Eli walikuwa wakorofi. Wao hawakumheshimu BWANA. Desturi ya makuhani na watu ilikuwa kwamba endapo mtu yeyote ametoa dhabihu, mtumishi wa kuhani angekuja akiwa na uma wa meno matatu mkononi mwake, nyama ilipokuwa inatokoswa. Naye angeutia uma huo sufuriani, au birikani au chomboni au chunguni; nyama yote ambayo ingeinuliwa na uma huo ingetwaliwa na kuhani mwenyewe. Ndivyo walivyofanya huko Shilo kwa Waisraeli wote waliokwenda huko. Tena, kabla ya kuteketeza mafuta, mtumishi wa kuhani alikuja, na kumwambia aliyekuwa akitoa dhabihu, “ Tenga nyama ya kuchoma kwa ajili ya kuhani; kwa sababu hataikubali ile ya kutokosa kutoka kwako, bali tu ile mbichi.” Ikiwa mtu atamwambia, “Wachome mafuta kwanza, na kisha uchukue kiasi utakacho.” Ndipo angesema, “Hapana, utanipatia sasa hivi; la sivyo; Nitaichukua kwa lazima.” Dhambi ya vijana hawa ilikuwa mbaya sana mbele za BWANA, kwa sababu waliidharau dhabihu ya BWANA.
  • Mwana mkaidi anashtakiwa kuwa “mlafi na mlevi”Kum 21:20
    Aya
    Kum 21:20Wanapaswa kuwaambia wazee wa mji, “Huyu mwanetu ni mkaidi na muasi; hataki kusikia sauti zetu; ni mwasherati na pia ni mlevi’.
  • Yesu anaitwa “mlafi na mlevi”Mt 11:19
    Aya
    Mt 11:19Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa na wakasema 'Angalia, ni mtu mlaji na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi!' Lakini hekima inadhihirishwa kwa matendo yake.''

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0