Bible Explorer

Gundua › Mada › Hasira

Maisha ya kila siku

Hasira katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (41), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

Misemo

  • Jawabu la upole hugeuza hasira; neno kali huichocheaMit 15:1
    Aya
    Mit 15:1Jawabu la upole huondoa ghadhabu, bali neno la ukatili huchochea hasira.
  • Mvumilivu ni bora kuliko shujaaMit 16:32, Mit 14:29
    Aya
    Mit 16:32Ni bora kukawia kuwa na hasira kuliko kuwa shujaa na mwenye kutawala roho yake ni imara zaidi kuliko yule anayeuteka mji.
    Mit 14:29Mtu mvumilivu anaufahamu mkubwa, bali mtu mwepesi wa kuhamaki hukuza upuuzi.
  • Mtu asiyejitawala ni kama mji wenye kuta zilizobomokaMit 25:28
    Aya
    Mit 25:28Mtu bila kujitawala ni kama mji ulibomolewa na usiokuwa na kuta.
  • Mpumbavu huimwaga hasira yake yote; mwenye hekima huizuiaMit 29:11
    Aya
    Mit 29:11Mpumabavu huonyesha hasira yake, bali mtu mwenye busara huishikilia na kujituliza mwenyewe.
  • Kama kusukasuka maziwa huleta siagi, kuchochea hasira huleta ugomviMit 30:33
    Aya
    Mit 30:33Kama kusuka maziwa hufanya siagi na pua ya mtu hutoa damu kama imepigwa, basi matendo yanayofanywa kwa hasira huzalisha mafarakano.
  • Hasira hukaa kifuani mwa wapumbavuMhu 7:9
    Aya
    Mhu 7:9Usikasirike haraka rohoni mwako, kwa sababu hasira hukaa katika mioyo ya wapumbavu.
  • Acha hasira; huleta madhara tuZab 37:8
    Aya
    Zab 37:8Usikasilile na kugadhabika. Usiogope. Hii huleta matatizo tu.
  • Jua lisichwe mkiwa bado na hasiraEfe 4:26
    Aya
    Efe 4:26Mwe na hasira, lakini msitende dhambi.” Jua lisizame mkiwa katika hasira zenu.
  • Mwepesi wa kusikia, si mwepesi wa kusema, si mwepesi wa hasiraYak 1:19–20
    Aya
    Yak 1:19–20Mnajua hili, ndugu zangu wapendwa. Kila mmoja anapaswa kuwa mwepesi wa kusikia, siyo mwepesi wa kuongea wala kukasirika, kwa kuwa hasira ya mwanadamu haiwezi kutenda haki ya Mungu.

Mifano

  • Kaini anakasirika sana na kumuua ndugu yake HabiliMwa 4:5–8
    Aya
    Mwa 4:5–8lakini Kaini pamoja na sadaka yake Mungu hakuikubali. Kwa hiyo Kaini alikasirika sana, na uso wake ukakunjamana. Yahwe akamwambia Kaini, “ kwa nini umekasirika na kwa nini uso wako umekunjamana? Kama ukifanya vema, je hutapata kibali? lakini kama hutafanya lilio jema, dhambi iko inakuotea mlangoni na inatamani kukutawala, lakini inakupasa uishinde. Kaini akamwambia Habili ndugu yake. Hata wakati walipokuwa shambani, Kaini aliinuka dhidi ya Habili ndugu yake na akamuua. (Katika tafsiri za kale zinasema, Kaini alimwambia Habili ndugu yake, “ twende mashambani.” Na wakati walipokuwa shambani, Kaini alimuinukia Habili ndugu yake na kumuua).
  • Yakobo kwa Raheli: “Je, mimi ni badala ya Mungu?”Mwa 30:2
    Aya
    Mwa 30:2Hasira ya Yakobo ikawaka juu ya Raheli. Akasema, “Mimi ni badala ya Mungu, aliyekuzuilia usipate watoto?
  • Yakobo, akiwa na hasira, anamkabili LabaniMwa 31:36
    Aya
    Mwa 31:36Yakobo akakasirika na kuojiana na Labani. Akamwambia, “Kosa langu ni nini? Dhambi yangu ni ipi, hata ukanifuatia kwa ukali?
  • Yakobo: Simoni na Lawi “waliua watu katika hasira yao”Mwa 49:5–7
    Aya
    Mwa 49:5–7Simoni na Lawi ni ndugu. Panga zao ni silaha za vurugu. Ee nafsi yangu, usiingie barazani pao; usiingie katika mikutano yao, kwani moyo wangu unaheshima kubwa kwa ajili yao. Kwani katika hasira yao waliua watu. Iliwapendeza kuwakata visigino ng'ombe. Hasira yao na ilaaniwe, kwani ilikuwa kali - na ukali wao, kwani ulikuwa ni katili. Nitawagawa katika Yakobo na kuwatawanya katika Israeli.
  • Bwana wa Yusufu anawaka hasira kwa habari ya mke wakeMwa 39:19
    Aya
    Mwa 39:19Ikawa, bwana wake aliposikia maelezo aliyoambiwa na mkewe, “Hivi ndivyo mtumishi wako alivyonitenda,” alikasirika sana.
  • Farao kwa Musa: “Usione uso wangu tena”Kut 10:28
    Aya
    Kut 10:28Farao alimwambia Musa, “Toka kwangu! Kuwa muangalifu na jambo moja, kwamba usinione tena, kwa kuwa siku utakapo uona uso wangu, utakufa.”
  • Akiwaka hasira, Musa anaondoka kwa FaraoKut 11:8
    Aya
    Kut 11:8Watumishi wote hawa wako, Farao, watakuja chini yangu na kunisujudu mimi. Watasema, 'Nenda, wewe na watu wote wanao kufuata!' Baada ya hapo nitaondoka.” Kisha akaondoka mbele ya Farao kwa hasira kubwa.
  • Musa anavunja mbao za mawe anapoona ndamaKut 32:19
    Aya
    Kut 32:19Hata alipoyakaribia kambini akaiona ile ndama, na watu wakicheza. Hasira ya Musa ikawaka. Akazitupa zile mbao mikononi mwake, akazivunja chini ya mlima.
  • Musa anaupiga mwamba mara mbiliHesabu 20:10–11
    Aya
    Hesabu 20:10–11Kisha Musa na Haruni wakawakusanya watu pamoja mbele ya ule mwamba. Ndipo Musa akawaambia, “Sasa sikilizeni, enyi wapinzani. Lazima tuwape maji kutoka kwenye huu mwamba?” Ndipo Musa akanyosha mkono wake na kuupiga ule mwamba mara mbili kwa fimbo yake, na maji mengi yakatoka. Wale watu wakanywa pamoja na wanyama wao.
  • Balaamu anampiga punda wake, naye anaongeaHesabu 22:27–29
    Aya
    Hesabu 22:27–29Yule Punda akamwona tena yule malaika wa BWANA, akalala chini ya Balaamu. Hasira za Balaamu zikawaka, akampiga yule punda kwa fimbo yake. Kisha BWANA akafungua kinywa cha punda na akaongea. Akamwambia Balaamu, “Nimekukosea nini kiasi kwamba umenipiga mara tatu?” Balaamu akamjibu yule punda, “Ni kwa sababu umenitendea kwa ujinga. Natamani kama ningekuwa na upanga mkononi mwangu, kama ningekuwa nao, sasa hivi ningekuwa nimekuua.”
  • Balaki anapiga makofi kwa hasira dhidi ya BalaamuHesabu 24:10
    Aya
    Hesabu 24:10Hasira za Balaki zikawaka dhidi ya Balaamu naye akaipiga mikono yake kwa pamoja. Balaki akamwambia Balaamu, “Nilkuita ili uwalaani maadui zangu, Lakini tazama, umewabariki mara tatu.
  • Gideoni anawatuliza watu wa Efraimu wenye hasira kwa jibu la upoleAmu 8:1–3
    Aya
    Amu 8:1–3Watu wa Efraimu wakamwambia Gideoni, “Ni nini hiki umetutenda? Haukuita wakati ulipokwenda kupigana na Midiani.” Wakamwambia kwa nguvu. Akawaambia, “Nimefanya nini sasa kulinganisha na mlichofanya ninyi? Je! Mavuno ya zabibu za Efraimu si bora zaidi kuliko mavuno ya zabibu ya Abiezeri? Mungu amewapa ushindi juu ya wakuu wa Midiani-Orebu na Zeeb! Mimi nimefanya nini ukilinganisha na ninyi?” Hasira yao ikashuka chini aliposema hili.
  • Eliabu anawaka hasira dhidi ya ndugu yake mdogo Daudi1 Sam 17:28
    Aya
    1 Sam 17:28Kaka yake mkubwa Eliabu, alisikia wakati akisema na watu. Hasira ya Eliabu ikawaka moto dhidi ya Daudi, naye akamuuliza, “Kwa nini umekuja hapa? Wale kondoo wachache umewaacha na nani huko nyikani? Nakijua kiburi chako, na utundu wa moyo wako; maana umekuja hapa ili uweze kuona mapigano.”
  • Sauli anamrushia mwanawe Yonathani mkuki1 Sam 20:30–34
    Aya
    1 Sam 20:30–34Ndipo hasira ya Sauli iliwaka juu ya Yonathani, na akamwambia, “Wee mwana wa mwanamke mkaidi na muasi! Wadhani kwamba sijui kuwa umemchagua Mwana wa Yese kwa ajili ya aibu yako, na kwa aibu ya uchi wa mama yako? Kwa kuwa mwana wa Yese anaishi duniani, siyo wewe wala ufalme wako utakaoimarika. Sasa basi, tuma watu wamlete kwangu, kwa sababu inampasa kufa.” Yonathani akamjibu Sauli baba yake, “Kwa sababu gani inampasa kuuwawa? Amefanya nini?” Ndipo Sauli akamtupia mkuki apate kumuua. Kwa hiyo Yonatani akatambua kwamba baba yake alinuia kumuua Daudi. Yonathani alitoka mezani akiwa na hasira kali bila kula chakula siku ya pili ya mwezi, kwa sababu alimhuzunikia Daudi, na kwa sababu baba yake amemwaibisha.
  • Daudi anawaka hasira kwa hadithi ya Nathani kuhusu tajiri2 Sam 12:5
    Aya
    2 Sam 12:5Hasira ya Daudi ikawaka dhidi ya tajiri yule, naye akamwambia Nathani kwa hasira, “Kama Yahwe aishivyo, mtu aliyelitenda jambo hili anastahili kufa.
  • Ahabu, mwenye huzuni na hasira, anakataa kula1 Fal 21:4
    Aya
    1 Fal 21:4Ahabu akaingia kwenye ikulu yake akiwa mchovu na mwenye hasira kwa sababu ya jibu ambalo Nabothi Myezreeli alimpa aliposema, “Sitakupa urithi wa mababu zangu.” Akalala kitandani kwake, akiwa amegeuza uso wake upande ule, na akagoma kula chakula chochote.
  • Naamani: je, mito ya Dameski si bora kuliko Yordani?2 Fal 5:11–12
    Aya
    2 Fal 5:11–12Lakini Naamani alikasirika na kuondoka na kusema, “Tazama, Nilidhani bila shaka angekuja kwangu na kusimama na kuliita jina la Yahwe Mungu wake, na kupitisha mkono wake kwenye sehemu ya ugonjwa na kuponya ukoma wangu. Je sio Abana na Faepari, mito ya Damaskasi, bora kuliko maji yote ya Israeli?” Je siwezi kuoga ndani yao na kuwa safi?” Hivyo akageuka na kwenda kwa hasira.
  • Asa anamtupa mwonaji gerezani2 Nya 16:10
    Aya
    2 Nya 16:10hili. Wakati huo huo, aliwagandamiza baadhi ya watu
  • Uzia anawakasirikia makuhani akiwa na chetezo mkononi2 Nya 26:19
    Aya
    2 Nya 26:19Kisha Uzia akakasirika. Alikuwa ameshikilia chetezo mkononi kwa ajili ya kufukiza uvumba. Wakati alipowaghadhabikia makuhani, ukoma ukatokea juu ya uso wake mbele ya makuhani katika nyumba ya Yahwe, pembeni mwa madhabahu ya uvumba.
  • Ahasuero anakasirika sana malkia Vashiti anapokataa kujaEst 1:12
    Aya
    Est 1:12Pamoja na maagizo ya Mfalme, Malkia Vashiti alikataa kwenda kama alivyokuwa amewaagiza viongozi wake. Hivyo mfalme akakasirika sana; ghadhabu yake ikawaka ndani yake
  • Hamani anajaa ghadhabu Mordekai asipomsujudiaEst 3:5
    Aya
    Est 3:5Hamani alipoona kuwa Modekai hapigi magoti wala kumsujudia, alipatwa na hasira.
  • Elihu anawaka hasira dhidi ya Ayubu na marafiki zake watatuAyu 32:2–3
    Aya
    Ayu 32:2–3Ndipo iliwaka hasira ya Elihu mwana wa Barakeli Mbuzi, wa familia ya Ramu, iliwaka dhidi ya Ayubu kwa kuwa alijihesabia haki mwenyewe kuliko Mungu. Hasira ya Elihu iliwaka pia kinyume cha marafiki zake watatu kwasababu hawakupata jibu kwa ajili ya Ayubu, na bado walimhukumu Ayubu.
  • Nebukadneza anaitia tanuru moto mara saba zaidiDan 3:13, Dan 3:19
    Aya
    Dan 3:13Ndipo Nebukadneza alijawa na hasira na ghadhabu, aliagiza kwamba Shadraka, Meshaki na Abednego waletwe kwake. Hivyo, waliwalete hawa watu mbele ya mfalme.
    Dan 3:19Ndipo Nebukadneza alijawa na ghadhabu; mwonekano wa uso wake ulibadilika kinyume na Shadraka, Meshaki na Abedinego. Aliagiza kuwa tanuru lichochewe ukali mara saba zaidi kuliko lilivyokuwa kawaida.
  • Yona kuhusu mmea uliokauka: “nina hasira hata kufa”Yon 4:1, Yon 4:9
    Aya
    Yon 4:1Lakini hili lilimchukiza Yona naye akakasirika.
    Yon 4:9Kisha Mungu akamwambia Yona, “Je, ni vema wewe kuwa na hasira juu ya mmea?” Yona akasema, Ni vyema kuwa nimekasirika hata kufa.
  • Herode, akidanganywa na wasomi wa mashariki, anajaa ghadhabuMt 2:16
    Aya
    Mt 2:16Kisha Herode, alipoona kuwa amedhihakiwa na watu wasomi, alikasirika sana. Aliagiza kuuawa kwa watoto wote wa kiume waliokuwa Bethelehemu na wote katika eneo lile ambao walikuwa na umri wa miaka miwili na chini yake kulingana na wakati aliokuwa amekwisha thibitisha kabisa kutoka kwa wale watu wasomi.
  • Watu wa sinagogi la Nazareti wanataka kumtupa Yesu gengeniLk 4:28–29
    Aya
    Lk 4:28–29Watu wote ndani ya sinagogi walijawa na gadhabu walipoyasikia haya yote. Walisimama na kumsukumizia nje ya mji, na kumwongoza mpaka kwenye ukingo wa mlima wa mji ambapo mji wao ulijengwa juu yake, ili waweze kumtupa chini.
  • Yesu anatazama pande zote kwa hasira kwa ugumu wa mioyo yaoMk 3:5
    Aya
    Mk 3:5Akawaangalia kwa hasira, akihuzunika kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao, na akamwambia yule mtu, “Nyoosha mkono wako”. Akaunyoosha na Yesu akamponya mkono wake.
  • Baraza, likiwa na ghadhabu, linamsagia meno StefanoMdo 7:54–58
    Aya
    Mdo 7:54–58Kisha wajumbe wa baraza waliposikia mambo haya, walichomwa mioyo yao, wakamsagia meno Stefano. Lakini yeye, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, alitazama mbinguni kwa makini na akauona utukufu wa Mungu,' na kumwona Yesu amesimama mkono wa kuume wa Mungu. Stefano akasema, “Angalia nimeona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adam amesimama mkono wa kuume wa Mungu.” Lakini wajumbe wa baraza wakapiga kelele kwa sauti za juu, wakaziba masikio yao, wakamkimbilia kwa pamoja, wakamtupa nje ya mji na wakampiga mawe: na mashahidi wakavua nguo zao za nje na kuweka chini karibu na miguu ya kijana aliyeitwa Sauli.
  • Paulo kwa kuhani mkuu: “Wewe ukuta uliopakwa chokaa!”Mdo 23:3
    Aya
    Mdo 23:3Ndipo Paulo akamwambia, “Mungu atakupiga wewe, ukuta uliopakwa chokaa. Umekaa ukinihukumu kwa sheria, nawe unaamuru nipigwe kinyume cha sheria?”

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0