Bible Explorer

Gundua › Mada › Kuzaliwa na utasa

Maisha ya kila siku

Kuzaliwa na utasa katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (39), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

Kuzaliwa

  • Mwanamke katika uchungu husahau maumivu yake kwa furaha ya kuzaliwaYn 16:21
    Aya
    Yn 16:21Mwanamke anakuwa na huzuni wakati anapokuwa na uchungu kwa sababu wakati wa kujifungua umefika; lakini anapojifungua mtoto, hakumbuki tena maumivu kwa sababu ya furaha yake kwamba mtoto amezaliwa duniani.
  • Wakunga Waebrania Shifra na Pua, na viti vya kuzaliaKut 1:15–16
    Aya
    Kut 1:15–16Kisha mfalme wa Misri akawaambia wakunga wa Kiebrania; mmoja wao aliitwa jina lake Shifra, na mwingine aliitwa Puha. Akasema, “Wakati mnapowasaidia wanawake wa Kiebrania wanapojifungua, chunguzeni wanapozaa. Ikiwa ni mtoto wa kiume, basi muueni; bali ikiwa ni mtoto wa kike, basi mwacheni aishi.”
  • Wanawake Waebrania “huzaa kabla mkunga hajafika”Kut 1:19
    Aya
    Kut 1:19Wale Wakunga wakamjibu Farao, “Hawa wanawake wa Kiebrania siyo kama wanawake wa Kimisri. Hawa wana nguvu na jasiri sana maana wao humaliza kuzaa kabla hata mkunga hajafika.”
  • Raheli anapata uchungu mzito; mkunga anasema, “Mwana mwingine”Mwa 35:16–17
    Aya
    Mwa 35:16–17Wakaendelea na safari kutoka Betheli. Walipokuwa kitambo kabla ya kufika Efrathi, Raheli akashikwa na uchungu. Akawa na utungu mzito. Alipokuwa katika utungu mzito zaidi, mkunga akamwambia, “Usiogope, kwani sasa utapata mtoto mwingine wa kiume.”
  • Raheli anakufa njiani kwenda BethlehemuMwa 35:18–19
    Aya
    Mwa 35:18–19Hata alipokaribia kufa, kwa pumzi yake ya mwisho akamwita jina lake Benoni, lakini baba yake akamwita jina lake Benjamini. Raheli akafa na kuzikwa katika njia iendayo Efrathi (ndio Bethlehemu).
  • Mke wa Finehasi anazaa akisikia habari na kufa1 Sam 4:19–20
    Aya
    1 Sam 4:19–20Basi mkwewe, mke wa Finihasi, alikuwa mjamzito akikaribia kujifungua. aliposikia habari kwamba sanduku la Mungu limetekwa nyara na kwamba baba mkwe na mme wake wamefariki, alichuchumaa chini akajifungua, lakini utungu wake ulimzidi na ulimtaabisha sana. Alipokaribia kufariki, wanawake waliokuwa wakimhudumia walisema, “Usiogope, maana umejifungua mtoto wa kiume.” Lakini hakuwajibu lolote au kuzingatia alichoambiwa.
  • Baada ya mwana, mama ni najisi siku saba, kisha anangoja kutakaswaLaw 12:2–4
    Aya
    Law 12:2–4“zungumza na watu wa Israeli, uwaambie, 'endapo mwanamke anakuwa mjamzito na kujifungua mtoto wa kiume, naye atakuwa najisi kwa muda wasiku saba, ni kama tu vile anavyokuwa najisi katika siku za kipindi chake kwa mwezi. Katika siku ya nane nyama ya govi la mtoto mvulana itatahiriwa. Kisha utakaso wa mama wa kutokwa damu yake utaendelea kwa muda wa siku tatu. Haimpasi kugusa kitu chochote kilicho kitakatifu au kukaribia eneo la hema mpaka zitakapomalizika siku za kutakaswa kwake.
  • Baada ya binti, wiki mbili za unajisi, kisha utakaso mrefu zaidiLaw 12:5
    Aya
    Law 12:5Lakini kama atajifungua mtoto wa kike, naye atakuwa najisi kwa mud wa majuma mawili, kama alivyo wakati wa kipindi chake. Kisha utakaso wa mama utaendelea kwa siku sitini sita.
  • Kisha mwana kondoo na ndege hutolewa, au ndege wawili ikiwa ni maskiniLaw 12:6, Law 12:8
    Aya
    Law 12:6Siku za kutakaswa kwake zitakapoisha, kwa ajili ya mwana au binti, atalazimika kuleta kwa kuhani mwana-kondoo wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa, na kinda la njiwa au huwa kuwa sadaka ya dhambi, mbele ya ingilio la hema la kukutania,
    Law 12:8Na kama hana uwezo wa kutoa mwana-kondoo, naye ataleta makinda mawili ya njiwa ua hua, mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na mwingine kuwa sadaka ya dhambi, naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake; naye atakuwa safi.”
  • Majirani na jamaa wa Elizabeti wanafurahi pamoja nayeLk 1:57–58
    Aya
    Lk 1:57–58Sasa wakati ulikuwa umewadia kwa Elizabeti kujifungua mtoto wake na akajifungua mtoto wa kiume. Jirani zake na ndugu zake walisikia jinsi Bwana alivyoikuza rehema kwake, na wakafurahi pamoja naye.

Walezi

  • Mlezi wa Rebeka anakwenda pamoja naye KanaaniMwa 24:59
    Aya
    Mwa 24:59Kwa hiyo wakampeleka dada yao Rebeka, pamoja na watumishi wake wa kike, kwenda njiani pamoja na mtumishi wa Abraham na watu wake.
  • Sara: “Nani angemwambia Abraham kwamba Sara atanyonyesha watoto?”Mwa 21:7
    Aya
    Mwa 21:7Pia akasema, “Nani angesema kwa Abraham kwamba Sara atalea mtoto, na sasa kweli nimemzalia mtoto wakiume katika uzee wake!”
  • Musa: “Uwabebe … kama mlezi ambebavyo mtoto mchanga”Hesabu 11:12
    Aya
    Hesabu 11:12Je, mimi ndiye niliyewatungia mimba hawa watu? Mimi ndiye niliyewazaa kiasi kwamba unaniambia, “wabebe kwa ukaribu vifuani mwako kama baba abebavyo mtoto wake? Je, nitawabeba mpaka kwenye nchi ambayo uliwaahidi mababu zao kuwapa?
  • Paulo: mpole, kama mama anayenyonyesha akiwatunza watoto wake1 The 2:7
    Aya
    1 The 2:7Badala yake tulikuwa wapole kati yenu kama mama awafarijivyo watoto wake mwenyewe.

Muda mrefu bila watoto

  • Sarai alikuwa tasa; hakuwa na watotoMwa 11:30
    Aya
    Mwa 11:30Sasa Sarai alikuwa Tasa; hakuwa na mtoto.
  • Sarai anampa Abram mjakazi wake Hagari ili apate jamaaMwa 16:1–2
    Aya
    Mwa 16:1–2Kisha Sarai mke wa Abram, alikuwa hajamzalia mtoto, lakini alikuwa na mtumishi wa kike, Mmisri ambaye jina lake aliitwa Hajiri. Kwa hiyo Sarai akamwambia Abram, “Tazama, Yahwe hajanifanya mimi kuwa na watoto. Nenda na ulale na mtumishi wangu. Ili kwamba niweze kupata watoto kupitia yeye.” Abram akasikiliza sauti ya Sarai.
  • Sara anacheka: amepita umri wa kuzaaMwa 18:11–14
    Aya
    Mwa 18:11–14Abraham na Sara walikuwa wazee, umri wao ulikuwa umeendelea sana, na Sara alikuwa amepita umri ambao mwanamke anaweza kuzaa watoto. Kwa hiyo Sara akajicheka mwenyewe, akijisemesha mwenyewe, “baada ya kuwa nimechakaa na bwana wangu ni mzee, je ni tapata furaha hii?” Yahwe akamwambia Abraham, “Kwa nini Sara amecheka na kusema, Je ni kweli nitazaa mtoto, nikiwa mzee'? Je kuna jambo lolote gumu sana kwa Yahwe? Itakuwa katika wakati nilioweka mimi majira ya machipuko, nitarejea kwako. Majira haya mwakani Sara atakuwa na mtoto wa kiume.”
  • Sara anamzaa Isaka; Abraham ana miaka mia mojaMwa 17:17, Mwa 21:2, Mwa 21:5
    Aya
    Mwa 17:17Kisha Abraham akainama uso wake hadi ardhini, na akacheka, akasema moyoni mwake, Je yawezekana mtoto azaliwe kwa mwanaume ambaye ana umri wa miaka miamoja? na Je Sara, ambaye ana umri wa miaka tisini anaweza kuzaa mwana?”
    Mwa 21:2Sara akachukua mimba na akamzalia Abraham mtoto wa kiume katika uzee wake, katika muda ule ule ambao Mungu alikuwa amemwambia.
    Mwa 21:5Abraham alikuwa na umri wa miaka mia moja wakati mwanawe Isaka anazaliwa kwake.
  • Isaka anamwombea Rebeka aliye tasa, naye anapata mimbaMwa 25:21
    Aya
    Mwa 25:21Isaka akamwomba Yahwe kwa ajili ya mke wake kwa sababu alikuwa tasa, na Yahwe akajibu maombi yake, Rebeka mkewe akabeba mimba.
  • Raheli: “Nipe watoto, la sivyo nitakufa!”Mwa 30:1–2
    Aya
    Mwa 30:1–2Raheli alipoona kwamba hamzalii Yakobo watoto, Raheli akamwonea wivu dada yake. Akamwambia Yakobo, “Nipe watoto, sivyo nitakufa.” Hasira ya Yakobo ikawaka juu ya Raheli. Akasema, “Mimi ni badala ya Mungu, aliyekuzuilia usipate watoto?
  • Raheli na Lea wanapatana kuhusu tungujaMwa 30:14–16
    Aya
    Mwa 30:14–16Siku za mavuno ya ngano Rubeni akaenda shambani na kuona tunguja. Akazileta kwa mama yake. Kisha Raheli akamwambia Lea, “Nipe baadhi ya tunguja za mwanao.” Lea akamwambia, “Je ni jambo dogo kwako, kumchukua mme wangu? Je na sasa unataka kuchukua tunguja za mwanangu pia? Raheli akasema, “Kisha atalala nawe leo usiku, kwa kubadilishana na tunguja za mwanao. Jioni Yakobo akaja kutoka uwandani. Lea akaenda kumlaki na kusema, “Leo usiku utalala nami, kwani nimekuajiri kwa tunguja za mwanangu.” Hivyo Yakobo akalala na Lea usiku huo.
  • Raheli anamzaa Yusufu: “Mungu ameondoa aibu yangu”Mwa 30:22–24
    Aya
    Mwa 30:22–24Mungu akamkumbuka Raheli na kumsikiliza. Akampa kushika mimba. Akashika mimba na kuzaa mwana. Akasema, “Mungu ameiondoa aibu yangu.” Akamwita jina lake Yusufu, akisema, Yahwe ameniongeza mwana mwingine.”
  • Mke wa Manoa, aliye tasa, anamzaa SamsoniAmu 13:2–3, Amu 13:24
    Aya
    Amu 13:2–3Kulikuwa na mtu kutoka Sora, wa jamaa ya Wadani, jina lake Manoa. Mke wake hakuweza kupata mimba na hivyo hakuzaa. Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke akamwambia, Tazame sasa, umeshindwa kupata mimba, wala hujazaa, lakini utakuwa na mimba na utazaa mtoto.
    Amu 13:24Baadaye mwanamke akamzaa mtoto, akamwita jina lake Samsoni. Mtoto alikua na Bwana akambariki.
  • Elkana anampa Hana asiye na mtoto sehemu mara mbili1 Sam 1:2, 1 Sam 1:5
    Aya
    1 Sam 1:2Mtu huyo alioa wanawake wawili, jina la mke wa kwanza aliitwa Hana, na yule wa pili aliitwa Penina, Penina alizaa watoto, lakini Hana hakuzaa.
    1 Sam 1:5Lakini kwa mgawo wa Hana daima alimpa mara mbili zaidi, kwa sababu alimpenda Hana, ingawa BWANA alikuwa amelifunga tumbo lake.
  • Penina anamchokoza Hana mwaka baada ya mwaka1 Sam 1:6–7
    Aya
    1 Sam 1:6–7Hasimu wake alimchokoza sana ili kumkasilisha, kwa sababu BWANA alikuwa amelifunga tumbo lake. 8 Hivyo kila mwaka, alipokuwa akienda katika nyumba ya BWANA pamoja na familia yake, hasimu wake alizidi kumchokoza, Hatimaye alikuwa mtu wa kulia kila wakati na hakula kitu chochote.
  • Hana analia na kuweka nadhiri; anamzaa Samweli1 Sam 1:10–11, 1 Sam 1:19–20
    Aya
    1 Sam 1:10–11Hana alijawa na uchungu sana; akamwomba BWANA na akalia mno. Aliweka nadhili na kusema, “BWANA wa majeshi, kama utalitazama teso la mjakazi wako na kunikumbuka, na usipomsahau mjakazi wako, na kumpatia mjakazi wako mtoto wa kiume, ndipo nitamtoa huyo mtoto kwa BWANA siku zote za maisha yake, na wembe hautapita juu ya kichwa chake kamwe”.
    1 Sam 1:19–20Waliamka asubuhi na mapema wakaenda wakamtukuza BWANA, na baadaye walirudi nyumbani kwao Rama. Elikana alilala na mke wake Hana, na BWANA akamkumbuka. Baada ya muda fulani, Hana alibeba mimba na akazaa mtoto wa kiume. Akamwita jina lake Samweli, akasema, “Kwa sababu huyu nilimuomba kutoka kwa BWANA.”
  • Baadaye Hana anapata watoto wengine1 Sam 2:21
    Aya
    1 Sam 2:21BWANA alimsaidia tena Hana, akawa amebeba mimba nyingine. Akazaa watoto watatu wa kiume na wa kike wawili. Wakati huo huo mtoto Samweli akakua akiwa mbele za BWANA.
  • Mshunami, ambaye mumewe ni mzee, anapata mwana mwaka unaofuata2 Fal 4:14–17
    Aya
    2 Fal 4:14–17Kisha Elisha akajibu, “Tumfanyie nini kwa ajili yake, sasa?” Gehazi akajibu, “Kweli hana mtoto, na mume wake ni mzee.” Hivyo Elisha akajibu, “Mwite.” Wakati alipomuita, akasimama kwenye mlango. Elisha akasema, “Katika kipindi kama hiki mwakani, katika kipindi cha mwaka mmoja, utakuwa ukimkumbatia mtoto.” Akasema “Hapana, bwana wangu na mtu wa Mungu, usidanganye kwa mtumishi wako.” Lakini yule mwanamke akabeba mimba na kujifungua mtoto wakume kipindi hicho hicho katika mwaka uliofuata, kama Elisha alivyokuwa amemwambia.
  • Mikali hakuwa na watoto mpaka siku ya kufa kwake2 Sam 6:23
    Aya
    2 Sam 6:23Hivyo Mikali, binti Sauli, hakuwa na watato hata alipokufa.
  • Elizabeti, tasa na mzee, anapata mimba na kujificha miezi mitanoLk 1:7, Lk 1:24–25, Lk 1:36
    Aya
    Lk 1:7Lakini hawakuwa na mtoto, kwasababu Elizabethi alikuwa tasa, na kwa wakati huu wote wawili walikuwa wazee sana.
    Lk 1:24–25Baada ya Zakaria kurudi nyumbani kutoka kwenye huduma yake hekaluni, mke wake akawa mjamzito. Naye hakutoka nyumbani mwake kwa muda wa miezi mitano. Akasema, “Hili ndilo amabalo Bwana amefanya kwangu aliponitazama kwa upendeleo ili kuiondoa aibu yangu mbele za watu.”
    Lk 1:36Na tazama, ndugu yako Elizabeti anaujauzito wa mwana kwenye umri wake wa uzee. Huu ni mwezi wa sita kwake, ambaye alikuwa anaitwa mgumba.
  • Humkalisha mwanamke tasa nyumbani mwake kama mama mwenye furahaZab 113:9
    Aya
    Zab 113:9Humpa watoto wanamke aliye tasa, humfanya yeye kuwa mama wa watoto mwenye furaha. Msifuni Yahwe!

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0