Bible Explorer

Gundua › Mada › Watoto

Maisha ya kila siku

Watoto katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (57), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

Wakati wa kuzaliwa

  • Watoto wachanga walioshwa, wakasuguliwa kwa chumvi na kufungwa nguoEze 16:4
    Aya
    Eze 16:4Katika siku ya kuzaliwa kwako, mama yako hakukata kitovu chako, wala hakukuosha kwenye maji usafishwe au kukuchua kwa chumvi, wala kukusitiri nguo.
  • Yesu anafungwa nguo za kitoto na kulazwa horiniLk 2:7, Lk 2:12
    Aya
    Lk 2:7Akajifungua mtoto wa kiume, mzaliwa wake wa kwanza, akamzungushia nguo mwilini kumkinga na baridi mtoto. Ndipo akamweka kwenye kihori cha kulishia wanyama, kwa sababu haikuwepo nafasi kwenye nyumba za wageni.
    Lk 2:12Hii ndiyo ishara ambayo mtapewa, mtamkuta mtoto amefungwa nguo na amelala kwenye hori la kulishia wanyama.”
  • Mkunga anafunga uzi mwekundu mkononi mwa pacha mmojaMwa 38:27–30
    Aya
    Mwa 38:27–30Muda wake wa kujifungua ukafika, tazama, mapacha walikuwa tumboni mwake. Ikawa alipokuwa akijifungua mmoja akatoa mkono nje, na mkunga akachukua kitambaa cha rangi ya zambarau na kukifunga katika mkono wake na kusema, “Huyu ametoka wa kwanza.” Ikawa aliporudisha mkono wake, tazama, ndugu yake akatoka kwanza. Mkunga akasema, “Umetokaje” Na akaitwa Peresi. Kisha ndugu yake akatoka, akiwa na utepe wa zambarau juu ya mkono wake, naye akaitwa Zera.
  • Esau anazaliwa mwekundu na mwenye nywele nyingi, Yakobo akishika kisigino chakeMwa 25:24–26
    Aya
    Mwa 25:24–26Ulipo wadia wakati wa kujifungua, tazama, kulikuwa na mapacha ndani ya tumbo lake. Wakwanza akatoka akiwa mwekundu mwili wote kama vazi la nywele. Wakamwita jina lake Esau. Baada ya hapo ndugu yake akatoka. Mkono wake ukiwa umeshika kisigino cha Esau. Akaitwa jina lake Yakobo. Isaka alikuwa na umri wa miaka sitini wakati mke wake alipo wazaa hawa watoto.
  • Wavulana walitahiriwa siku ya naneMwa 17:12, Law 12:3, Lk 2:21
    Aya
    Mwa 17:12Kila mwanaume wa kwenu aliye na umri wa siku nane lazima atahiriwe, katika vizazi ya watu wenu. Hii ni pamoja na yule azaliwaye katika nyumba yako na yeye ambaye amenunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni yeyote ambaye si mmoja wa wazao wako.
    Law 12:3Katika siku ya nane nyama ya govi la mtoto mvulana itatahiriwa.
    Lk 2:21Ilipofika siku ya nane na ilikuwa ni wakati wa kumtahiri mtoto, wakamwita jina Yesu, jina alilokwishapewa na yule malaika kabla mimba haijatungwa tumboni.
  • Wazazi walioomba mtoto: Isaka, Hana, ZakariaMwa 25:21, 1 Sam 1:11, 1 Sam 1:20, Lk 1:13
    Aya
    Mwa 25:21Isaka akamwomba Yahwe kwa ajili ya mke wake kwa sababu alikuwa tasa, na Yahwe akajibu maombi yake, Rebeka mkewe akabeba mimba.
    1 Sam 1:11Aliweka nadhili na kusema, “BWANA wa majeshi, kama utalitazama teso la mjakazi wako na kunikumbuka, na usipomsahau mjakazi wako, na kumpatia mjakazi wako mtoto wa kiume, ndipo nitamtoa huyo mtoto kwa BWANA siku zote za maisha yake, na wembe hautapita juu ya kichwa chake kamwe”.
    1 Sam 1:20Baada ya muda fulani, Hana alibeba mimba na akazaa mtoto wa kiume. Akamwita jina lake Samweli, akasema, “Kwa sababu huyu nilimuomba kutoka kwa BWANA.”
    Lk 1:13Lakini malaika akamwambia, “Usiogope Zakaria, kwasababu maombi yako yamesikika. Mke wako Elizabeth atakuzalia mwana. Jina lake utamwita Yohana.

Kupewa jina

  • Lea na Raheli wanampa kila mwana jina pamoja na sababu yakeMwa 29:32–35, Mwa 30:6–13, Mwa 30:22–24
    Aya
    Mwa 29:32–35Lea akashika mimba na kuzaa mwana, naye akamwita Rubeni. Kwani alisema, “Kwa sababu Yahwe ameliangalia teso langu; bila shaka mme wangu sasa atanipenda.” Kisha akashika mimba tena na kuzaa mwana. Akasema, “Kwa sababu Yahwe amesikia kwamba sipendwi, kwa hiyo amenipa mwana mwingine,” na akamwita Simoni. Kisha akashika mimba tena na kuzaa mwana. Akasema, “Wakati huu mme wangu ataungana nami, kwa kuwa nimemzalia wana watatu.” Kwa hiyo akaitwa Lawi. Akashika mimba tena na kuzaa mwana. Akasema, “Wakati huu nitamsifu Yahwe.” Kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; kisha akaacha kuzaa watoto.
    Mwa 30:6–13Kisha Raheli akasema, “Mungu ameamua kwa faida yangu. Ameyasikiliza maombi yangu na kunipa mwana.” Kwa sababu hiyo akamwita jina lake Dani Bilha, mjakazi wa Raheli, akashika mimba tena na kumzalia Yakobo mwana wa pili. Raheli akasema, “Kwa mashindano yenye nguvu nimeshindana na dada yangu na kushinda.” Akamwita jina lake Naftali. Lea alipoona kwamba ameacha kuzaa, akamchukua Zilpa, mjakazi wake, na kumpa Yakobo kama mke wake. Zilpa, mjakazi wa Lea, akamzalia Yakobo mwana. Lea akasema, “Hii ni bahati njema!” Hivyo akamwita jina lake Gadi. Kisha Zilpa, mjakazi wa Lea, akamzalia Yakobo mwana wa pili. Lea akasema, “Nina furaha! Kwa maana mabinti wataniita furaha.” Hivyo akamwita jina lake Asheri.
    Mwa 30:22–24Mungu akamkumbuka Raheli na kumsikiliza. Akampa kushika mimba. Akashika mimba na kuzaa mwana. Akasema, “Mungu ameiondoa aibu yangu.” Akamwita jina lake Yusufu, akisema, Yahwe ameniongeza mwana mwingine.”
  • Raheli akifa anamwita mwanawe Benoni; Yakobo anamwita BenjaminiMwa 35:18
    Aya
    Mwa 35:18Hata alipokaribia kufa, kwa pumzi yake ya mwisho akamwita jina lake Benoni, lakini baba yake akamwita jina lake Benjamini.
  • Hana anamwita Samweli: “Nilimwomba kutoka kwa Yahwe”1 Sam 1:20
    Aya
    1 Sam 1:20Baada ya muda fulani, Hana alibeba mimba na akazaa mtoto wa kiume. Akamwita jina lake Samweli, akasema, “Kwa sababu huyu nilimuomba kutoka kwa BWANA.”
  • Ikabodi: “Utukufu umeondoka Israeli”1 Sam 4:21
    Aya
    1 Sam 4:21Akamwita mtoto Ikabodi, akisema, “Utukufu umetoweka Israeli!” Kwa sababu sanduku la Mungu limetekwa nyara, na kwa sababu ya kifo cha baba mkwe na mme wake.
  • Binti wa Farao anamwita Musa: “Nilimtoa majini”Kut 2:10
    Aya
    Kut 2:10Mtoto alipokuwa mkubwa, akamleta kwa binti Farao, na akawa mtoto wake. Akamwita jina lake Musa akisema, “Kwa sababu nilimtoa katika maji.”
  • Ndugu wanataka mtoto aitwe jina la baba yake; Elizabeti anasema YohanaLk 1:59–63
    Aya
    Lk 1:59–63Sasa ilitokea siku ya nane kwamnba walikuja kumtahiri mtoto. Ingewapasa kumwita jina lake, “Zekaria,” kwa kuzingatia jina la baba yake, Lakini mama yake akajibu na kusema, “Hapana; ataitwa Yohana.” Wakamwambia, hakuna hata mmoja katika ndugu zako anayeitwa kwa jina hili.” Wakamfanyia ishara baba yake kuashiria yeye alitaka jina aitwe nani. Baba yake akahitaji kibao cha kuandikia, na akaandika, “Jina lake ni Yohana.” Wote wakashangazwa na hili.
  • Wanawake jirani wanampa mjukuu wa Naomi jina ObediRut 4:17
    Aya
    Rut 4:17Na majirani wa yule mwanamke, wakampa jina, wakisema, “Mtoto amezaliwa kwa Naomi.” Wakawita Obedi. Ambaye alikuja kuwa baba yake na Jese, ambaye alikuja kuwa baba yake na Daudi.

Kunyonyesha na kuachisha ziwa

  • Abraham anafanya karamu kubwa siku Isaka anapoachishwa ziwaMwa 21:8
    Aya
    Mwa 21:8Mtoto akakua na akaachishwa kunyonya, na Abraham akafanya sherehe kubwa katika siku ambayo Isaka aliachishwa.
  • Hana anamtunza Samweli mpaka aachishwe ziwa, kisha anampeleka Shilo1 Sam 1:22–28
    Aya
    1 Sam 1:22–28Lakini Hana hakwenda huko; alikuwa amekwisha mwambia mmewe, “Sitaenda huko hadi mtoto aache kunyonya; ndipo nitamleta, ili ahudhurie mbele za BWANA na akae huko daima.” Mme wake Hana, Elikana, akamwambia, “Fanya yale yakupendezayo. Ngojea hadi utakapokuwa umemwachisha kunyonya; BWANA aweze peke yake kuthibitisha neno lake.” Hivyo yule mwanamke alibaki akimnyonyesha mtoto wake mpaka pale alipomwachisha ziwa. Alipokuwa amemwachisha kunyonya, alimbeba, akimchukua pamoja ng'ombe dume wa miaka mitatu, unga kama kilo thelathini na chupa ya mvinyo, akampeleka katika nyumba ya BWANA huko Shilo. Na mtoto huyo alikuwa bado mdogo. Walimchinja yule ng'ombe, na wakamkabidhi mtoto kwa Eli. Akasema, “Ee bwana wangu! Kama uishivyo, bwana wangu, Mimi ndiye yule mwanamke niliyesimama hapa karibu nawe nikimwomba BWANA. Niliomba kwa ajili ya mtoto huyu na BWANA akawa amenijibu ombi la dua yangu nililomwomba. Nami nimemtoa kwa BWANA; kwa maisha yake yote, nimempa BWANA.” Ndipo Elikana na familia yake wakamtukuza BWANA huko Shilo.
  • Mama yake Musa mwenyewe analipwa ili amnyonyesheKut 2:7–9
    Aya
    Kut 2:7–9Basi dada wa yule mtoto akamwambia binti Farao, “Je naweza kwenda kukutafutia mwanamke wa Kiebrania aje akulele mtoto kwa ajili yako?” Binti Farao akamwambia, “Nenda.” Hivyo yule binti akaenda na kumwita mama yake yule mtoto. Binti Farao akamwambia mama yake yule mtoto, “Mchukue mtoto huyu ukaninyonyeshee, nami nitakupa posho.” Hivyo yule mwanamke akamchukua mtoto na kumnyonyesha.
  • Naomi anamweka mtoto Obedi kifuani pakeRut 4:16
    Aya
    Rut 4:16Kisha naomi akamchukua mtoto, akamlaza kifuani pake, na kumhudumia.
  • Mlezi anakimbia na Mefiboshethi, wa miaka mitano; anaanguka na kuwa kiwete2 Sam 4:4
    Aya
    2 Sam 4:4Basi Yonathani, mwana wa Sauli, alikuwa na mwana mlemavu wa miguu. Alikuwa na umri wa miaka mitano habari kuhusu Sauli na Yonathani ilipofika Yezreeli. Yaya wake akamchukua ili akimbie. Lakini wakati anakimbia, mwana wa Yonathani alianguka na akawa kirema. Jina lake aliitwa Mefiboshethi.
  • Mtoto Yoashi anafichwa pamoja na mlezi wake mbali na Athalia2 Fal 11:2
    Aya
    2 Fal 11:2Lakini Yehosheba, binti wa mfalme Yehoramu na dada wa Ahazia, akamchukua Yoashi mwana wa Ahazia, na kumficha mbali mwa miongoni mwa watoto wa mfalme waliokuwa wameuawa, wakati wote pamoja na mlezi wake; akawaweka kwenye chumba cha kulala. Wakamficha kutoka Athalia kwa hiyo hakuuawa.

Kukua

  • Kila mwaka Hana alimshonea mtoto Samweli joho dogo1 Sam 2:18–19
    Aya
    1 Sam 2:18–19Lakini Samweli alimtumikia BWANA akiwa mdogo akivaa nguo ya naivera ya kitani. Kila mwaka mama yake alimtengenezea kanzu dogo na kumletea, wakati wakija na mmewe kutoa dhabihu ya kila mwaka.
  • Wazazi waliwafundisha watoto wao nyumbani na njianiKum 6:7, Kum 11:19
    Aya
    Kum 6:7na mtayafundisha kwa bidii kwa watoto wenu, mtayazungumza wakati mkaapo katika nyumba zenu, wakati mlalapo, na wakati mwinukapo.
    Kum 11:19Utayafundisha kwa watoto na kuongea juu yake wakati uketipo ndani ya nyumba yako, wakati utembeapo barabarani, wakati ulalapo, na wakati uinukapo.
  • Mwanao akiuliza, “Hii ina maana gani?” — mwambie habari hiyoKut 13:14
    Aya
    Kut 13:14Mwanae atakapo kuuliza baadae, 'Hii ina maana gani?' kisha utamwambia, 'Ni kwa mkono hodari Yahweh katutoa Misri, kutoka nyumba ya utumwa.
  • Mlee mtoto katika njia impasayoMit 22:6
    Aya
    Mit 22:6Mfundishe mtoto njia inayompasa na wakati akiwa mzee hatayaacha mafundisho hayo.
  • Misemo ya Mithali kuhusu fimbo ya marudiMit 13:24, Mit 29:15
    Aya
    Mit 13:24Yeye ambaye hamrudi mwanawe humchukia, bali yule anayempenda mwanawe humjali kwa kumwadibisha.
    Mit 29:15Fimbo na maonyo huleta hekima, bali mtoto huru mbali na makaripio humwaibisha mama yake.
  • Watoto walisikiliza Sheria iliposomwa kwa sautiYos 8:35, Neh 8:2–3
    Aya
    Yos 8:35Halikusalia hata neno moja katika yote ambayo Musa alimwagiza Yoshua ambalo halikusomwa mbele ya kusanyiko la Waisraeli lilojumuisha wanawake, watoto wadogo na wageni walioishi miongoni mwao.
    Neh 8:2–3Siku ya kwanza ya mwezi wa saba, Ezra, kuhani, akaleta sheria mbele ya mkutano, wanaume na wanawake, na wote waliokuwa na uwezo wa kusikia na kuelewa. Akatizama eneo lililo wazi mbele ya lango la Maji, na akasoma toka asubuhi hadi adhuhuri, mbele ya wanaume na wanawake, na yeyote ambaye angeweza kuelewa. Na wote wakasikiliza kwa makini kitabu cha Sheria.
  • Watoto wanarukaruka na kucheza mitaaniAyu 21:11, Zek 8:5
    Aya
    Ayu 21:11Wanawapeleka wadogo wao kama kundi la kondoo, na watoto wao hucheza.
    Zek 8:5Pia mitaa ya mji itajazwa na vijana wa kiume na kike wachezao.
  • Yesu akiwa na miaka kumi na mbili hekaluni, akiwauliza walimu maswaliLk 2:41–47
    Aya
    Lk 2:41–47Wazazi wake kila mwaka walikwenda Yerusalemu kwaajili ya sikukuu ya Pasaka. Alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, walikwenda tena wakati mwafaka kidesturi kwa ajili ya sikukuu. Baada ya kubaki siku zote kwa ajili ya sikukuu, walianza kurudi nyumbani. Lakini mvulana Yesu alibaki nyuma mle Yerusalemu na wazazi wake hawakujua hili. Walidhani kwamba yumo kwenye kundi walilokuwa wakisafiri nalo, hivyo walisafiri safari ya siku. Ndipo wakaanza kumtafuta miongoni wa ndugu na marafiki zao. Waliposhindwa kumpata, walirudi Yerusalemu na wakaanza kumtafuta humo. Ikatokea kwamba baada ya siku tatu, wakampata hekaluni, akiwa ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. Wote waliomsikia walishangazwa na ufahamu wake na majibu yake.
  • Yesu aliendelea kukua katika hekima na kimoLk 2:40, Lk 2:52
    Aya
    Lk 2:40Mtoto alikua, na akawa na nguvu, akiongezeka katika hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.
    Lk 2:52Lakini Yesu aliendelea kukua katika hekima na kimo, na akazidi kupendwa na Mungu na watu.
  • Paulo alifundishwa miguuni pa GamalieliMdo 22:3
    Aya
    Mdo 22:3“Mimi ni myahudi, nimezaliwa mji wa Tarso eneo la Kilikia, ila nilipata elimu katika mji huu, miguuni pa Gamalieli. Nilifundishwa kulingana na njia sahihi za sheria za baba zetu. Mimi ninabidii ya Mungu, kama ninyi nyote mlivyo leo.
  • Timotheo alijifunza kutoka kwa bibi yake Loisi na mama yake Yunisi2 Tim 1:5, 2 Tim 3:15
    Aya
    2 Tim 1:5Nimekuwa nikikumbushwa kuhusu imani yako halisi, ambayo hapo kwanza ilikaa kwa bibi yako Loisi na mama yako Yunisi. Na nina hakika ya kwamba imani hiyo inakaa ndani yako pia.
    2 Tim 3:15Unatambua ya kuwa tangu utotoni mwako uliyajua maandiko matakatifu. Haya yanaweza kukuhekimisha kwa ajili ya wokovu kwa njia ya imani katika kristo Yesu.
  • Watoto wanapiga kelele “Hosana” katika nyua za hekaluMt 21:15
    Aya
    Mt 21:15Lakini wakati wakuu wa makuhani na waandishi walipoona maajabu aliyoyatenda, na waliposikia watoto wakipiga kelele hekaluni na kusema, “Hosana kwa Mwana wa Daudi,” walishikwa na hasira.
  • Yesu anawabariki watoto wadogoMt 19:13–15, Mk 10:13–16
    Aya
    Mt 19:13–15Kisha akaletewa baadhi ya watoto wadogo ili awawekee mikono juu yao na kuomba, lakini wanafunzi wake wakawakemea. Bali Yesu akasema, “Waruhusuni watoto wadogo, wala msiwakataze kuja kwangu, kwa maana ufalme wa mbinguni ni wa watu kama wao. Naye akaweka mikono yake juu yao, na kisha akaondoka pale.
    Mk 10:13–16Nao walimletea watoto wao wadogo ili awaguse, lakini wanafunzi wakawakemea. Lakini Yesu alipotambua hilo, hakufurahishwa nalo kabisa akawaambia, “Waruhusuni watoto wadogo waje kwangu, na msiwazuie, kwa sababu walio kama hawa ufalme wa Mungu ni wao. Ukweli nawaambia, yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hakika hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu. Kisha akawachukua watoto mikononi mwake na akawabariki akiwawekea mikono yake juu yao.

Mifano

  • Yakobo anampenda Yusufu kuliko wote na kumpa kanzu ya rangi nyingiMwa 37:3–4
    Aya
    Mwa 37:3–4Basi Israeli akampenda Yusufu kuliko wanawe wote kwa sababu alikuwa mwana wa uzee wake. Akamshonea vazi zuri. Ndugu zake wakaona kwamba baba yao alimpenda sana kuliko ndugu zake wote. Wakamchukia na hawakuongea naye vema.
  • Sheria inalinda fungu mara mbili la mzaliwa wa kwanza wa mke asiyependwaKum 21:15–17
    Aya
    Kum 21:15–17Iwapo mwanamume ana wake wawili na mmoja wao ampenda na mwingine kumchukia, na wote wamekwisha mzalia watoto –wote mwanamke mpendwa na mwanamke achukiwae – basi katika siku ambayo mwanamume atakapowarithisha mali zake wanawe, hapaswi kumfanya mwana wa mke ampendaye kuwa mzawa wa kwanza kabla ya mwana wa mke amchukiaye, ambaye ndiye mwana wa kwanza. Badala yake, anapaswa kumtambua mwana wa kwanza, mwana wa mke asiyempenda, kwa kumpatia mara mbili ya mali zake; kwa maana huyo mwana ni mwanzo wa nguvu zake; haki za mzawa wa kwanza ni zake.
  • Msichana mdogo Mwisraeli anamweleza mke wa Naamani habari za nabii2 Fal 5:2–3
    Aya
    2 Fal 5:2–3Washami walikuwa wametoka kuongoza kikosi na kumchukua kijana mdogo wa kike kutoka nchi ya Israeli. Akamuhudumia mke wa Naamani. Yule binti akamwambia bibi yake, “Natamani kwamba bwana wangu angelikuwa na nabii ambaye yupo Samaria! Halafu angelimponya bwana wangu ukoma wake.
  • Yoashi anakuwa mfalme akiwa na miaka saba, Yosia akiwa na minane2 Fal 11:21, 2 Fal 22:1
    Aya
    2 Fal 11:21Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba tangu alipoanza kutawala.
    2 Fal 22:1Yosia alikuwa na umri wa miaka minane wakati alipoanza kutawala; alitawala kwa mda wa miaka thelathini na moja katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Yedida (Alikuwa binti wa Adaye wa Bozkathi).
  • Watoto wanachukuliwa kuwa watumwa kwa madeni ya wazazi wao2 Fal 4:1, Neh 5:5
    Aya
    2 Fal 4:1Ndipo mke wa mmoja wa watoto wa manbii alipokuja kwa Elisha akilia, akisema, “Mtumishi wako mme wangu amukufa, na unajua kwamba mtumishi wako alikuwa anamcha Yahwe. Basi aliyemuwia amekuja kuwachukua watoto wangu wawili kwenda kuwa watumwa.”
    Neh 5:5Hata hivyo sasa miili yetu na damu ni sawa na ndugu zetu, na watoto wetu ni sawa na watoto wao. Tunalazimishwa kuuza wana wetu na binti zetu kuwa watumwa. Baadhi ya binti zetu tayari wamekuwa watumwa. Lakini hatuna nguvu za kusaidia kwa sababu watu wengine sasa wana mashamba yetu na mizabibu yetu.”
  • Farao anaamuru watoto wa kiume wa Waebrania watupwe mtoni NileKut 1:22
    Aya
    Kut 1:22Farao akawaagiza watu wote, “Lazima mmutupe kila mtoto wa kiume anayezaliwa katika mto, lakini kila mtoto wa kike wamwache aishi.”
  • Herode anawaua wavulana wa Bethlehemu wenye miaka miwili na chiniMt 2:16
    Aya
    Mt 2:16Kisha Herode, alipoona kuwa amedhihakiwa na watu wasomi, alikasirika sana. Aliagiza kuuawa kwa watoto wote wa kiume waliokuwa Bethelehemu na wote katika eneo lile ambao walikuwa na umri wa miaka miwili na chini yake kulingana na wakati aliokuwa amekwisha thibitisha kabisa kutoka kwa wale watu wasomi.
  • Wajukuu ni taji ya wazeeMit 17:6
    Aya
    Mit 17:6Wajukuu ni taji ya wazee na wazazi huleta heshima kwa watoto wao.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0