Bible Explorer

Gundua › Mada › Mahema

Maisha ya kila siku

Mahema katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (29), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Yabali ni baba wa wale wakaao hemani na kufuga wanyamaMwa 4:20
    Aya
    Mwa 4:20Ada akamzaa Yabali. Huyu ndiye alikuwa baba yao na wale walioishi hemani ambao wanafuga wanyama.
  • Abram anapiga hema lake kati ya Betheli na Ai, kisha anahamia MamreMwa 12:8, Mwa 13:18
    Aya
    Mwa 12:8Kutoka pale akaenda kwenye nchi ya mlima mashariki mwa Betheli, ambapo alipiga hema yake, magaribi kukiwa na Betheli na mashariki kukiwa na mji wa Ai. Akajenga madhabahu ya Yahwe pale na kuliitia jina la Yahwe.
    Mwa 13:18Kwa hiyo Abram akachukua hema yake, akaja na kukaa katika mwaloni wa Mamre, ambao uko Hebroni, na pale akajenga Madhabahu ya Yahwe.
  • Lutu naye ana makundi, ng’ombe na mahemaMwa 13:5
    Aya
    Mwa 13:5aliyekuwa anasafiri na Abram, alikuwa pia na ngo'mbe, makundi ya mifugo, na mahema.
  • Abraham ameketi mlangoni pa hema lake wakati wa joto la mchanaMwa 18:1–2
    Aya
    Mwa 18:1–2Yahwe alimtokea Abraham katika Mialoni ya Mamre, alipokua ameketi mlangoni pa hema wakati wa jua. Akatazama juu na, tazama, akaona wanaume watatu wamesimama mbele yake. Alipo waona, alikimbia kupitia mlango wa hema kuwalaki na kuinama chini hadi ardhini.
  • Sara anasikiliza mlangoni pa hemaMwa 18:9–10
    Aya
    Mwa 18:9–10Wakamwambia, “Mke wako Sara yuko wapi?” akajibu. “pale hemani.” akasema, “Hakika nitarejea kwako majira ya machipuko, na tazama Sara mkeo atakuwa na mtoto wa kiume.” Sara alikuwa akisikiliza mlangoni pa hema iliyokuwa nyuma yake.
  • Isaka anamleta Rebeka katika hema la mama yake SaraMwa 24:67
    Aya
    Mwa 24:67Kisha Isaka akamleta katika hema ya Sara mama yake na akamchukua Rebeka, na akawa mke wake, na akampenda. Kwa hiyo Isaka akafarijika baada ya kifo cha mama yake.
  • Isaka anapiga hema lake, na watumishi wake wanachimba kisimaMwa 26:25
    Aya
    Mwa 26:25Isaka akajenga madhabahu pale na akaliita jina la Yahwe. Akapiga hema yake pale, na watumishi wake wakachimba kisima.
  • Yakobo, Lea, Raheli na wajakazi kila mmoja ana hema lakeMwa 31:33
    Aya
    Mwa 31:33Labani akaingia katika hema ya Yakobo, katika hema ya Lea, na katika hema za wale wajakazi wawili, lakini hakuviona. Akatoka katika hema ya Lea na kuingia katika hema ya Raheli.
  • Abraham, Isaka na Yakobo waliishi katika mahemaEbr 11:9
    Aya
    Ebr 11:9Ilikuwa ni kwa imani kwamba aliishi katika nchi ya ahadi kama mgeni. Aliishi katika mahema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi wenzake wa ahadi ile ile.
  • Mahema yalikuwa na mapazia, kamba na vigingiIsa 54:2, Yer 10:20
    Aya
    Isa 54:2Fanya hema lako kuwa kubwa na tawanya mapazia mbali, sio kidogo; nyoosha kamba zako na imarisha vigingi vyako.
    Yer 10:20Hema yangu imeharibiwa, na kamba za hema yangu zote zimekatwa. Wamewachukua watoto wangu wote, Kwa hiyo hawaishi tena. Hakuna tena mtu wa kuitandaza hema yangu au wa kuziinua pazia za hema yangu.
  • Weusi kama mahema ya KedariWim 1:5
    Aya
    Wim 1:5Mimi ni mweusi lakini mzuri, enyi mabinti wa wanaume wa Yerusalemu - mweusi kama hema za Kedari, muzuri kama mapazia ya Sulemani.
  • Paulo, Akila na Prisila walikuwa mafundi wa kushona mahemaMdo 18:2–3
    Aya
    Mdo 18:2–3Huko akampata Myahudi aitwaye Akwila mtu wa kabila la Ponto, yeye na mke wake aitwaye Prisila walikuja kutoka huko Italia, kwa sababu Klaudia aliamuru Wayahudi wote waondoke Roma; Paulo akaja kwao; Paulo akaishi na kufanya kazi nao kwani yeye anafanya kazi inayofanana na yao. Wao walikuwa ni watengeneza mahema.

Jangwani

  • Musa anamsalimu baba mkwe wake, nao wanaingia hemaniKut 18:7
    Aya
    Kut 18:7Musa alitoka kwenda kukutana na baba mkwe wake, akamwinamia, na kumbusu. Wakajuliana hali na wakaingia ndani ya hema.
  • Israeli wanapiga kambi kwa vikosi, kila mtu chini ya bendera yakeHesabu 1:52, Hesabu 2:2
    Aya
    Hesabu 1:52Wakati watu wa Israeli watakaposimamisha hema zao, kila mwanaume lazima awe karibu na bango la jeshi lake.
    Hesabu 2:2Kila mtu atapanga kulingana na mahali pake, pamoja na mabango ya baba zao. Watapanga kuzunguka hema ya kukutania kila upande.
  • Watu wanasimama milangoni pa mahema yao wakimtazama MusaKut 33:8
    Aya
    Kut 33:8Kisha Musa alipo enda kwenye hema, watu wote walisima kando ya hema yao na kumuangalia Musa hadi alipo ingia ndani.
  • Balaamu: “Jinsi yalivyo mazuri mahema yako, ee Yakobo”Hesabu 24:5
    Aya
    Hesabu 24:5Jinsi zilivyo nzuri hema zako, ewe Yakobo, mahali unapoishi, Israeli!
  • Akani anaficha fedha na dhahabu ardhini ndani ya hema lakeYos 7:21–22
    Aya
    Yos 7:21–22Nilichofanya ni hiki: Nilipoona miongoni mwa nyara mkoti mzuri kutoka Babeli, shekeli mia mbili za fedha, na kipande cha dhahabu chenye uzito wa shekeli hamsini, nilivitamani na nikavichukua. Vimefichwa chini ardhini katikati ya hema langu, na fedha iko chini yake.” Yoshua akatuma wajumbe waliokimbia mpaka kwenye hema mahali palipokuwa na vile vitu. Walipoangalia, waliviona vimefichwa katika hema lake, na fedha chini yake.

Katika masimulizi

  • Yaeli anampa Sisera maziwa hemani na kumuua kwa kigingi cha hemaAmu 4:18–21, Amu 5:25–26
    Aya
    Amu 4:18–21Jaeli akatoka kumlaki Sisera, akamwambia, karibu, bwana wangu; karibu kwangu, wala usiogope. Basi akakaribia kwake, akaingia hemani kwake, naye akamvika bushuti. Akamwambia, Tafadhali nipe maji kidogo ninywe, kwa maana nina kiu. Alifungua mfuko wa ngozi ya maziwa akampa anywe, kisha akamfunika tena. Akamwambia, “Simama mlangoni pa hema. Ikiwa mtu atakuja na kukuuliza, 'Je, kuna mtu hapa?', Sema 'Hapana'.” Kisha Jaeli (mke wa Heberi) akachukua kigingi cha hema na nyundo mkononi mwake akamwendea kwa siri, kwa sababu alikuwa amelala usingizi mzito, naye akakitia kigingi cha hema upande wa kichwa chake akamchoma na kikapenya kushuka chini. Hivyo akafa.
    Amu 5:25–26Mtu yule aliomba maji, naye akampa maziwa; akamletea siagi katika sahani inayofaa kwa wakuu. Aliweka mkono wake kwenye kigingi cha hema, na mkono wake wa kuia katika nyundo ya mfanyakazi; kwa nyundo akampiga Sisera, alimpiga kichwani kwake. Aliligawanya fuvu lake vipande vipande wakati alipompiga pembeni ya kichwa chake.
  • Wamidiani wanakuja na mifugo yao na mahema kama nzigeAmu 6:5
    Aya
    Amu 6:5Kila wakati wao na mifugo yao na mahema walipokuja, walikuja kama kundi la nzige, na haikuwezekana kuhesabu watu au ngamia zao. Walivamia ardhi ili kuiharibu.
  • Daudi anaweka silaha za Goliathi katika hema lake1 Sam 17:54
    Aya
    1 Sam 17:54Daudi akachukua kichwa cha Mfilisti na kukipeleka Yerusalemu, lakini akaliweka vazi la vita katika hema lake.
  • Uria: sanduku, Israeli na Yuda wanakaa katika mahema2 Sam 11:11
    Aya
    2 Sam 11:11Uria akamjibu Daudi, “Sanduku, na Israeli na Yuda wamo kwenye mahema, na Yoabu na watumishi wa bwana wangu wamepiga hema uwandani. Jinsi gani basi mimi naweza kwenda nyumbani kwangu kula kunywa na kulala na mke wangu? kwa hakika kama uishivyo, sitafanya hivyo.
  • “Kila mtu hemani kwake, ee Israeli!”2 Sam 20:1, 1 Fal 12:16
    Aya
    2 Sam 20:1Ikatukia pia kuwa katika eneo lilelile kulikuwa mfanya fujo jina lake Sheba mwana wa Bikri Mbenjamini. Akapiga tarumbeta na kusema, “Sisi hatuna sehemu katika Daudi, wala hatuna urithi katika mwana wa Yese. Haya kila mtu na aende nyumbani kwake, Israeli.”
    1 Fal 12:16Israeli yote ilipoona kuwa mfalme hakuwasikiliza, watu wakamjibu wakimwambia, “Je, tuna sehemu gani kwa Daudi? Hatuna urithi kwa mwana wa Yese! Nenda kwenye hema zako, ewe Israeli. Sasa tazama kwenye nyumba yako, Daudi.” Kwa hiyo Israeli akarudi kwenye hema zake.
  • Jeshi la Asa linashambulia mahema ya wachungaji na kuchukua kondoo na ngamia2 Nya 14:15
    Aya
    2 Nya 14:15Jeshi pia likaipiga hema ya makazi yawachungaji; wakabeba kondoo kwa wingi, ngamia vile vile, na kisha wakarudi Yerusalemu.
  • Hema la mchungaji linang’olewa na kuhamishwaIsa 38:12
    Aya
    Isa 38:12Maisha yangu yameondolea na kupelekwa mbali na mimi kama hema la mchungaji; Niliyakunja maisha yangu juu kama mfumaji; ameniondoa katika kifungo; kati ya mchana na usiku ameyakomesha maisha yangu.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0