Maisha ya kila siku
Meza na milo katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (36), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
Meza
- Kitanda, meza, kiti na taa katika chumba kidogo cha Elisha2 Fal 4:10
Aya
2 Fal 4:10Ngoja tutengeneze chumba kidogo kwenye paa kwa ajili ya Elisha, na tuweke kitanda juu ya hicho chumba, meza, na taa. Kisha atakapokuwa anakuja kwetu, atakuwa anakaa hapo.”
- Wafalme sabini waliokota makombo chini ya meza ya Adoni BezekiAmu 1:7
Aya
Amu 1:7Adoni Bezek akasema, “Wafalme sabini, ambao na vidole gumba vyako na vidole vikubwa vilivyokatwa, walikusanya chakula chao chini ya meza yangu. Kama nilivyofanya, hata hivyo Mungu amefanya kwangu.” Wakamleta Yerusalemu, naye akafa huko.
- Meza ya maskani: mti wa mshita uliofunikwa dhahabu, na mipiko ya kubebeaKut 25:23–28
Aya
Kut 25:23–28Nawe fanya meza ya mti wa mshiti. Urefu wake utakuwa dhiraa mbili, na upana wake dhiraa moja, na kwenda juu kwake dhiraa moja na nusu. Uifunike dhahabu safi na kuifanyia ukingo wa dhahabu wa kuizunguka pande zote. Lazima ufanyie fremu ya kuizunguka pande zote, upana wake utakuwa nyanda nne, ukingo wa dhahabu wa kuuzunguka fremu pande zote. Uifanyie viduara vinne vya dhahabu na kuvitia vile viduara katika pembe zake nne, katika miguu yake minne ilipo kuwa. Vile viduara na viwe karibu na ile fremu ili viwe mahali pa kutilia ile miti, ya kuichukulia meza. Fanya ile miti ya mti wa mshita, na kuifunika dhahabu, kwamba ile meza ichukuliwe kwayo.
- Mikate kumi na miwili kwa safu mbili juu ya meza ya dhahabu kila SabatoLaw 24:5–8
Aya
Law 24:5–8Yawapasa kuchukua unga laini na kuoka kwa huo mikate kumi na miwili. Ni lazima kuwe na mbili za kumi za efa za unga katika kila mkate. Kisha mtaipanga juu ya meza ya dhahabu safi mbele za Yahweh katika safu mbili, mikate sita katika kila safu, Mtaweka uvumba safi kando ya kila safu ya mikata kuwa sadaka ya kuwakilisha. Uvumba huo utachomwa kwa moto kwa ajili ya Yahweh. Kila siku ya Sabato kuhani mkuu sharti aipange kwa utaratibu hiyo mikate mbele za Yahweh kwa niaba ya watu wa Israeli, iwe ishara ya agano la milele.
- Meza za dhahabu na meza za fedha kwa ajili ya hekalu1 Nya 28:16
Aya
1 Nya 28:16Alitoa uzito wa dhahabu kwa meza za mkate wa uwepo, kwa kila meza, na uzito wa fedha kwa meza za fedha.
- Yesu anapindua meza za wabadilisha fedhaYn 2:15
Aya
Yn 2:15Yesu akatengeneza mjeledi wenye vifundo, akawatoa wote walikuwemo katika hekalu, ikijumuisha ng'ombe na kondoo. Akamwaga fedha za wabadili fedha na kuzipindua meza zao.
- Mbwa chini ya meza hula makombo ya watotoMt 15:27, Mk 7:28
- Lazaro anatamani makombo kutoka meza ya tajiri (mfano)Lk 16:21
Aya
Lk 16:21Naye alikua akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri hata mbwa wakaja wakamlamba vidonda vyake.
- Wana wako kama machipukizi ya mizeituni kuzunguka meza yakoZab 128:3
Aya
Zab 128:3Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao katika nyumba yako; wanao watakuwa kama miche ya mimea ya mizeituni wakaapo kuzunguka meza yako.
Kuketi na kuegemea
- Abraham anasimama karibu na wageni wake chini ya mti wanapokulaMwa 18:8
Aya
Mwa 18:8Akatwaa siagi na maziwa na ndama aliye kwisha andaliwa, na akaweka chakula mbele yao, naye akasimama karibu nao chini ya mti wakati wanakula.
- Ruth anaketi kando ya wavunaji wakati wa chakulaRut 2:14
Aya
Rut 2:14Wakati wa chakula Boazi alimwambia Ruth, “Njoo hapa, ule baadhi ya mikate, na uchovye kipande katika divai.” Alikaa kando ya wavunaji, na Boazi akampatia kiasi cha nafaka zilizo kaangwa. Ruth alikula mpaka alipotosheka na kusaza.
- Hamani anaanguka juu ya kitanda alichokuwa ameegemea malkia EstaEst 7:8
Aya
Est 7:8Mfalme akarudi kutoka katika bustani ya ikulu, na kuingia katika chumba ambamo kulikuwamo mvinyo. Hamani alikuwa ameanguka chini ya kochi alilokuwa ameketi Esta. Mfalme akakasirika na kusema, “atamdharirisha malkia mbele zangu katika nyumba yangu?” Mara tu maneno haya yalipotoka kinywani mwa mfalme, watumizhi wakafunika uso wa Hamani.
- Yesu ameketi mezani pamoja na wale Kumi na WawiliMt 26:20
Aya
Mt 26:20Ilipofika jioni, aliketi kula chakula pamoja na wale wanafunzi Kumi na Wawili.
- Mwanafunzi aliyeegemea kando ya Yesu anaegemea nyuma kumwulizaYn 13:23–25
Aya
Yn 13:23–25Kulikuwa katika meza, mmoja wa wanafunzi wake ameegama kifuani mwa Yesu yule ambaye Yesu alimpenda. Simoni Petro alimuuliza mwanafunzi huyu na kusema, “Twambie ni yupi ambaye kwake anazungumza.” Mwanafunzi yule aliye egama kifuani mwa Yesu na akamwambia, “Bwana, ni nani?”
- Farisayo anamkaribisha Yesu kula, naye anaketi mezaniLk 7:36
Aya
Lk 7:36Mmoja wa mafarisayo alimwomba Yesu aende kula pamoja naye. Baada ya Yesu kuingia kwenye nyumba ya farisayo, aliegemea kwenye meza ili ale.
- Martha anahudumia, na Lazaro ameketi mezani pamoja na YesuYn 12:2
Aya
Yn 12:2Basi wakamwandalia chakula cha jioni huko, na Martha akamtumikia, wakati huo Lazaro alikuwa mmoja wapo wa wale walioketi chakulani pamoja na Yesu.
- Elfu tano wanaketi juu ya majani kwa makundi ya mia na hamsiniMk 6:39–40, Lk 9:14
Aya
Mk 6:39–40Akawaamuru watu waketi katika makundi juu ya majani mabichi. Wakawaketisha katika makundi; makundi ya mamia kwa hamsini.
Lk 9:14Kulikua na wanaume wapatao elfu tano pale. Akawambia wanafunzi wake. “Wakalisheni chini katika makundi ya watu wapatao hamsini kwa kila kundi.
Nani alikula na nani
- Kiti cha Daudi mezani pa Sauli ni kitupu; Yonathani anaondoka kwa hasira1 Sam 20:29, 1 Sam 20:34
Aya
1 Sam 20:29Alisema, 'Tafadhali niruhusu niende. Maana familia yetu wanayo dhabihu huko mjini, na kaka yangu ameniagiza niwe huko. Basi kama nimepata kibali machoni pako, tafadhali niruhusu niende nikawaone kaka zangu.' Hakuja kwenye meza ya mfalme kwa sababu hii.”
1 Sam 20:34Yonathani alitoka mezani akiwa na hasira kali bila kula chakula siku ya pili ya mwezi, kwa sababu alimhuzunikia Daudi, na kwa sababu baba yake amemwaibisha.
- Maliwali wanaleta chakula kwa wote wanaokuja mezani pa Sulemani1 Fal 4:27
Aya
1 Fal 4:27Na maakida walileta chakula kwa Sulemani na kwa wale walioketi kwenye meza ya mfalme Sulemani, kila mtu katika mwezi wake. Walihakikisha hakuna kinachopungua.
- Meza ya Sulemani na kuketi kwa watumishi wake vinamshangaza malkia wa Sheba1 Fal 10:4–5
Aya
1 Fal 10:4–5Malkia wa Sheba alipoona hekima yote ya Sulemani, na ikulu aliyokuwa amejenga, chakula cha mezani kwake, kuketi kwa watumishi wake, kazi ya watumishi wake na kuvaa kwao, pia wanyweshaji wake, na jinsi alivyotoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya BWANA, roho yake ilizimia.
- Wayahudi wengi na maafisa wanakula mezani pa Nehemia, pamoja na wageniNeh 5:17
Aya
Neh 5:17Katika meza yangu walikuwa Wayahudi na maafisa, watu 150, isipokuwa wale waliokuja kwetu kutoka kwa mataifa waliokuwa wakituzunguka.
- Yekonia anakula mezani pa mfalme wa Babeli maisha yake yote2 Fal 25:29
Aya
2 Fal 25:29Evil-Merodaki akamvua Yekonia nguo za gerezani,
- Yesu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi nyumbani kwa MathayoMt 9:10–11, Mk 2:15–16, Lk 15:2
Aya
Mt 9:10–11Na Yesu alipoketi ili ale chakula ndani ya nyumba, wakaja watoza ushuru wengi na watu waovu wakashiriki chakula pamoja na Yesu na wanafunzi wake. Ndipo Mafarisayo walipoona hayo, wakawaambia wanafunzi “Kwa nini mwalimu wenu anakula chakula pamoja na watoza ushuru na watu waovu?”
Mk 2:15–16Na wakati Yesu alipokuwa akipata chakula katika nyumba ya Lawi, wakusanya kodi wengi na watu wenye dhambi walikuwa wakila na Yesu na wanafunzi wake, kwa kuwa walikuwa wengi nao walimfuata. Wakati waandishi, ambao walikuwa Mafarisayo, walipoona kwamba Yesu alikuwa akila na watu wenye dhambi na wakusanya kodi, waliwaambia wanafunzi wake, “Kwa nini anakula na wakusanya kodi na watu wenye dhambi?”
Lk 15:2Mafarisayowaote na waandishi wakanung'unika wakisema, “Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi na hata hula nao.”
- “Mkono wake anayenisaliti uko pamoja nami mezani”Lk 22:21
Aya
Lk 22:21Lakini angalieni. Yule anisalitie yuko pamoja nami mezani.
- Yesu aliyefufuka: “Njooni mle kifungua kinywa”Yn 21:12
Aya
Yn 21:12Yesu akawaambia, “Njoni mpate kifungua kinywa.” Hakuna hata mmoja wa wanfunzi aliyethubutu kumwuliza, “Wewe ni nani?” Walijua kuwa alikuwa ni Bwana.
- Waumini wa kwanza wanamega mkate nyumba kwa nyumbaMdo 2:46
Aya
Mdo 2:46Hivyo siku baada ya siku waliendelea wakiwa na lengo moja katika hekalu, na walimega mkate kwenye kaya, na walishiriki chakula kwa furaha na unyenyekevu wa moyo;
- Wale Kumi na Wawili hawataki kuacha kuhubiri ili kuhudumu mezaniMdo 6:2
Aya
Mdo 6:2Mitume kumi na wawili waliwaita kusanyiko lote la wanafunzi na kusema, “Siyo sahihi kwetu kuliacha neno la Mungu na kuhudumia mezani.
- Petro analaumiwa kwa kula pamoja na watu wasiotahiriwaMdo 11:3
Aya
Mdo 11:3“Umeshikamana na watu wasiotahiriwa na kula nao!”
- Huko Antiokia Petro anajitenga na kula pamoja na MataifaGal 2:12
Aya
Gal 2:12Kabla ya watu kadhaa kuja kutoka kwa Yakobo, Kefa alikuwa akila pamoja na watu wa mataifa. Lakini hawa watu walipokuja, aliacha na kuondoka kutoka kwa watu wa mataifa. Alikuwa anaogopa watu ambao walihitaji tohara.
- Mlinzi wa gereza anawaandalia Paulo na Sila chakulaMdo 16:34
Aya
Mdo 16:34Akawaleta Paulo na Sila nyumbani kwake na kuwatengea chakula. Naye akawa na furaha kuu pamoja na watu wa nyumbani mwake kwa sababu walimwamini Mungu.
- Umealikwa na asiyeamini? Kula chochote unachowekewa1 Kor 10:27
Aya
1 Kor 10:27Na mtu asiyeamini akiwaalika kula, na mnataka kwenda, kuleni chochote awapacho pasipo kuuliza maswali ya dhamiri.
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0