Bible Explorer

Gundua › Mada › Madeni na mikopo

Maisha ya kila siku

Madeni na mikopo katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (28), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Msiwiwe na mtu kitu chochote, isipokuwa kupendanaRum 13:8
    Aya
    Rum 13:8Msidaiwe na mtu kitu chochote, isipokuwa kupendana ninyi kwa ninyi. Kwa kuwa yeye ampendaye jirani yake ametimiliza sheria.
  • Akopaye ni mtumwa wa akopeshayeMit 22:7
    Aya
    Mit 22:7Watu matajiri huwatawala watu masikini na mwenye kukopa ni mtumwa wa yule anayekopesha.
  • Usiwe mdhamini wa madeni, usije ukanyang’anywa kitanda chakoMit 22:26–27, Mit 11:15
    Aya
    Mit 22:26–27Usiwe miongoni mwao wapigao mikono, mwenye kuahidi madeni. Kama umekosa njia za kulipa, nini kitaweza kuzuia mtu kuchukua kitanda chako chini yako?
    Mit 11:15Anayemdhamini mkopo wa mgeni ataumia kwa usumbufu, bali anayechukia kutoa rehani kwa namna ya ahadi yupo salama.
  • Umemdhamini jirani yako? Nenda ujiokoe mara mojaMit 6:1–5
    Aya
    Mit 6:1–5Mwanangu, kama utaweka pesa zako kuwa dhamana kwa mkopo wa jirani yako; kama ukitoa ahadi yako katika mkopo wa mtu usiyemjua, basi umejiwekea mtego mwenyewe na umenaswa kwa maneno ya kinywa chako. Mwanagu, ukinaswa kwa maneno yako mwenyewe, fanya haya ili kujiokoa, kwa kuwa umeangukia kwenye mikono ya jirani yako; nenda unyenyekee na ufanye shauri mbele ya jirani yako. Usiruhusu usingizi katika macho yako wala kope za macho yako kusinzia. Jiokoe mwenyewe kama swala kutoka katika mkono wa mwindaji, kama ndege kutoka katika mkono wa mwinda ndege.

Katika Sheria

  • Hakuna riba kwa ndugu maskini; kwa mgeni iliruhusiwaKut 22:25, Kum 23:19–20
    Aya
    Kut 22:25Ukiazima hela kwa watu wangu walio maskini, haupaswi kuwa kama anaye kopesha hela kwake au kutoza faida.
    Kum 23:19–20Hutakiwi kumkopesha Muisraeli mwenzako kwa riba – riba ya fedha, riba ya chakula, au riba ya kitu chochote kinachokopeshwa kwa riba. Kwa mgeni unaweza kukopesha kwa riba; lakini kwa Muisraeli mwenzako haupaswi kukopesha kwa riba, ili kwamba Yahwe Mungu wako aweze kukubariki katika kila jambo uwekalo mkono wako, katika nchi ambayo mnaenda kumiliki.
  • Vazi lililochukuliwa kama rehani linarudishwa kabla jua halijazamaKut 22:26–27, Kum 24:12–13
    Aya
    Kut 22:26–27Ukichukuwa vazi la jirani yako kwa deni, lazima umrudishie kabla jua kuzama, kwa kuwa hilo ndilo funiko lake, ni vazi la mwili wake. Nini tena ambacho anaweza kulalia? Atakapo niita mimi, nitasikia, kwa kuwa mimi ni mwenye huruma.
    Kum 24:12–13Iwapo ni mtu maskini, hautakiwi kulala na dhamana yake ikiwa mikononi mwako. Hakika unapaswa kumrejeshea dhamana yake kabla jua halijazama, ili aweze kulala ndani ya vazi lake na akubariki; itakuwa utakatifu kwako mbele za Yahwe Mungu wako.
  • Mkopeshaji anasubiri nje mpaka rehani iletwe kwakeKum 24:10–11
    Aya
    Kum 24:10–11Utoapo mkopo wa aina yoyote kwa jirani yako, hautakiwi kwenda ndani ya nyumba yake kutafuta dhamana yake. Utasimama nje, na mwanamume aliyekopa kwako ataleta dhamana yake nje kwako.
  • Mawe ya kusagia hayachukuliwi kama rehaniKum 24:6
    Aya
    Kum 24:6Mwanamume yeyote hatachukua kinu wala jiwe la kinu kama dhamana, kwa maana hivyo itakuwa kuchukua Maisha ya mtu kama dhamana.
  • Madeni yanafutwa kila mwaka wa sabaKum 15:1–3
    Aya
    Kum 15:1–3Kila mwisho wa kila miaka saba, mnapaswa kufuta madeni. Hii ni tabia ya ukombozi. Kila mkopeshaji atafuta kile alichompa jirani yake, hata dai kutoka kwa jirani yake au ndugu yake kwa sababu ufutaji wa madeni wa Yahwe umetangazwa. Kutoka kwa mgeni mnaweza kudai; lakini kwa chochote chenu kilicho na ndugu yenu mnapaswa mkitoe.
  • Ndugu anayejiuza anafanya kazi kama mtumishi wa mshaharaLaw 25:39–41
    Aya
    Law 25:39–41Iwapo mwananchi mwenzako atakuwa masikini na kujiuza mwenyewe kwako, hutamfanyisha kazi kama mtumwa. Mtendee kama mtumishi wa kuajiriwa. Ni lazima awe kama yule ahudumuye nawe kwa muda mpaka mwaka wa Yubile. Kisha ataondoka kwako, yeye mwenyewe na watoto wake pamoja naye, na atarejea kwenye familia yake mwenyewe na kwenye miliki ya baba yake.
  • Mnyama aliyeazimwa akifa lazima alipwe kikamilifuKut 22:14
    Aya
    Kut 22:14Kama mwanaume akiazima mnyama kutoka kwa jirani yake na mnyama akajeruhia au akafa pasipo mmiliki kuwa naye, mwanaume mwengine lazima afanya malipo.

Mifano

  • Yuda anaacha muhuri wake, kamba na fimbo kama rehaniMwa 38:17–18
    Aya
    Mwa 38:17–18Akasema, “Nitakuletea mwana mbuzu wa kundi.” Akasema, “Je utanipa rehani hata utakapo leta?” Akasema, “Nikupe rehani gani?” Naye akasema, “Mhuri wako na mshipi, na fimbo iliyo mkononi mwako.” Akampa na kulala naye. Akawa mjamzito.
  • Kila mwenye deni anakusanyika kwa Daudi1 Sam 22:2
    Aya
    1 Sam 22:2Kila mmoja aliyekuwa na mahangaiko, kila mmoja aliyekuwa na deni, na kila mmoja ambaye hakuwa na furaha moyoni-wote walijikusanya kwake, na Daudi akawa jemedari wao. Kulikuwa na wanaume wapatao mia nne waliokuwa pamoja naye.
  • Mdai anakuja kuwachukua wana wawili wa mjane kuwa watumwa2 Fal 4:1–7
    Aya
    2 Fal 4:1–7Ndipo mke wa mmoja wa watoto wa manbii alipokuja kwa Elisha akilia, akisema, “Mtumishi wako mme wangu amukufa, na unajua kwamba mtumishi wako alikuwa anamcha Yahwe. Basi aliyemuwia amekuja kuwachukua watoto wangu wawili kwenda kuwa watumwa.” Hivyo Elisha akamwambia, “Nikusaidie nini? Niambie una nini kwenye nyumba yako?” Akamwambia “Mtumishi wako hana kitu kwenye nyumba, isipokuwa chupa ya mafuta.” Kisha Elisha akasema, “Nenda kaazime vyombo kwa majirani zako, vyombo vitupu. Azima vyombo vingi uwezavyo. Kisha lazima uende ndani na kujifungia mlango wewe na watoto wako, na kumiminia mafuta vyombo vyote; vile vilivyojaa ukavitenge.” Basi akamuacha Elisha na kujifungia mlango yeye na watoto wake. Wakavileta vile vyombo kwake, na akivijaza kwa mafuta. Ikawa vyombo vilipojaa, akamwambia mtoto wake, “Niletee chombo kingine.” Ila akamwambia, “Hakuna vyombo vingine.” Kisha mafuta yakakoma kutoka. Ndipo akaja na kumwambia mtu wa Mungu. Akasema, “Nenda kauze mafuta; lipa deni lako, na yatakayobaki waachie watoto wako.”
  • “Lilikuwa la kuazima!” — kichwa cha shoka kinaanguka Yordani2 Fal 6:4–6
    Aya
    2 Fal 6:4–6Kwa hiyo akaenda pamoja nao, na wakati walipokuja Yordani, wakaanza kukata miti. Lakini mmoja wao alipokuwa akikata, kichwa cha shoka kikaangukia kwenye maji; akalia kwa sauti na kusema, “la hasha, bwana wangu, kilikuwa kimeazimwa!” Basi mtu wa Mungu akasema, “kiliangukia wapi?” Yule mtu akamwonyesha Elisha ile sehemu. akakata fimbo, akarusha kwenye maji, na kufanya chuma kuelea.
  • Njaa: watu wanaweka rehani mashamba na nyumba; Nehemia anakomesha ribaNeh 5:3–5, Neh 5:10–12
    Aya
    Neh 5:3–5Pia kulikuwa na baadhi ya watu ambao walisema, “Tunaweka rehani mashamba yetu, mizabibu yetu, na nyumba zetu ili tupate nafaka wakati wa njaa.” Wengine pia walisema, “Tumekopesha pesa kulipa kodi ya mfalme kwenye mashamba yetu na mashamba yetu ya mizabibu. Hata hivyo sasa miili yetu na damu ni sawa na ndugu zetu, na watoto wetu ni sawa na watoto wao. Tunalazimishwa kuuza wana wetu na binti zetu kuwa watumwa. Baadhi ya binti zetu tayari wamekuwa watumwa. Lakini hatuna nguvu za kusaidia kwa sababu watu wengine sasa wana mashamba yetu na mizabibu yetu.”
    Neh 5:10–12Mimi na ndugu zangu na watumishi wangu tunawapa fedha na nafaka. Lakini lazima tuache kutoza riba juu ya mikopo hii. Warudishieni leo leo mashamba yao, mizabibu yao, mashamba yao ya mizeituni, na nyumba zao na asilimia ya fedha, nafaka, divai mpya, na mafuta mliyowatoza.” Wakasema, “Tutarudisha kile tulichochukua kutoka kwao, wala hatutahitaji kitu kutoka kwao. Tutafanya kama unavyosema.” Ndipo nikawaita makuhani, na kuwaapisha kuwafanya kama walivyoahidi.
  • Mtoto anayenyonya wa familia maskini anachukuliwa kwa deniAyu 24:9
    Aya
    Ayu 24:9Kuna waovu wanaowapokonya yatima katika kifua cha mama zao, na waovu wawachukuao watoto kama dhamana kutoka kwa masikini.
  • Mavazi yanachukuliwa kama rehaniAyu 22:6, Amo 2:8
    Aya
    Ayu 22:6Kwa maana umechukua dhamana kutoka kwa ndugu yako bila sababu; umechukua mavazi ya mtu na kumwacha uchi.
    Amo 2:8Nao hulala chini karibu na kila madhabahu kwenye nguo zilizowekwa dhamana, na katika nyumba ya Mungu wao hunywa divai ya wale ambao walitozwa faini.
  • Mfano: mtumishi anayedaiwa talanta elfu kumiMt 18:23–34
    Aya
    Mt 18:23–34Kwa sababu hiyo ufalme wa mbinguni ni sawa na mfalme fulani aliyetaka kusahihisha hesabu kutoka kwa watumwa wake. Alipoanza kusahihisha hesabu, mtumwa moja akaletwa kwake ambaye alikuwa anamdai talanta elfu kumi. Kwa kuwa hakuwa na njia ya kulipa, bwana wake aliagiza auzwe, mke wake pamoja na watoto wake na kila kitu alichokuwa nacho, na malipo yafanyike. Hivyo mtumwa alianguka, akapiga magoti mbele yake, akisema, 'Bwana, uwe na uvumilivu pamoja nami, na nitakulipa kila kitu.' Hivyo bwana wa yule mtumwa, kwa kuwa alisukumwa sana na huruma, alimwachilia na kumsamehe deni hilo Lakini mtumwa yule alitoka na kumpata mmoja kati ya watumwa wenzake, aliyekuwa anamdai denari mia. Alimvuta, akamkaba kooni, na kumwambia, 'Nilipe kile ninachokudai.' Lakini yule mtumwa mwenzake alianguka na kumsihi sana, akisema, 'Uwe na uvumilivu nami, na nitakulipa.' Lakini mtumwa yule wa kwanza alikataa. Badala yake, alienda na kumtupa gerezani, mpaka atakapo mlipa kile anachomdai. Na walipoona watumwa wenzake kile kilichotokea. Walisikitishwa sana. Walikuja na kumwambia bwana wao kila kitu kilichotokea. Ndipo yule bwana wa mtumwa yule alimwita, na kumwambia, 'Ewe mtumwa mwovu, nilikusamehe wewe deni langu lote kwa sababu ulinisihi sana. Je! Haukutakiwa kuwa na huruma kwa mtumwa mwenzio, kama mimi nilivyokuhurumia wewe? Bwana wake alikasirika na kumkabidhi kwa wale watesaji mpaka atakapolipa kiasi chote alichokuwa anadaiwa.
  • Mfano: wadeni wawili wanaodaiwa dinari mia tano na hamsiniLk 7:41–42
    Aya
    Lk 7:41–42Yesu akasema “Kulikuwa na wadaiwa wawili kwa mkopeshaji mmoja. Mmoja alikuwa anadaiwa dinari mia tano na wa pili alidaiwa dinari hamsini. Na walipokuwa hawana pesa ya kumlipa aliwasamehe wote. Sasa ni nani atampenda zaidi?
  • Patana na mshitaki wako mkiwa njiani kwenda mahakamaniMt 5:25–26
    Aya
    Mt 5:25–26Patana na mshitaki wako upesi, ukiwa pamoja naye njiani kuelekea mahakamani, vinginevyo mshtaki wako anaweza kukuacha mikononi mwa hakimu, na hakimu akuache mikononi mwa askari, nawe utatupwa gerezani. Amini nawaambieni, kamwe hutawekwa huru hadi umelipa senti ya mwisho ya pesa unayodaiwa.
  • Kopesheni bila kutarajia kitu chochoteLk 6:34–35
    Aya
    Lk 6:34–35Kama mkikopesha vitu kwa watu ambao mnategemea watawarudishia, hiyo ni thawabu gani kwenu? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, na hutegemea kupokea kiasi hicho hicho tena. Lakini wapendeni adui zenu na watendeeni mema. Wakopesheni na msihofu kuhusu kurudishiwa, na thawabu yenu itakuwa kubwa. Mtakuwa wana wa Aliye Juu, kwasababu yeye mwenyewe ni mwema kwa watu wasio na shukurani na waovu.
  • Paulo kwa Filemoni: “Hesabu hilo juu yangu. Nitalipa”Flm 1:18–19
    Aya
    Flm 1:18–19Lakini kama amekukosea jambo lolote, au unamdai kitu chochote, kidai hicho kutoka kwangu. Mimi Paulo, ninaandika kwa mkono wangu mwenyewe: mimi nitakulipa. Sisemi kwako kwamba nakudai maisha yako hasa.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0