Bible Explorer

Gundua › Mada › Uvivu

Maisha ya kila siku

Uvivu katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (26), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

Katika Mithali

  • Mwendee chungu, ewe mvivu: hukusanya chakula wakati wa kiangaziMit 6:6–8
    Aya
    Mit 6:6–8Wewe mtu mvivu, mwangalie mchwa, zitafakari njia zake ili kupata busara. Hana akida, afisa au mtawala, lakini huandaa chakula chake wakati wa joto na wakati wa mavuno huweka hazina ili kula baadaye.
  • Usingizi kidogo, na umaskini unakuja kama mnyang’anyiMit 6:9–11
    Aya
    Mit 6:9–11Ewe mtu mvivu, utalala hata lini? Wakati gani utainuka usingizini?” Lala kidogo, sizia kidogo, kunja mikono kupumzika kidogo” - ndipo umasikini wako utakapokujia kama mporaji na uhitaji wako kama askari wa vita.
  • Shamba la mvivu: miiba, michongoma na ukuta wa mawe uliobomokaMit 24:30–34
    Aya
    Mit 24:30–34Nilikwenda jirani na shamba la mtu mvivu, nikapita kwenye shamba la mzabibu la mtu asiye na akili. Miiba imeota kila sehemu, ardhi ilikuwa imefunikwa kwa upupu, na ukuta wake wa mawe ulikuwa umebomoka. Kisha nikaliona na kufikiria juu yake; nikatazama na kupokea mafundisho. Kulala kidogo, kusinzia kidogo, kupumzika kwa kukunja mikono kidogo- na umasikini huja kwa kutembea juu yako, na mahitaji yako kama askari mwenye silaha.
  • Mikono mivivu humfanya mtu maskiniMit 10:4
    Aya
    Mit 10:4Mkono mlegevu humfanya mtu awe masikini, bali mkono wa mtu mwenye bidii hupata utajiri.
  • Alalaye wakati wa mavuno ni mwana aletaye aibuMit 10:5
    Aya
    Mit 10:5Mwana mwenye busara hukusanya mazao wakati wa kiangazi, bali ni aibu kwake alalaye wakati wa mavuno.
  • Kama siki kwa meno na moshi kwa machoMit 10:26
    Aya
    Mit 10:26Kama siki kwenye meno na moshi kwenye macho, ndivyo alivyo mvivu kwa wale waliomtuma.
  • Uvivu huishia katika kazi ya shokoaMit 12:24
    Aya
    Mit 12:24Mkono wa mwenye bidii utatawala, bali watu wavivu watawekwa katika kazi za kulazimishwa.
  • Mvivu hachomi mawindo yakeMit 12:27
    Aya
    Mit 12:27Watu wavivu hawawezi kubanika mawindo yao wenyewe, bali mtu wenye bidii atapata mali zenye thamani.
  • Mvivu hutamani lakini hana kituMit 13:4, Mit 21:25
    Aya
    Mit 13:4Hamu ya watu wavivu ni uchu lakini hawapati kitu, bali hamu ya watu wenye bidii hutoshelezwa sana.
    Mit 21:25Shauku ya mtu mvivu itamuua, maana mikono yake hukataa kufanya kazi.
  • Njia ya mvivu ni kama ugo wa miibaMit 15:19
    Aya
    Mit 15:19Mapito ya mtu goigoi ni kama sehemu yenye uwa wa miiba, bali mapito ya mtu mwadilifu ni njia kuu iliyojengwa imara.
  • Mlegevu katika kazi yake: ndugu yake mharibifuMit 18:9
    Aya
    Mit 18:9Basi, ambaye ni mzembe katika kazi yake ni ndugu yake anayeharibu wengi.
  • Huzamisha mkono wake katika sahani, wala haurudishi kinywaniMit 19:24, Mit 26:15
    Aya
    Mit 19:24Mtu goigoi huuzika mkono wake ndani ya dishi; hataurudisha juu ya kinywa chake.
    Mit 26:15Mtu mvivu hutia mkono wake kwenye sufuria na bado hana nguvu kuunyanyua kwenda kwenye kinywa chake.
  • Halimi kwa wakati wake, na hapati kitu wakati wa mavunoMit 20:4
    Aya
    Mit 20:4Mtu mvivu halimi majira ya kipupwe; hutafuta mazao wakati wa mavuno lakini hapati kitu.
  • “Kuna simba nje!”Mit 22:13, Mit 26:13
    Aya
    Mit 22:13Mtu mvivu husema, “ Kuna simba mtaani! Nitauwawa sehemu za njia.”
    Mit 26:13Mtu mvivu husema “ Kuna simba kwenye barabara! Kuna simba katikati ya njia kuu!”
  • Kama mlango ugeukavyo kwenye bawaba zake, ndivyo mvivu kitandani mwakeMit 26:14
    Aya
    Mit 26:14Kama mlango unavyogeuka kwenye bawaba zake, ndivyo alivyo mtu mvivu kwenye kitanda chake.
  • Mwenye hekima machoni pake kuliko watu saba wajibuo kwa busaraMit 26:16
    Aya
    Mit 26:16Mtu mvivu ni mwenye hekima kwenye macho yake mwenyewe kuliko watu saba wenye ufahamu.

Mahali pengine

  • Kwa uvivu dari hubomoka na nyumba huvujaMhu 10:18
    Aya
    Mhu 10:18Kwa sababu ya uvivu paa huanguka. Na kwa sababu isiyo fanya kazi nyumba hupata ufa.
  • Mpumbavu hukunja mikono yakeMhu 4:5
    Aya
    Mhu 4:5Mpumbavu hukunja mikono yake na hafanyi kazi, hivyo chakula chake in mwili wake.
  • Mtumishi aliyeificha talanta yake anaitwa mvivuMt 25:26
    Aya
    Mt 25:26Lakini bwana wake alijibu na kusema, 'Wewe mtumwa mwovu na mzembe, ulijua kwamba ninachuma mahali ambapo sijapanda na kuvuna mahali ambapo sikusia.
  • Msilegee katika bidiiRum 12:11
    Aya
    Rum 12:11Kuhusu bidii, msiwe walegevu. Kuhusu roho, iweni na shauku. Kuhusu Bwana, mtumikieni.
  • “Mtu asiyetaka kufanya kazi, asile”2 The 3:10–12
    Aya
    2 The 3:10–12Wakati tulipokuwa pamoja nanyi tuliwaagiza, “Ikiwa mmoja wenu hataki kufanya kazi, na asile.” Kwa kuwa tunasikia kwamba baadhi wanaenenda kwa uvivu miongoni mwenu. Hawafanyi kazi lakini badala yake ni watu wasio na utaratibu. Sasa hao nao tunaagiza na kuwaasa katika Bwana Yesu Kristo, kwamba lazima wafanye kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe.
  • Wajane vijana hujifunza uvivu, wakizunguka nyumba kwa nyumba1 Tim 5:13
    Aya
    1 Tim 5:13Na pia huingia kwenye mazoea ya uvivu. Wao huzunguka nyumba kwa nyumba. Si tu kwamba ni wavivu, bali pia huwa wasengenyaji na na wenye kuingilia mambo ya wengine. Wao husema mambo wasiyopaswa kuyasema.
  • Msiwe wavivuEbr 6:12
    Aya
    Ebr 6:12Hatutaki muwe wavivu, lakini muwe wafuasi wa wale warithio ahadi kwa sababu ya imani na uvumilivu.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0