Bible Explorer

Gundua › Mada › Urafiki

Maisha ya kila siku

Urafiki katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (45), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Rafiki hupenda nyakati zote; ndugu huzaliwa kwa ajili ya taabuMit 17:17
    Aya
    Mit 17:17Rafiki hupenda kwa nyakati zote na ndugu amezaliwa kwa ajili ya nyakati za taabu.
  • Yupo rafiki aambatanaye kuliko nduguMit 18:24
    Aya
    Mit 18:24Anayejidai kwa marafiki wengi watamleta katika uharibifu, bali yupo rafiki ambaye huwa karibu kuliko ndugu.
  • Majeraha ya rafiki ni ya uaminifuMit 27:6
    Aya
    Mit 27:6Mwaminifu ni jeraha zilizosababishwa na rafiki, lakini adui anaweza kukubusu kwa kuomba radhi mno.
  • Afadhali jirani aliye karibu kuliko ndugu aliye mbaliMit 27:10
    Aya
    Mit 27:10Usimwache rafiki yako na rafiki wa baba yako, na usiende kwenye nyumba ya ndugu yako katika siku ya msiba wako. Ni bora rafiki ambaye yupo karibu kuliko ndugu ambaye yupo mbali.
  • Kama chuma kinoavyo chuma, ndivyo mtu amnoavyo mwenzakeMit 27:17
    Aya
    Mit 27:17Chuma hunoa chuma; kwa njia ile ile; mtu humnoa rafiki yake.
  • Usiende mara nyingi nyumbani kwa jirani yako, asije akakuchokaMit 25:17
    Aya
    Mit 25:17Usiweke mguu wako kwenye nyumba ya jirani yako mara nyingi, anaweza kuchoshwa nawe na kukuchukia.
  • Baraka ya sauti kubwa alfajiri huhesabiwa kuwa laanaMit 27:14
    Aya
    Mit 27:14Anayempa jirani yake baraka kwa sauti ya juu mapema asubuhi, baraka hiyo itafikiriwa kuwa laana!
  • Usifanye urafiki na mtu mwenye hasiraMit 22:24–25
    Aya
    Mit 22:24–25Usifanye urafiki na mtu mwenye kutawaliwa na hasira na wala usiambatane pamoja na mwenye hasira kali, au utajifunza njia zake na utakuwa chambo kwa nafsi yako.
  • Mali huleta marafiki wengi; maskini huachwaMit 19:4, Mit 19:6
    Aya
    Mit 19:4Utajiri huongeza marafiki wengi, bali mtu masikini hutengwa na rafiki zake.
    Mit 19:6Wengi wataomba fadhila kutoka kwa mtu mkarimu na kila mtu ni rafiki wa yule anayetoa zawadi.
  • Kurudia kosa hutenganisha marafikiMit 17:9
    Aya
    Mit 17:9Anayesamehe kosa hutafuta upendo, bali yeye anayerudia jambo huwatenganisha marafiki wa karibu.
  • Wawili ni bora kuliko mmoja; kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesiMhu 4:9–12
    Aya
    Mhu 4:9–12Watu wawili wanafanya vizuri zaidi ya mmoja; kwa pamoja wanaweza kupata malipo mazuri kwa ajili ya kazi yao. Kwa kuwa kama mmoja akianguka, mwingine anaweza kumwinua rafiki yake. Ingawa, huzuni humfuata yeye aliye peke yake anapoanguka kama hakuna mtu wa kumwinua. Na kama wawili wakilala pamoja, wanaweza kupata joto, lakini mtu mmoja anawezaje kupata joto akiwa mwenyewe? Mtu akiwa peke yake anaweza kushindwa nguvu, lakini wawili wanaweza kusimama katika shambulio, na kama ya nyuzi tatu haikatika upesi.
  • Rafiki wa karibu aliyeshiriki mkate alimgeuka mtunga zaburiZab 41:9, Zab 55:12–14
    Aya
    Zab 41:9Kweli, hata rafiki yangu wa karibu, ambae nilimuamini, aliye kula mkate wangu, ameinua kisigino chake dhidi yangu.
    Zab 55:12–14Kwa maana hakuwa adui aliye nikemea, hivyo ningevumilia; wala ingekuwa ni yule aliye nichukia aliyejiinua mwenyewe dhidi yagu, hivyo ningejificha asinione. Lakini ulikuwa wewe, mtu sawa na mimi, mwenzangu na rafiki yangu. Tulikuwa na ushirika mtamu pamoja; tuliingia katika nyumba ya Mungu tukiwa na umati mkubwa.
  • Ayubu analalamika kwamba marafiki zake wamemgeukaAyu 6:14–15, Ayu 16:20, Ayu 19:19
    Aya
    Ayu 6:14–15Kwa mtu ambaye yu karibu kuzirai, inapasa uaminifu uonyeshwe na rafiki zake; hata kwake yeye aachaye kumcha Mwenyezi. Lakini ndugu zangu wamekuwa waaminifu kwangu kama mkondo wa maji jangwani, mfano wa mifereji ya maji ipitayo mpaka pasipo kitu,
    Ayu 16:20Rafiki zangu wananicheka kwa dharau, lakini jicho langu linamwaga machozi kwa Mungu.
    Ayu 19:19Rafiki zangu wote ninaowazoea wananichukia sana mimi; wale ambao Mimi ninawapenda wamegeuka kinyume na mimi.
  • Katika utetezi wa kwanza wa Paulo, kila mtu alimwacha2 Tim 4:16
    Aya
    2 Tim 4:16Katika utetezi wangu wa kwanza, hakuna mtu yeyote aliyesimama pamoja nami, badala yake, kila mmoja aliniacha. Mungu asiwahesabie hatia.
  • Yesu: hakuna upendo mkuu kuliko wa kuutoa uhai kwa ajili ya rafikiYn 15:13–15
    Aya
    Yn 15:13–15Hakuna mtu aliye na upendo mkuu kuliko huu, kwamba ayatoe maisha yake kwa ajiliya rafiki zake. Ninyi ni rafiki zangu ikiwa mtafanya yale niwaagizayo. Siwaiti watumwa, kwa kuwa mtumwa hajui kile afanyacho bwana wake. Nimewaita ninyi marafiki, kwa sababu nimewajulisheni mambo yote ambayo nimesikia kutoka kwa Baba.

Mifano

  • Abram anamwokoa ndugu yake Lutu kwa watu 318 waliofunzwa vitaMwa 14:14–16
    Aya
    Mwa 14:14–16Abram aliposikia kuwa maadui wamemteka ndugu yake, akawaongoza wanaume waliofunzwa na kuzaliwa nyumbani mwake 318 na akawaongoza hadi Dani. Akawagawanya watu wake dhidi yao usiku na kuwavamia, na kuwafukuza mpaka Hoba, ambayo iko kaskazini mwa Dameski. Kisha akarudisha mali zote, pia akamrudisha ndugu yake Lutu na mali zake, pamoja na wanawake na watu wengine.
  • Ruth hamwachi Naomi: “Uendako wewe, nami nitakwenda”Rut 1:16–17
    Aya
    Rut 1:16–17lakini Ruth alisema, “Usiniache niondoke mbali nawe, kwa kuwa uendako, nitakwenda, utakapoishi, nitaishi; watu wako watakuwa watu wangu, na Mungu wako atakuwa Mungu wangu. Mahali utakapofia, nitafia hapo, na hapo nitazikwa. Yahweh aniwezeshe, na hata zaidi, ikiwa kuna chochote isipokuwa kifo kamwe hakiwezi kututenganisha.
  • Samweli anamwombolezea Sauli1 Sam 15:35, 1 Sam 16:1
    Aya
    1 Sam 15:35Samweli hakumuona tena Sauli hadi siku ya kifo chake, lakini alimwombolezea Sauli. Na BWANA alijuta kwa kumfanya Sauli awe mfalme juu ya Israeli.
    1 Sam 16:1BWANA akamwambia Samweli, “Utamlilia Sauli kwa muda gani, ikiwa nimemkataa asiwe mfalme juu ya Israeli? Ijaze pembe yako mafuta na uende. Nitakutuma kwa Yese akaaye Bethlehemu, maana nimejichagulia mfalme katika wanawe.
  • Yonathani anampenda Daudi kama nafsi yake na kumpa joho lake1 Sam 18:1–4
    Aya
    1 Sam 18:1–4Daudi alipokuwa amemaliza kuongea na Sauli, roho ya Yonathani ilishikana na roho ya Daudi, na Yonathani akampenda kama roho yake mwenyewe. Sauli akamweka kazini Daudi siku hiyo, hakumwacha arudi nyumbani kwa baba yake. Kisha Yonathani na Daudi wakafanya makubaliano ya urafiki kwa sababu Yonathani alimenda kama roho yake mwenyewe. Yonathani akavua kanzu aliyokuwa amevaa na kumpa Daudi, akampa na vazi lake la kivita, pamoja na upanga, upinde, na mshipi.
  • Daudi na Yonathani wanabusiana, wanalia na kuagana kwa kiapo1 Sam 20:41–42, 1 Sam 23:16–18
    Aya
    1 Sam 20:41–42Punde tu kijana alipoondoka, Daudi akasimama kutokea upande wa kusini, akiwa amelala kifudifudi, akainama mara tatu. Walibusiana wao kwa wao na wote wakalia kwa pamoja, Daudi akilia zaidi. Yonathani akamwambia Daudi, “Nenda kwa amani, kwa sababu wote tumeapa kwa jina la BWANA na tulisema, 'BWANA awe kati yangu na wewe, na awe kati ya uzao wangu na uzao wako, milele.'” Kisha Daudi alisimama na akaondoka, na Yonathani akarudi mjini.
    1 Sam 23:16–18Kisha Yonathani, mwana wa Sauli, akaamuka akaenda kwa Daudi huko Horshi, naye akamtia moyo amtumainie Mungu. Akamwambia, “Usiogope. Kwa maana mkono wa baba yangu Sauli hautakupata. Utakuwa mfalme juu ya Israeli, na mimi nitakuwa msaidizi wako. Baba yangu Sauli pia anajua hivyo.” Basi wote wawili wakafanya agano mbele za BWANA. Kisha Daudi alibaki Horeshi, na Yonathani akaenda nyumbani.
  • Maombolezo ya Daudi: “Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu”2 Sam 1:26
    Aya
    2 Sam 1:26Nimesikitishwa sana kwa ajili yako, Yonathani ndugu yangu. Ulikuwa mpendwa wangu sana. Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu, ukipita upendo wa wanawake.
  • Kwa ajili ya Yonathani, Mefiboshethi hula daima mezani pa Daudi2 Sam 9:1, 2 Sam 9:7
    Aya
    2 Sam 9:1Daudi akasema, “Je kuna yeyote aliyesalia wa familia ya Sauli ambaye naweza kumwonyesha kwa fadhiri kwa ajili ya Yonathani?
    2 Sam 9:7Daudi akamwambia, “Usiogope, maana hakika nitakufadhiri kwa ajili ya Yonathani baba yako, nami nitakurudishia ardhi yote ya Sauli babu yako, nawe utakula katika meza yangu daima.”
  • Daudi kwa kuhani Abiathari: “Kaa nami; utakuwa salama”1 Sam 22:23
    Aya
    1 Sam 22:23Kaa pamoja nami na usiogope. Maana mtu anayetafuta roho yako anatafuta pia roho yangu. Utakuwa salama ukiwa pamoja nami.”
  • Hiramu mfalme wa Tiro alikuwa rafiki wa Daudi siku zote1 Fal 5:1
    Aya
    1 Fal 5:1Hiramu mfalme wa Tiro aliwatuma watumishi wake kwa Sulemani kwa kuwa alisikia kuwa walikuwa wamemtawaza kuwa mfalme mahali pa baba yake, kwani Hiramu alimpenda Daudi.
  • Rafiki wa Daudi, Hushai, anabaki mwaminifu wakati wa uasi wa Absalomu2 Sam 15:32–37, 2 Sam 16:16–17
    Aya
    2 Sam 15:32–37Ikawa Daudi alipofika juu njiani mahala Mungu alipokuwa akiabudiwa, Hushai Mwarki akaja kumlaki vazi lake limeraruliwa na mavumbi kichwani pake. Daudi akamwambia, “Ikiwa utaenda nami utakuwa mzigo kwangu. Lakini ukirudi mjini na kumwambia Absalomu, 'Nitakuwa mtumishi wa mfalme kama nilivokuwa mtumishi wa baba yako, ndivyo nitakavyokuwa mtumishi wako,' ndipo utayageuza mashauri ya Ahithofeli kwa ajili yangu. Je haunao pamoja nawe Sadoki na Abiathari makuhani? Hivyo chochote ukisikiacho katika kasri, uwaambie Sadoki na Abiathari makuhani. Tazama wanao pamoja nao wana wao wawili, Ahimaasi, mwana wa Sadoki, na Yonathani mwana wa Abiathari. Mniletee habari juu ya kila mnachokisikia.” Hivyo Hushai, rafiki wa Daudi, akaja mjini wakati Absalomu anafika na kuingia Yerusalemu.
    2 Sam 16:16–17Ikawa Hushai Mwarki, rafiki yake Daudi, akaja kwa Absalomu, naye akamwambia Absalomu, “Mfalme aishi daima! mfalme aishi daima. Absalomu akamwambia Hushai, “Je huu ndiyo utiifu wako kwa rafiki yako? Kwa nini haukwenda pamoja naye?”
  • Itai Mgiti anakataa kumwacha Daudi anayekimbia2 Sam 15:19–21
    Aya
    2 Sam 15:19–21Kisha mfalme akamwambia Itai Mgiti, “Kwa nini wewe pia uende nasi? Rudi na ukae na mfalme Absalomu kwa kuwa wewe ni mgeni tena mfungwa. Rudi mahali pako mwenyewe. Kwani ni jana tu umeondoka, kwa nini nikufanye uzunguke nasi popote? Hata sijui niendako. Hivyo rudi pamoja na wenzako. Utiifu na uaminifu viambatane nawe.” Lakini Itai akamjibu mfalme na kusema, “Kama Yahwe aishivyo na kama bwana wangu mfalme aishivyo, kwa hakika mahali popote bwana wangu mfalme aendako, mtumishi wako pia ndipo atakapokwenda, kwamba ni maisha au kifo.”
  • Mfalme Ahazia anamtembelea Mfalme Yoramu aliyejeruhiwa2 Fal 8:28–29
    Aya
    2 Fal 8:28–29Ahazia akaenda pamoja na Yoramu mwana wa Ahabu, kupigana dhidi ya Hazaeli, mfalme wa Shamu, katika Ramath Geleadi. Washami wakamjeruhi Yoramu. Mfalme Yoramu akarudi ili auguzwe huko Yezreeli kwenye yale majeraha ambayo Washami walimpatia huko Rama. Wakati alipopigana dhidi ya Hazaeli mfalme wa Shamu. Hivyo Ahazi mwana wa Yehoramu, mfalme Yuda, akashuka kwa Yezreeli kumuona Yoramu mwana wa Ahabu, kwa sababu Yoramu alikuwa amejeruhiwa.
  • Marafiki watatu wa Ayubu wanakaa naye siku saba kimyaAyu 2:11–13
    Aya
    Ayu 2:11–13Sasa wakati rafiki zake watatu wa Ayubu walipopata habari ya mabaya yaliyompata, kila mmoja wao akaja kutoka mahali pake: Elifazi Mtemani, Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi. Wakatenga muda ili waende kuomboleza naye na kumfariji. Walipoinua macho yao wakiwa mbali, hawakuweza kumtambua. Wakapaza sauti zao na kulia; kila mmoja wao akararua joho lake na kurusha majivu hewani na juu ya kichwa chake. Kisha wakaketi chini pamoja naye kwa muda wa siku saba-mchana na usiku. Hakuna hata mmoja aliyesema naye neno, kwa kuwa waliona kuwa huzuni yake ilikuwa kuu mno.
  • Danieli anamwomba mfalme awapandishe cheo marafiki zake watatuDan 2:17–18, Dan 2:49
    Aya
    Dan 2:17–18Kisha Danieli aliingia ndani ya nyumba na aliwaelezea Hanania, Mishaeli, na Azaria, kile kilichotokea. Aliwasihi kutafuta rehema kutoka kwa Mungu wa mbinguni kuhusiana na siri hii ili kwamba yeye na wao wasije wakauawa pamoja na watu wengine waliosalia waliojulikana kuwa na hekima katika Babeli.
    Dan 2:49Danieli alipeleka ombi kwa mfalme, na mfalme aliwateua Shadraka, Meshaki na Abedinego kuwa watawala juu ya jimbo la Babeli. Lakini Danieli alisalia katika ikulu ya mfalme.
  • Yesu aliwapenda Martha, dada yake na LazaroLk 10:38–39, Yn 11:5, Yn 11:11
    Aya
    Lk 10:38–39Sasa walipokuwa wakisafiri, waliingia katika kijiji fulani, na mwanamke mmoja jina lake Martha alimkaribisha nyumbani kwake. Alikuwa na dada aliyeitwa Mariamu, aliekaa miguuni pa Bwana na kusikiliza neno lake.
    Yn 11:5Yesu alimpenda Martha na dada yake na Lazaro.
    Yn 11:11Yesu akasema mambo haya, na baada ya mambo haya, akawaambia, “Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini ninakwenda ili kwamba nipate kumuamsha kutoka usingizini.”
  • Mpwa wa Paulo anamwonya juu ya njamaMdo 23:16
    Aya
    Mdo 23:16Lakini mtoto wa dada yake na Paulo akasikia kwamba kulikuwa na njama, akaenda akaingia ndani ya ngome na kumwambia Paulo.
  • Prisila na Akila walihatarisha maisha yao kwa ajili ya PauloRum 16:3–4
    Aya
    Rum 16:3–4Msalimu Priska na Akila, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu, ambao kwa maisha yangu waliyahatarisha maisha yao wenyewe. Ninatoa shukrani kwao, na siyo tu mimi, bali pia kwa makanisa yote ya mataifa.
  • Paulo kuhusu Timotheo: “Sina mwingine kama yeye”Flp 2:19–22
    Aya
    Flp 2:19–22Lakini natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo kwenu hivi karibuni, ili kwamba niweze kutiwa moyo nitakapojua mambo yenu. Kwa kuwa sina mwingine aliye na mtazamo kama wake, mwenye nia ya kweli kwa ajili yenu. Wengine wote ambao ningewatuma kwenu wanatafuta mambo yao binafsi tu, na siyo mambo ya Yesu Kristo. Lakini mnaijua thamani yake, kwa sababu kama mtoto anavyomhudumia baba yake, ndivyo alivyotumika pamoja nami katika injili.
  • Epafradito: ndugu, mtenda kazi mwenzake na askari mwenzake wa PauloFlp 2:25
    Aya
    Flp 2:25Lakini nafikiri ni muhimu kumrejesha kwenu Epafradito. Yeye ni ndugu yangu na mtenda kazi mwenzangu na askari mwenzangu, mjumbe na mtumishi wenu kwa ajili ya mahitaji yangu.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0