Maisha ya kila siku
Kodi katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (35), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
- Kila aliyehesabiwa katika sensa alilipa nusu shekeliKut 30:11–16, Kut 38:26
Aya
Kut 30:11–16BWANA akanena na Musa, “Utakapowahesabu wana wa Israeli, kama itakavyotokea hesabu yao, ndipo watakapompa BWANA kila mtu ukombozi kwa ajili ya roho yake, hapo utakapowahesabu; ili kwamba yasiwe maradhi kati yao, hapo utakapowahesabu. Kila mtu apitaye kwa wale waliohesabiwa atatoa nusu shekeli kwa kuiandama shekeli ya mahali patakatifu; (shekeli ni gera ishirini). Nusu shekeli kwa sadaka ya Yahweh. Kila mtu apitaye kwa wale waliohesabiwa tangu huyo ambaye umri wake ni miaka ishirini, au zaidi, atatoa hiyo sadaka kwangu. Watu watakapo leta hii sadaka kwangu kufanya upatananisho, matajiri hawataleta zaidi, wala maskini hawataleta kilichopungua katika hiyo nusu shekeli. Nawe utapokea hizo fedha za upatanisho mikononi mwa hao wana wa Israeli, na kuziweka kwa ajili ya utumishi wa hema ya kukutania. Ili kwamba ziwe ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli mbele yangu ili kufanya upatanisho kwa ajili ya roho zenu.
Kut 38:26ile nusu shekeli kwa ajili ya mtu mmoja ilikuwa nusu shekeli kulingana na shekeli ya mahali patakatifu,. Kwa kila mtu aliyekuwa akipita kuingia upande wa wale waliokuwa wameandikishwa kuanzia miaka ishirini na zaidi, jumla ya watu 603,550.
- Theluthi moja ya shekeli kila mwaka kwa ajili ya nyumba ya MunguNeh 10:32
Aya
Neh 10:32Tulikubali amri za kutoa shilingi ya shekeli kila mwaka kwa ajili ya huduma ya nyumba ya Mungu wetu,
- Yusufu: sehemu ya tano ya mavuno ya Misri ni ya FaraoMwa 41:34, Mwa 47:24
- Ni ardhi ya makuhani wa Misri peke yake isiyo mali ya FaraoMwa 47:26
Aya
Mwa 47:26Hivyo Yusufu akaifanya kuwa sheria inayofanya kazi hata leo katika nchi ya Misri, kwamba moja ya tano ni ya Farao. Eneo la makuhani peke yake ndo halikufanywa kuwa la Farao.
- Mfalme wa Uajemi anawasamehe kodi makuhani na watumishi wa hekaluEzr 7:24
Aya
Ezr 7:24Tutawapa taarifa wao kuhusu ninyi kwamba wasiwatoze ushuru wowote au kodi kwa kuhani, mlawi, mwimbaji, mlinzi au kwa mtu aliyechaguliwa kwenye huduma ya Hekalu na mtumishi katika nyumba ya Mungu.
- Familia ya atakayemuua Goliathi haitalipa kodi1 Sam 17:25
Aya
1 Sam 17:25Watu wa Israeli walisema, “Umemuona mtu huyu aliyejitokeza? Amekuja kuipa changamoto Israeli. Basi mfalme atampa mali nyingi mtu atakayemua, atamuozesha binti yake, na familia ya baba yake haitalipa kodi katika Israeli.”
- Msamaha wa kodi kwa ajili ya karamu ya EstaEst 2:18
Aya
Est 2:18mfalme akawafanyia karamu kubwa wasimamizi na wahudumu wake wote, karamu ya Esta na akawapa unafuu wa kodi katika majimbo. Pia akawapa zawadi kwa ukarimu.
- Ahasuero anatoza ushuru hadi pwani za mbali kabisaEst 10:1
Aya
Est 10:1Kisha Mfalme Ahusiero akaweka kodi juu ya nchi na maeneo ya bahari.
Wafalme na kodi
- Maafisa kumi na wawili wa Sulemani kila mmoja anaihudumia ikulu mwezi mmoja1 Fal 4:7
Aya
1 Fal 4:7Sulemani alikuwa na maakida kumi na wawili juu ya Israeli yote, ambao walitoa chakula kwa mfalme na watu wake wote. Kila mtu alikuwa na zamu ya kuhudumia kwa mwezi mmoja katka mwaka.
- Chakula cha Sulemani kwa siku moja tu1 Fal 4:22–23
Aya
1 Fal 4:22–23Mahitaji ya Sulemani kwa siku moja yalikuwa ni Kori thelathini za unga mzuri na kori unga wa ngano, makisai kumi walionona, na fahari ishirini wa malisho, na kondoo mia moja, nje ya ayala, paa, na kulungu na kuku walionona.
- Kazi ya shokoa kwa majengo ya Sulemani1 Fal 9:15
Aya
1 Fal 9:15Vifuatavyo ndivyo vigezo ambavyo mfalme Sulemani aliweka: ili kulijenga hekalu la BWANA na ikulu yake, kuijenga Milo na ukuta wa Yerusalemu, na Hazori, Megido, na Gezari.
- Adoramu alisimamia kazi ya shokoa2 Sam 20:24, 1 Fal 4:6
Aya
2 Sam 20:24Adoramu alikuwa juu ya watu waliofanya kazi ya shokoa na Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mkumbushaji.
1 Fal 4:6Ahishari alikuwa mkuu wa nyumba. Adoniramu mwana wa Abda alikuwa mkuu wa watenda kazi.
- Israeli inamwomba Rehoboamu aipunguze nira nzito1 Fal 12:4
Aya
1 Fal 12:4Baba yako aliifanya nira yetu kuwa nzito. Sasa ifanye kazi ngumu ya baba yako kuwa nyepesi kuliko nira ngumu ambayo baba yako alituwekea, nasi tutakutumikia.”
- Israeli inampiga Adoramu kwa mawe hadi kufa; Rehoboamu anakimbia1 Fal 12:18
Aya
1 Fal 12:18Kisha mfalme Rehoboamu akamtuma Adoramu, aliyekuwa juu ya shokoa, lakini Waisraeli wote wakampiga kwa mawe wakamwua kwa mawe. Mflme Rehoboamu akakimbia haraka kwa gari lake kwenda Yerusalemu.
- Menahemu anampa Pulu talanta elfu moja za fedha2 Fal 15:19–20
Aya
2 Fal 15:19–20Kisha Pulu mfalme wa Ashuru akaja kinyume cha nchi, na Menahemu akampatia Pulu talanta elfu moja za fedha, hivyo msaada wa Pulu ungeweza kuwa na yeye kuimarisha utawala wa Israeli katika nchi yake. Menahemu akatoza hii pesa kutoka Israeli kwa kumtaka kila mtu tajiri alipe shekeli hamsini za fedha kwake kumpatia mfalme wa Ashura. Hivyo mfalme wa Ashuru akarudi na hakukaa pale katika ile nchi.
- Yehoyakimu anaitoza nchi kodi ili kumlipa Farao Neko2 Fal 23:35
Aya
2 Fal 23:35Yehoyakimu akalipa fedha na dhahabu kwa Farao. Ili akutane na amri ya Farao, Yehoyakimu akaitoza nchi na kulazimisha kila mtu miongoni mwa watu wa nchi wamlipe fedha na dhahabu kulingana na makadirio yao.
- Maadui wanamwonya mfalme: Yerusalemu utaacha kulipa ushuruEzr 4:13, Ezr 4:20
- Watu wanakopa fedha ili kulipa kodi ya mfalme kwa mashamba yaoNeh 5:4
Aya
Neh 5:4Wengine pia walisema, “Tumekopesha pesa kulipa kodi ya mfalme kwenye mashamba yetu na mashamba yetu ya mizabibu.
- Kodi ya nafaka inachukuliwa kutoka kwa maskiniAmo 5:11
Aya
Amo 5:11Kwa sababu mnamkanyaga chini maskini na kuchukua sehemu ya ngano kutoka kwake- ingawa mmejenga nyumba za mawe yaliyochongwa, hamtaishi kwenye nyumba hizo. Mmependezwa na mashamba ya mizabibu, lakini hamtakunywa mvinyo wake.
Katika Injili
- Kaisari Agusto anaamuru sensa ya ufalme woteLk 2:1–3
Aya
Lk 2:1–3Sasa katika siku hizo, ikatokea kwamba Kaisari Agusto alitoa agizo akielekeza kwamba ichukuliwe sensa ya watu wote wanaoishi duniani. Hii ilikuwa ni sensa ya kwanza iliyofanyika wakati Krenio akiwa gavana wa Siria. Hivyo kila mmoja akaenda mjini kwake kuandikishwa sensa.
- Kodi ya hekalu: sarafu kinywani mwa samakiMt 17:24–27
Aya
Mt 17:24–27Nao walipofika Kapenaumu, watu wakusanyao kodi ya nusu shekeli wakamwendea Petro na kusema, “Je mwalimu wenu hulipa kodi ya nusu shekeli?” Akasema, “Ndiyo” Lakini Petro alipoingia ndani ya nyumba, Yesu akaongea na Petro kwanza na kusema, “ Unafikiria nini Simon? Wafalme wa dunia, hupokea kodi au ushuru kutoka nani? Kwa wale wanaowatawa kutoka kwa wageni? Na wakati Petro aliposema, “Kutoka kwa wageni” Yesu akamwambia, hivyo watawaliwa wameondolewa katika ulipaji. Lakini tusije tukawafanya watoza ushuru wakatenda dhambi, nenda baharini, tupa ndoano, na umtwae yule samaki ajaye kwanza. Baada ya kuufungua mdomo wake, utakuta mle shekeli moja. Ichukue na uwape watoza ushuru kwa ajili yangu na wewe.
- “Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari au la?”Mt 22:17–21
Aya
Mt 22:17–21Kwa hiyo tuambie, unafikiri nini? Je, ni sahihi kisheria kulipa kodi kwa Kaisari au hapana?” Yesu alifahamu uovu wao na akasema, “Kwa nini mnanijaribu, enyi wanafiki? Nionesheni pesa itumikayo kulipia kodi.” Ndipo wakamletea dinari. Yesu akawauliza, “Sura na jina hili ni vya nani?” Wakamjibu, “Vya Kaisari.” Ndipo Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari vitu vilivyo vyake na vya Mungu mpeni Mungu.”
- Yohana kwa watoza ushuru: “Msitoze zaidi ya mlivyoagizwa”Lk 3:12–13
Aya
Lk 3:12–13Kisha baadhi ya watoza ushuru walikuja pia kubatizwa, na wakamwambia, “Mwalimu, tunatakiwa kufanya nini? Akawaambia, “Msikusanye fedha zaidi kuliko mnachotakiwa kukusanya.”
- Lawi anaitwa kutoka mahali pa kukusanyia kodiMk 2:14, Lk 5:27
- Yesu anakula pamoja na watoza ushuru, na Mafarisayo wanalalamikaMt 9:10–11, Mt 11:19
Aya
Mt 9:10–11Na Yesu alipoketi ili ale chakula ndani ya nyumba, wakaja watoza ushuru wengi na watu waovu wakashiriki chakula pamoja na Yesu na wanafunzi wake. Ndipo Mafarisayo walipoona hayo, wakawaambia wanafunzi “Kwa nini mwalimu wenu anakula chakula pamoja na watoza ushuru na watu waovu?”
Mt 11:19Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa na wakasema 'Angalia, ni mtu mlaji na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi!' Lakini hekima inadhihirishwa kwa matendo yake.''
- Mfano: Farisayo na mtoza ushuru hekaluniLk 18:10–13
Aya
Lk 18:10–13'Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali: mmoja Mfarisayo mwingine mtoza ushuru. Farisayo akasimama akaomba mambo haya juu yake mwenyewe, 'Mungu, nakushukuru kwa vile mimi si kama watu wengine ambao ni wanyang'anyi, watu wasio waadilifu, wazinzi, au kama huyu mtoza ushuru. Nafunga mara mbili kila wiki. Natoa zaka katika mapato yote ninayopata. ' Lakini yule mtoza ushuru, alisimama mbali, bila hakuweza hata kuinua macho yake mbinguni, akagonga kifua chake akisema, 'Mungu, nirehemu mimi mwenye dhambi.'
- Zakayo, mkuu wa watoza ushuru, atarudisha mara nneLk 19:2, Lk 19:8
- Paulo: lipeni kodi kwa wanaostahili kodiRum 13:6–7
Aya
Rum 13:6–7Kwa ajili hii pia unalipa kodi. Kwa kuwa wenye mamlaka ni watumishi wa Mungu, ambao wanaendelea kufanya jambo hili. Mlipeni kila mmoja ambacho wanawadai: kodi kwa astahiliye kodi; ushuru kwa astahiliye ushuru; hofu kwa astahiliye hofu; heshima kwa astahiliye heshima.
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0