Maisha ya kila siku
Wajane katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (37), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
Katika Sheria
- Msimtendee vibaya mjane wala yatimaKut 22:22–24
Aya
Kut 22:22–24Hauruhusiwi kumtendea vibaya mjane au mtoto asiye kuwa na baba. Ukiwadhuru ata kidogo, na kama wakiniita mimi, hakika nitasikia sauti yao. Hasira yangu itawaka, na nitakuua kwa upanga; wake zenu watakuwa wajane, na watoto wenu pasipo baba.
- Miganda, zeituni na zabibu zilizobaki zinaachwa kwa ajili ya mjaneKum 24:19–21
Aya
Kum 24:19–21Utakapovuna zao lako shambani mwako, na ukasahau kipande cha mbegu shambani, haupaswi kurudi na kukichukua; kinapaswa kuwa cha mgeni, cha yatima, au cha mjane, ili Yahwe Mungu wako akubariki katika kazi ya mikono yako. Utakapotikisa mti wako wa mzeituni, haupaswi kupanda juu ya matawi tena; itakuwa kwa ajili ya mgeni, kwa yatima na kwa mjane. Utakapokusanya mizabibu shambani mwako, haupaswi kukusanya masazo yake tena. Kinachobaki kitakuwa cha mgeni, cha yatima na cha mjane.
- Zaka ya kila mwaka wa tatu inawalisha mjane, yatima na mgeniKum 14:28–29
Aya
Kum 14:28–29Mwisho mwa kila miaka mitatu mtawasilisha mafungu yote ya kumi ya mazao kwa mwaka huo huo, na mtatunza katika malango yenu; na Mlawi, kwa sababu hana sehemu wala urithi pamoja nanyi, na mgeni, na yatima, na wajane walio ndani ya malango yenu, watakuja na kula na kurithika. Fanya hivyo kwa Yahwe Mungu wenu aweze kuwabariki katika kazi zote za mikono yenuo mnazofanya.
- Wajane wanashiriki furaha ya sikukuuKum 16:11, Kum 16:14
Aya
Kum 16:11Utafurahi mbele ya Yahwe Mungu wako- wewe, kijana wako, binti wako, mjakazi wako wa kiume, mjakazi wako wa kike, Mlawi aliye katika malango yako, na mgeni, yatima, na mjane alio miongoni mwenu, katika eneo ambalo Yahwe Mungu wako atachagua kwa ajili ya patakatifu pake.
Kum 16:14Utafurahi wakati wa sherehe- wewe, kijana wako, binti wako, mjakazi wako wa kiume, mjakazi wako wa kike, Mlawi, na mgeni, na yatima na mjane walio ndani ya malango yako.
- Usichukue vazi la mjane kama rehaniKum 24:17
Aya
Kum 24:17Haupaswi kutumia nguvu kuchukua haki inayomhusu mgeni au yatima, wala kuchukua vazi la mjane kama dhamana.
- Nadhiri ya mjane inamfungaHesabu 30:9
Aya
Hesabu 30:9Lakini kwa mjane au kwa mwanamke aliyetalikiwa, kila kitu amabacho atakisema kufunga nafsi yake lazima kitabaki na nguvu kinyume na yeye.
- Binti wa kuhani, mjane asiye na mtoto, anaweza kula mezani pa baba yakeLaw 22:13
Aya
Law 22:13Lakini ikiwa huyo binti wa kuhani ni mjane au ametalikiwa, na ikiwa hana mtoto, na anarudi kuishi knyumbani kwa baba yake kama alivyokuwa wakati wa ujana wake, anaweza kula kutoka katika chakula cha baba yake. Lakini hakuna yeyote asiye wa familia ya kikuhani anatakayeruhusiwa kula kutoka katika chakula cha kuhani.
- Kuhani mkuu hawezi kumwoa mjaneLaw 21:14
Aya
Law 21:14Hataoa mjene, mwanamke mtalaka au mwanamke aliye kahaba. Anaweza kuoa mwanamke bikira kutoka kwa watu wake,
- Ndugu humwoa mjane asiye na mtoto wa ndugu yakeKum 25:5–10
Aya
Kum 25:5–10Iwapo kaka wanaishi pamoja na mmoja wao akafariki bila kuwa na mwana, basi mke wa marehemu hatakiwi kuolewa na mtu nje ya familia. Badala yake, kaka yake mumewe anapaswa kulala naye na kumchukua kuwa mke wake na kutekeleza wajibu wa kaka wa mume kwake. Hii ni kwamba mtoto wa kwanza atakayezaliwa arithi chini ya jina la kaka yake mwanamume aliyefariki, ili jina lake lisiangamie ndani ya Israeli. Lakini kama mwanamume hataki kumchukua mke wa kaka yake awe wake, basi mke wa kaka yake anapaswa kwenda malangoni mpaka kwa wazee na kusema, “Kaka wa mume wangu amekataa kuwajibika kwa niaba ya jina la kaka yake humu Israeli; hataki kufanya wajibu wa kaka wa mume kwangu”. Kisha wazee wa mji wake wanapaswa kumuita na kuzungumza naye. Lakini tuseme atasisitiza na kusema, “Sitaki kumchukua”. Basi mke wa kaka yake anatakiwa kuja kwake mbele ya wazee, kumvua ndara zake miguuni mwake, na kumtemea usoni. Anapaswa kumjibu na kusema, “Hivi ndivyo kinachofanyika kwa mwanamume asiyetaka kujenga nyumba ya kaka yake”. Jina lake Israeli litaitwa, “Nyumba ya mtu aliyevuliwa ndara zake”.
Misemo
- Mungu ni “mlinzi wa wajane”Zab 68:5, Zab 146:9
- Manabii: teteeni haki ya mjaneIsa 1:17, Yer 22:3, Zek 7:10
Aya
Isa 1:17jifunze kutenda mema; tafuta ukweli; msiwanyanyase, wapeni haki yatima, walindeni wajane.''
Yer 22:3Bwana asema hivi, “Fanya haki na uadilifu, na mtu yeyote ambaye ameibiwa-muokoeni kutoka mkononi mwa mshindani. Usimtendee mabaya mgeni yeyote katika nchi yako, au yatima au mjane. Usifanye vurugu au kumwaga damu isiyo na hatia mahali hapa.
Zek 7:10Juu ya mjane na yatima, mgeni, na masikini - usiwanyanyase, na asiwepo miongoni mwenu anayepanga madhara yoyote dhidi ya mwingine mioyoni mwenu.
- Ayubu: “Nilifanya moyo wa mjane uimbe kwa furaha”Ayu 29:13, Ayu 31:16
- Yesu anaonya juu ya watu wanaowanyang’anya wajane nyumba zaoMk 12:40
Aya
Mk 12:40Pia wanakula nyumba za wajane na wanaomba maombi marefu ili watu wawaone. Hawa watu watapokea hukumu iliyo kuu.”
- Paulo: familia ziwasaidie wajane wao wenyewe1 Tim 5:3–5, 1 Tim 5:16
Aya
1 Tim 5:3–5Waheshimu wajane, wale walio wajane kweli kweli. Lakini kama mjane ana watoto au wajukuu, waache kwanza wajifunze kuonesha heshima kwa watu wa nyumbani mwao wenyewe. Waache wawalipe wazazi wao mema, kwa kuwa hii inapendeza mbele za Mungu. Lakini mjane kweli kweli ni yule aliyeachwa peke yake. Naye huweka tegemeo lake kwa Mungu. Siku zote hudumu katika sala na maombi usiku na mchana.
1 Tim 5:16Kama mwanamke yeyote aaminiye ana wajane, basi na awasaidie, ili kanisa lisilemewe, ili liweze kuwasaidia wale walio wajane kweli kweli.
- Mjane aliyeandikishwa kusaidiwa ilibidi awe na miaka sitini angalau1 Tim 5:9–10
Aya
1 Tim 5:9–10Basi mwanamke aandikishwe kwenye orodha kama mjane akiwa na umri usiopungua miaka sitini, na ni mke wa mume mmoja. Lazima awe amejulikana kwa matendo mema, ikiwa ni kwamba amewajali watoto, au ameshakuwa mkarimu kwa wageni, au ameosha miguu ya waaminio, au alimesaidia ambao wamekuwa wakiteswa, au alijitoa kwa kazi yeyote njema.
- Mjane yuko huru kuolewa tena1 Kor 7:39
Aya
1 Kor 7:39Mwanamke amefungwa na mmewe wakati yu hai. Lakini kama mmewe akifa, yuko huru kuolewa na yeyote ampendaye, lakini katika Bwana tu.
Mifano
- Tamari anaishi kama mjane nyumbani kwa baba yake, akivaa mavazi ya ujaneMwa 38:11, Mwa 38:14, Mwa 38:19
Aya
Mwa 38:11Kisha Yuda akamwambia Tamari, mkwewe, “Ukakae mjane katika nyumb aya baba yako hadi Shela, mwanangu, atakapokuwa.” Kwani aliogopa, “Asije akafa pia, kama nduguze.” Tamari akaondoka na kuishi katika nyumba ya babaye.
Mwa 38:14Akavua mavazi yake ya ujane na akajifunika kwa ushungi. Akakaa katika lango la Enaimu, lililoko kando ya njia iendayo Timna. Kwa maana aliona kwamba Shela amekua lakini akupewe kuwa mke wake.
Mwa 38:19Akaamka na kuondoka. Akavua ushungi wake na kuvaa vazi la ujane wake.
- Naomi anafiwa na mumewe na wanawe wawili huko MoabuRut 1:3–5
Aya
Rut 1:3–5Ndipo Elimeleki, mume wa Naomi, alikufa, na Naomi aliachwa na watoto wake wa kiume wawili. Watoto hawa walioa wanawake wa Moabu; jina la mmoja lilikuwa Oripa, na jina la mwingine lilikuwa Ruth. waliishi huko kwa takribani miaka kumi. Kisha wote Mahiloni na Kileoni walikufa, na kumuacha Naomi bila mme wake na bila watoto wake wawili.
- Ruth anaokota masazo mashambani ili amlishe NaomiRut 2:2–3
Aya
Rut 2:2–3Ruth, Mmoabu, alimwambia Naomi, “Ngoja niende nikakusanye mabaki ya chakula katika shamba. Nitamfuata yeyote ambaye nitapata kibali machoni pake.” Hivyo naomi akamwambia, “Nenda, mwanangu.” Ruth alienda kuvuna kwenye shamba akiwafuata kwa nyuma wavunaji. Na kumbe ile sehemu ya shamba ilikuwa ni mali ya Boazi, aliyekuwa na mahusiano na Elimeleki.
- Mwanamke wa Tekoa anajifanya mjane mbele ya Daudi2 Sam 14:2–5
Aya
2 Sam 14:2–5Hivyo Yoabu akatuma neno huko Tekoa kumleta kwake mwanamke mwelevu. Akamwambia, “Tafadhari, vaa mavazi ya uombolezaji ujifanye kuwa mwombolezaji. Usijipake mafuta, lakini uwe kama mwanamke ambaye ameomboleza kwa muda mrefu kwa ajili yake aliyekufa. Kisha ingia kwa mfalme na umwambiye maneno nitakayokueleza.” Hivyo Yoabu akamwambia maneno ambayo angeyasema kwa mfalme. Wakati mwanamke kutoka Tekoa alipoongea na mfalme, aliinamisha uso wake chini na kusema, “Mfalme, anisaidie.” Mfalme akamwambia, “Shida yako ni nini?” Akajibu, Ukweli ni kwamba mimi ni mjane, mme wangu alikufa.
- Huramu, fundi shaba wa Sulemani, alikuwa mwana wa mjane1 Fal 7:14
Aya
1 Fal 7:14Huramu alikuwa mwana wa mjane wa kabila ya Naftali; baba yake alikuwa mtu wa Tiro, mfua shaba. Huramu alikuwa mwingi wa hekima na ufahamu na stadi za kufanya kazi kubwa za shaba. Aliletwa kwa mfalme ili kufanya kazi zilizohusiana na shaba kwa mfalme.
- Mama yake Yeroboamu, Serua, alikuwa mjane1 Fal 11:26
Aya
1 Fal 11:26Kisha Yeroboamu mwana wa Nebati, mwefraimu wa Sereda, akida wa Sulemani, ambaye jina la mama yake lilikuwa Serua, mjane, pia akainua mkono wake dhidi ya mfalme.
- Mjane wa Sarepta ana konzi moja tu ya unga na mafuta kidogo1 Fal 17:10–16
Aya
1 Fal 17:10–16Kwa hiyo akainuka na akaenda Sarepta, na alipofika kwenye lango la mji, kulikuwa na mjane akiokota kuni. Kwa hiyo akamwita na akamwambia, “Tafadhali niletee maji kidogo kwenye jagi ninywe.” Naye alipokuwa akienda kuleta maji alimwita, akamwambia, “tafadhali uniletee na kipande cha mkate mkononi.” Naye akamjibu, “Kama BWANA Mungu wako aishivyo, sina mkate wowote, bali konzi moja ya unga katika chombo na mafuta kidogo kwenye chupa. Tazama, ninaokota kuni mbili ili niende kupika kwa ajili yangu na mwanangu, ili tule, na tusubiri kufa.” Eliya akamwambia, “Usiogope. Nenda ukafanye kama usemavyo. lakini nitengenezee kwanza mimi na uniletee. Ndipo baadaye ujitenegenezee wewe na mwanao. Kwa kuwa BWANA, Mungu wa Israeli anasema 'Lile pipa la unga halitaisha, wala ile chupa ya mafuta kukoma kutoa mafuta, mpaka siku ile BWANA atakapotuma mvua duniani.” Kwa hiyo yule mjane akafanya kama Eliya alivyomwelekeza, yeye, na Eliya, na mwanae wakala kwa siku nyingi. Lile pipa la Unga halikuisha, wala ile chupa ya mafuta haikukoma kutoa mafuta, kama vile neno la BWANA lilivyosema, kupitia kinywa cha Eliya.
- Elisha anawaokoa wana wa mjane kutoka kwa mdai wake kwa mafuta2 Fal 4:1–7
Aya
2 Fal 4:1–7Ndipo mke wa mmoja wa watoto wa manbii alipokuja kwa Elisha akilia, akisema, “Mtumishi wako mme wangu amukufa, na unajua kwamba mtumishi wako alikuwa anamcha Yahwe. Basi aliyemuwia amekuja kuwachukua watoto wangu wawili kwenda kuwa watumwa.” Hivyo Elisha akamwambia, “Nikusaidie nini? Niambie una nini kwenye nyumba yako?” Akamwambia “Mtumishi wako hana kitu kwenye nyumba, isipokuwa chupa ya mafuta.” Kisha Elisha akasema, “Nenda kaazime vyombo kwa majirani zako, vyombo vitupu. Azima vyombo vingi uwezavyo. Kisha lazima uende ndani na kujifungia mlango wewe na watoto wako, na kumiminia mafuta vyombo vyote; vile vilivyojaa ukavitenge.” Basi akamuacha Elisha na kujifungia mlango yeye na watoto wake. Wakavileta vile vyombo kwake, na akivijaza kwa mafuta. Ikawa vyombo vilipojaa, akamwambia mtoto wake, “Niletee chombo kingine.” Ila akamwambia, “Hakuna vyombo vingine.” Kisha mafuta yakakoma kutoka. Ndipo akaja na kumwambia mtu wa Mungu. Akasema, “Nenda kauze mafuta; lipa deni lako, na yatakayobaki waachie watoto wako.”
- Ana, mjane mpaka miaka themanini na minne, hakuondoka hekaluniLk 2:36–38
Aya
Lk 2:36–38Nabii mwanamke aliyeitwa Ana pia alikuwako hekaluni. Yeye alikuwa binti wa Fanueli kutoka kabila la Asheri. Alikuwa na miaka mingi sana. Naye aliishi na mume wake kwa miaka saba baada ya kuoana, na ndipo akawa mjane kwa miaka themanini na minne. Naye hakuwahi kuondoka hekaluni na alikuwa akiendelea kumwabudu Mungu pamoja na kufunga na kuomba, usiku na mchana. Na kwa wakati huo, alikuja pale walipo akaanza kumshukuru Mungu. Aliongea kumhusu mtoto kwa kila mtu ambaye alikuwa akisubiri ukombozi wa Yerusalemu.
- Mjane maskini anatia sarafu mbili ndogo za shaba katika hazinaMk 12:41–44
Aya
Mk 12:41–44Kisha Yesu aliketi chini karibu na sanduku la sadaka ndani ya eneo la hekalu; alikuwa akitazama watu waliokuwa wakitia pesa zao ndani ya sanduku. Watu wengi matajiri waliweka kiasi kikubwa cha pesa. Kisha mwanamke mjane maskini alikuja na kutia vipande viwili, thamani ya senti. Kisha akawaita wanafunzi wake na kuwaambia, “Amini nawaambia, mwanamke huyu mjane ametia kiasi kikubwa zaidi ya wote ambao wameshatoa katika sanduku la sadaka. Kwani wote wametoa kutokana na wingi wa mapato yao. Lakini mwanamke mjane huyu, kutoka katika umaskini wake, katia pesa yote ambayo alipaswa kuitumia kwa maisha yake.”
- Yesu anamfufua mwana pekee wa mjane wa NainiLk 7:11–15
Aya
Lk 7:11–15fulani baada ya haya, ilitokea kuwa Yesu alikuwa anasafiri kwenda mji ulioitwa Naini. wanafunzi wake wakaenda pamoja naye wakiambana na umati wa watu. Alipofika karibu na Lango la jiji tazama, mtu aliyekufa alikuwa amebebwa, na ni mtoto wa pekee kwa mama yake. aliyekuwa mjane, na umati wa wawakilishi kutoka kwenye jiji walikuwa pamoja naye. Alipomwona, Bwana akamsogelea kwa huruma kubwa sana juu yake na akamwambia, “Usilie”. Kisha akasogea mbele akaligusa jeneza ambalo walibebea mwili, na wale waliobeba wakasimama akasema “Kijana nasema amka” Mfu akainuka na kukaa chini na akaanza kuongea. Kisha Yesu akamkabidhi kwa mama yake.
- Wajane wa Wayahudi wa Kiyunani wanasahaulika katika mgao wa chakulaMdo 6:1
Aya
Mdo 6:1Sasa katika siku hizi, wakati idadi ya wanafunzi ilipokuwa inaongezeka, lalamiko la Wayahudi wa Kiyunani lilianza dhidi ya Waebrania, kwa sababu wajane wao walikuwa wanasahaulika katika mgao wa kila siku wa chakula.
- Wajane wanamwonyesha Petro nguo alizoshona DorcasMdo 9:39
Aya
Mdo 9:39Petro akaamka na akaondoka pamoja nao. Alipofika, walimleta katika chumba cha juu. Na wajane wote walisimama karibu naye wakilia, wakimwonyesha koti na nguo ambazo Dorcas aliwashonea wakati akiwa pamoja nao.
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0