Bible Explorer

Gundua › Mada › Wivu na husuda

Maisha ya kila siku

Wivu na husuda katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (26), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Wivu humkasirisha mumeMit 6:34
    Aya
    Mit 6:34Maana vivu humghadhibisha mtu; hatakuwa na huruma wakati wa kulipa kisasi chake.
  • Hasira ni kama gharika, lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu?Mit 27:4
    Aya
    Mit 27:4Kuna ukatili wenye ghadhabu kali na mafuriko ya hasira, lakini ni nani anayeweza kusimama mbele ya wivu?
  • Husuda huozesha mifupaMit 14:30
    Aya
    Mit 14:30Moyo wenye raha ni uzima wa mwili, bali husuda huozesha mifupa.
  • Kazi na mafanikio hutokana na husuda dhidi ya jiraniMhu 4:4
    Aya
    Mhu 4:4Kisha nikaona kwamba kila tendo la kazi na kila kazi ya utashi ikawa wivu wa jirani ya mtu. Huu pia ni mvuke na kujaribu kuchunga upepo.
  • Upendo una nguvu kama mauti, wivu wake hauachi kama kuzimuWim 8:6
    Aya
    Wim 8:6Nieka kama muhuri kwenye moyo wako, kama muhuri kwenye mkono wako, kwa kuwa mapenzi yana nguvu kama mauti. Mapenzi mazito hayana kurudi kama kwenda kuzimu; miale yake yalipuka; ni miale ya moto inayo waka, miale yenye joto kuliko moto wowote.
  • Palipo na wivu, pana machafukoYak 3:16
    Aya
    Yak 3:16Kwa kuwa palipo na wivu na ubinafsi upo, kuna vurugu na kila matendo maovu
  • Kipimo cha Sheria kwa mke anayeshukiwa na mume mwenye wivuHesabu 5:12–31
    Aya
    Hesabu 5:12–31“Nena na wana wa Israel. Uwaambie, 'kama mke wa mtu ataasi na kufanya dhambi dhidi ya mume wake. Halafu mtu mwingine akalala naye. Kwa sababu, hiyo atakuwa amenajisika. Na hata kama mume wake hakuona na hajui, hata kama hakuna mtu aliyemkamta akiwa katika tendo na hakuna mtu wa kushuhudia dhidi yake; hata hivyo ile roho ya wivu itaendele kumjulisha yule mume kuwa mke wake amenajisika. Ingawa, roho ya wivu inaweza kumdanganya yule mwanamume wakati mke wake hajanajisika. Kwa mazingira hayo, yule mwanamume anapaswa kumpeleka mke wake kwa kuhani. Yule mwanamume anapaswa kutoa sadaka ya divai kwa ajili yake. Atapaswa kuleta sehemu ya kumi ya efa ya unga wa shayiri. Asitie mafuta juu yake wala asitie ubani juu yake maana ni sadaka ya unga ya wivu, ni sadaka ya unga ya ukumbusho wa uovu. Ndipo kuhani atasogeza karibu na kumweka mbele ya BWANA. Kuhani atachukua kikombe cha maji matakatifu na atachukua mavumbi ya kwenye masikani. Ataweka yale mavumbi kwenye maji. Kisha kuhani atamweka huyo mwanamke mbele za BWANA na atazifungua nywele kichwani kwa huyo mwanamke. Atamwekea mikononi mwake hiyo sadaka ya unga kwa ajili ya ukumbusho, ambayo ni sadaka ya unga kwa ajili ya wivu. Kuhani atashikilia mikononi mwake maji machungu yanayoweza kuleta laana. Kuhani atamweka huyo mwanamke chini ya kiapo na kumwambia. 'Kama haujafanya uzinzi na mwanaume mwingine, na kama hajakengeuka na kufanya uovu, basi utakuwa huru na maji haya yanayoweza kuleta laana. Lakini kama wewe, mwanamke uliye chini ya mume wako, umekengeuka, na kama umenajisika, na kama mwanamume mwingina amelala nawe, ndipo, (kuhani atamtaka huyo mwanamke aape kiapo kinachoweza kuleta laana kwake, na kwamba ataendelea kumwambia yule mwanamke) 'BWANA atakufanya wewe kuwa laana itakayooneshwa kuwa hivyo kwa watu wako. Hii itatokea pale BWANA atakapoyafanya mapaja yako kuoza na tumbo lako kuvimba. Haya maji ambayo huleta laana yataingia tumboni mwako na kulifanya tumbo lako kuvimba na mapaja yako kuoza,' mwanamke alitakiwa kujibu, 'Ndiyo, hayo yanipate kama mimi ni mwenye hatia.' Naye kuhani ataziandika laana hizi kwenye kitabu, na kisha kuzifuta laana zilizoandikwa kwa maji ya uchungu. Naye kuhani atamwelekeza yule mwanamke kunywa yale maji machungu yaletayo laana. Yale maji yaletayo laana yataingia na kuwa machungu. Kuhani ataitwaa ile sadaka ya unga ya wivu mikononi mwa yule mwanamke. Atailekeza ile sadaka ya unga mbele ya BWANA na kuileta madhabahuni. Kuhani atachukua konzi ya sadaka ya unga mkononi mwake kama sadaka ya kuwakilisha, na kuiteketeza madhabahuni. Ndipo atakapompatia mwanamke yale maji machungu ili ayanywe. Wakati wa kumpa yale maji ili anywe, kama amenajisika kwa sababu alifanya uovu dhidi ya mume wake, ndipo yale maji yaletayo laana yatamwingia na kuwa machungu. Tumbo lake litavimba na paja lake litaoza. Yule mwanamke atalaaniwa kati ya watu wake. Lakini kama yule mwanake hajanajisika na kama ni msafi, basi atakuwa huru. Tena ataweza kubeba uja uzito. Hii ndiyo sheria ya wivu. Ni sheria ya mwanamke anayekengeuka kwa mumewe na kunajisika. Ni sheria ya mwanamume mwenye roho ya wivu kwa mkewe. Atamleta mwanamke mbele ya BWANA, na kuhani atamfanyia huyo mwanamke kila kitu ambacho sheria ya wivu inamtaka kufanya. Yule mwanamume atakuwa hana hatia kwa kumleta mke wake kwa kuhani. Na yule mwanmke atauchukua uovu wake.”

Mifano

  • Kaini, akikasirika kwamba sadaka ya Habili imekubaliwa, anamuuaMwa 4:4–8
    Aya
    Mwa 4:4–8Habili pia, alileta sehemu ya wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona. Yahwe akamkubali Habili pamoja na sadaka yake, lakini Kaini pamoja na sadaka yake Mungu hakuikubali. Kwa hiyo Kaini alikasirika sana, na uso wake ukakunjamana. Yahwe akamwambia Kaini, “ kwa nini umekasirika na kwa nini uso wako umekunjamana? Kama ukifanya vema, je hutapata kibali? lakini kama hutafanya lilio jema, dhambi iko inakuotea mlangoni na inatamani kukutawala, lakini inakupasa uishinde. Kaini akamwambia Habili ndugu yake. Hata wakati walipokuwa shambani, Kaini aliinuka dhidi ya Habili ndugu yake na akamuua. (Katika tafsiri za kale zinasema, Kaini alimwambia Habili ndugu yake, “ twende mashambani.” Na wakati walipokuwa shambani, Kaini alimuinukia Habili ndugu yake na kumuua).
  • Hajiri mwenye mimba anamdharau Sarai, naye Sarai anamtesaMwa 16:4–6
    Aya
    Mwa 16:4–6Kwa hiyo akawa na mahusiano na Hajiri, na akabeba mimba. Na alipoona kuwa amebeba mimba, akamdharau bibi yake. Kisha Sarai akamwambia Abram, “Jambo hili baya kwangu ni kwa sababu yako. Nilimtoa mtumishi wangu wa kike katika kumbatio lako. Na alipoona kuwa amebeba mimba, nilidharaulika machoni pake. Na sasa acha Yahwe aamuwe kati yangu na wewe.” Lakini Abram akamwambia Sarai, “Tazama, hapa, mtumishi wako yuko katika uwezo wako, fanya unachofikiri ni kizuri sana kwake.” Kwa hiyo Sarai akakabiliana naye kwa ukatili, na akatoroka.
  • Wafilisti wanamwonea wivu Isaka kwa sababu ya mifugo yakeMwa 26:14
    Aya
    Mwa 26:14Alikuwa na kondoo na ngombe na familia kubwa. Wafilisiti wakamwonea wivu.
  • Raheli anamwonea wivu Lea: “Nipe watoto, la sivyo nitakufa!”Mwa 30:1
    Aya
    Mwa 30:1Raheli alipoona kwamba hamzalii Yakobo watoto, Raheli akamwonea wivu dada yake. Akamwambia Yakobo, “Nipe watoto, sivyo nitakufa.”
  • Ndugu za Yusufu wanamwonea wivu na kumuuzaMwa 37:4, Mwa 37:11, Mwa 37:18–28
    Aya
    Mwa 37:4Ndugu zake wakaona kwamba baba yao alimpenda sana kuliko ndugu zake wote. Wakamchukia na hawakuongea naye vema.
    Mwa 37:11Ndugu zake wakamwonea wivu, lakini baba yake akaliwema jambo hilo moyoni.
    Mwa 37:18–28Wakamwona kutokea mbali, na kabla hajawakaribia, wakapanga njama ya kumwua. Ndugu zake wakaambiana wao kwa wao, “Tazama, mwotaji anakaribia. Njoni sasa, na tumwue na kumtupa katika mojawapo ya mashimo haya. Nasi tutasema, 'Mnyama mkali amemrarua.' Nasi tutaona ndoto zake zitakuwaje.” Rubeni alilisikia hilo na kumwokoa kutoka katika mikono yao. Alisema, “Tusiuondoe uhai wake.” Rubeni aliwambia, “Msimwage damu. Mtupeni katika shimo hili lililopo nyikani, lakini msiweke mikono yenu juu yake” - ili kwamba aweze kumwokoa katika mikono yao na kumrudisha kwa baba yake. Ikawa Yusufu alipowafikia ndugu zake, walimvua vazi lake zuri. Wakamchukua na kumtupa shimoni. Shimo lilikuwa tupu bila maji. Wakakaa chini kula mkate. Walipoinua macho yao na kuangalia, na, tazama, msafara wa Waishmaeli ulikuwa ukija kutoka Gileadi, pamoja na ngamia wao waliochukua viungo, malhamu na manemane. Walikuwa wakisafiri kuvichukua kuelekea Misri. Yuda akawambia ndugu zake, “Ni faida gani kama tutamwua ndugu yetu na kufunika damu yake? Haya, na tumwuze kwa Waishmaeli na wala tusiweke mikono yetu juu yake. Kwani yeye ni ndugu yetu, nyama yetu.” Ndugu zake wakamsikiliza. Wafanyabiashara wa Kimidiani wakapita. Ndugu zake wakamwinua na kumtoa Yusufu shimoni. Wakamwuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande ishirini vya fedha. Waishmaeli wakamchukua Yusufu mpaka Misri.
  • Musa kwa Yoshua: “Je, unaona wivu kwa ajili yangu?”Hesabu 11:28–29
    Aya
    Hesabu 11:28–29Joshua mwana wa Nuni, msaidizi wa Musa, ambaye ni miongoni mwa wale aliowachagua akamwambia Musa, “Bwana wangu Musa, wazuie.” Musa akamwambia, “una wivu kwa niaba yangu? Natamani kama watu wote wa BWANA wangekuwa manabii na kwamba angeweka Roho yake juu yao wote!”
  • Miriamu na Haruni: “Je, Yahwe amesema kupitia Musa peke yake?”Hesabu 12:1–2
    Aya
    Hesabu 12:1–2Kisha Miriamu na Haruni wakasema kinyume na Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi ambaye alikuwa amemwoa. Walisema. “ Hivi BWANA amesema na Musa tu? Ni kweli hajawahi kusema nasi pia? Sasa BWANA akasikia kile walichokuwa wanaongea. Sasa
  • Watu wa Efraimu wanawalaumu Gideoni na Yeftha kwa kutowaitaAmu 8:1, Amu 12:1
    Aya
    Amu 8:1Watu wa Efraimu wakamwambia Gideoni, “Ni nini hiki umetutenda? Haukuita wakati ulipokwenda kupigana na Midiani.” Wakamwambia kwa nguvu.
    Amu 12:1Watu wa Efraimu walitoka pamoja; nao wakapitia Zafoni, wakamwambia Yeftha, Kwa nini umetangulia kupigana na wana wa Amoni, wala hukutuita twende pamoja nawe? Tutachoma nyumba yako.
  • Sauli anachukizwa na wimbo “Daudi ameua makumi elfu yake”1 Sam 18:7–9
    Aya
    1 Sam 18:7–9Hao wanawake waliimba kwa kupokezana huku wakicheza; Wakiimba: “Sauli ameua maelfu yake, Na Daudi ameua makumi elfu yake.” Sauli alikasirika sana, na wimbo huu haukumpendeza. Naye akasema, “Wamemsifia Daudi juu ya makumi elfu, lakini wamenisifia melfu tu mimi! Atapata kitu gani zaidi isipokuwa ufalme? Kuanzia siku hiyo na kuendelea, Sauli alimuangalia Daudi kwa mashaka.
  • Yoabu anamuua Abneri, ambaye Daudi alikuwa amemuaga kwa amani2 Sam 3:24–27
    Aya
    2 Sam 3:24–27Kisha Yoabu akaja kwa mfalme na kusema, “Umefanya nini? Tazama, Abneri alikuja kwako! Kwa nini umemruhusu kuondoka, naye amenda? Haujui kwamba Abneri mwana wa Neri alikuja kukudanganya na kupeleleza hali yako na kuangalia kila unalofanya?” Yoabu alipoondoka kwa Daudi, alituma wajumbe kumfuatia Abneri, nao wakamrudisha kutoka katika kisima cha Sirah, lakini Daudi hakulijua hili. Abneri aliporudi Hebroni, Yoabu alimchukua kando kati ya lango ili aongee naye faraghani. Hapohapo Yoabu alimchoka tumboni na kumuua. Hivyo, akalipa kisasi cha damu ya Asaheli nduguye.
  • Israeli na Yuda wanagombana ni nani aliyemrudisha mfalme2 Sam 19:41–43
    Aya
    2 Sam 19:41–43Mara watu wa Israeli wote wakaanza kuja kwa mfalme na kumwambia, “Kwa nini ndugu zetu, watu wa Yuda, wamemwiba na kumleta mfalme na familia yake juu ya Yordani na watu wote wa Daudi pamoja naye? Hivyo watu wa Yuda wakawajibu watu wa Israeli, “Ni kwa kuwa mfalme anahusiana nasi kwa karibu zaidi. Kwa nini basi mkasirike juu ya hili? Je sisi tumekula chochote ambacho mfalme amekitoa? Je ametupa zawadi yoyote? Watu wa Israeli wakawajibu watu wa Yuda, Sisi tuna kabila kumi zaidi kwa mfalme hivyo tuna sehemu kubwa zaidi kwa Daudi kuliko ninyi. Kwa nini basi mlitudharau? Je hatukuwa wa kwanza kupendekeza kumrudisha mfalme wetu? Lakini maneno ya watu wa Yuda hata yakawa makali kuliko maneno ya watu wa Israeli.
  • Kaka mkubwa wa mwana mpotevu anakataa kuingiaLk 15:25–30
    Aya
    Lk 15:25–30Basi yule mwanae mkubwa alikuwako shamba. Alipokuwa akija na kuikaribia nyumba alisikia sauti ya nyimbo na michezo. Akaita mtumishi mmoja akamuuliza mambo haya maana yake nini? Mtumishi akamwambia mdogo wako amekuja na baba yako amemchinjia ndama aliyenona kwa sababu amerudi salama.' Mwana mkubwa akakasirika akakataa kuingia ndani na babaye alitoka nje kumsihi. Ila akamjibu babayake akisema, 'Tazama mimi nimekutumikia miaka mingi, wala sijakosa amri yako, lakini hujanipa mwana mbuzi, ili niweze kusherehekea na rafiki zangu. Lakini alipokuja huyu mwana wako aliyetapanya mali yako yote pamoja na makahaba umemchinjia ndama alienona.
  • Pilato alijua kwamba walimtoa Yesu kwa sababu ya husudaMt 27:18
    Aya
    Mt 27:18Kwa sababu alijua kwamba wamekwisha kumkamata kwa sababu ya chuki.
  • Kuhani mkuu na Masadukayo wanajawa na wivuMdo 5:17
    Aya
    Mdo 5:17Lakini kuhani mkuu aliinuka, na wote waliokuwa pamoja naye (ambao ni wa dhehebu la masadukayo); na walijawa na wivu
  • Umati wenye wivu unampinga Paulo huko Antiokia na ThesalonikeMdo 13:45, Mdo 17:5
    Aya
    Mdo 13:45Wayahudi walipoona makutano, walijawa na wivu na kuongea maneno yaliyopinga vitu vilivyosemwa na Paulo na walimtukana.
    Mdo 17:5Lakini baadhi ya Wayahudi wasioamini, waliojawa na wivu, walienda sokoni na kuwachukuwa baadhi ya watu waovu, wakakusanya umati wa watu pamoja, na kusababisha ghasia mjini, kisha wakaivamia nyumba ya Jason, wakitaka kuwakamata Paulo na Sila ilikuwaleta mbele za watu.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0