Bible Explorer

Gundua › Mada › Biashara na wafanyabiashara

Maisha ya kila siku

Biashara na wafanyabiashara katika Biblia

Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (37), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.

  • Abraham anapima fedha “kwa kipimo cha wafanyabiashara”Mwa 23:16
    Aya
    Mwa 23:16Abraham akamsikiliza Efroni na akampimia Efroni kiwango cha fedha alizosema mbele ya wana wa Helthi wakisikiliza, shekeli mia nne za fedha, kwa mujibu wa viwango vya vipimo vya kibiashara.
  • Msafara wa Waishmaeli unabeba manukato, zeri na manemane kwenda MisriMwa 37:25
    Aya
    Mwa 37:25Wakakaa chini kula mkate. Walipoinua macho yao na kuangalia, na, tazama, msafara wa Waishmaeli ulikuwa ukija kutoka Gileadi, pamoja na ngamia wao waliochukua viungo, malhamu na manemane. Walikuwa wakisafiri kuvichukua kuelekea Misri.
  • Yusufu anauzwa kwa wafanyabiashara kwa shekeli ishirini za fedhaMwa 37:28, Mwa 37:36
    Aya
    Mwa 37:28Wafanyabiashara wa Kimidiani wakapita. Ndugu zake wakamwinua na kumtoa Yusufu shimoni. Wakamwuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande ishirini vya fedha. Waishmaeli wakamchukua Yusufu mpaka Misri.
    Mwa 37:36Wamidiani wakamwuza huko Misri kwa Potifa, afisa wa Farao, kepteni wa walinzi.
  • Hiramu anatuma mwerezi na msonobari; Sulemani analipa kwa ngano na mafuta ya zeituni1 Fal 5:8–11, 2 Nya 2:15
    Aya
    1 Fal 5:8–11Hiramu akatuma neno kwa Sulemani, akisema, “Nimeupata ujumbe ule ulionitumia. Nitatoa miti yote ya mierezi na miti ya miberoshi ambayo unahitaji. Watumishi wangu wataileta miti kutoka Lebanoni hadi baharini, nami nitaiendesha baharini mpaka mahali utakaponielekeza. Nitaigawa pale, nawe utaichukua. Utafanya kile ninachohitaji kwa kuwapa chakula watumishi wangu.” Kwa hiyo Hiramu akampa Sulemani miti yote ya mierezi na miti ya miberoshi ambayo alihitaji. Sulemani akampa Hiramu kori ishirini elfu za ngano kwa ajili ya chakula cha watumishi wake na kori ishirii za mafuta safi. Sulemani akavitoa hivi kwa Hiramu mwaka baad ya mwaka.
    2 Nya 2:15Sasa, ngano na shayiri, mafuta na mvinyo, ambayo bwana wangu aliisema, na apeleke sasa vitu hivi kwa watumishi wake.
  • Merikebu za Sulemani zinaleta talanta 420 za dhahabu kutoka Ofiri1 Fal 9:26–28
    Aya
    1 Fal 9:26–28Tena Sulemani alitengeneza merikebu kule Ezioni Geberi, ambayo iko karibu na Elathi katika ufukwe wa bahari ya shamu, katika nchi ya Edomu. Hiramu alituma watumishi kwenye merikebu ya Sulemani, wanamaji wanaoijua bahari, pamoja na watumishi wake Sulemani. Walikwenda kwa Ofri pamoja na watumishi wa Sulemani. Kutoka huko walileta takribani tani 14. 5 za dhahabu kwa Sulemani.
  • Sulemani anapokea mapato kutoka kwa wafanyabiashara na wachuuzi1 Fal 10:15, 2 Nya 9:14
    Aya
    1 Fal 10:15zaidi ya dhahabu ambazo wafanya biashara na wachuuzi walileta. Wafame wote wa Uarabuni na maliwali wa nchi pia walileta dhahabu na fedha kwa Sulemani.
    2 Nya 9:14nje na dhahabu ambayo waliileta wachukuzi na wafanya biashara. Walme wote wa Arabuni na maliwali katika nchi pia wakamletea Selemanai dhahabu na fedha.
  • Naomi anauza shamba lililokuwa la ElimelekiRut 4:3
    Aya
    Rut 4:3Boazi alimwambia yule jamaa wa karibu, “Naomi aliyerudi kutoka mji wa Moabu, anauza sehemu ya aridhi ambayo ilikuwa ni miliki ya kaka yetu Elimeleki.
  • Wafua dhahabu na wafanyabiashara wanakarabati sehemu ya ukuta wa YerusalemuNeh 3:32
    Aya
    Neh 3:32Wafanyabiashara wa dhahabu na wafanyabiashara walijenga kati ya chumba cha juu cha kona na Lango la Kondoo.
  • Watu wa Tiro wanauza samaki Yerusalemu siku ya SabatoNeh 13:16
    Aya
    Neh 13:16Watu kutoka Tiro waliokaa Yerusalemu walileta samaki na kila aina ya bidhaa, na wakawauza siku ya Sabato kwa watu wa Yuda na katika mji!
  • Nehemia anafunga malango; wafanyabiashara wanalala nje ya mjiNeh 13:19–20
    Aya
    Neh 13:19–20Mara ilipokuwa giza kwenye milango ya Yerusalemu kabla ya Sabato, niliamuru milango ifungwe na kwamba haifai kufunguliwa hadi baada ya Sabato. Niliwaweka baadhi ya watumishi wangu kwenye malango ili mzigo wowote usiweze kuletwa siku ya Sabato. Wafanyabiashara na wauzaji wa kila aina ya bidhaa walikimbia nje ya Yerusalemu mara moja au mbili.
  • Mke hodari ananunua shamba na kuuza mavazi ya kitaniMit 31:16, Mit 31:24
    Aya
    Mit 31:16Hulifikiria shamba na kulinunua, kwa tunda la mikono yake hupanda shamba la mizabibu.
    Mit 31:24Hutengeneza mavazi ya kitani na kuyauza, na naleta mishipi kwa wafanyabiashara.
  • Meli ya Paulo inashusha mizigo yake huko TiroMdo 21:2–3
    Aya
    Mdo 21:2–3Tulipopata meli inayovuka kwenda Foinike, tulipanda tukasafiri. Tulipofika mbele ya kisiwa cha Kipro, tukaiacha upande wa kushoto, tukasafiri hadi Siria, tukaweka nanga katika mji wa Tiro, kwa sababu huko ndiko meli ilikuwa ipakuliwe shehena yake.
  • Lidia, muuzaji wa nguo za zambarau kutoka TiatiraMdo 16:14
    Aya
    Mdo 16:14Mwanamke mmoja aitwaye Lidia, muuzaji wa zambarau, kutoka katika mji wa Tiatira, mwenye kumwabudu Mungu, alitusikiliza. Bwana alimfungua moyo wake na kuweka maanani maneno yaliyosemwa na Paulo.
  • Wabadilisha fedha na wauzaji wa njiwa katika nyua za hekaluYn 2:14
    Aya
    Yn 2:14Akawakuta wauzaji wa ng'ombe, kondoo, na njiwa ndani ya Hekalu. Pia na wabadilisha fedha walikuwa wameketi ndani ya Hekalu.
  • Mfanyabiashara anauza vyote alivyo navyo kwa lulu moja ya thamani (mfano)Mt 13:45–46
    Aya
    Mt 13:45–46Tena, ufalme wa mbinguni ni kama mtu anayefanya biashara atafutaye lulu yenye thamani. Wakati alipoiona ile yenye thamani, alienda akauza kila kitu alichokuwa nacho na akainunua.
  • Watumishi wanapewa fedha ya kufanyia biashara (mfano)Lk 19:13, Mt 25:16
    Aya
    Lk 19:13Aliwaita watumishi wake kumi, akawapa mafungu kumi, akawaambia, 'fanyeni biashara mpaka nitakaporudi.'
    Mt 25:16Mapema yule aliyepokea talanta tano alienda kuziwekeza, na kuzalisha talanta zingine tano.
  • “Kesho tutakwenda mji huu au ule na kufanya biashara”Yak 4:13
    Aya
    Yak 4:13Sikilizeni, ninyi msemao, “Leo au kesho tutakwenda katika mji huu, na kukaa mwaka huko, na kufanya biashara, na kutengeneza faida.”

Biashara na Tiro (Ezekieli 27)

  • Tarshishi: fedha, chuma, bati na risasiEze 27:12
    Aya
    Eze 27:12Tarshishi alikuwa mdau wa biashara pamoja nawe kwa sababu ya wingi wa utajiri wako wa kuuza mizigo: fedha, chuma, bati, na risasi. Walinunua na kuuza bidhaa za biashara!
  • Yavani, Tubali na Mesheki: watumwa na vyombo vya shabaEze 27:13
    Aya
    Eze 27:13Yavani, Tubali, na Mesheki-waliwauza watumwa na katika vitu kutengeneza shaba. Walibeba bidhaa zako.
  • Beth Togarma: farasi, farasi wa vita na nyumbuEze 27:14
    Aya
    Eze 27:14Beth Togarma waliandaa farasi, farasi dume, na nyumbu kama kama bidhaa zako.
  • Dedani: matandiko ya tandiko; visiwa: pembe za ndovu na mpingoEze 27:15, Eze 27:20
    Aya
    Eze 27:15Watu wa Dedani walikuwa wafanya biashara wako kwenye pwani nyingi. Bidhaa zilikuwa mkononi mwako; walikutumia pembe, pembe za ndovu, na mpingo kama ushuru!
    Eze 27:20Dedani alikuwa mchuuzi katika nguo nzuri za kutandika.
  • Aramu: feruzi, zambarau, nakshi, kitani safi, matumbawe na yakutiEze 27:16
    Aya
    Eze 27:16Shamu alikuwa mchuuzi katika bidhaa zako nyingi; waliandaa zumaridi, zambarau, nguo zenye rangi mbali mbali, kitambaa kizuri, lulu, na kito chekundu cha thamani kama bidhaa zako.
  • Yuda na Israeli: ngano, asali, mafuta na zeriEze 27:17
    Aya
    Eze 27:17Yuda na nchi ya Israeli walikuwa wafanyabiashara pamoja nawe. Waliandaa ngano kutoka Minithi, keki, asali, mafuta, na lihamu kama bidhaa zako.
  • Dameski: divai ya Helboni na sufuEze 27:18
    Aya
    Eze 27:18Dameski alikuwa mfanya biashara wa bidhaa zako zote, za utajiri mkubwa mno, na ya divai ya Helboni na sufu ya Zahari.
  • Arabia na Kedari: wana kondoo, kondoo dume na mbuziEze 27:21
    Aya
    Eze 27:21Arabuni na wakuu wote wa Kedari walikuwa wafanyabiashara pamoja nawe; walikuandalia wanakondoo, kondoo dume na mbuzi.
  • Sheba na Raama: manukato, mawe ya thamani na dhahabuEze 27:22
    Aya
    Eze 27:22Wafanya biashara wa Sheba na Raama walikuja kukuuzia kila aina ya viungo vizuri katika vito vyote vya thamani; waliuza dhahabu kwa ajili ya bidhaa.

Katika Sheria

  • Mizani, mawe ya kupimia na vipimo vya hakiLaw 19:35–36, Kum 25:13–15
    Aya
    Law 19:35–36Unapopima urefu, uzito, au wingi usitumie vipimo vya udanganyifu. Tumia mizani iliyo halali, mawe ya kupimia uzito yaliyo halali, efa halali, hini iliyo halali. Mimi ndimi Yahweh Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya utumwa ya Misri.
    Kum 25:13–15Haupaswi kuwa na mizani ya uzito tofauti katika mfuko wako, mkubwa na mdogo. Hautakiwi kuwa na vipimo tofauti ndani ya nyumba yako, vikubwa na vidogo. Unatakiwa kuwa na uzito kamili na wa haki; unatakiwa kuwa na vipimo kamili na vya haki, ili siku zako ziwe ndefu katika nchi ambayo Yahwe Mungu wako anakupatia.
  • Mnunuzi na muuzaji wasidhulumianeLaw 25:14
    Aya
    Law 25:14Iwapo utauza ardhi yoyote ya jirani yako au kununua ardhi yake, ni shrti msipunjane au kutendeana kwa hila.

Misemo

  • “Haifai kitu!” asema mnunuzi, kisha ajivuna akiondokaMit 20:14
    Aya
    Mit 20:14“Mbaya! Mbaya!” anasema mnunuzi, lakini akiondoka anajisifu.
  • Wafanyabiashara wanaongoja Sabato iishe ili wauze nafakaAmo 8:5
    Aya
    Amo 8:5wakisema, “Wakati mwezi mpya utakapoisha, hivyo tunaweza kuuza mazao tena? Wakati siku ya Sabato itakapoisha, ili kwamba tuuze ngano? Tutafanya kipimo kidogo na kuongeza bei, tukidanganya kwa mizani za udanganyifu.

Vyanzo

Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0