Maisha ya kila siku
Nyumba katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (38), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
- Nyumba za mawe, zenye boriti za mwerezi na kombamoyo za msonobariAmo 5:11, Wim 1:17
Aya
Amo 5:11Kwa sababu mnamkanyaga chini maskini na kuchukua sehemu ya ngano kutoka kwake- ingawa mmejenga nyumba za mawe yaliyochongwa, hamtaishi kwenye nyumba hizo. Mmependezwa na mashamba ya mizabibu, lakini hamtakunywa mvinyo wake.
Wim 1:17Nguzo za nyumba yetu ni za matawi ya mierezi, na dari letu ni la matawi ya miberoshi.
- Kuta zilipakwa chokaaLaw 14:42, Dan 5:5
Aya
Law 14:42Lazima wayachukue mawe mengine na kuyaweka katika sehemu ya mawe yaliyoondolewa, na lazima watumie udongo mpya kupigia lipu nyumba.
Dan 5:5Kwa wakati huo huo vidole vya mkono wa mtu vilionekana mbele ya kinara cha taa na kuandika katika ukuta uliopigwa lipu katika ikulu ya mfalme. Mfalme aliweza kuona sehemu ya mkono ulipokuwa unaandika.
- Misingi ya mawe makubwa ya thamani, dhiraa kumi na nane kwa urefu1 Fal 7:9–10
Aya
1 Fal 7:9–10Majengo haya yalipmbwa kwa vitu vya thamaini, mawe ya thamani, yaliyochongwa na kukatwa kwa msimeno kufuata vipimo sahihi na kulainishwa pande zote. Mawe ya namna hii ndiyo yale yaliyotumika kuanzia kwenye msingi hadi juu, pia na nje hadi kwenye baraza. Msingi ulijengwa kwa mawe makubwa sana na ya thamani yenye urefu wa mita 3. 7 na mengine mita 4. 8.
- Sulemani anachukua miaka kumi na mitatu kujenga jumba lake1 Fal 7:1
Aya
1 Fal 7:1Ilimchukua Sulemani miaka kumi na tatu kujenga ikulu yake.
- Daudi anaishi katika nyumba ya mwerezi2 Sam 7:2
Aya
2 Sam 7:2mfalme akamwambia nabii Nathani, “Tazama, mimi ninaishi katika nyumba ya mierezi, lakini sanduku la Mungu lipo hemani.
- Nyumba zilizopambwa kwa mbaoHag 1:4
Aya
Hag 1:4“Je ni wakati kwenu wenyewe kuishi katika nyumba zilizokamilika, na wakati nyumba hii inaharibika?
- Nyumba ya Rahabu imejengwa ndani ya ukuta wa mjiYos 2:15
Aya
Yos 2:15hivyo aliwashusha chini kwa kupitia dirishani kwa kutumia kamba. Nyumba ambayo alikuwa anaishi ilijengwa katika ukuta wa mji.
- Makanisa yalikutana katika nyumba za wauminiMdo 12:12, Rum 16:5, Kol 4:15, Flm 1:2
Aya
Mdo 12:12Baada ya kujua haya, akaja kwenye nyumba ya Mariamu mama yake Yohana ambaye ni Marko; Wakristo wengi walikusanyika wakiomba.
Rum 16:5Lisalimie kanisa ambalo liko nyumbani kwao. Msalimie Epanieto mpendwa wangu, ambaye ni mzaliwa wa kwanza wa Kristo katika Asia.
Kol 4:15Wasalimu ndugu zangu walioko Laodekia, na Nimfa, na kanisa lile lililoko nyumbani kwake.
Flm 1:2na kwa Afia dada yetu, na kwa Arkipas askari mwenzetu, na kwa kanisa lile linalokutana nyumbani kwako.
Mapaa
- Rahabu anawaficha wapelelezi chini ya kitani kilichotandazwa juu ya paa lakeYos 2:6
Aya
Yos 2:6Lakini yeye aliwapandisha juu darini na kuwaficha kwa mabua ya kitani ambayo alikuwa ameyalaza darini.
- Samweli anaongea na Sauli juu ya paa, na Sauli analala huko1 Sam 9:25–26
Aya
1 Sam 9:25–26Walipokuwa wamekwisha shuka chini kutoka sehemu ya juu na kuingia mjini, Samweli akazungumza na Sauli darini. Na kulipopambazuka, Samweli alimwita Sauli darini na kusema, “Amka, kusudi nikusindikize uende zako,” Hivyo Sauli aliamka, na wote wawili, yeye na Samweli walitoka kwenda mtaani.
- Daudi anatembea jioni juu ya paa la jumba la kifalme2 Sam 11:2
Aya
2 Sam 11:2Hivyo ikawa siku moja wakati wa jioni Daudi akaamka kutoka kitandani na akatembea katika dari la kasri. Akiwa pale akamwona mwanamke aliyekuwa akioga, mwanamke yule alikuwa mzuri sana kwa mwonekano.
- Vibanda vinajengwa juu ya mapaa na uani kwa ajili ya sikukuuNeh 8:16
Aya
Neh 8:16Basi watu wakatoka na kuleta matawi, wakajifanyia mahema, kila mmoja juu ya paa zao, katika ua zao, katika mahakama za nyumba ya Mungu, mahali pa wazi pa lango la Maji, na katika mraba wa lango la Efraimu.
- Watu wapatao elfu tatu juu ya paa la hekalu la WafilistiAmu 16:27
Aya
Amu 16:27Sasa nyumba ilikuwa imejaa wanaume na wanawake. Watawala wote wa Wafilisti walikuwa huko. Juu ya paa kulikuwa na wanaume na wanawake elfu tatu, ambao walikuwa wakiangalia wakati Samsoni alipokuwa akiwafurahisha.
- Marafiki wanatoboa paa na kumshusha mtu aliyepooza kupitia vigaeMk 2:4, Lk 5:19
Aya
Mk 2:4Wakati waliposhindwa kumkaribia kwa sababu ya umati wa watu, waliondoa paa juu ya mahali pale alipokuwa. Na walipokuwa wamekwishatoboa tundu, walishusha kitanda ambacho mtu aliyepooza alikuwa amelala.
Lk 5:19Hawakupata njia ya kumwingiza ndani kwa sababu ya umati, hivyo walipanda juu ya paa la nyumba na kumshusha yule mtu chini kupitia kwenye vigae, juu mkeka wake katikati ya watu, mbele kabisa ya Yesu.
- Minong’ono ya vyumba vya ndani inatangazwa juu ya mapaaLk 12:3
Aya
Lk 12:3Na lolote mlilolisema katika giza, litasikiwa katika mwanga. Na yoyote mliyoyasema kwenye sikio ndani ya vyumba vyenu vya ndani vilivyofungwa yatatangazwa juu ya paa la nyumba.
Vyumba, milango na madirisha
- Mfalme Egloni anakaa peke yake katika chumba chake cha juu chenye ubaridiAmu 3:20
Aya
Amu 3:20Ehudi akaja kwake. Mfalme alikuwa amekaa peke yake, peke yake katika chumba cha juu cha baridi. Ehudi akasema, 'Nina ujumbe kutoka kwa Mungu kwa ajili yeko.' Mfalme akasimama kutoka katika kiti chake.
- Eliya anakaa katika chumba cha juu cha nyumba ya mjane1 Fal 17:19
Aya
1 Fal 17:19Naye Eliya akamjibu, “Nipe hapa mwanao.” Akambeba mtoto mikononi mwake na akampeleka mpaka chumbani alimokuwa akikaa, akamlaza yule mtoto kitanadani pake mwenyewe.
- Chumba kikubwa cha juu, kilichotandikwa na tayari kwa PasakaMk 14:14–15
Aya
Mk 14:14–15Nyumba atakayoingia, mfuateni na mmwambie mwenye nyumba hiyo, 'Mwalimu asema, “Kiko wapi chumba cha wageni mahali nitakapokula Pasaka na wanafunzi wangu?” Atawaonesha chumba cha juu kikubwa chenye samani ambacho kiko tayari. Fanyeni maandalizi kwa ajili yetu pale.”
- Yusufu anaingia chumbani kwake kuliaMwa 43:30
Aya
Mwa 43:30Yusufu akaharakisha kutoka chumbani, kwani aliguswa sana kuhusu nduguye. Akatafuta mahali pa kulia. Akaingia chumbani mwake na kulia umo.
- Ahazia anaanguka kupitia kimia cha chumba chake cha juu2 Fal 1:2
Aya
2 Fal 1:2Baada hapo Ahazi akaanguka chini ya dirisha lenye waya zinazikinzana kwenye chumba chake juu katika Samaria, na alikuwa amejeruhiwa. Kwa hiyo alituma wajumbe na kuwaambia, “Nendeni, muulizeni Baal Zebubu, mungu wa Ekroni, kama nitapona hili jeraha.”
- Mama yake Sisera anachungulia kupitia kimia cha dirishaAmu 5:28
Aya
Amu 5:28Aliangalia dirishani - mama yake Sisera aliangalia kupitia kamba na akasema kwa huzuni, 'Kwa nini gari lakelimechelewa kuja? Kwa nini viboko vya farasi vinavyovuta magari yake vimechelewa? '
- Eutiko anasinzia dirishani na kuanguka kutoka ghorofa ya tatuMdo 20:9
Aya
Mdo 20:9Katika dirisha alikuwa amekaa kijana mmoja jina lake Utiko, ambaye alielemewa na usingizi mzito. Hata Paulo alipokuwa akihutubu kwa muda mrefu, kijana huyu, akiwa amelala, akaanguka chini kutoka ghorofa ya tatu na aliokotwa akiwa amekufa.
Katika Sheria
- Nyumba mpya inahitaji ukingo kuzunguka paa lakeKum 22:8
Aya
Kum 22:8Ujengapo nyumba mpya, basi unapaswa kujenga kitalu kwa ajili ya paa yako ili usilete damu juu ya nyumba yako mtu akianguka kutoka pale.
- Maneno ya Sheria yaliandikwa kwenye miimo ya milango na malangoniKum 6:9
Aya
Kum 6:9Utaziandika kwenye miimo ya mlango ya nyumba yako na kwenye malango.
- Ukungu ndani ya nyumba: mawe hubadilishwa, kuta hukwanguliwa na kupakwa upyaLaw 14:40–45
Aya
Law 14:40–45Kama hivyo, ndipo kuhani ataamuru kwamba wayaondoe mawe ambayo ukungu umepatikana na yatupwe katika sehemu najisi nje ya mji. Yeye atataka kuta zote za ndani ya nyumba zikwanguliwe, na lazima achukue vitu vilivyochafuliwa na hivyo vilivyokwanguliwa nje ya mji na kuvitupa kwenye eneo lisilosafi. Lazima wayachukue mawe mengine na kuyaweka katika sehemu ya mawe yaliyoondolewa, na lazima watumie udongo mpya kupigia lipu nyumba. Kama ukungu unakuja tena na unaingia katika nyumba ambayo mawe yameondolewa na kuta zimekwanguliwa na kupigwa lipu upya, ndipo kuhani lazima aje aingie ndani na kuchunguza nyumba kuona kama ukungu umeenea ndani ya nyumba. Kama hivyo, huo ni ukungu mbaya, na nyumba ni najisi. Nyumba hiyo lazima iangushwe chini. Hayo mawe, mbao, na lipu yote ndani ya nyumba lazima vibebwe kupelekwa nje ya mji kwenye sehemu najisi.
- Nyumba iliyouzwa katika mji wenye ukuta ingeweza kukombolewa ndani ya mwakaLaw 25:29–30
Aya
Law 25:29–30Ikiwa mtu anauza nyumba iliyo kwenye mji uliozungushiwa ukuta, naye anaweza kuinunua tena ndani ya mwaka baada ya kuuzwa. kwa kuwa, kwa mwaka mzima atakuwa na haki ya ukombozi. Kama nyumba hiyo haitakombolewa kabla ya mwaka mzima, ndipo hiyo nyumba iliyoko kwenye mji uliozungushiwa ukuta itakuwa mali ya kudumu ya yule aliyeinunua, katika vizazi vyote vya uzao wake. Nyumba hiyo haitakuwa ya kurejeshwa katika mwaka wa Yubile.
- Nyumba za vijiji visivyo na ukuta hurudi kwa wenyewe katika YubileLaw 25:31
Aya
Law 25:31Lakini nyumba za vijijini zisizokuwa na ukuta kuzizunguuka, zitahesabiwa kuwa shamba la nchi. Zaweza kukombolewa, na ni lazima zirejeshwe katika mwaka wa Yubile.
- Mtu mwenye nyumba mpya ambayo bado hajaiweka wakfu anarudishwa nyumbani kutoka vitaniKum 20:5
Aya
Kum 20:5Maakida wanapaswa kuzungumza na watu na kusema, “Ni mtu yupi aliyejenga nyumba mpya na hajaiweka wakfu? Acha aende na arudi nyumbani kwake, ili kwamba asife vitani na mtu mwingine aiweke wakfu.
Misemo
- Mtu mwenye hekima hujenga nyumba yake juu ya mwamba (mfano)Mt 7:24–27, Lk 6:48
Aya
Mt 7:24–27Kwa hiyo, kila mmoja asikiaye maneno yangu na kutii atafanana na mtu mwenye hekima aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba. Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, na upepo ukaja na ukaipiga nyumba hiyo, lakini haikuweza kuanguka chini, kwa kuwa ilikuwa imejengwa juu ya mwamba. Lakini kila mtu anayesikia neno langu na asilitii, atafananishwa na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga. Mvua ikaja, mafuriko yakaja, na upepo ukaja na kuipiga nyumba hiyo. Na ikaanguka, na uharibifu wake ukakamilika.”
Lk 6:48Anafanana na mtu ajengae nyumba yake, ambaye huchimba chini sana, na kujenga msingi wa nyumba juu ya mwamba imara. Mafuriko yalipokuja, maporomoko ya maji yaliipiga nyumba, lakini hayakuweza kuitikisa, kwa sababu ilikuwa imejengwa vizuri.
- Kwa hekima nyumba hujengwaMit 24:3
Aya
Mit 24:3Kwa hekima nyumba hujengwa na kwa ufahamu huimarishwa.
- Kila mwanamke mwenye hekima hujenga nyumba yakeMit 14:1
Aya
Mit 14:1Mwanamke mwenye busara huijenga nyumba yake, bali mwanamke mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0