Gundua › Mada › Harusi na ndoa
Maisha ya kila siku
Harusi na ndoa katika Biblia
Vifungu vya Swahili Unlocked Literal Bible (53), mstari kwa mstari, kutoka Nave’s Topical Bible.
Desturi
- Wazazi waliwatafutia wana wao wakeMwa 21:21, Mwa 24:3–4, Mwa 28:1–2, Yer 29:6
Aya
Mwa 21:21Akaishi katka jangwa la Parani, na mama yake akampatia mke kutoka Misri.
Mwa 24:3–4na nitakufanya uape kwa Yahwe, Mungu wa Mbingu na nchi, kwamba hutampatia mwanangu mke kutoka kwa mabinti wa Wakanaani, miongoni mwao wale nikaao kati yao. Lakini utakwenda kwenye nchi yangu, na kwa ndugu zangu, na kumtafutia mwanangu Isaka mke.”
Mwa 28:1–2Isaka akamwita Yakobo, akambariki, na kumwagiza, “Usichukuwe mwanamke katika wanawake wa Kikanaani. Inuka, nenda Padani Aramu, katika nyumba ya Bethueli baba wa mama yako, na uchukue mwanamke pale, mmojawapo wa binti za Labani, kaka wa mama yako.
Yer 29:6Chukueni wake na mzae wana na mabinti. Kisha Kisha chukueni wake kwa ajili ya wana wenu, na wapatieni waume binti zenu. Wazae wana na mabinti na waongezeke ili msiwe wachache sana.
- Samsoni anawaomba wazazi wake wamtafutie mke MfilistiAmu 14:2
Aya
Amu 14:2'Nimemwona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti. Sasa mkanichukulie awe mke wangu.
- Rebeka anaulizwa: “Utakwenda na mtu huyu?”Mwa 24:57–58
Aya
Mwa 24:57–58Wakasema, “Tutamwita binti na kumuuliza.” Kwa hiyo wakamwita Rebeka na kumuuliza, “Je utakwenda na mtu huyu?” Akajibu, “Nitakwenda.”
- Rebeka anajifunika kwa shela anapokutana na IsakaMwa 24:65
Aya
Mwa 24:65Akamwambia mtumwa, “mtu huyo ni nani anaye tembea shambani akija kutupokea?” Mtumwa akasema, “Ni bwana wangu.” Hivyo Rebeka akachukua shela yake akajifunika.
- Vito na mavazi kwa bibi harusi, zawadi kwa familia yakeMwa 24:53
Aya
Mwa 24:53Mtumwa akaleta vipande vya fedha na vipande vya dhahabu, na nguo, akampatia Rebeka. Akampatia pia kaka yake na mama yake zawadi zenye thamani.
- Mahari ililipwa kwa baba wa bibi harusiMwa 34:12, Kut 22:16–17
Aya
Mwa 34:12Niambieni kiasi kikubwa chochote cha mahari na zawadi kama mtakavyo, nami nitatoa chochote msemacho, lakini mnipe msichana kuwa mke wangu.”
Kut 22:16–17Kama mwanaume akimtongoza bikra ambaye hana mchumba, na kama akilala naye, lazima amfanye kuwa mke wake kwa kulipa gharama za bibi arusi zinazo stahili. Kama baba yake akikataa kabisa kumpatia, lazima alipe hela inayo lingana na gharama za bibi arusi bikra.
- Labani: si desturi yetu kumwoza mdogo kabla ya mkubwaMwa 29:26
Aya
Mwa 29:26Labani akamwambia, “Siyo utamaduni wetu kumtoa bindi mdogo kabla ya mzaliwa wa kwanza.
- Wiki moja ya sherehe ya harusiMwa 29:22, Mwa 29:27–28
Aya
Mwa 29:22Hivyo Labani akawaalika watu wa mahali hapo na kuandaa sherehe.
Mwa 29:27–28Timiza juma la bibi arusi, na tutakupa yule mwingine pia kwa mbadala wa kunitumikia miaka mingine saba.” Yakobo akafanya hivyo, na akatimiza juma la Lea. Kisha Labani akampa Raheli binti yake kuwa mke wake.
- Bwana harusi alifanya karamu ya siku saba na wenzake thelathiniAmu 14:10–12
Aya
Amu 14:10–12Baba yake Samsoni akaenda chini alipokuwa mwanamke, na Samsoni akafanya sikukuu huko, kwa maana hii ilikuwa desturi ya vijana. Mara tu ndugu zake walipomwona, walimletea rafiki zao thelathini kuwa pamoja naye. Samsoni akawaambia, Hebu nawaambieni kitendawili. Ikiwa mmoja wenu anaweza kuipata na kuniambia jibu wakati wa siku saba za sikukuu, nitatoa nguo za kitani thelathini na seti ya nguo thelathini.
- Vito vya bibi harusi na mshipi wa harusiYer 2:32, Isa 61:10
Aya
Yer 2:32Je, mwanamwali anaweza kusahau mapambo yake, na bibi arusi mavazi yake? Lakini watu wngu wamenisahau mimi kwa siku nyingi!
Isa 61:10Nitafurahia sana katika Yahwe; Katika Mungu nitafurahia. Maana amenivika mimi kwa vazi la wokovu; amenivika mimi kwa vazi la haki, kama bwana harusi aliyejipamba mwenywe kwa kilemba, na kama bibi harusi aliyejipamba kwa vito.
- Binti wa mfalme katika vazi lililofumwa kwa dhahabu, pamoja na wenzakeZab 45:13–14
Aya
Zab 45:13–14Binti mfalme katika jumba la kifahari ana utukufu wote; mavazi yake yametengenezwa kwa dhahabu. Naye ataongozwa kwa mfalme akiwa katika mavazi ya dhahabu; mabikra, wenzake wanoumfuata, wataletwa kwako mafalme.
- Taji ya Sulemani kutoka kwa mama yake siku ya harusi yakeWim 3:11
Aya
Wim 3:11Nenda nje, mabinti wa wanaume wa Sayuni, na mtazame mfalme Sulemani, akivikwa taji ambalo mamaye alimvika siku ya arusi yake, katika siku ya furaha ya maisha yake.
- Sauti za bwana harusi na bibi harusi zilijaa mitaaniYer 7:34
Aya
Yer 7:34Nitazikomesha katika miji ya Yuda na mitaa ya Yerusalaemu sauti za kuiniuliwa na vicheko, Sauti ya bwana arusi na ya bibi arusi; kwa kuwa nchi hiyo itakuwa ukiwa.”
- Wanawali kumi wenye taa wanatoka kumlaki bwana harusi (mfano)Mt 25:1–6
Aya
Mt 25:1–6Ndipo ufalme wa mbinguni utafananishwa na wanawali kumi waliochukua taa zao na kuondoka kwenda kumpokea bwana harusi. Watano miongoni mwao walikuwa wapumbavu na watano wengine walikuwa werevu. Wanawali wapumbavu walipochukua taa zao, hawakuchukua mafuta yoyote. Bali wanawali welevu walichukua vyombo vyenye mafuta pamoja na taa zao. Sasa wakati bwana harusi amechelewa kufika, wote walishikwa usingizi na wakalala. Lakini wakati wa usiku wa manane kulikuwa na yowe, 'Tazama, bwana harusi! Tokeni nje mkampokee.'
- Wageni walitarajiwa kuvaa mavazi ya harusi (mfano)Mt 22:11–12
Aya
Mt 22:11–12Lakini mfalme alipoingia kuwatazama wageni, alimuona mtu mmoja ambaye hakuvaa vazi rasmi la harusi! Mfalme alimwuliza, 'Rafiki, ulipataje kufika hapa ndani bila vazi la harusi?' Na mtu huyo hakujibu chochote.
- Ndoa ilishuhudiwa na wazee langoni mwa mjiRut 4:9–11
Aya
Rut 4:9–11Ndipo Boazi akawaambia viongozi na watu wote, “Ninyi ni mashaidi kuwa nimenunua kila kilichokuwa cha Elimeleki na kila kilichokuwa na Kileoni na Mahilon kutoka kwenye mikono ya Naomi. Zaidi ya hayo kumhusu Ruth Mmoabu, mke wa Mahlon: nimempa kibali cha kuwa mke wangu, ili kuendeleza jina na urithi wa marehumu, ili kwamba jina lake lisipotee kati ya ndugu zake na lango la watu wake. Ninyi ni mashahidi leo.” Watu wote na viongozi waliokuwa katika lango, walisema, “Tu mashahidi. Yahweh amfanye mwanamke huyu ambaye amekuja nyumbani kwako kama Raheli na Leya, ambao wawili hawa wameijenga nyumba ya Israeli. Na ubarikiwe katika Efrata na kuwa mashuhuri katika Bethelehem.
- Yusufu anaitwa mume wa Mariamu wakati walikuwa wamechumbiana tuMt 1:18–19, Lk 1:27
Aya
Mt 1:18–19Kuzaliwa kwa Yesu Kristo kulikuwa kwa namna hii. Mama yake, Mariamu, alichumbiwa na Yusufu, lakini kabla hawajakutana, alionekana kuwa na mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Mume wake Yusufu, alikuwa mtu mwenye haki hakutaka kumwaibisha hadharani. Aliamua kusitisha uchumba wake naye kwa siri.
Lk 1:27kwa bikra aliyekuwa ameposwa na mwanaume ambaye jina lake lilikuwa Yusufu. Yeye alikuwa wa ukoo wa Daudi, na jina la bikra huyo lilikuwa Mariamu.
Katika Sheria
- Mtu aliyeoa karibuni yuko huru na vita kwa mwaka mmojaKum 24:5
Aya
Kum 24:5Mwanamume atakapochukua mke mpya, hatakwenda vitani na jeshi, na wala hataamrishwa kwenda kwenye shughuli yoyote ya kulazimishwa; atakuwa huru kuwa nyumbani kwa mwaka mzima na atamfurahisha mke wake aliyemchukua.
- Ndugu humwoa mjane asiye na mtoto wa ndugu yakeKum 25:5–10, Mwa 38:8, Mk 12:19
Aya
Kum 25:5–10Iwapo kaka wanaishi pamoja na mmoja wao akafariki bila kuwa na mwana, basi mke wa marehemu hatakiwi kuolewa na mtu nje ya familia. Badala yake, kaka yake mumewe anapaswa kulala naye na kumchukua kuwa mke wake na kutekeleza wajibu wa kaka wa mume kwake. Hii ni kwamba mtoto wa kwanza atakayezaliwa arithi chini ya jina la kaka yake mwanamume aliyefariki, ili jina lake lisiangamie ndani ya Israeli. Lakini kama mwanamume hataki kumchukua mke wa kaka yake awe wake, basi mke wa kaka yake anapaswa kwenda malangoni mpaka kwa wazee na kusema, “Kaka wa mume wangu amekataa kuwajibika kwa niaba ya jina la kaka yake humu Israeli; hataki kufanya wajibu wa kaka wa mume kwangu”. Kisha wazee wa mji wake wanapaswa kumuita na kuzungumza naye. Lakini tuseme atasisitiza na kusema, “Sitaki kumchukua”. Basi mke wa kaka yake anatakiwa kuja kwake mbele ya wazee, kumvua ndara zake miguuni mwake, na kumtemea usoni. Anapaswa kumjibu na kusema, “Hivi ndivyo kinachofanyika kwa mwanamume asiyetaka kujenga nyumba ya kaka yake”. Jina lake Israeli litaitwa, “Nyumba ya mtu aliyevuliwa ndara zake”.
Mwa 38:8Yuda akamwambia Onani, “Lala na mke wa nduguyo. Fanya wajibu wa shemeji kwake, na umwinulie nduguyo mwana.”
Mk 12:19“Mwalimu, Musa alituandikia kuwa, 'Ikiwa ndugu ya mtu akifa na kumwacha mke nyuma yake, lakini hakuacha mtoto, mtu atamchukua mke wa ndugu yake, na kujipatia watoto kwa ajili ya ndugu yake.'
- Binti za Zelofehadi lazima waolewe ndani ya kabila la baba yaoHesabu 36:6–8
Aya
Hesabu 36:6–8Hiki ndicho BWANA anaagiza kuhusu mabinti wa Zelofehadi. Anasema, 'Acha waolewa na wale ambao wao wanaofikri ni vizuri zaidi, lakini lazima waolewe ndani ya kabila ya baba yao.' Hakuna mgawo wa watu utakaobadilika kutoka kabila moja kwenda jingine. Kila mtu wa Israeli ataendelea na mgawo wa kabila ya baba y ake. Kila mwanamke wa watu wa Israeli aliye na mgao kwenye kabila lake lazima aolewe na mtu wa ukoo unaotoka kwenye kabila la baba yake. Hii itafanyika hivyo ili kila mtu wa wana wa Israeli aweze kuwa na urithi kutoka kwa mababa zake.
- Makuhani hawaruhusiwi kumwoa mwanamke aliyetalikiwaLaw 21:7, Law 21:13–14
Aya
Law 21:7Hawataoa mwanamke aliye kahaba na aliyetiwa unajisi, na hawataoa mwanamke aliyetalikiwa kutoka kwa mume wake kwa sababu wametengwa kwa ajili ya Mungu wao.
Law 21:13–14Kuhani mkuu nilazima aoe bikira kuwa mke wake. Hataoa mjene, mwanamke mtalaka au mwanamke aliye kahaba. Anaweza kuoa mwanamke bikira kutoka kwa watu wake,
- Mwanamke mateka kwanza anawaombolezea wazazi wake mwezi mzimaKum 21:10–13
Aya
Kum 21:10–13Utakapokwenda kupigana vita dhidi ya maadui zako na Yahwe Mungu wako atakapokupa ushindi na kuwaweka chini ya mamlaka yako, na ukawachukua mbali kuwa mateka, kama kati ya mateka ukamwona mwanamke mzuri, nawe ukamtamani na kutaka kujitwalia awe mke wako, basi utamleta nyumbani kwako; atanyoa nywele zake na kukata kucha zake. Kisha atazivua nguo alizokuwa amezivaa wakati alipochukuliwa mateka na atabaki nyumbani kwako na kuwaomboleza baba yake na mama yake kwa mwezi mzima. Baada ya hapo unaweza kulala naye na kuwa mume wake, naye atakuwa mke wako.
- Waisraeli waliambiwa wasioane na mataifa ya KanaaniKum 7:3
Aya
Kum 7:3Wala hamtapanga ndoa zozote pamoja nao, hamtawatoa binti zenu kwa vijana wao, na hamtawachukua binti zao kwa vijana wenu.
Mifano
- Abraham alimwoa Sara, dada yake kwa babaMwa 11:29, Mwa 20:12
- Isaka alimpenda Rebeka na akafarijiwa baada ya kifo cha mama yakeMwa 24:67
Aya
Mwa 24:67Kisha Isaka akamleta katika hema ya Sara mama yake na akamchukua Rebeka, na akawa mke wake, na akampenda. Kwa hiyo Isaka akafarijika baada ya kifo cha mama yake.
- Yakobo anafanya kazi miaka saba kwa ajili ya Raheli; inaonekana siku chacheMwa 29:18–20
Aya
Mwa 29:18–20Yakobo alimpenda Raheli, hivyo akasema, “Nitakutumikia miaka saba kwa ajili ya Raheli, binti yako mdogo.” Labani akasema, Itakuwa vema kukupa wewe, kuliko kumpa mtu mwingine. Kaa nami.” Hivyo Yakobo akamtumikia kwa miaka saba kwa ajili ya Raheli; nayo ilionekana kwake kama siku chache tu, kwa ajili ya upendo aliokuwa nao kwake.
- Yakobo anapewa Lea kwanza, kisha RaheliMwa 29:21–28
Aya
Mwa 29:21–28Kisha Yakobo akamwambia Labani, “Nipe mke wangu, kwani siku zangu zimetimia - ili kwamba nimwoe! Hivyo Labani akawaalika watu wa mahali hapo na kuandaa sherehe. Wakati wa jioni, Labani akamchukua Lea binti yake mkubwa na kumleta kwa Yakobo, aliyelala naye. Labani akampa mtumishi wake wakike Zilpa kuwa mjakazi wa Lea. Ilipofika asubuhi, tazama, kumbe ni Lea! Yakobo akamwambia Labani, “Ni nini hiki ulichonifanyia? Je sikukutumikia kwa ajili ya Raheli? Kwa nini basi umenihadaa? Labani akamwambia, “Siyo utamaduni wetu kumtoa bindi mdogo kabla ya mzaliwa wa kwanza. Timiza juma la bibi arusi, na tutakupa yule mwingine pia kwa mbadala wa kunitumikia miaka mingine saba.” Yakobo akafanya hivyo, na akatimiza juma la Lea. Kisha Labani akampa Raheli binti yake kuwa mke wake.
- Kalebu anamwoza binti yake Aksa kwa atakayeiteka Kiriath-seferiAmu 1:12–13
Aya
Amu 1:12–13Kalebu akasema, Yeyote atakayeivamia Kiriath-seferi na kuichukua, nitampa Aksa, binti yangu, awe mkewe. Otinieli, mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu, akaiteka Debiri, naye Kalebu akampa Aksa, binti yake, awe mkewe.
- Sauli anamwahidi binti yake mtu atakayemuua Goliathi1 Sam 17:25, 1 Sam 18:17
Aya
1 Sam 17:25Watu wa Israeli walisema, “Umemuona mtu huyu aliyejitokeza? Amekuja kuipa changamoto Israeli. Basi mfalme atampa mali nyingi mtu atakayemua, atamuozesha binti yake, na familia ya baba yake haitalipa kodi katika Israeli.”
1 Sam 18:17Kisha Sauli akamwambia Daudi, “Huyu hapa ni binti yangu mkubwa Merabu. Nitakupatia awe mke wako. Ila tu uwe jasiri kwa ajili yangu na upigane vita vya BWANA.” Maana Sauli alifikiri, “Usije mkono wangu ukawa juu yake, ila acha mkono wa Wafilisti uwe juu yake.”
- Sauli anaomba magovi mia moja ya Wafilisti; Daudi analeta mia mbili1 Sam 18:25–27, 2 Sam 3:14
Aya
1 Sam 18:25–27Na Sauli akasema, “Hivi ndivyo mtakavyo mwambia Daudi, 'Mfalme haitaji mahari yoyote, isipokuwa govi mia moja za Wafilisti, ili ajilipize kisasi kwa adui wa mfalme.”' Basi Sauli alifikiri atamwangusha Daudi kwa mkono wa Wafilisti. Watumishi wake walipomwambia maneno haya, yakamvutia Daudi awe mkwe wa mfalme. Kabla siku hizo hazijapita, Daudi aliondoka na watu wake na kuwaua Wafilisti mia mbili. Daudi akazileta govi zao, na kumkadhi mfalme kulingana na idadi yake, ili aweze kufanyika mkwe wa mfalme. Kwa hiyo Sauli akamwoza Mikali, binti yake, awe mkewe.
2 Sam 3:14Kisha Daudi akatuma wajumbe kwa Ishboshethi, mwana wa Sauli, kusema, “Nipe Mikali, mke wangu niliyetoa kwa ajili yake govi mia moja za Wafilisti.”
- Boazi anamchukua Ruth kuwa mke wake mbele ya mashahidiRut 4:5, Rut 4:10
Aya
Rut 4:5Kisha Boazi akasema, “Ile siku utakayonunua shamba kutoka mkononi mwa Naomi, yakupasa pia kumchukua Ruth Mmoabu, mjane wa mtoto wa Elimeleki, ili kuliinua jina la marehemu kama urithi wake.”
Rut 4:10Zaidi ya hayo kumhusu Ruth Mmoabu, mke wa Mahlon: nimempa kibali cha kuwa mke wangu, ili kuendeleza jina na urithi wa marehumu, ili kwamba jina lake lisipotee kati ya ndugu zake na lango la watu wake. Ninyi ni mashahidi leo.”
- Wabenjamini wanajinyakulia wake kati ya wachezaji wa ShiloAmu 21:21–23
Aya
Amu 21:21–23Tazama wakati ambapo wasichana kutoka Shilo watatoka kucheza, Tokeni nje ya mizabibu na kila mmoja wenu anapaswa kunyakua mke kutoka kwa wasichana wa Shilo, kisha kurudi kwenye nchi ya Benyamini. Wakati baba zao au ndugu zao watakapokuja kutupinga, tutawaambia, 'Tupeni neema! Waache wabaki kwa sababu hatukupata wake kwa kila mtu wakati wa vita. Na ninyi hamna hatia juu ya ahadi, kwa sababu hamkuwapa wao binti zenu.'” Watu wa Benyamini walifanya hivyo. Walichukua idadi ya wake waliowahitaji kutoka kwa wasichana waliokuwa wakicheza, nao wakawachukua ili wawe wake zao. Wakaenda na kurudi mahali pa urithi wao; wakajenga tena miji, na wakaishi ndani yao.
- Ahasuero anamfanya Esta malkia na kufanya karamu ya EstaEst 2:17–18
Aya
Est 2:17–18Mfalme alimpenda Esta zaidi kuliko wanawake wengine, na alipata kibali kuliko na wema mbele zake zaidi kuliko mabikira wengine na hivyo mfalme akamvika taji ya kimalkia badala ya Vashiti. mfalme akawafanyia karamu kubwa wasimamizi na wahudumu wake wote, karamu ya Esta na akawapa unafuu wa kodi katika majimbo. Pia akawapa zawadi kwa ukarimu.
- Hosea ananunua mwanamke kwa shekeli kumi na tano za fedha na shayiriHos 3:2
Aya
Hos 3:2Kwa hiyo nimemnunulia mwenyewe kwa vipande kumi na tano vya fedha na homeri na letheki ya shayiri.
- Yesu na wanafunzi wake kwenye harusi huko KanaYn 2:1–10
Aya
Yn 2:1–10Baada ya siku tatu, kulikuwa na arusi huko Kana ya Galilaya na mama yake Yesu alikuwa huko. Yesu na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa katika arusi. Wakati walipoishiwa na divai, mama yake Yesu akamwambia, “Hawana divai.” Yesu akajibu, “Mwanamke hiyo inanihusu nini mimi? Muda wangu mimi bado haujatimia.” Mama yake akawambia watumishi, “Chochote atakachowambia fanyeni.” Basi kulikuwa na mitungi sita ya mawe pale iliyowekwa kwa ajili ya kunawa katika sikukuu za Wayahudi, kila moja lilikuwa na ujazo wa nzio mbili tatu. Yesu akawambia, “Ijazeni maji mitungi ya mawe.” Wakajaza hadi juu. Kisha akawambia wale watumishi, “Chukueni kiasi sasa na mpeleke kwa muhudumu mkuu wa meza.” Wakafanya kama walivyoagizwa. Mhudumu mkuu aliyaonja yale maji yaliyokuwa yamebadilika na kuwa divai, ila hakujua yalikotoka (lakini watumishi waliochota maji walijua yalikotoka). Kisha akamwita bwana harusi na kumwambia, “Kila mmoja huanza kuwahudumia watu divai nzuri na wakiishalewa huwapa divai isiyo nzuri. Lakini wewe umeitunza divai nzuri hadi sasa”
- Mitume waliwachukua wake zao katika safari zao1 Kor 9:5
Aya
1 Kor 9:5Hatuna haki kuchukua mke aliye amini kama wafanyavyo mitume wengine, na ndugu wa Bwana, na Kefa?
Katika Mithali
Vyanzo
Kutoka Biblia ya Mada ya Nave (Orville J. Nave, 1896; mali ya umma): mada zimechaguliwa, mistari imefupishwa kwa lugha ya sasa, bila tafsiri za maana; kila aya imehakikiwa.
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0